Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

HustlerOG

Senior Member
Dec 27, 2022
143
183
Ndugu, Mhe. Rais wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN

Nakusalimu kwa jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mhe. Rais, Mimi ni kijana Mtanzania (Mzalendo), umri wangu ni miaka 40, na nina Postgraduate Diploma in Accountancy.

Ninaomba kuonana na wewe Mhe. Rais, ili niweze kusikia busara zako, Utashi wako na Mwongozo wako kabla sijafanya uamuzi wa kuivunja KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria, Kanuni na Taratibu zake kwa kujitoa uhai wangu.

Nasikitika kila kukicha kuona Karama, Kipaji, kipawa na Talanta, nilivyopewa na Mungu wangu havitumiki katika kulisukuma gurudumu la Taifa. Najiona sina maana ya kuendelea kuishi hapa duniani.

Msongo wa mawazo unanitesa sana. Natamani kujinyonga au kufanya tukio kubwa nipelekwe gerezani nikafie huko, au niende hata msituni nikaliwe na wanyama wakali.

Tafadhali Mhe. Rais, ninaomba msaada wako ili niweze kutoka katika kipindi hiki cha mateso makali. Nina watoto wawili ambao sipo nao, mke alishanikimbia muda mrefu sana.

Nina amini, nikipata kitu cha kufanya chenye uhakika, hata kama ni kuosha magari ya Serikali, Kazi yeyote ile (permanent) ya kuniingizia kipato, nitapata utulivu wa akili na wa Moyo.

Natanguliza shukurani za dhati.

Wako Mtiifu na Mnyenyekevu,
 
Aise! Kama unashida hiyo si uweke wazi usaidiwe? Weka hata huko twita watu wataufikisha ujumbe. Huku utapatikanaje? Au weka hata anuani zako basi.

Pole sana.
1. Nimeweka wazi tayari.
2. Nilikua sina Account twitter, Asante kwa ushauri
 
Unaongelea kufa kufa tu hapo
Kama unahitaji kazi usitafute tu ulichosomea mzee we sio kijana tena
Piga kazi yeyote humu hatujuani ila laiti kama tunajuana na kuaminiana mbona tungesaidiana sana tu

Pole sana ila kujiuwa kwako humu hakuna anaejali ila utaumiza familia tu na hao watoto ingawa unasema hauko nao, Wanaishi na watakuwa na maisha yao pia.
 
Unaongelea kufa kufa tu hapo
Kama unahitaji kazi usitafute tu ulichosomea mzee we sio kijana tena
Piga kazi yeyote humu hatujuani ila laiti kama tunajuana na kuaminiana mbona tungesaidiana sana tu

Pole sana ila kujiuwa kwako humu hakuna anaejali ila utaumiza familia tu na hao watoto ingawa unasema hauko nao
Wanaishi na watakuwa na maisha yao pia
Issue ya vyeti nilishaiweka pembeni kitambo sana. Napiga Kazi yeyote ili mradi mkono uende kinywani.
 
True that, .alinikimbia baada ya kile nilichowekeza kwake kufanikiwa. Akaniacha na watoto baada ya kuona napitia wakati mgumu.

Watoto nikaamua kuwapeleka kwa Ndugu.
 
Kama una postgraduate na umeshindwa kuwa creative ukapata cha kufanya hata ku audit biashara zako wa std 7 asemeje sasa....
Ur Disgracing ur educational level
 
Kumbe wahasibu wenye post graduate ndo mnaakili mgando kama hizi.😂😂😂😂 Mtu unaposema kulitumikia taifa sio lazima uajiriwe serikalini ww play part yako kama mwananchi kwa kujishughulisha kujiingizia kipato sasa wasomi wote wakiakijinyonga ndio nini sasa ww sema huna connection ya ajira na mambo kama hayo habari za sjui kumuona samia kisa unataka kuitumikia nchi kwa ulichoandika anakuona tegemezi hivi unamiaka 40 bado unalia lia kwamba huwezi kuitumikia nchi yako what a fakeni mind unauelewa finyu sana na unaaibisha vyuo vinavyotoa hizo elimu za uhasibu na mambo kama hayo ni aibu sana jitu la miaka 40 kulilia kukutana na viongozi wakati unatakiwa upambanie maisha yako yaliobakia
 
Nina amini , nikipata kitu cha kufanya chenye uhakika, hata kama ni kuosha magari ya Serikali, Kazi yeyote ile ( permanent) ya kuniingizia kipato,..nitapata utulivu wa akili na wa Moyo.

Nimefika hapa nimejikuta nasikitika sana.. kuusoma huu uzi wako ulioanza vizuri na ukajimaliza kwa kujishusha kwa njia mbaya ya mwendo kasi.

Hata mimi binafsi siwezi kukuajiri.. ila serikalini lolote lawezekana.. kila la Kheri .
 
Back
Top Bottom