Barua ya wazi kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JUST, Oct 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mkurugenzi mkuu usalama wa taifa,


  Utangulizi:

  Mimi kama mwananchi wa nchi yangu ya Tanzania ninayo dhamana na wajibu wa kuilinda nchi yangu na kuishauri kwa nafasi nitakayopata, kwa kuwa sina pa kusemea nashukuru JF inaweza kuwa ndio uwanja wangu wa kufikisha ujumbe. ndugu mkurugenzi kwa uwezo wangu wa kifikra kwangu usalama wa taifa ni taasisi inayohakikisha nchi inakuwa salama na pale penye hatari yeyote basi taasisi yako inakuwa ya kwanza kuliona na kulitafutia ufumbuzi kwa kuhusisha wadau wnegine.

  Tatizo:

  Ni wazi kuwa nchi yetu sasa imeharibika kimaadili kwa rushwa kutawala vichwa na maamuzi ya viongozi walio wengi na baadhi ya wananchi, mbaya zaidi dalili zinaonyesha rushwa hii imefikia hatua hatari kabisa ya kutaka kununua uongozi wa juu kabisa wa nchi. wewe kama msimamizi wa Usalama wa nchi, Je? umejiuliza ni uchungu gani alionao mtanzania kwa watanzania wenzake mpaka atumie pesa zake alizozipata kwa shida kununua madaraka kama sio hela zisizo na uchungu yaani za ufisadi?

  kuna tetesi kuwa taasisi yako inasaidia chama cha mapinduzi kuwepo madarakani lakini nimekuwa nikijiuliza kama ni kweli je kwa hali ilivyo sasa kwa chaguzi zote za CCM kutawaliwa na rushwa taasisi yako bado inaona ni chama cha kuendelea kutawala kupitia viongozi wanaupatikana kwa staili hii ya rushwa za wazi na katika kipindi hiki cha kuwapo na hazina kubwa ya gesi? kwa busara kabisa ni dhahiri nchi iko hatarini kuongozwa na wabinafsi watakao kuwa tayari kusaini mikataba ya kiunyonyaji dhidi ya uchumi wa nchi yetu.


  Ombi:

  Ndugu mkurugenzi ni matumaini yangu kuwa hautokubali nchi hii iendelee kuwa kichaka cha wabinafsi na wanyonyaji maana kama sio usawa hata wewe sio ajabu usingekuwa hapo ulipo. kwa hiyo ninakuomba usaidie nchi kwa kuhakikisha wabinafsi na watoa rushwa hawapewi nafasi ya kutawala tena.

  Hitimisho:
  Watanzania zaidi ya milioni arobaini watasaidiwa kutoka kwenye dhiki zinazowakabili ndani ya nchi tajiri duniani kwa maamuzi madhubuti na ya kizalendo kutoka kwenye taasisi yako.

  Mungu ibariki Tanzania, naomba kuwasilisha
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  By the way, Tukimwambia othman ku-deal na rushwa, je Hoseah??
  Basi tuifute PCCB
   
 3. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Maombi ya nguvu yanahitajika. Tulipofika ni pabaya sana. Mungu isaidie nchi yangu Tanzania. Viongozi watabadilikaje? Tutampata wapi mwenye uzalendo wa kweli?
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  si kweli kwamba kila jambo taasisi ya ujasusi popote duniani inakuwa ya kwanza kuona ndio maana serikali zote zina vyombo vyake vinavyowajibika kwa jambo husika.

  kuitwisha lawama zote Idara ya Usalama wa Taifa ni kutaka kupuuza uwepo wa vyombo vinavyowajibika kwa serikali iliyopo madarakani.
   
 5. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Pole sana kwani haitakiwi kuwa na elimu ya darasa la SABA kujua kwamba tasisi uliyoitaja hapo juu na zingine nyingi ni sehemu ya CCM. Kuwa mpole wala usipoteze muda wako kufikilia kuwa kuna mtu/ watu au Taasisi hizi ya KiCCM zitawaambua CCM.
  Kama wewe unao uchungu na Nchi unayo kazi moja tu kuanzia sasa, nayo ni KUFIKIRIA KUINGOA MADARAKANI CCM. Rushwa/ Ufisadi ni MFUMO , hiyo basi ni zaidi unavyofiria kwani kama Ugojwa wa UKIMWI upo potepote mwilini na zaidi virusi ujikita kwenye moyo maana ndio usambaza DAMU.
  Sasa basi RUSHWA ni kama Virusi vya Ugojwa wa UKIMWI nayo ipo kwenye Top level na hao ndio waasisi na wanao isambaza kenye CHAMA caho a JAMII kwa ujumla.
  Na kwa vile JAMII imefisadika na ina dhiki kuu kinachotokea wao utumia udhaifu huo na baadae urudi na kujikosa kwamba RUSHWA haikubaliki.
  = CCM ikitoka madarakani tunaweza kuwa na mwanzo mzuri wa kupamabana na rushwa, vinginevyo tumekwisha hasa ikatokea kwamba wameshida tena 2015 basi kwishenea WATANGANYIKA.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tuambie kwanza chombo kilichoaundwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa kimeshindwa au kimefikia wapi (TAKUKURU).
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Duh hii imekaa vizuri
   
 8. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mwana mpotevu hii sio rushwa tena hii ni hali inayohatarisha usalama wa taifa kwa sababu tukishafikia hatua ya uongozi kununuliwa hakuna haki na usawa utakaopatikana tena na ni rahisi vurugu na makosa ya jinai kuongezeka
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  si kweli kwamba kila jambo taasisi ya ujasusi popote duniani inakuwa ya kwanza kuona ndio maana serikali zote zina vyombo vyake vinavyowajibika kwa jambo husika.

  kuitwisha lawama zote Idara ya Usalama wa Taifa ni kutaka kupuuza uwepo wa vyombo vinavyowajibika kwa serikali iliyopo madarakani.
   
 10. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  ni wazi kuwa TAKUKURU ipo kisheria na kina mamlaka lakini tumeona ya kuwa wameshindwa kivitendo na kushindwa huku ndipo umuhimi wa mwuombwaji kuhakikisha sasa maslahi ya taifa yanatangulizwa na sio ya watu wachache
   
 11. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  nakubaliana na wewe maana hata nilipoanza nimesema kwa fikra zangu nimeona wanaweza kusaidia
   
 12. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  PCCB mi naona wanakula hela zetu za kodi bure kabisa,sijawahi kuwaona wana deal affective na wala rushwa wakubwa,tatizo kubwa la hii nchi yetu viongozi wanapewa madaraka specifically kukilinda chama!!
  Ukienda against huchukui round
  Mungu ibariki Tanganyika,Mungu ibariki Africa!
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tatizo letu ni la kimfumo na kukosa kuwajibika kwa vyombo husika.

  Kumbuka kila chombo kinawajibika kwa serikali iliyopo madarakani ikiwemo TISS yenyewe.

  vyombo vinavyohusika mapungufu unayosema vinawajibika vipi hata ukiifumua TISS tatizo litakuwa lilelile.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Rushwa si kosa la TISS wakati TAKUKURU ipo kwa mujibu wa sheria na chombo kinatumia kodi zetu kujiendesha.

  Kama tunataka kazi ya TAKUKURU kuwa ya TISS fungu la kupambana na rushwa kutoka hazina lipelekwe TISS na TAKUKURU ivunjwe
   
 15. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kweli Usalama wa Taifa lazima uingilie kati mambo haya ya rushwa pamoja na kumchunguza waziri Mulugo kuhusiana na elimu yake.
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Bila shaka TISS wanaweza kusaidia lakini sio kuwapa lawama kwa kila jambo baya linalotokea nchini kwa kisingizio cha vyombo husika kushindwa kutoa ufanisi
   
 17. M

  MTZmakini Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo yalivyo ndani ya ccm kwa sasa, kwa yeyote yule anayeipenda nchi hii hawezi kamwe kukubali tena chama hiki kuendelea kuongoza nchi hii. CCM ni chama ambacho kwa sasa huwezi kukitenganisha na RUSHWA, UFISADI, UBINAFI, UZEMBE na UDINI.

  Haya yote yameondoa kabisa moyo wa uzalendo kuanzia kwa Rais mwenyewe mpaka balozi wa nyumba kumi anayejidai kuitumikia ccm. Tumefikia hali hii kutokana na CCM. Kupona kwa nchi hii ni lazima CCM sio iondolewa madarakani bali ife kabisa kwa maana kimekiuka misingi yake na hali hii sio kusema itarekebishwa, hilo ndani ya CCM kwa sasa haliwezekani, kwani uozo wa CCM upo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifani, sasa hali hii utairekebishaje.

  Tunachotaka kwa sasa Tanzania ni kujenga mfumo mpya kabisa wa uongozi chini ya chama kingine, mimi sijali ni chama gani, iwe ni CUF, CHADEMA, NCCR, UDP nasema chama chochote kile kingine ambacho kwa pamoja tutajenga nchi yetu katika usawa na uwazi katika kuwahudumia wananchi. Wenzetu walioendelea wameweza kujenga nchi zao sio kwa miujiza bali ni kwa kuamua kuwajibika na yeyote anayeonesha uzembe anawajibishwa kwani anakuwa ni adui wa Taifa.

  Sasa serikali ya CCM uzembe mwingi unatokea, watu wanauwawa hakuna anayewajibishwa, katika hali hii utegemee maendeleo yatoke wapi? tena bado watu hawa wanataka waendelee kuongoza nchi. CCM wameshindwa na wamekiuka miiko ya uongozi na misingi ya taifa hili, ccm ni lazima iondoke na nilazima ife, huku ndio kupona kwa Tanzania.
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hili halihitaji Usalama wa Taifa ni suala la utendaji kama kuna mashaka na elimu yake na pia kama uwaziri haujatungiwa kiwango cha elimu ambacho waziri anatakiwa kuwa nacho TISS hawana ubavu wa kuchunguza elimu ya Mulugo
   
 19. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mama porojo nimependa mchango huu ila tatizo sio kuifumua TISS bali kuhakikisha mfumo wa serikali hauingiliwi na masilahi ya chama na tatizo kubwa hapa kwetu bado watendaji wengi bado wana dhana ya chama chasika hatamu(party supremacy)
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wengi wetu hatutaki kuelewa kuwa TISS nacho ni chombo chini ya serikali kama vyombo vingine, kwa matatizo ya kimfumo TISS itaonekana inapwaya hata kama inafanya kazi vizuri
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...