Barua ya wazi kwa walimu

Barua ya wazi kwa walimu

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,890
Reaction score
29,413
CHAMA CHA WALIMU KIFUTWE!
Ningependa kuona Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kinafutiliwa mbali kabisa kwani kimeshindwa kuondoa ama kupunguza matatizo yanayowakabili walimu. Chama hiki kimeshindwa kutetea maslahi ya walimu na kimeonyesha udhaifu mkubwa katika ufuatiliaji wa madai mbalimbali ya wanachama wake. Baadhi ya madai haya ni posho ya kufundishia ktk mazingira magumu, kupandishwa madaraja, malimbikizo ya posho mbalimbali na nyongeza ya mishahara.

Kwa jinsi hali inavyojionyesha, ni vigumu sana hiki chama cha sasa kuwatetea walimu ipasavyo. Wakuu wa CWT (Gratian Mukoba, Ezekiel Olucho na wengine) wanaofaidi matunda ya michango ya walimu katika chama, wameshindwa kabisa kuwasemea walimu dhidi ya ukandamizaji wa serikali wa muda mrefu. Kwanza nashangaa kwanini hawa viongozi wapo madarakani kwa muda mrefu hivi! Michango ya walimu kwa CWT imetumika kuwekeza vitega uchumi mbali mbali, kama vile Mwalimu House, ambapo matunda yake hayamnufaishi mwalimu isipokuwa mchwa wachache wanaojiita viongozi wa CWT.

Walimu hukatwa jumla ya mabilioni ya shilingi kila mwezi kutoka kwenye mishahara yao na pesa zote hizi hutumika kutunisha vitambi vya viongozi wa walimu huku walimu wakifa njaa bila sababu ya msingi. Wala matumizi ya michango ya uanachama hayajawahi kukaguliwa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuona jinsi gani michango ya walimu inavyotumika na kama walimu wananufaika na pesa hizo au fedha inayotokana na uwekezaji wa fedha hizo. Ingekuwa jambo la msingi endapo michango hii ingewarejea walimu kupitia SACCOS au namna nyingine ambayo ingewanufaisha walimu kuliko kubunguliwa na bungu wachache kwa maslahi yao binafsi. Hatuwezi kuwa na chama kimoja kikubwa kabisa lakini ambacho hakina tija kwa wanachama wake.

Kwa kuwa chama hiki kimeshindwa kuleta tija kwa walimu, napendekeza kivunjwe kabisa na kusahaulika katika ardhi ya Tanzania.
Chama hiki kivunjiliwe mbali ili kila mwalimu ashughulikie matatizo mwenyewe badala ya kuendelea kuwakamua walimu michango ya chama ambacho hakiwezi kuwatetea. Baada ya kuvunjwa, mali zake ziuzwe na pesa zitakazopatikana zigawanywe kwa walimu kulingana na muda wa mwalimu kazini na kiasi alichokuwa akichangia kwa mwezi.

Kufanya hivyo kutawapunguzia walimu wingi wa matatizo yanayowakabili kwani inaonekana kwamba hata chama chenyewe ni mzigo kwa walimu. Ndiyo. Kiasi cha michango kinachokatwa kutoka kwenye mishahara ya walimu kinatosha kabisa kupunguza umasikini wa kipato unaowakabili walimu endapo CWT itavunjwa na hivyo makato ya wanachama kusitishwa.

Lakini, kama nilivyodokeza hapo awali, adui wa walimu ni walimu wenyewe. Wengi wao wana uelewa mdogo wa mambo, hivyo CWT imekuwa ikitumia udhaifu huo kuwakandamiza walimu kwa muda mrefu sasa. Na serikali nayo, kwa upande mwingine, imekuwa ikitumia mwanya huo huo kugoma kuwaboreshea walimu mishahara, kuwapandisha madaraja au kuwalipa posho mbalimbali wanazostahili. Kwa mtaji huu, walimu watazidi kukandamizwa hadi pale watakapojitambua, kumjua adui yao wa kweli na kuchukua jitihada za kupambana naye hadi kumtokomeza.

Nategemea kwamba walimu mtaamuka kutoka usingizi wa pono mliolala na kuanza kushughulikia matatizo yenu kwa njia nyingine badala ya kuendelea kukitegemea Chama Cha Walimu ambacho kimeshindwa kushughulikia matatizo yenu ipasavyo. Inavyoelekea ni kwamba viongozi wa chama chenu ama wameamua kuwasaliti kwa kushirikiana na serikali kuwakandamiza au hawana uwezo wa kutosha kuikabili serikali iweze kuwatatulia matatizo lukuki yanayowakabili na ambayo yamekuwa yakichangia kushuka kwa ubora wa elimu. Na ni bahati mbaya kushuka kwa kiwango cha elimu hakiwaathiri watoto wa vigogo ambao husoma kwenye shule za binafsi zilizo walimu wa kutosha na bora, mazingira mazuri ya kujifunzia na vifaa kufundishia vya kutosha. Watoto wanaotabika katika shule hizi mbovu za serikali ni wale wa walalahoi ambao hata kula kwao ni kwa shida na taabu na ambao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule binafsi.
 

Attachments

  • mwalimu at work.jpg
    mwalimu at work.jpg
    30.6 KB · Views: 230
  • mwalimu at work.jpg
    mwalimu at work.jpg
    44.7 KB · Views: 144
Nashukuru kwa mchango wako ila nimeshindwa kujua kama wewe ni mwalimu au la kwani katika maelezo yako hujaonyesha.
 
ni kweli naunga mkono hoja hii,mwalimu akistafu cwt inamkumbukaje mwalimu?baada ya kukatwa kwa muda wote,?wakigoma hakuna wa kutetea,
 
"adui wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe!"

na ndio hapo kuna usemi kuwa walimu ni waoga! toeni kauli moja CHAMA KIVUNJWE!
 
Walimu wamezubaa mno na hawajielewi isipokuwa wachache wetu. So acha watutie adabu hadi tutakapo amka.

Ninachotaka hiki Chama isiwe lazima kila mwl kujiunga.
Uwe ni utash wa mtu kujiunga au kuacha huu udikteta wa sasa huishe.
 
Walimu wamezubaa mno na hawajielewi isipokuwa wachache wetu. So acha watutie adabu hadi tutakapo amka.

Ninachotaka hiki Chama isiwe lazima kila mwl kujiunga.
Uwe ni utash wa mtu kujiunga au kuacha huu udikteta wa sasa huishe.

Kwa walioajiriwa.kuanzia mwaka huu si lazima
 
Ndoto za asubuhi,eti ujisimamie? Jaman cwt ikifa ccm itakuwa imeweza kutugawanya walimu tusiwe na umoja na wameanza kufanikiwa.tatzo walimu cc ni waoga na wa kwanza kulalamika, yafanyika mapnduz kukinusuru ktk ufisadi unaoudai bt kife kabsa ckuungi mkono.kwa taarifa yako nilipo mm kikaz cwt imekuwa mtetez wetu sana kias kwamba mkurugenz anaipga vita sna,ukionwa wakat wa kaz umevaa ktambulsho au tshirt zake.uongoz wa hapa uko imara tunapata posho za vikao vya kila mwez kulingana na idadi yetu vle vle tunavyochangia.kwa hapa ni mwiba wa serikali.
 
Mleta uzi unajichanganya,kama ww ni mwalimu au mtumishi wa umma.

Kufutwa/kuvunjwa kwa CWT sio suluhisho la kudumu la kumaliza kero za muda mrefu kwa walimu ndani ya wizara ya elimu na tamisemi.
Kidole kimoja hakivunji chawa na umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Soma chimbuko la vyama vya wafanyakazi duniani 1890.
Marehemu Thomas Mboya aliwahi kusema mwajiri hata awe baba yako au mama yako au mjomba wako au shangazi yako au ndugu yako wote wana asili ya unyonyaji.

Haki za walimu zipo kisheria na kila mwaka serikali inatenga bajeti yenu kwa nn haziwafikii?madai ya posho ya kufundishia ktk mazingira magumu, kupandishwa madaraja, malimbikizo ya posho mbalimbali,nyongeza ya mishahara ,likizo,uhamisho n.k zinaliwa na CWT?

1.Madai hayo ya walimu watumishi wengine wa umma nchini wanalipwa/wanadai?
2.Adui NO.1 wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe na serkali wala sio CWT.
3.walimu kuwa na waajiri/wasimamizi wa kazi wengi ndani ya serikali moja ni tatizo.
4.aira za walimu kutosimamiwa na chombo kimoja ni janga.
5.walimu na CWT ni waoga na hawawezi kuwa kitu kimoja wakati wa kupingania/kudai haki maana haki haiji yenyewe kwenye kisahani bali hudaiwa na mdai.
6.Kuunda vyama vidogox2 vya walimu ni uroho wa madaraka na kujimaliza wenyewe[divide & rule].
7.Kuanzisha chama ni haki na kujiunga ni haki kwa mjibu wa katiba 1977.
8.walimu ndio huwaingiza baadhi ya watoa maamuzi yao kwenye ngazi za maamuzi[chama kitakacho kubali pilau yetu ndio changuo la wafanyakazi nchini..Nicolus Mgaya]
 
baadhi ya viongozi wa cwt wapo kwaajili ya kwenda kwenye vikao na kupokea posho.lakin unaweza kuta kuna tatizo unamwambia mwakilishi anakwambia mim nifanye nn.wawakilishi weng wanachaguliwa hawajui majukum yao na kama wanajua basi ni waoga.
 
Wanochangia kwa woga eti kisivunjwe nashindwa kuwaelewa kwani kama kilianzishwa kkwa malengo ya kuwasaidia nlakini kimekuwa kinyume na matarajio/malengo its better to discard it why should you keep a junk with cost!Mleta mada kutobainisha yeye ni mwl au la hiyo haja haina msingi kwani tunachotakiwa ni kujadili hoja/ukweli/uwongo au mada wala sii yeye.Waalimu wamekuwa waoga hasa kutokana na uduni wa maisha yao ndo sababu wanapelekwa kama ng`ombe aliyeshikwa mkia au beberu aliyekamatwa sharubu.waalimu amkeni sikilizeni maneno ya Bob Marley ..Its better die while fighting for freedom than living in slavery life.
 
Nilisikia waziri husika akisema kwamba kujiunga na cwt ni hiari na sio lazima
kotokana na kauli hiyo ya waziri napenda kujiaminisha kuwa walim wanaokatwa ni vihehere vyao coz walijiunga wenyewe kwa hiari yao.
 
Vipi kuhusu kujitoa CWT na Kujiunga na mtandao wa walimu TTN.Waalimu nchi hii Hamjithamini kabisa!?
 
Wanochangia kwa woga eti kisivunjwe nashindwa kuwaelewa kwani kama kilianzishwa kkwa malengo ya kuwasaidia nlakini kimekuwa kinyume na matarajio/malengo its better to discard it why should you keep a junk with cost!Mleta mada kutobainisha yeye ni mwl au la hiyo haja haina msingi kwani tunachotakiwa ni kujadili hoja/ukweli/uwongo au mada wala sii yeye.Waalimu wamekuwa waoga hasa kutokana na uduni wa maisha yao ndo sababu wanapelekwa kama ng`ombe aliyeshikwa mkia au beberu aliyekamatwa sharubu.waalimu amkeni sikilizeni maneno ya Bob Marley ..Its better die while fighting for freedom than living in slavery life.
Baadhi ya walimu ni wanafiq sana. Hawajui wajibu wa CWT katika kutetea maslahi yao. Inasikitisha sana.
 
Changeni kwanza hela ya kuchukulia fomu ya Samia kugombea urais 2025.
 
Changeni kwanza hela ya kuchukulia fomu ya Samia kugombea urais 2025.
Mkuu mimi ni mwalimu lakini siungi mkono ujinga wa kumchukulia Samia fomu. Dili hii inafabywa na baadhi ya chawa waliopandikizwa huku kwenye ualimu.
 
Back
Top Bottom