Barua hii iliandikwa kwa Mkapa mara tu baada ya jina la Kikwete kupitishwa kuwa mgombea wa CCM. Kwa mfano, angalia haya yafuatayo;
Mwenyekiti hakuwa tayari kuwasaidia wajumbe wenzake kupewa ushahidi wa vitendo vya kukiuka au kuvunja maadili ya chama ingawa kamati ya maadili ya CCM, na vyombo vya dola, vilikuwa vimeandaa taarifa kamili. Kwa hiyo, vikao vya chama havikufanya maamuzi yaliyozingatia ukweli wote uliojitokeza. Hata pale baadhi ya viongozi walipodai kupewa ushahidi, Mwenyekiti hakutaka kufanya hivyo, eti ushahidi ulikuwa ni aina ya majungu.
Maneno haya yalilenga tuhuma za utumiaji mkubwa wa fedha katika kampeni ya kuteuliwa kuwa mgombea uraisi ambazo zilikuwa zimekusanywa dhidi ya JK, TISS wakiwa walihusika kukusanya taarifa hizo. Ikiwa Mkapa angetoa huo ushahidi JK angekuwa disqualified wabaki Salim na Mwandosya kama wagombea.
Zanzibar walikuwa wametoa tuhuma dhidi ya Salim, kwamba alihusika sijui na kumuua Karume nk. Pia inasemekana Mkapa somehow alikuwa anamwogopa Mwandosya, kwamba asingemhifadhi katika madhambi yake. Mkapa aliambiwa Mwandosya huwa haogopi mtu, akiwa raisi kama Mkapa alifanya rushwa Mwandosya angekubali Mkapa ashitakiwe kama walivyofanyiwa kina Chiluba kule Zambia. Licha ya JK kutishia kugombea na chama cha upinzani kama CCM wasingempitisha, inasemekana JK na Mkapa walifikia muafaka kwamba Mkapa ampitishe JK kwa udi na uvumba, na JK angemhifadhi Mkapa dhidi ya tuhuma zozote atakapokuwa raisi wa nchi. Kilichofuata ni Mkapa kuamua bila aibu kumpigia debe JK ali wajumbe wampitishe.
Mkapa alikataa kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya JK, akidai kila kiongozi ana madhambi yake na hakuna kiongozi safi (CCM?). Baada ya JK kuchaguliwa kuwa raisi kitu cha kwanza ilikuwa ni kumwondoa mkurugenzi wa TISS aliyehusika moja kwa moja na kukusanywa kwa ushahidi dhidi ya JK.
The rest ni historia.