Barua ya Vitali Maembe kwa Rais Magufuli

Barua ya Vitali Maembe kwa Rais Magufuli

BAKOI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Posts
1,211
Reaction score
2,330
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu John Joseph Pombe Magufuli,
Heshima yako Mkuu!

Mimi ni mtumishi mdogo, mswahili Mtanzania kasoro Chama Cha Siasa. Kwanza nikupongeze kwa Mazuri unayoyafanya wewe na Serikali yako kwa Manufaa ya Taifa hili, pia nikuombee wepesi, umakini na marekebisho pale unapokosea kama Mwanadamu.

Ndugu,
Najaribu kukufikishia barua hii ambayo ninaamini ndiyo ya Mwisho kuja kwako kutoka kwangu na naituma nikitumaini itakufikia na utaifanyia kazi.
Na kwa wote mnaoisoma barua hii ndefu kwa Rais wangu naomba mkichangia changieni kwa kuheshimu Mamlaka zilizowekwa, bila kuongopa wala kuogopa.

Ndugu Rais,
Sisi waswahili tuna usemi usemao 'Atafutaye hachoki, akichoka keshapata' Nasimama tena leo mbele ya watanzania wako wema wengi na wabaya wachache, naandika wazi kuitafuta haki yangu, yako na ya watanzania wenzetu, naitafuta kwasababu imefichwa na baadhi ya Maafisa wa Serikali yetu, mwishowe tunadhalilishwa na Taifa linaaibika.
Ninaishi hatarini, Mimi na walio wangu, Scom

Ulinzi sina usalama na sitaki kuikimbia nchi yangu nabahatisha kuwa Salama.
Napata picha kuwa ukisimamia haki na Ukweli katika nchi hii nje ya Chama au Dini zao wewe ni kama Mnyama wa nyumbani, Nyama yako inaliwa, utachinjwa na watu watanyamaza kwa kuona kuwa kifo chako ni halali.

Najua fika katika hili la kuimba na kutumia Sanaa yangu Kuipinga waziwazi Rushwa, wizi wa Mali za Umma nipo peke yangu na jamaa zangu wanyonge wachache.

Kwa juhudi ya hila wanayifanya Polisi wako na hao wanaowatuma najua fika siku moja wataniua, lakini Dunia ijue sitakufa kama nipo usingizini, nitarusha mikono na miguu. Je, aliye karibu na kifo changu atanusurika?

Na wanyonge wa leo wataendelea kuwa wanyonge hata baada ya kuona nimeuawa kwakuwa nimesema ukweli wenye manufaa kwa Taifa lao?

Naishi nchi hii kwa kulipa gharama kubwa sana, sasa naona naelekea kuchoka
Nimefichua wizi, uzembe na rushwa na serikali imeufanyia kazi na kufanya Mabadiliko, lakini kwa kitendo hicho hicho nimetumiwa Polisi nimepigwa nusura ya kuuawa, nimenyimwa fomu namba tatu ya Polisi kwaajili ya matibabu, sasa nimeshtakiwa na Jamhuri hihi hii kanakwamba ni Makosa kuilinda Katiba ya Jamhuri kwa kutimiza wajibu wako, kuwa raia mwema kwa kusema wazi na kupinga wizi na Ubadhirifu unaoendelezwa na Watumishi wa Umma katika Jamhuri hii.

Kwanini nidhalilishwe na kunyanyaswa alafu Serikali yangu inachukulia poa?

Mheshimiwa Rais, unataka niamini kuwa Mnataka mniue au mnifunge ili iwe fundisho kwa wengine wasirudie kuipinga Rushwa na wizi na kusema ukweli kwa faida yao na nchi yao?
Naomba ulishughulikie hili Mkuu, moyo wangu umeuma na umeelemewa kwa maumivu ya Dharau na Dhurma inayoelekezwa kwangu, ni vema ikakumbukwa kuwa ukiondoa Utanzania Mimi ni Mtu pia.

Na sasa nipo hatua chache kutokea kwenya Mauti ya uvumilivu. Naomba Serikali yako itende haki kabla alijachwa Jua la Uzalendo wangu!
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Vitali Maembe 'mswahili'
 
Dah aiseee sijui niseme nini ,hivi ule upendo tuliokuwa nao Watanzania umeenda wapi ?

Yako wapi maneno mazuri kama yale ya wimbo wa mwenge


Kuwasha mwenge
Kuwasha mwenge
Nakuuweka Kilimanjaro
Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini
Pale ambapo hapana matumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau.

Tulipokosea ni wapi ee Mungu
Naomba utusamehe bure ,Ukarudishe upendo wetu Watanzania
 
JAMAA HUWA ANA MAWAZO MAZURI SANA..
Inauma sana kama ayasemayo ni kweli. apewe ulinzi kama walivyopewa akina dr.slaa na Jecha ingawa hao hata sidhan kama walitishiwa maisha. Polis waliompiga watafutwe na kujieleza.

LAKINI KWA UPANDE MWINGINE HUYU JAMAA SIJUI ANA PARANOIA, YEYE ANAHIS ATAUWAWA TU....
 
Dah aiseee sijui niseme nini ,hivi ule upendo tuliokuwa nao Watanzania umeenda wapi ?

Yako wapi maneno mazuri kama yale ya wimbo wa mwenge


Kuwasha mwenge
Kuwasha mwenge
Nakuuweka Kilimanjaro
Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini
Pale ambapo hapana matumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau.

Tulipokosea ni wapi ee Mungu
Naomba utusamehe bure ,Ukarudishe upendo wetu Watanzania
Unapomkaribisha shetani.. Malaika wanakimbia.
 
Dah aiseee sijui niseme nini ,hivi ule upendo tuliokuwa nao Watanzania umeenda wapi ?

Yako wapi maneno mazuri kama yale ya wimbo wa mwenge


Kuwasha mwenge
Kuwasha mwenge
Nakuuweka Kilimanjaro
Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini
Pale ambapo hapana matumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau.

Tulipokosea ni wapi ee Mungu
Naomba utusamehe bure ,Ukarudishe upendo wetu Watanzania
Mkuuu huu wimbo naupenda sana nikisikiaga natokwa machoz ya furaha.
 
Dah yaani hii nchi ipo siku.kuna watu wanadhani wataishi milele.time will tell
 
Sumu ya teja..sumu ya teja segerea..afande nilimwambia...wamwachie Maembe
 
Dah aiseee sijui niseme nini ,hivi ule upendo tuliokuwa nao Watanzania umeenda wapi ?

Yako wapi maneno mazuri kama yale ya wimbo wa mwenge


Kuwasha mwenge
Kuwasha mwenge
Nakuuweka Kilimanjaro
Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini
Pale ambapo hapana matumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau.

Tulipokosea ni wapi ee Mungu
Naomba utusamehe bure ,Ukarudishe upendo wetu Watanzania
Ben mashujaa wa taifa hili wameficha silaha ya ujasiri uvunguni.
Umebaki umbea wa vijiweni,
Wenye dhamana ya kupaza sauti badala yetu wamebaki kupiga pambio za kuwasifu wakubwa ilimradi tonge lipatikane,
Wamebaki kupigia makofi miswada kandamizi.
Nani atatuokoa taifa hili
 
Back
Top Bottom