Barua ya Wazi kwa Mh. Samweli Sitta

Barua ya Wazi kwa Mh. Samweli Sitta

Bonson

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
183
Reaction score
147
Ndugu Mheshimiwa,
Kwa muda mrefu umejijengea sifa ya kuwa kiongozi shupavu na usie na hofu kwa yale unayoyaamini. Katika kipindi chako cha Uspika Wa Bunge ulijinadi na kuthibitisha kwamba wewe ni MTU WA SPEED NA VIWANGO. Bila kuonyesha upendeleo wala woga uliwashugulikia mafisadi wanaoliibia Taifa letu. Kwa sababu tusizo zijua, uliondolewa ktk nafasi ya uspika. Hii ilikuumiza na iliwaumiza wengi.

Mheshimiwa, wakati wa sakata la ugonjwa wa ajabu wa Dr. Mwakyembe, ulitoa kauli nyingi kwamba kuna mkono wa mtu (mafisadi). Wengi walishutumu msimamo wako lakini hukujali. Hii yote ilikua inadhihirisha wewe ni MTU JASIRI Na unaeweza aminiwa kwa nafasi ya juu ya uongozi.

Mheshimiwa, Jina lako limekua likitajwa tajwa kwamba utawania URAIS wa nchi yetu. Kwangu binafsi, ni jambo zuri. Lakini nimepata hofu kubwa sana kuhusu kauli yako uliyoitoa bila hofu ukiwa kama MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA. Kauli yako ya kupinga UHURU WA HABARI NA UHURU WA KUJIELEZA umeleta mkanganyiko mkubwa kwa wananchi wengi hasa wale walokua wakikuona kama Rais ajae.

Mheshimiwa, JE, WAWEZA TOA KAULI KUHUSU ULILOLISEMA KUHUSU UHURU WA HABARI?? Je, huo ndio msimamo wako au ni "ULIMI ULITELEZA??"

Kwa mtazamo wangu, kauli hii uliyoitoa inaweza fanyika KABURI la kuzika ndoto zako zote. Tafadhali toa msimamo wako rasmi kuhusu uhuru wa habari na vyombo vya habari.

Asante kwa kua msikivu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
afadhali ametuonyesha upande wake wa pili, kumbe ni mnafiki sana
 
Mi chadema pure ila ccm jembe ni lowasa tu hawawengine wote ni toilet pepa inatumika kokote kutokana na mazingira.
 
Jamani 6 amechoka, ni mzee wa mwili na uwezo wake unazidi kupungua. Ana hasira na kutokuwa na uhakika wa kuwa raisi wa nchi hii tena...anajaribu kumwaga MBOGA. ............ To be honest, sifa zake za viwango zilikufa siku nyingi na sasa imefika wakati Mhe Anna Makinda na Mhe Job Ndugai wana uwezo wa kuongoza mbunge kama hili zaidi yake. Sitta amekosa weledi na mapenzi kwa taifa lake kwani anayofanya yaweza kuwa chanzo cha fujo hapa nchini.
 
Tatizo anazeeka vibaya sana !
 
Yanamwisho haya! Kuna siku wajumbe wa bunge maalumu la katiba watakosa imani na 6, hapo watataka mwenyekiti awe mwanamke kama bibi Kiroboto! 6 atakuwa chali na sina shaka ataanza kubwabwaja!
Unadhan atakosa sababu?atasema kuna maadui wake wa KISIASA wanamhujumu,mbona kabla ya leo watanzania wengi walimuamini mzee huyu
 
Ni huyu huyu Sitta aliyehusika na ufisadi wa CDA. Tatizo lenu watanzania wengi mnafikiri Sitta wa CDA ni tofauti na Sitta wa BMK. Same old wine in the new bottle!
 
Chezea Gamba, Samwel Six Alishaonywa Na Alipewa Huo Uspika Wa Bmlk Kwa Sharti La Kukandamiza Upinzani Na Kulibeba Chama La Gamba, Hivyo Sita Hana Meno Tena Limebaki Koti Tu Hapo, Na Urais Atausikia Tu Shame 2 U Mnyamwezi Mnafiki Sijawahi Ona Huyu Ni Balaa.
 
Sita mnafiki kama wanafiki wengine na nimbinafsi nashukuru Mungu kamuumbua mapema manake angetupa shida huyu baadae.
 
Nilishangaa siku ile kwa baadhi ya wajumbe kutaka hotuba yake ichapishwe kwenye magazeti ili wananchi wengi wafahamu. Nimejiuliza inakuwaje unashutumu vyombo vya habari kisha uvitake kuandika hotuba yako. Kama ni Uhuru,Mzalendo na Habari leo ni sawa!
 
Kwa sababu watanzania ni wanafiki huyo jamaa anaweza akawa presida wa bongo 2015
 
Chezea Gamba, Samwel Six Alishaonywa Na Alipewa Huo Uspika Wa Bmlk Kwa Sharti La Kukandamiza Upinzani Na Kulibeba Chama La Gamba, Hivyo Sita Hana Meno Tena Limebaki Koti Tu Hapo, Na Urais Atausikia Tu Shame 2 U Mnyamwezi Mnafiki Sijawahi Ona Huyu Ni Balaa.
Muoneeni huruma! Kapanick alipoona ndoto zake zinatiwa dowa na kumbe panick zake zitamtumbikiza zaidi kizani.
Ni kuwa Watanzania si wafatiliaji kwa viongozi wakiondoka madarakani , lakini huyu bwana alikwisha ​kimaadili kabisa mpaka alipopewa uspika na Kikwete.
 
Sitta amefika mwisho. Kila kitu kina mwanzo na mwisho, na Sitta kafika mwisho full stop.
 
Back
Top Bottom