Barua ya wazi kwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Jan 10, 2016
78
62
Kabla ya yote ninatoa pongezi na pole nyingi kwa majukumu mazito ya kulijenga taifa letu uliyonayo.
Baada ya hapo mimi ninaitwa Theodory Byabatto mkazi wa Dar es Salaam. Ni mjasiliamali ninajishughulisha na biashara ya kutengeneza vitafunio mbali mbali (bakery), ambayo niliianza mwaka 2008, mwaka 2010 tuliisajili rasimi kama bakery na tukapewa vibali vyote vinavyohusiana na biashara ya usindikaji vyakula.
Biashara ilipanuka na tukalazimika kuchukua mkopo benki na tukanunua mashine kubwa na za kisasa. Pia tukaanza kujenga jengo la bakery kwa ajili ya hizo mashine. Wakati ujenzi haujakamilika mwaka 2016 mwezi April bakery yetu ilibomolewa na TAN ROADS. Ubomoaji huo ulifanywa bila kuwepo notisi wala taarifa yoyote.
Mheshimiwa Raisi Ubomoaji huo ulitusababishia hasara kubwa ya vifaa na mali zingine kwa kuibiwa na baadhi ya mashine kuvunjika kwakuwa muda tuliopewa wa kutoa vitu ni dakika tano na hatukupewa ulinzi wowote wa mali zetu zitoke salama.
Baada ya mkasa huo biashara ilisimama, kitendo hicho kilituathiri kisaikolojia. Wakati tunaanza biashara hii mimi na mke wangu hatukuwa na mtaji tulianzia kwenye mazingira magumu, tulikuwa tunapika maandazi, Half cake, karanga na crisp za viazi kwenye chumba tulichokuwa tunalala na baada ya kupika tunabeba kwenye mfuko wa Rambo tunatembeza kwenye maduka, tuliendelea hivyo mpaka tukapata pesa ya Kukodi chumba cha biashara. Hapo ndipo tukaanza kutengeneza mkate kwa kwa kutumia oven ya kupikia chakula oven ambayo ilikuwa inaoka mikate minne (4) kwa wakati mmoja. Uvumilivu jitihada na kujituma ndivyo vilitufikisha hatua ya kuwa na biashara inayoonekana mpaka benki wakashawishika kutukopesha.
Leo hii biashara imeharibiwa hatuwezi kulipa tena deni la benki na benki wanataka kuuza nyumba tunayoishi ambayo tuliiweka kama dhamana ya mkopo. Na pia taswira yetu mbele ya taasisi za kifedha imechafuka maana tunaonekana wadaiwa sugu hivyo hawako tayari kutukopesha kwa ajili ya kuifufua tena biashara yetu.
Mheshimiwa Raisi tumelazima kuandika barua hii ya wazi kwako baada ya kupeleka suala letu kwa mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa bila kupata ufumbuzi/msaada. Sifahamu taratibu rasimi za kuleta malalamiko kwenye ofisi yako. Ndio maana nikatumia njia hii na endapo nimekosea ninaomba nisamehewe nimefanya kwa nia njema.
Katika hotuba zako mheshimiwa raisi umekuwa unatusisitiza Watanzania tufanye kazi, tupo Watanzania ambao tuko tayari kufanya kazi halali na kwa kufuata taratibu za nchi. Kazi ya kusindika chakula ina taratibu zake ambazo tunatakiwa kuzifuata. Pamoja na shinikizo kubwa la madeni ya benki lililonyuma yetu sipendi kuwaumiza Watanzania wenzangu kwa kufanya kazi/ biashara hii pasipo kufuata taratibu hivyo ninakuomba serikali yako inisaidie.
Mwisho ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kukupa nguvu na afya njema ili uendelee kututumikia Watanzania.
Ni mimi mwananchi wako,
Theodory Theonest Byabatto.
0713 39 64 54.
 
Pole sana kwa mkasa uliokukuta. Mara nyingi unapopatwa na matatizo hua unafungika na kutojua au kusahau kuchua hatua muhimu na kwa wakati unaofaa. Ila bado hujakosea kumuelezea muheshimiwa rais matatizo yako inaonesha utayari wako. Pia muombe muungu akupe wepesi katika mahangaiko yako ya kimaisha kwani yeye ndio kila kitu kina tokana na yeye.
Asante.
 
umetwanga maji kwenye kinu mkuu..... serikali hii ya asaivi inamsikiliza mtu kweli..!!!!
 
ila kwa wanaoweza kumpa msaada hasa wa kimawazo ya kumtoa kwenye hili janga naombeni mjitokeze... alivyoandika naona kabisa maumivu aliyokuwa nayo... pole sana mkuu...!!!!
 
You are just one, there are thousand others drinking from the same cup. Ujenzi karibu na barabara unahitaji umakini mkubwa kujirdhisha reserve ya barabara ni ipi. Pole sana mkuu.
 
Pole sana kwa mkasa uliokukuta. Mara nyingi unapopatwa na matatizo hua unafungika na kutojua au kusahau kuchua hatua muhimu na kwa wakati unaofaa. Ila bado hujakosea kumuelezea muheshimiwa rais matatizo yako inaonesha utayari wako. Pia muombe muungu akupe wepesi katika mahangaiko yako ya kimaisha kwani yeye ndio kila kitu kina tokana na yeye.
Asante.
Asante mkuu ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom