Barua ya kuposa...

Barua ya kuposa...

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,956
Reaction score
3,245
Naomba msaada wenu wana Jf.

Hivi, Barua ya Posa inaandikwaje?

Lengo la barua ni kuomba uchumba na kuoa (Ndoa/Harusi).

Sasa wajameni, saidieni. Tafadhali mwenye kuweza aitupie hapa jamvini sample ili isaidie.

Asanteni.

Huwezi andika barua ya kuomba ndoa. Hii ni mipango yako baada ya posa yako kukubaliwa pamoja na taratibu za kutoa mahari kama zipo kutimia.

Barua ya posa inaandikwa kama barua za kawaida za maombi, yaani yaweza kuwa na anwani yako na ile ya wakwe zako ingawa haina madhara kama ukiandika anwani yako tu. kuhusu maudhui huwa haina mambo mengi.
mfano

S.L.P.
678
KAKUNDI
12.3.2013.​
FAMILIA YA (TAJA JINA LA FAMILIA YA MTARAJIWA WAKO)
S.L.P.................
(MAHALI WALIPO)

WAPENDWA WAZAZI,

YAH: KUMPOSA BINTI YENU ................................

KICHWA CHA BARUA HAPO JUU CHA HUSIKA, MIMI (TAJA MAJINA YAKO ) WA (TAJA NYUMBANI KWAKO, (ila kama uko mahali tofauti na nyumbani kwako ni bora kusema wapi uliko kwa wakati huu na ukibainisha nyumbani kwako hasa.)

Ninayoheshima kubwa kuomba kumposa Binti yenu (..j...................).kwa shilingi Taja kiwango na pesa hiyo huwekwa ndani kwenye barua hiyo. Kiwango hutegemea na mila na desturi za mahali.

Wakishaipokea posa yako wanaweza kukupangia mahali siku hiyohiyo au wakakupangia siku nyingine kutegemea na nafasi yako, baada ya hapo unaweza kuendelea na mipango yako ya harusi.



bila shaka wanaJF wengine wataongezea yao pia.kila la heri ndugu.
 
Naomba msaada wenu wana Jf.

Hivi, Barua ya Posa inaandikwaje?
~Inaandikwa na Mshenga au mzazi kwa familia ya binti unaetaka 'kumuoa'

Lengo la barua ni kuomba uchumba na kuoa (Ndoa/Harusi).
~Lengo ni kuomba Ndoa.
Sasa wajameni, saidieni. Tafadhali mwenye kuweza aitupie hapa jamvini sample ili isaidie.
~Sina sample ila maelezo yanatosha wewe kufikiria, inategemea na makabila kila kabila liko na utaratibu wake e.g vitu vinavyoambatanishwa na barua.
Asanteni
~Karibu sana.
 
Huwezi andika barua ya kuomba ndoa. Hii ni mipango yako baada ya posa yako kukubaliwa pamoja na taratibu za kutoa mahari kama zipo kutimia.

Barua ya posa inaandikwa kama barua za kawaida za maombi, yaani yaweza kuwa na anwani yako na ile ya wakwe zako ingawa haina madhara kama ukiandika anwani yako tu. kuhusu maudhui huwa haina mambo mengi.
mfano

S.L.P.
678
KAKUNDI
12.3.2013.​
FAMILIA YA (TAJA JINA LA FAMILIA YA MTARAJIWA WAKO)
S.L.P.................
(MAHALI WALIPO)

WAPENDWA WAZAZI,

YAH: KUMPOSA BINTI YENU ................................

KICHWA CHA BARUA HAPO JUU CHA HUSIKA, MIMI (TAJA MAJINA YAKO ) WA (TAJA NYUMBANI KWAKO, (ila kama uko mahali tofauti na nyumbani kwako ni bora kusema wapi uliko kwa wakati huu na ukibainisha nyumbani kwako hasa.)

Ninayoheshima kubwa kuomba kumposa Binti yenu (..j...................).kwa shilingi Taja kiwango na pesa hiyo huwekwa ndani kwenye barua hiyo. Kiwango hutegemea na mila na desturi za mahali.

Wakishaipokea posa yako wanaweza kukupangia mahali siku hiyohiyo au wakakupangia siku nyingine kutegemea na nafasi yako, baada ya hapo unaweza kuendelea na mipango yako ya harusi.



bila shaka wanaJF wengine wataongezea yao pia.kila la heri ndugu.
 
Hauna bibi au baau yako. Kama walishatangulia, panda gari au treni uende kijijini kwenu ukaulize. Sidhani kama kuna mzee Jf wa kukusaidia. Wengi wa jf ni wa kukutana jf na kuachana jf. Kama yupo mzee jf aje asaidie jahazi.
 
Asanteni sana wana JF hasa Ndugu Don Mangi na Ndugu Makinya. Mungu awabariki. Sasa nimepata mwanga na nimeweza.

Makabila mengine hawaandiki barua, wanatuma washenga ama wazee. Na kuuliza si ujinga maana kabila letu hawaandiki barua, ila hilo kabila kunatakiwa barua
 
Pia katika hiyo barua usisahau kuweka japo elf 20 na pia bahasha ifungwe na kitambaa cheupe nakumbuka hizi process lakini kama walivyosema wengine inategemea makabila na makabila.
 
Asanteni sana wana JF hasa Ndugu Don Mangi na Ndugu Makinya. Mungu awabariki. Sasa nimepata mwanga na nimeweza.

Makabila mengine hawaandiki barua, wanatuma washenga ama wazee. Na kuuliza si ujinga maana kabila letu hawaandiki barua, ila hilo kabila kunatakiwa barua

Karibu sana.
 
Naomba msaada wenu wana Jf.

Hivi, Barua ya Posa inaandikwaje?

Lengo la barua ni kuomba uchumba na kuoa (Ndoa/Harusi).

Sasa wajameni, saidieni. Tafadhali mwenye kuweza aitupie hapa jamvini sample ili isaidie.

Asanteni


Na kipindi watu walikuwa hawajui kusoma na kuandika walifanyaje?
Mambo ya kuandika barua ya posa yanaanza kupitwa na wakati.

Unapoandika barua ya posa husiwe peke yako uwe na mashahidi wawili, unao waamini sana na sana, mkuu wa dini yako au wazazi wako,au kaka yako au mjomba wako.

Shahidi hasiwe jerani yako wala hasiwe rafiki yako, hasiwe mfanya kazi mwenzio.

Na mashahidi hao unawataja ktk barua (BW.JUMA SEMBE SLP 231 Magomeni Mapipa, Dar es salaam, na BW.VITA MATESO SLP 456 Kinondoni, Dar es salam, ni mashahidi wangu. Na inabidi wapige sign pia ktk hiyo barua.
Mara nyingi barua ya posa inaandikwa na kiongozi wa dini, padri na shehe, wao ndio kazi yao kusaidia watu kama nyie, sababu wanafaham utaratibu.

Ukiandika bila utaratibu, pengine husijibiwe, wakwe zako wataona hauna nidhamu.
 
Back
Top Bottom