Barua ya wazi kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa

Status
Not open for further replies.
CCM wameshindwa na wamekiuka miiko ya uongozi na misingi ya taifa hili, ccm ni lazima iondoke na nilazima ife, huku ndio kupona kwa Tanzania.

Na sasa hivi wamegundua siku zao zinahesabika,hivyo wanakula kadiri ya uwezo wao
wanahakikisha kila mtu anachukua chake before its too late, hakika wananchi wa sasa sio kama wale
wa miaka ile,hayo yatadhibitika uchaguzi wa 2015,hawata amini kitakachotokea hawa ccm!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Bila shaka TISS wanaweza kusaidia lakini sio kuwapa lawama kwa kila jambo baya linalotokea nchini kwa kisingizio cha vyombo husika kushindwa kutoa ufanisi

MAMA POROJO unajuwa kitu inaitwa Vetting na nani wanahusika nacho? Why defending blindly?
 
Last edited by a moderator:

Na kwa idara hii kushindwa kubaini jambo lolote linalohatarisha usalama na utangamano wa nchi ni kushindwa kazi yake ya msingi na inastahili kuvunjwa mara moja...Idara hii ipo kila mahali na wana mafungu ya kufa mtu. Cha ajabu matumizi yao hayahojiwi popote hata Utoh hatii mguu pale.

Kujua chombo kimeshindwa kazi ni lazima kuwepo na mizania ya mafanikio na kutofanikiwa kwa majukumu yake.

Ni bahati mbaya mambo ambayo TISS haijashindwa kuyatatua hatuwezi kuyajua kwa kuwa taifa halitangaziwi mafanikio ya TISS, lakini mabaya ni mepesi kuonekana kwa sababu tu jamii inayaona bayana.
 
Hili halihitaji Usalama wa Taifa ni suala la utendaji kama kuna mashaka na elimu yake na pia kama uwaziri haujatungiwa kiwango cha elimu ambacho waziri anatakiwa kuwa nacho TISS hawana ubavu wa kuchunguza elimu ya Mulugo
Uchunguzi unakuja kama alipika vyeti, Kupika vyeti ni kosa kisheria na ndio maana tunataka kujua kweli anahodhi vyeti alivyoonyesha wakati wa kuomba kura?
 
MAMA POROJO unajuwa kitu inaitwa Vetting na nani wanahusika nacho? Why defending blindly?

dadavua zaidi.

Kila taasisi inatakiwa kufanya vetting (upekuzi) nje ya upekuzi wa TISS naamni vetting ya TISS ina ngazi yake na hasa kama inahusiana moja kwa moja na Usalama wa Taifa hasa kwa viongozi lakini pia kama serikali inataka kujiridhisha kwa mtu anayetakiwa kufanyiwa vetting (upekuzi) inatumia chombo cha juu zaidi TISS.

Kwa mfano, ni makosa BOT kuajiri bila kufanya vetting yake hata ufisi binafsi haitakiwi kuajiri mtu bila vetting yake.
 
Uchunguzi unakuja kama alipika vyeti, Kupika vyeti ni kosa kisheria na ndio maana tunataka kujua kweli anahodhi vyeti alivyoonyesha wakati wa kuomba kura?

Lakini hili pia linaweza kufanywa na mahakama kwa kupitia kwa watu wenye ushahidi sio lazima TISS. kama TISS hawajafanya kazi yao kwa nini waliona ushahidi wasiende kisheria.
 
Naomba nichangie hivi>>>>>>

Hosea mwenye kapu la silaha zote za kupambana na rushwa, aling'aka kwamba sheria ya rushwa bado ni dhaifu sana kwa yeye kuitumia vyema kupambana na rushwa, kabla hata hajamaliza na kufafanua vizuri madhaifu yaliyopo kwenye sheria, alitoka mwanaseria mkuu wa serikali akasema kwamba sheria ni nzuri na inatosheleza kwa kila haja haihitaji maboresho. basi ikaishia hapo................, tukirudi nyuma kidogo, tutakumbuka kwamba sheria hii ya TAKUKURU iliundwa baada ya JK kulazimishwa na wafadhili, haikuwa yakwake akajikuta ametengeneza mswada ukapelekwa bungeni ili kuwafurahisha hao wafadhili, siyo kwa ajili ya watanzania, sasa kwa mazingira hayo tutegemee nini?

Kwa ufupi ni kwamba mwanasheria mkuu anayajua mapungufu ya sheria lakini pia anajua kuwa mapungufu hayo yapo kwa sababu gani, ndiyo maana alikuja juu kukemea kwamba sheria haina mapungufu.

"ilinikumbusha kisa cha kitoto kilichokuwa kimekaa mlangoni na kinajua kwamba baba yake ameficha bunduki mahali fulani, mgeni akaja akauliza baba yako yuko wapi? mtoto akajibu, yupo ndani amejificha lakini amesema ukija nikwambie hayupo! na akasema aliposema anaondoka aliondoka na silaha yake? yule baba kusikia hivyo alikurupuka ndani na kuuliza wewe unaulizia silaha yangu uifanyie nini??? basi kicheko hahahaha tehehee. hao ndio vongozi wa TZ karne ya 21.
 
mama porojo nimependa mchango huu ila tatizo sio kuifumua TISS bali kuhakikisha mfumo wa serikali hauingiliwi na masilahi ya chama na tatizo kubwa hapa kwetu bado watendaji wengi bado wana dhana ya chama chasika hatamu(party supremacy)

Kweli kabisa na ndipo najiuliza TISS inaweza kuwajibika vipi kwenye mfumo huu. Leo hii TAKUKURU ingekuwa inawajibika bungeni pengine mambo yangekuwa tofauti kuliko kuilaumu TISS badala ya mfumo.
 
dadavua zaidi.

Kila taasisi inatakiwa kufanya vetting (upekuzi) nje ya upekuzi wa TISS naamni vetting ya TISS ina ngazi yake na hasa kama inahusiana moja kwa moja na Usalama wa Taifa hasa kwa viongozi lakini pia kama serikali inataka kujiridhisha kwa mtu anayetakiwa kufanyiwa vetting (upekuzi) inatumia chombo cha juu zaidi TISS.

Kwa mfano, ni makosa BOT kuajiri bila kufanya vetting yake hata ufisi binafsi haitakiwi kuajiri mtu bila vetting yake.

hivi watu wanaoutaka ukuu wa nchi iwe CCM au chama kingine hawapaswi kufanyiwa hiyo vetting. maana tusijekuweka madarakani mtu kumbe ni mfuasi wa al queda.
 
Kweli kabisa na ndipo najiuliza TISS inaweza kuwajibika vipi kwenye mfumo huu. Leo hii TAKUKURU ingekuwa inawajibika bungeni pengine mambo yangekuwa tofauti kuliko kuilaumu TISS badala ya mfumo.

unajua tunapokuwa kwenye mazungumzo wananchi wengi tumekuwa tukiaminishwa kwamba TISS ikiamua kitu kisiwezekane wanaweza, sasa kwa hili ndio maana unaona tunadhani ndio msaada ulipobakia sasa na hawa kama hawawezi ni kusali tu kumebakia
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Bado naafiki wazo lako ni zuri na kama litawafikia wanaTISS itakuwa nzuri zaidi kwani hawawezi kujiondoa kabisa na mtikisiko wa nchi japo lawana hatuwezi kuwapa peke yao.
 
Pamoja na hasira tulizonazo, Ebu soma habari hii ucheke kidogo na mambo ya TZ yalivyofika mbali:

Eti kuna mtu mmoja alikufa na kwasababu alikuwa na dhambi nyingi alifika moja kwa moja Jehanamu. Kufika kule akakuta kuna Jehanamu za nchi mbalimbali ambapo mtu unachagua ipi inamfaa kutumikia adhabu. Mtu huyu aliamua kuzunguu kidogo kuchunguza ni Jehanamu ya nchi gani inaadhabu nafuu kidogo. Alifika Jehanamu ya Ujerumani akaambiwa, kwanza unalazwa kwenye kitanda cha umeme masaa 6, baada ya hapo anakuja shetani wa kijerumani anakuchapa bakora kwa muda wa masaa mawili kisha unasubiri adhamu nyingine ambazo sio nzito kama hizi za mwanzo. Jamaa akaamua kwenda Jehanamu ya Uingereza akakuta mambo ni yaleyale. Akazunguuka zaidi jehanamu ya marekani na urusi akakuta adhabu zinafanana labda tofauti ni kwenye bakora maana mashetani wengine walionekana wanamisuli na mikono ya nguvu hivyo bakora zao ziliumiza sana. Alipofika Jehanamu ya kitanzania akakuta kuna foleni ndefu sana akajiuliza haya kulikoni. Akasogea sehemu ya maulizo akauliza hadhabu za hapa zikoje mbona watu ni wengi sana hata wazungu wengine wanakimbilia huku, akaambiwa kwanza mtu analazwa kwenye kitanda cha umeme kwa muda wa masaa sita kisha anakuja shetani wa kitanzania anakucharaza bakora kwa muda wa masaa mawili. Jamaa akasema mbona adhabu ni ileile kama Jehanamu nyingine. Mtu moja aliyekuwa kwenye mstari akamvuta pembeni akamwambia. Sikia wewe usiwe mjinga, Jehanamu ya Kitanzania haina umeme wa uhakika hivyo kitanda chake mara nyingi akifanyi kazi na hata umeme ukiwepo unakuwa low voltage hivyo badala ya kupigwa shoti ya umeme unabaki unatekenywa tu ndiyo maana unasikia watu huko ndani wanacheka ujue umeme leo upo, alafu shetani wa kitanzania alikuwa mtumishi serikalini hivyo mara nyingi anakuja anasaini kitabua alafu anaondoka na kwenda kwenye shughuli zake au mara nyingi anakua amechelewa sana, hivyo hapa mambo ni poa sana watu wanapeta tu ni sawa na hakuna adhabu yoyote.
 
unajua tunapokuwa kwenye mazungumzo wananchi wengi tumekuwa tukiaminishwa kwamba TISS ikiamua kitu kisiwezekane wanaweza, sasa kwa hili ndio maana unaona tunadhani ndio msaada ulipobakia sasa na hawa kama hawawezi ni kusali tu kumebakia

vyombo vya kiserikali vimeundwa kisheria na vinawajibika kwa walioviunda, kwanza tujue kama walioviunda wanavisimamia ipasavyo na kuviwajibisha

Leo hii CIA au MOSAD wana nguvu kwa sababu ya uwajibikaji kila sekta inawajibishwa kwa mapungufu yake.
 
ndugu wembe wenge,

Huyo mwanasheria unayemzungumzia si ndio yule alisema katiba ni nzuri haina haja ya mpya ila tunaweza kuiwekea viraka. nakushauri mtu yule muogope kama ukoma maana kimatendo amejidhihirisha udhaifu wake. ni kweli sheria ya PCCB ina mapungufu maana haiwezi kumfungulia mtu mashitaka bila kibali cha mwendesha mashitakaa mkuu wa serikali hivyo yeye asipokitoa ndio kesi imekufa.
 
Lakini hili pia linaweza kufanywa na mahakama kwa kupitia kwa watu wenye ushahidi sio lazima TISS. kama TISS hawajafanya kazi yao kwa nini waliona ushahidi wasiende kisheria.
TISS ni chombo kilichoundwa kisheria kufanya vetting kabla Rais au mamlaka husika haijateua viongozi wakuu wa serikali. Kama kulifanyika kosa, wanaweza kurudia tena, na ukipatikana ushahidi, wamfungulie mashitaka kwa kughushi vyeti. If you wanna urgue any more, today you can't be my guest, duce
 
vyombo vya kiserikali vimeundwa kisheria na vinawajibika kwa walioviunda, kwanza tujue kama walioviunda wanavisimamia ipasavyo na kuviwajibisha

Leo hii CIA au MOSAD wana nguvu kwa sababu ya uwajibikaji kila sekta inawajibishwa kwa mapungufu yake.

kwa kweli katika nchi yetu linapokuja swala la usimamizi na uwajibikaji hatuna cha kujivunia na hii ndio sababu ya kushindwa saa hii ndio inanifanya nifikiri nani paka wa kumshika panya kwa hali tuliofikia?
 
Kweli kabisa na ndipo najiuliza TISS inaweza kuwajibika vipi kwenye mfumo huu. Leo hii TAKUKURU ingekuwa inawajibika bungeni pengine mambo yangekuwa tofauti kuliko kuilaumu TISS badala ya mfumo.
Rushwa kwa siku za karibuni imekuwa an economic- socio-political problem na ndio maana halitaweza kushughulikiwa na sheria kikamilifu.
Sheria haizibi mianya yote kama uadilifu wa mtu, msimamo wa kisiasa kama upo na mambo yanayoendana na hayo.

Kuyatupia matatizo ya rushwa kwa TAKUKURU na TISS, kama political will ya kuyashughulikia haipo, ni kazi bure, maana kila mtu anajua mambo yanayoendelea.

Kama tumeweza kupuuzia ufisadi wa kutisha na kuuhalalisha kwa visingizio kuwa hakuna ushahidi wa kuyashughulikia , basi leo ndo tunavuna matokeo ya kutoyashughulikia matatizo hayo.
 
hivi watu wanaoutaka ukuu wa nchi iwe CCM au chama kingine hawapaswi kufanyiwa hiyo vetting. maana tusijekuweka madarakani mtu kumbe ni mfuasi wa al queda.

wote hao wanafanyiwa vetting lakini kwa sheria za nchi yetu na mfumo wetu TISS wakibaini tatizo ni nini wanatakiwa kufanya kisheria si kimtazamo wetu. Je, wanamwambia TENDWA, Mahakama, RAIS au nani? Rais ni wa CCM je akiondolewa mgombea wa upinzani!!!!

Ama kuna mapungufu kwenye sheria zetu au mfumo wetu wa kuwajibishana. sheria mbovu zinatakiwa kuondolewa na TISS au Bunge????
 
Rushwa kwa siku za karibuni imekuwa an economic- socio-political problem na ndio maana halitaweza kushughulikiwa na sheria kikamilifu.
Sheria haizibi mianya yote kama uadilifu wa mtu, msimamo wa kisiasa kama upo na mambo yanayoendana na hayo.

Kuyatupia matatizo ya rushwa kwa TAKUKURU na TISS, kama political will ya kuyashughulikia haipo, ni kazi bure, maana kila mtu anajua mambo yanayoendelea.
Kama tumeweza kupuuzia ufisadi wa kutisha na kuuhalalisha kwa visingizio kuwa hakuna ushahidi wa kuyashughulikia , basi leo ndo tunavuna matokeo ya kutoyashughulikia matatizo hayo.

siku hizi ukimtuhumu mtu kwa kutoa rushwa wanasiasa wanarukia mara moja kwamba toa ushahidi hata kabla ya kuvipa vyombo husika vya uchunguzi. Maanake nini hapo? jibu limeshapatikana hata kabla ya uchunguzi.

Hata ukimwajibisha Rashid Othman kwa matatizo ya mfumo wetu mbadala wake atakutana na mfumo ule ule ulimwondoa mwenzake...... kwanza tufumue mfumo hata kwa gharama kubwa kwa kuanza na uwajibikaji wa kisiasa.
 
kwa kweli katika nchi yetu linapokuja swala la usimamizi na uwajibikaji hatuna cha kujivunia na hii ndio sababu ya kushindwa saa hii ndio inanifanya nifikiri nani paka wa kumshika panya kwa hali tuliofikia?

Tatizo kubwa la nchi yetu kimfumo liko kwenye sheria na siasa huko kukikaa sawa vyombo vingine vyote vitakuwa vimejipanga mstari mmoja.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom