Barua ya wazi kwako nikupendae

Barua ya wazi kwako nikupendae

mkanyikivega

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2016
Posts
215
Reaction score
225
KIPENZI MKE WANGU, KOMBE LA DUNIA LINAKARIBIA KUANZA.

NAKUMEGEA VIPANDE VYA KANUNI ZITAKAZO PELEKEA UZURI WAKO ULIONAO UBAKI SALAMA KWA KIPINDI CHOTE CHA WORLD CUP

KANUNI

1: Remote ya TV hakikisha muda wote iko mikononi mwangu.

2: Wakati game linaendelea, jizuie kuniuliza maswali ya kipuuzi. Mfano; Barcelona inachaza na ujerumani???

3: Wakati game linaendelea uwe unanitizama usoni. Ukihisi natabasamu nawe tabasamu, nimenuna aidha nawe nuna au chomoka ingia chumbani kimya kimya.

4: huyu dogo anayenyonya haki kisha wakati wa game hajui kitu kinachoitwa kulia.

5: Wakati game linaendelea pita mgongoni kwangu au km ni lazma upite mbele ya uso wangu basi pita kwa kutambaa sakafuni, sawa mama??

6: tumia mbinu zako kutambua kuwa kila game moyo wangu uko timu ipi. Ukiona niko timu usiyoipenda nyooka jikoni au chumbani uchezee simu yako hadi uchoke. Ni muda mzuri kwako kuchart hata na watu ambao huwa sipendi skia eti umewasiliana nao.

7: Km moyo wako hauko Argentina au Spain, basi si mbaya ukaona umuhimu wa kwenda home kwenu wasalimia wazazi. Tuna muda mrefu hatujaenda wajulia hali. Utaniwakilisha si mbaya.

8: replay au marudio ya game iliyokwisha pita ni sawa na game iko live, nidhamu iwe juu mama.

9:habari ya kutamka kuwa eti unafuatilia tamthilia ya sultan au mydebra, ni sawa na kunichoma kidole machoni.

10: usisahau kanuni namba 1 hapo juu.

UKIZINGATIA HIZO KANUNI MAMA, AAH KOMBE LA DUNIA LITAKUJA NA KUPITA UKIWA NA UZURI WAKO HUO. Wasalaam mumeo kipenzi..
 
copy kwa espy
uwe makini mwezi huu unaweza ukameza meno yako
 
Back
Top Bottom