Barua ya Wazi kwa Mh. Samweli Sitta

Barua ya Wazi kwa Mh. Samweli Sitta

Maskini sitta ndo amekufa hivyo sijui atakuja na lugha gani watu wamuelewe....finished...
 
Hata udiwani hapati yaani hasijisumbue kugombea nafasi yoyote mwakani.......kikaragosi huyo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Masikio yake ameziba pamba na macho yake amejipofusha, hasikii wala haoni...!
NADHANI TUNAKWANGA MAJI KWENYE KINU, SIKIO LA KUFA HILO...........................!
 
Huyu Mhs Sitta alisifiwa akajisahau mono. Hii ni sawa na Zitto Kabwe! Hawa watu wamepoteza nafasi ya pekee ambayo ingewasaidia kuandika historia zao upya! Huyu mzee sijui hicho kiti kimemfanya akalewa au sijui ni nini? Mhs Sitta kwaheri kwani ndoto zako umezizika mwenyewe.
Note. Hata Mhs Zitto ulikuwa unakimbilia wapi wakati nyote yako ilikuwa ina hitaji uvumilivu wa muda fulani ili iweze kuwaka! Basi Mkuu Zitto labda the future will tell us...
 
Ndugu Mheshimiwa,
Kwa muda mrefu umejijengea sifa ya kuwa kiongozi shupavu na usie na hofu kwa yale unayoyaamini. Katika kipindi chako cha Uspika Wa Bunge ulijinadi na kuthibitisha kwamba wewe ni MTU WA SPEED NA VIWANGO. Bila kuonyesha upendeleo wala woga uliwashugulikia mafisadi wanaoliibia Taifa letu. Kwa sababu tusizo zijua, uliondolewa ktk nafasi ya uspika. Hii ilikuumiza na iliwaumiza wengi.

Mheshimiwa, wakati wa sakata la ugonjwa wa ajabu wa Dr. Mwakyembe, ulitoa kauli nyingi kwamba kuna mkono wa mtu (mafisadi). Wengi walishutumu msimamo wako lakini hukujali. Hii yote ilikua inadhihirisha wewe ni MTU JASIRI Na unaeweza aminiwa kwa nafasi ya juu ya uongozi.

Mheshimiwa, Jina lako limekua likitajwa tajwa kwamba utawania URAIS wa nchi yetu. Kwangu binafsi, ni jambo zuri. Lakini nimepata hofu kubwa sana kuhusu kauli yako uliyoitoa bila hofu ukiwa kama MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA. Kauli yako ya kupinga UHURU WA HABARI NA UHURU WA KUJIELEZA umeleta mkanganyiko mkubwa kwa wananchi wengi hasa wale walokua wakikuona kama Rais ajae.

Mheshimiwa, JE, WAWEZA TOA KAULI KUHUSU ULILOLISEMA KUHUSU UHURU WA HABARI?? Je, huo ndio msimamo wako au ni "ULIMI ULITELEZA??"

Kwa mtazamo wangu, kauli hii uliyoitoa inaweza fanyika KABURI la kuzika ndoto zako zote. Tafadhali toa msimamo wako rasmi kuhusu uhuru wa habari na vyombo vya habari.

Asante kwa kua msikivu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Huyo Mzee Ni mnafiki na mbinafsi sana anapenda Sana kuvutia kwake wala mamboyenye maslahi kwa nchi hana mpango nayo,mungu wetu Ni mwema Sana huwa hamfichi mnafki!movie ndio kwanza imeanza many more to come...
 
Chezea Gamba, Samwel Six Alishaonywa Na Alipewa Huo Uspika Wa Bmlk Kwa Sharti La Kukandamiza Upinzani Na Kulibeba Chama La Gamba, Hivyo Sita Hana Meno Tena Limebaki Koti Tu Hapo, Na Urais Atausikia Tu Shame 2 U Mnyamwezi Mnafiki Sijawahi Ona Huyu Ni Balaa.

Heri ya joka la kibisa kuliko 6 mroho wa mkate na siagi.
 
Back
Top Bottom