kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,785
- 20,158
Salaam,
Ni wazi na inajulikana kwamba nyie TCRA ndio mamlaka inayodeal na mawasiliano Tanzania.
Lakini ukweli ni kuwa mmegeuka kuwa jipu, wanafiki waongo na kuwaongopa watanzania walipa kodi wanaotoa kodi zao na ndizo zinazotumika kila siku kodi hukusanywa hatimae kupelekwa serikalini na nyie mnapewa fungu la kujiendesha
Siku za hivi karibuni mmekua hamuambiliki hamsikii mmegeuka jipu la kwapa ambalo linajificha mahala pabaya sana tena lahitaji kutumbuliwa
Mnaendesha mamlaka kwa kodi zetu ila hamsimamii kwa haki wala kufata sheria
Wananchi wamegeuka watumwa ndani ya nchi yao kwa mateso wanayopata na kuumia kila siku Tulitarajia nyie ndo wa kuwasemea lakini mmegeuka viziwi msiosikia hamuambiliki hata kwa chembe Mlitudanganya na mliweka sheria kwamba tukiingia digital local channel kuonekana zitakua bure lakini leo hii tunalipia mpaka mpaka kuona television ya taifa Tbc ambayo ni kodi zetu
Tuliingia ubia na kampuni ya startimes wakatumia mitambo ya Tbc ambayo ni mali ya umma kuendeshea mambo yao lakini bado wanaendelea kutukandamiza wakati sheria inasema local channel ziwe bure Kuna makampuni ambayo local channel hata zisipoonekana bure wao hawahusiki kwa sababu wanatoa huduma kimataifa mfano wake ni Azam na Dstv
Lakini ving'amuzi vyote vilivyobaki hatupaswi kulipia local zinapaswa ziwe bure
Hivi hii serikali kwanini inawaogopa hawa wachina wa startimes kiasi hiki, kwanini wanaiogopa continental? zuku jee? ting jee?
Huyu waziri wa habari sijui anafanya kazi gani yupo yupo tu
Na mjue kwamba sio watanzania wote wana uwezo wa kumudu kulipia hizo local channel kwa kifurushi cha 9000 ama 11000 kwa mwezi
Tcra nyie mmekua bize kutunyanyasa watanzania mpo bize kukamata wakosoaji wa serikali huku mkiendelea kuwaacha hawa mapebari na wanyonyaji hususani haya makampuni ya kichina
Nyinyi TCRA najua mnabeba ajenda za kuzima uhuru wa kujieleza mfano ni mnavyoiandama JamiiForums bila sababu.
Hamustahili Kuwa mamlaka ya mawasiliano tanzania kwanza hamna faida yoyote kwetu tumechoka na ufumbiaji macho wenu wa malalamiko
Wananchi wamelalamika mpaka wamechoka lakini mpo kimya mnadili tu na kukandamiza uhuru wa kujieleza
Kwanini startimes waliingia mkataba na tbc? tunataka mkataba uwekwe wazi kama kuna harufu ya ufisadi tujue Na taarifa zinajulikana wazi kuwa mna mkakati wa kuminya vyombo vya habari kupitia makampuni ya vingamuzi mkakati wa kuhakikisha tbc ndo inatizamwa tu ili muendelee na mikakati yenu ya kubana uhuru wa habari
Na hili suala la kubaki tbc tu halikubaliki tutaenda mahakamani kulipinga na hatutokubali kamwe kuwa watumwa ndani ya nchi yetu
Hamna maana yoyote ya kuwepo kwenu ninyi TCRA
Naombeni watanzania wenzangu tusikubali kuona tukiburuzwa ama kunyanyaswa ndani ya nchi yetu wenyewe
Huu udhalimu tuukatae Kwa nguvu zetu zote kwani kadri zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya sana
Tunalipa kodi zinaendesha mamlaka km hizi ambazo hazina faida yoyote kwenu kimegeuka ni chombo cha kuzima uhuru wa habari na chombo cha kusimamia wananchi kunyima haki ya local channel
Nape mnauye naomba ujiuzulu
TCRA ifutwe ama kuvunjwa kabisa
@FreeLocalChannel