Angyelile99
Member
- Oct 9, 2023
- 94
- 171
BARUA YA WAZI KWA RAIS @SuluhuSamia
Mhe. Rais, ninaamini barua hii inakukuta ukiwa na uzima tele. Nina takwimu kidogo nahitaji kukushirikisha.
1. Shule ya Sekondari Chamazi hapo jijini Daresalaam yenye wanafunzi 2,800 ina mwalimu 1 tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 409 kati ya 624 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2024 kwenye hii shule walipata division four na zero.
2. Shule ya sekondari Mbande yenye wanafunzi 2,426 hapo hapo jijini ina walimu wanne (4) tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 586 kati ya 743 waliopata mtihani wa kidato cha Nne kwenye hii shule walipata division four na zero.
3. Shule ya sekondari Saku yenye wanafunzi 2,548 hapo hapo jijini ina mwalimu mmoja tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 459 kati ya 536 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2024 kwenye hii shule walipata division four na zero.
4. Shule ya sekondari Nzasa yenye wanafunzi 3,000 hapo hapo jijini ina walimu 6 tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 494 kati ya 683 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2024 walipata division four na zero.
5. Shule ya sekondari Kijichi yenye wanafunzi 2,460 hapo hapo jijini ina walimu 7 tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 334 kati ya 441 waliofanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2024 walipata division four na zero.
6. Shule ya sekondari Mbagala yenye wanafunzi 3,500 hapo hapo jijini DSM ina walimu wanne (4) tu wa somo la kiingereza.
Wanafunzi 725 kati ya 929 waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2024 walipata division four na zero.
Hali ipo hivi kwenye shule karibu zote za serikali nchini. Kwenye hii mifano michache tu, kila mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi zaidi ya 500.
Sishangazwi sana na hili kwa sababu mimi mwenyewe wakati nafundisha pale Morogoro sekondari, mikondo yangu mitatu niliyokuwa nafundisha ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 210.
Mhe. Rais @SuluhuSamia , hivi ni mwalimu gani duniani anayeweza kuleta matokeo kwa workload hii?🤔🤔🤔🤔
Hivi kweli ungeweza kukubali mwanao au hata mtoto wa ndugu yako tu asome kwenye shule zenye hali kama hii?🤔
Ajira za walimu zilizozuiliwa na serikali toka mwaka 2016 kwa lengo la kupambana na wafanyakazi hewa zimeenda wapi?🤔
Mhe., wakati Rais Magufuli anaondoka madarakani, darasa la form four lilikuwa na candidates 483,000, leo tunavyoongea hii idadi imedouble. Kama sikosei, kuanzia mwakani kila kidato cha nne kitakuwa na wahitimu karibu au zaidi ya 1,000,000.
Mwaka 2022 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ni 1,073,941; mwaka 2023 ni 1092984; na mwaka 2025 ni 974,332.
Ndani ya hii miaka tisa tu, yani kutoka 2016 - 2025, idadi ya wanafunzi shule za sekondari imeongezeka kutoka 1,500,000 mpaka 3,000,000+. Kipindi chote hiki cha ongezeko, ajira zilikuwa zimezuiliwa. Tunategemea hawa watoto wafundishwe na nani?🤔🤔
Katika kipindi hiki hiki, vyuo vyetu vikuu na elimu ya juu vimezalisha walimu zaidi ya 500,000. Ni lini serikali itafungua zile ajira ilizozizuia ili kupunguza hili tatizo?🤔
Lakini pia Mh. Rais @SuluhuSamia tujiulize kwa pamoja, hivi serikali ina mpango wowote na kesho ya hawa watoto kweli? Inayajali maisha yao kwa namna yoyote ile?🤔
Embu jaribu kufikiria tu namna hawa watoto wa watanzania maskini walivyorundikwa kwenye hizi shule, bila walimu kama hawa wa somo la kiingereza, wala vitabu vya kutosha, halafu wakati huo huo wanatakiwa kusoma kwa lugha ya kiingereza na kuandika mtihani wa Taifa kwa lugha hiyo hiyo ambayo hawaifahamu hata chembe. Tunawatakia nini kwenye maisha yao?🤔
Vyanzo vya takwimu: TAMISEMI, NECTA.
Ahsante sana!
Onesmo Mushi