Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,524
- 51,200
Barua yangu hii ni ya msingi mno kuliponya Taifa
Assalam Aleikum Sheikh.
Bila shaka utakuwa u-mzima wa hali na afya.
Ndugu Sheikh Ponda, kumekuwa kukijiri mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli yanahitaji watu wenye hekima waliojaliwa kipawa cha uongozi kuyasemea ili angalau sisi wananchi nyoyo zetu zipate kutulia na kuendelea kupata matumaini katika Taifa letu. Sheikh pole pole tunaanza kukata tamaa na msutakbali wa Taifa hili, tunaona waziwazi tunaelekea gizani!
Ndugu Sheikh Ponda, Mimi nakupongeza sana kwa kuisemea hali halisi mapema sana pale ulipoitisha mkutano wa waandishi ukazungumzia hali ya viashiria vya kupotea kwa amani nchini, ukaelezea kuhusu kutekwa na kupotea kwa watu, ulielezea hilo mapema sana kabla hata umma haujaanza kuamini ipasavyo kuwa hilo jambo linatokea nchini.
Kauli yako baadae ilikuja kuungwa mkono na viongozi wengine wa Dini waliotoa nyaraka zenye ujumbe mkali sana na wenye maana sana kwa mustakbali wa amani na haki nchini.
Ndugu Shekh Ponda, kazi zenu nyinyi viongozi wa Kiroho zilizaa matunda ya muda, kiasi kwamba tukadhani haya mambo ya aibu yameisha nchini. Hata hivyo kutekwa kwa Mfanyabiashara mkubwa nchini, ambaye anachangia zaidi ya ASILIMIA TATU NA NUSU ya Pato la Taifa na Kuajiri zaidi ya Watanzania 25000 kumeniogopesha sana na kunifanya nione ni Busara kukuomba ndugu Sheikh Utoke Tena Ukemee haya mambo.
Ninajua wanayoyafanya hayo ni wanafiki ambao pengine nao huswali misikitini au Makanisani, kwa hiyo naamini Ukilisemea hili jambo tena na tena huenda nyoyo zao zikawa Laini.
Ndugu Ponda, Bila shaka unafahamu vizuri kwenye Qur'an Mwenyezi Mungu alipomtuma nabii Musa akamwambia aongee na Firauni kwa maneno laini na Mazuri huenda moyo wake ukawaonea huruma wana wa Israel那hivyo kuwaachia huru, hata hivyo Firauni alishupaza shingo na mwisho wake ukawa mbaya sana. Sheikh Ponda nakuomba Uwaeleze hao Madhalimu waliojificha waelewe kwamba Mwenyezi Mungu Anayaona yale wanayoyaficha , wanayoyatenda na Wasipoacha na kisha Kutubu basi mwisho wao ni mbaya sana hapa duniani na Akhera.
Sheikh Ponda, sisi katika mazingira haya ya sasa, kusema kweli tunahitaji a MORAL LEADER wa kumfuata, ambaye atatufunika kwa mbawa zake kwa rehma, utu, ukarimu, kutupenda na kutusemea. Kwa hivyo basi, wewe mara nyingi umekuwa jasiri kutoka mbele na kukemea dhulma na uonevu si kwa Waislamu peke yao basi na Watanzania wengine mfano kipindi kile ulipokemea mauaji na kutekwa kwa watu.
Ndugu Sheikh Ponda, Kwa niaba ya wapenda haki nchini, nakuomba Utolee kauli suala hili tena na tena maana mpaka sasa, Hatujui Ben Saanane alipo, Hatujui Ndugu Azory alipo, Hatujui ndugu Kanguye alipo, Roma Mkatoliki alitekwa na kisha kuachiwa, Tundu Lissu alipigwa risasi, Kuna maiti zilikuwa zinakotwa kwenye Viroba ikiwemo maiti moja ya mtendaji wa chama cha Chadema iliokotwa Coco-beach.
Katika hali kama hii ndugu Sheik nategemea wewe uendelee kutupa Moral leadership katika kukemea haya masuala. Nangoja Kauli yako kwa hamu sana huenda Madhalimu wakaogopa na kuacha udhalimu wao!.
Nimalizie kwa Kauli Sahihi ya Nabii Muhammad aliyesema kwamba, Ukiona Uovu basi Uondoe kwa Mkono wako, Ukishindwa basi Ukemee na mwisho kama kukemea huwezi basi chukia tu japo kuchukia bila kuchukua hatua ni udhaifu wa Imani. NAOMBA KAULI YAKO SHEIKH JUU YA YANAYOJIRI NCHINI.
Asante mimi ni ndugu yako katika Adam
Missile of the Nation (Kombora la Taifa)