Wafalme Hawakosolewi!!!!
Hakuna mfalme anayeweza kufanikiwa kutawala watu wa Mungu ikiwa yeye hana Mungu. Nikitumia Biblia kama kitabu cha rejea, watawala wengi sana wametajwa kushindwa au kuangamia kwa sababu hawakudumu katika maagizo ya Mungu.
Sauli alikuwa ni mfalme wa kwanza katika taifa la Uyahudi. Halikuwa kusudi la Mungu kuruhusu Wayahudi wawe na mfalme. Lakini Wayahudi walitaka kuwa na mfalme wafanane na mataifa mengine yenye wafalme wao.
Kabla ya wafalme, Mungu alikuwa ni mwamuzi wao. Lakini Wayahudi walitaka na wao wawe na wafalme ili wawaamulie. Mungu aliwaonya Wayahudi kwa kuwafunulia madhara ya wafalme. Haya ni baadhi ya madhara ambayo Mungu aliwaonya Wayahudi (1 Samweli 8:10-22):
Mfalme atawatwaa watoto wenu ili wamtumikie
Mfalme atawafanya watoto wenu wawe askari wa jeshi lake
Mfalme atawatwaa mabinti zenu wamtumikie.
Mfalme atatwaa mashamba yenu mazuri na mazao yake awape maakida wake
Mfalme atawatoza ushuru ili awalishe watumishi na maakida wake
Mfalme atawatoza fungu la kumi katika mapato yenu
Nanyi mtalia sana mkijuta kuwa na mfalme mliyejichagulia wenyewe.
Hata hivyo Wayahudi walimtaka mfalme licha ya madhara hayo ambayo Mungu aliwaonya hapo mwanzo. Mungu akawapa Sauli kuwa mfalme wa kwanza wa Uyahudi.
Sauli alikuwa na shida yake kubwa iliyosababisha miisho yake mibaya. Cheo kile alipewa na Mungu lakini hakuhitaji busara ya Mungu akajiinua kwa hekima yake. Uovu ukamwingia akamkosea Mungu.
Sio kusudi langu kumzungumzia mfalme Sauli. Nia yangu ni mfalme Daudi, mrithi wake. Mfalme aliyepata kumpendeza Mungu kwa kiasi kikubwa sana.
Siku moja mfalme Daudi akiwa katika kasri yake, alimwona mwanamke mzuri sana kupitia dirishani. Mwanamke yule alikuwa ni mke wa Uria, mmoja wa askari wake waliokuwa vitani. Mfalme Daudi akamtamani mke wa Uria na akagizwa alatwe kwake.
Mfalme Daudi alifanya ngono na mke wa askari wake aliyekuwa vitani akimpigania! Kitendo kile kilipelekea mke wa Uria kupata ujauzito. Mfalme akaagiza Uria arudishwe nyumbani akiamini akija atalala na mkewe hivyo ataangushiwa jumba bovu juu ya ujauzito ule.
Hata hivyo Uria aliporudi alikataa kulala na mkewe akihoji kuwa ana furaha gani ya kulala na mkewe wakati askari wenzake wako vitani! Mpango huo wa mfalme Daudi ukafeli. Uovu ukazidi kumtafuna mfalme Daudi naye akaona ni heri kumwua Uria. Basi aliamuru askari yule arudi vitani huku akimtaka jemedari wa jeshi kumweka Uria kwenye mstari wa mbele wa mapambano. Mfalme Daudi alikusudia kusikia Uria akifia vitani.
Baada ya mapambano kuendelea, kweli Uria akafia vitani. Mfalme Daudi akapumua maana alijua sasa siri yake iko salama. Lakini kwa bahati mbaya mfalme Daudi alisahau kuwa Mungu alikuwa anaona uovu wake. Machoni pa watu mfalme Daudi alikuwa ni mtu mwema sana lakini alikuwa amemkosea Mungu na mwanadamu pia.
Dhambi yake ilikuwa ni kubwa sana na alistahili kufa. Ndipo Mungu alipomtuma Nathani kupeleka ujumbe kwa mfalme Daudi. Nathani alijua nguvu za wafalme. Nathani alijua wafalme hawapendi kukosolewa. Nathani alijua siku zote wafalme huamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kutoa haki. Hivyo lilikuwa ni jambo la hatari sana kwa Nathani kumkosoa au kumwonya mfalme Daudi juu ya dhambi yake.
Nathani akaamua kumtupia mfalme Daudi kitanzi ili ajinyonge mwenyewe. Ndipo alipomsimulia kisa kilichopo katika kitabu cha Samweli wa Pili Sura ya kumi na mbili (2 Samweli 12:1ff). Nakusihi kabla ya kuendelea kusoma makala hii naomba usome sura niliyoitaja hapo juu ili ujue kile ambacho mfalme Daudi aliambiwa na Nathani mjumbe wa Mungu.
Jambo alilolifanya Nathani ndilo ambalo watumishi wa Mungu nchini wanapaswa kufanya. Wafalme wengi wanapenda sana kubarikiwa ila hawapendi kuoneshwa kuwa ni wakosaji mbele za watu wao maana watapoteza sifa ya kutawala. Ndio maana hata wakifanya makosa huwa hawataki yajulikane kwa watu wao maana kuishi kwao kunategemea watu! Mamlaka zao hazitakuwa na nguvu iwapo watapoteza imani kwa watu wao wanaowatawala.
Hivyo usitarajie kuwa unaweza kumkosoa mfalme hadharani na ukabakia salama. Huu ni utaratibu ambao uko tangu siku nyingi. Maana siku zote mfalme yuko sahihi! Kama si kwa kauli ya mfalme mwenyewe, basi maakida au watumishi wake watakushughulikia mara moja itakapobainika umejaribu kumkosoa mfalme maana kuishi kwao hutegemea hisani ya mfalme. Haya ndio Mungu aliyowaonya Wayahudi maana alijua desturi za wafalme.
Haki wanayosema wanaitoa si haki ya kweli bali ni haki yenye kuwatukuza wao zaidi. Si kweli watawaliwa wanaweza wasione uovu wa mfalme wao, lahasha! Wengi wanajua hatima yao iwapo watamkosoa mfalme hadharani.
Kwa jinsi hiyo, Mungu pekee ndiye hushughulika moja kwa moja na wafalme. Hata hivyo Mungu hawezi kuruhusu watu wake waumie kwa sababu ya uovu wa mfalme. Ipo njia itakayojitokeza katika kuwanusuru watu wake maana kilio cha wanyonge ni kelele kubwa sana mbele za Mungu.
Askofu Kakobe ulitakiwa utumie hekima ya Nathani katika kufikisha ujumbe wako kwa mfalme. Kile kinachoweza kukutokea kingeweza kumtokea pia Nathani kama angekifanya kama ulivyokifanya.
Uria yawezekana mpaka kufa kwake hakujua kwamba mfalme Daudi alizini na mke wake na kumpa ujauzito. Yawezekana Uria atastaajabu sana siku ya hukumu pale atakapo baini kuwa kufa kwake vitani haikuwa ushujaa wa kumpigania mfalme wake bali ilikuwa ni hukumu yake ili kuficha uovu wa mfalme anayemtumikia. Ni kweli wafalme hawakosolewi maana ni jambo wasilolipenda!
Ni mwenye akili pekee za kibinadamu ndiye anayeweza kunielewa! Wafalme hukosolewa kwa nguvu ya watu maana watu ndio huwapa mamlaka kwa niaba ya Mungu!