Barua ya haraka kwa Tundu Lissu

Barua ya haraka kwa Tundu Lissu

Hakuna mtu mwepesi kama Tundu Lisu kwanza bora hata hao akina Mdee, huyo Tundu sema CCM tu hawana shida naye wala hawamuhitaji lkn ni mwepesi kama unyoya, akiahidiwa kacheo tu kesho hautamsikia tena.

Wakati ufike muache kuwekeza kwa binadamu msiowajua, ...
Aiseee. Watu wanahongwa vyeo kwa gharama ya walipa kodi kwa maslahi ya kundi flani. Interesting! Hii ndiyo Tanzania, nyingine ni photocopy!
 
Saalam ndugu yangu Lissu,

Mimi Mtanzania niliyekuwa na imani na vyam vya upinzani na viongozi wa juu leo hii nimevunjika moyo sana.

Nimetambua kuwa kumbe viongozi wengi wa upinzani ni njaa tupu na siyo viongozi wa kuwakomboa Watanzania na mkoloni wa ndani.

Hivyo basi, mimi ninaimani na wewe tu kuwa utalikomboa taifa hili na hili shatani kubwa CCM.

Ili mbegu iote lazima itangulie kufa, ni wewe ndiye uliyemwagwa damu kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii, maana hakuna ukombozi pasipo kumwaga damu.

Kwa uchungu uleule uliokupata miaka 3 kitandani nakuomba uwashawishi hao wazungu waje watukomboe maana huku hatuna upinzani wala viongozi wenye uchungu kwa mateso tunayopata watanzania.

Leo hii ninaamini mioyo ya wapenda mabadiriko,wapenda haki na maendeleo ya watu mioyo yao inalia na inavuja damu.

Kitendo cha hawa wamama wa BAWACHA kujipeka bungeni kimeua imani zetu.

NAKUOMBA UBAKI HUKOHUKO UWAOMBE HAO WAZUNGU WATUKOMBOLEE TAIFA LETU
Asante
Imwaga damu wapi?alikuwa ameshika Silaha ipi?ukombozi kutoka mkoloni yupi?
 
Back
Top Bottom