Barua ndefu kutoka Baghdad

Barua ndefu kutoka Baghdad

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI

mwanadishi kutoka nchini Tanzania, Erick Justo akiwa amechaguliwa kuwa mwandishi bora wa habari kwa Bara la Afrika mwaka huo. Ukiachana na furaha za Watanzania hao, hata yeye mwenyewe alifurahia kwa kuona kwamba ndoto ambayo alijiwekea toka kipindi cha nyuma, kwa wakati huo ilikuwa imetimia.
Uso wake ulikuwa na furaha, moyo wake ulikuwa umefanana na furaha ambayo alikuwa nayo wakati huo. Kila alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, Erick hakuificha furaha yake.
Watu ambao walikuwa wamekusanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl uliokuwepo Ubungo Jijini Dar es Salaam ndani ya Jengo la Ubungo Plaza bado walikuwa wakimpongeza mwandishi Erick ambaye alichukua tuzo hiyo iliyokuwa ikitetewa na Boniface Youssour, mwandishi wa habari kutoka nchini Ivory Coast.
Kila alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari, ni watu watatu tu ndio ambao walikuwa wakisikika akiwazungumzia, wa kwanza alikuwa mama yake, Bi Magreth ambaye alifariki kwa ajali ya gari miama minne iliyopita, baba yake, mzee Justo ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kwa bahati mbaya na wa tatu alikuwa mkewe mpendwa, Christina ambaye alikuwa mjauzito.
Machozi ya furaha yalikuwa yakimtoka, ushindi ambao alikuwa ameupata ulionekana kuwa mkubwa katika maisha yake. Waandishi wa habari wa Shirika la Habari la CNN ambao ndiyo walikuwa wameitoa zawadi hiyo wakaamua kuandaa kipindi maalumu cha kufanya na Erick, kipindi ambacho waliamini kingemfanya kuonekana duniani kote.
“Siamini mke wangu... siamini mpenzi...” Erick alimwambia mkewe mara baada ya kufika nyumbani.
“Amini mume wangu. Wewe ndiye mwandishi bora katika mwaka huu” Christina alimwambia mumewe kipenzi, Erick.
Siku ziliendelea kukatika, Watanzania waliendelea kujivunia kwa kumpata mwandishi aliyeonekana kuwa bora katika kipindi hicho. Watu wengine wakaanza kufuatilia makala mbalimbali ambazo alikuwa akiziandika Erick katika magazeti ya sehemu alipokuwa akifanyia kazi.
Kila mtu aliyezisoma makala zake alipigwa na mshangao. Hawakuweza kuamini kama kulikuwa na mwandishi ambaye alikuwa akiandika mambo mengi mazuri na ya kuvutia kama ilivyokuwa kwa Erick.
Baada ya siku tatu kupita Erick akatumiwa tiketi na viza kwa ajili ya kusafiri kuelekea nchini Marekani. Huko alihitajika kwa ajili ya kufanya mahojiano na mtangazaji maarufu duniani, Larry King wa Kituo cha CNN. Erick hakukuamini kama alitarajiwa kusafiri kuelekea nchini Marekani ndani ya siku chache zijazo.
Kila kitu kilichokuwa kikitokea katika maisha yake kwa wakati huo kilikonekana kuwa kama ndoto ambapo baada ya muda fulani angeshtuka kutoka usingizini na kujikuta kitandani akiwa na mkewe. Kila wakati macho yake yalikuwa yakiangalia saa yake, dakika zilionekana kwenda taratibu sana tofauti na siku nyingine.
Alitamani muda uende harakaharaka ili asafiri na kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano juu ya ushindi wake huo. Kila siku alikuwa akipokea pongezi mbalimbali kutoka kwa watu tofautitofauti huku wakiendelea kumtakia mafanikio katika maisha yake.
Baada ya siku tatu kumalizika Erick akaanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake bado kilionekana kuwa kama ndoto, hakuamini kama siku moja ingetokea kwake na kusafiri kuelekea nchini Marekani, nchi ambayo alikuwa akiisikia tu au kuiona katika televisheni.
Ndani ya ndege hakulala, kila wakati alionekana kuwa na mawazo tu. Aliifikiria sana nchi ya Marekani, kuanzia uzuri na hadi maendeleo yaliyokuwa yakipatikana nchini humo. Hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa akielekea katika jengo kubwa la habari la kimataifa la CNN lililokuwa katika jiji la Atalanta.
Kwake, ilionekana kama ndoto. Jina la Larry King mara kwa mara lilikuwa likisomeka kichwani mwake. Hakuamini kama alikuwa akielekea kuhojiwa na mwandishi huyo ambaye alikuwa akiwahoji masupastaa wengi duniani.
Ingawa mara kwa mara alikuwa macho lakini akajikuta akianza kulala mara baada ya ndege kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri. Ndege iliendelea na safari huku Erick akiwa amepitiwa na usingizi mzito.
Alikuja kuamka saa mbili asubuhi mara baada ya ndege kuingia katika Uwanja wa Amstadam nchini Uholanzi ambako walitakiwa kubadilisha ndege ili kuendelea na safari ya kuelekea nchini Marekani.
Erick akateremka kutoka katika ndege na kuanza kupiga hatua kuelekea katika vyumba vya kupumzikia. Baridi kali ambalo lilikuwa likipatikana katika nchi mbalimbali za Ulaya lilionekana kumpa tabu. Kila wakati alikuwa akitetemeka tu japokuwa alikuwa amevaa koti zito.
Aliyapitisha macho yake katika majengo mbalimbali marefu na yaliyokuwa yakivutia, hakuamini kama majengo yale yalikuwa yakipatikana katika dunia moja iliyokuwa ikipatikana nchi ya Tanzania.
Hali ya hewa ikaonekana kubadilika mara baada ya kuingia ndani ya jengo la uwanja wa ndege. Hali ya joto ikaanza kupatikana, hiyo ilitokana na viyoyozi ambavyo vilikuwa vinaendelea kutumika ndani ya jengo hilo.
“Do I know you? (Hivi nakufahamu?)” Erick alishtushwa na sauti ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa amekaa katika kiti cha pembeni ndani ya jego lile.
Erick akageuza macho yake na kuanza kumwangalia mwanaume yule, alimwangalia kwa makini huku akijaribu kuvuta kumbukumbu kama alikuwa amekwishawahi kumuona sehemu fulani lakini jibu lilikuwa hapana.
“I don’t know. I mean, I don’t know you (Sifahamu. Namaanisha sikufahamu)” alijibu Erick.
“Are you a famous? Maybe a musician, footballer or someone else (Wewe ni maarufu? labda mwanamuziki, mchezaji mpira au mtu mwingine?)” Mwanaume yule aliendelea kumuuliza Erick.
“No. I’m just a journalist (Hapana. Mimi ni mwandishi wa habari)” alijibu Erick.
“Are you Erick Justo? The Best Journalist of Africa this year? ( Wewe ni Erick Justo? Mwandishi bora wa Afrika?)” Mwanaume yule aliendelea kuuliza.
“Yes,” alijibu Erick.
“I’m Brian Michael, a jouranalist from BBC (Mimi ni Brian Michael, mwandishi wa habari kutoka BBC)” Mwanaume yule alijitambulisha.
Huo ndio ukawa mwanzo wa mazoea baina ya Erick na Brian. Wakaanza kuongea pamoja mpaka kufikia kipindi kuonekana kama walikuwa wamekutana siku nyingi zilizopita.
Mara baada ya kupumzika kwa muda wa dakika thelathini, abiria wote wakatakiwa kuelekea katika ndege yao kwa ajili ya kuendelea na safari ya kuelekea nchini Marekani.
Brian na Erick wakakaa katika viti vya pamoja huku wakiongea mambo mengi kuhusiana na uandishi pamoja na maisha kwa ujumla. Mazoea yao yakaongezeka zaidi, mpaka inafikia muda wa kulala, walionekana kuwa kama watu waliofahamiana kwa miaka mingi iliyopit *****
Hakukuwa na mtu ambaye alijua kwamba walikuwa wamefika nchini Marekani mpaka pale sauti ya kike ilipoanza kusikika wakitakiwa kufunga mikanda yao. Ndege ikaanza kutua huku saa ya ukutani ndani ya ndege hiyo ikinyesha kuwa saa tisa usiku.
Mara baada ya ndege kusimama, abiria wote wakaanza kuteremka. Erick alibaki akiangalia majengo makubwa yaliyokuwa yakivutia ambayo yalikuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atlanta. Baridi lilikuwa kali nchini Marekani tofauti na Uholanzi au Tanzania alipotoka.
Abiria wote wakaanza kutembea na kuelekea nje ya jengo la uwanja ule. Kila kitu kilichokuwa kikionekana mbele yake kilikuwa kigeni. Erick alijisikia kumuuliza Brian mambo mengi kuhusu nchi hiyo, alisita kufanya hivyo kwani alijua fika kwamba Brian hakuwa mwenyeji sana nchini Marekani.
‘ERICK JUSTO’ Bango moja lililoshikwa na kijana mmoja lilisomeka vizuri machoni mwake.
Erick akaanza kupiga hatua kumfuata kijana yule na mara baada ya salamu wote wawili wakaanza kuelekea nje ya jengo lile na kupanda ndani ya gari moja dogo na safari ya kuelekea hotelini kuanza.
Jiji lilionekana kupendeza mno, majengo mengi makubwa na marefu yalikuwa yakionekana machoni mwake. Kila alipokuwa akiangalia mandhari ya jiji lile na alipokuwa akifananisha na mandhari ya jiji la Dar es Salaam, aliona kulikuwa na sababu nyingi zilizowafanya vijana wengi kuzamia nchini humo.
Gari likasimama nje ya hoteli moja kubwa iliyoitwa Jupiter Hill. Mhudumu ambaye alikuwa akihusika katika hoteli ile, akalisogelea gari lile na kumfungulia Erick mlango. Akaanza kuelekea moja kwa moja mpaka mapokezi.
Kila kitu kilionekana kuwa tayari, akapelekwa katika chumba ambacho alitakiwa kukaa. Wala haukuchukua muda mrefu, chakula kikaletwa, alipokula akaelekea bafuni kuoga.

Huu ni mwanzo tu.
Je unajua nini kiliendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 2
WHATSAPP: 0758860093

“Unafikiri ni kitu gani kimekufanya kuwa mwandishi bora barani Afrika?” Lilikuwa swali lililosikika vyema masikioni mwa Erick.
Erick alibaki kimya kwa muda, alimwangalia Larry King, mtangazaji maarufu wa kituo cha habari cha CNN. Majibu mengi yakaanza kumiminika kichwani mwa Erick, hakujua atoe jibu gani kwani kila jibu ambalo alikuwa akilifikiria lilikuwa likistahili kutolewa.
“Uandishi wangu. Mambo mengi ambayo ninayaandika katika makala zangu. Nafikiri na hata upangaji wangu ambao nauona kuwa tofauti na waandishi wengine” alijibu Erick.
Larry King akatingisha kichwa chake juu na chini hali iliyoonyesha kwamba alikubaliana na jibu ambalo alilitoa Erick.
Mahojiano yaliendelea zaidi na zaidi, Erick aliendelea kutoa majibu mengi na yaliyokuwa yakimvutia kila aliyekuwa akikiangalia kipindi kile kupitia televisheni ile. Erick alizidi kuonekana bora na kuzidi kukubalika kwa kila aliyekuwa akimsikiliza.
Mara baada ya kipindi hicho kumalizika, moja kwa moja Erick akachukuliwa na kuanza kupitishwa katika sehemu mbalimbali ndani jengo la kituo hicho cha habari. Kila wakati Erick alikuwa akionekana kuwa na furaha, hakuamini kama angepata nafasi maishani mwake ya kutembelea kituo hicho cha habari.
“Nimefurahi sana, ninajiona kutokumini kama leo hii niko ndani ya jengo hili kubwa la habari la CNN” Erick alimwambia mkurugenzi wa kituo hicho, Bwana Swan Godlove.
Muda wa kula ulipofika, Erick akaitwa ndani ya chumba maalumu kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Ingawa chakula alicholetewa kilionekana kuwa kigeni lakini kilikuwa ni chakula kitamu ambacho hakuwahi kula hata siku moja.
Erick hakutamani kurudi nchini Tanzania, siku tatu ambazo tayari alikuwa ameishi nchini Marekani zilionekana kubadilisha maisha yake na hata afya yake.
“Utasafiri na kuelekea nchini Iraq” Mkurugenzi wa habari wa kituo hicho cha CNN, Bwana Swan alimwambia Erick.
“Umesemaje?” Erick aliuliza kwa mshtuko.
“Utasafiri na kuelekea nchini Iraq, huko utakwenda kuandika mambo mengi ambayo yanaendelea nchini humo, yaani katika hili namaanisha utakuwa mwakilishi wetu nchini humo kwa muda wa wiki tatu” Bwana Swan alimwambia.
Furaha yote iliyokuwepo ndani ya moyo mwake ikatoweka, jina Iraq likaonekana kumtisha kupita kawaida. Kwa haraka sana kichwa chake kikaanza kurudisha matukio kadhaa ambayo yalikuwa yametokea nchini Iraq.
Alivikumbuka vita ambavyo vilikuwa vikiendelea nchini humo, alimkumbuka hata mwandishi wa habari wa Kijapan ambaye alichinjwa mbele ya kamera na picha ile kuwekwa katika mitandao mingi ya Internet duniani.
Kila alipokuwa akifikiria zaidi, Erick aliendelea kukosa amani kabisa. Mwisho wa maisha yake ukaonekana kukaribia. Safari ya kwenda nchini Iraq ikaonekana kuwa mwisho wa kila kitu maishani mwake.
Hiyo ilimaanisha kuwa ndio ulikuwa mwisho wa kuvuta hewa ya dunia hii, hiyo ilimaanisha kuwa ndio mwisho wa kumuona mke wake mpendwa, Christina ambaye alikuwa mjauzito kwa wakati huo.
Hakuamini kama angeweza kunusurika kutoka nchini Iraq salama. Safari hiyo ilimfanya kujiona kuishi kama mfu ambaye alikuwa akitembea. Tumaini la kuendelea kuishi likapotea moyoni mwake, alijiona kuwa tayari alikwishakufa.
Hotelini hakulala vizuri, mambo mbalimbali ambayo alikuwa akiyaangalia katika televisheni, mambo ambayo yalikuwa yakitokea nchini Iraq bado yalikuwa yakiendelea kumtisha. Aliyakumbuka vizuri majambia ambayo Waarabu walikuwa wakiyashika, katika kipindi hicho, alikumbuka kila kitu.
“Usiogope Erick. Nitakuwa nawe bega kwa bega” Bria alimwambia Erick alipomtembelea hotelini.
“Utakuwa nami bega kwa bega? Kivipi?” Erick aliuliza.
“Namini nitakwenda huko Iraq pamoja nawe. Kuna vitu vingi sana ningependa kujifunza kutoka kwako” Brian aimwambia.
“Inamaanisha tutakwenda wote?”
“Utanikuta huko, ila tutakuwa wote na kufanya kazi pamoja” Brian alimwambia Erick.
Siku iliyofuata, safari ya kurudi Tanzania ikaanza. Kila mara alikuwa akiifikiria safari hiyo ya kuelekea nchini Iraq. Amani ikaonekana kutoweka moyoni mwake. Mwisho wa kila kitu ukaonekana kutimia.
Erick alifika nchini Tazania baada ya masaa thelathini na saba. Akaanza kuteremka ngazi pamoja na abiria wengine mpaka ndani ya jengo la uwanja ule. Baadhi ya wafanyakazi wenzake walikuwa wamekuja kumpokea wakiwa na mkewe.
Uso wake haukuonekana kuwa na furaha, muda wote alikuwa akiifikiria safari ya kuelekea nchini Iraq, nchi ambayo aliiona kujaa damu. Akakumbatiana na mkewe, kwa mbali machozi yalikuwa yakianza kumlenga.
“Usiogope mume wangu. Amini Mungu yuko pamoja nawe” Christina alimwambia Erck.
“Naamini hilo”
Erick alikaa nchini Tanzania kwa takribani wiki moja na ndipo safari yake ya kuelekea nchini Iraq ikaanza. Ndani ya ndege, Erick hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, kila wakati alikuwa na mawazo kupita kawaida.
Hakujua kama angeweza kurudi salama nchini Tanzania, hakuamini kama angeweza kurudi na kumkuta mkewe akiwa amekwishajifungua. Alitamani kumuona mkewe kwa mara nyingine lakini uhakika wa kumuona tena haukuwa moyoni mwake.
“Naomba unilinde Mungu, naomba unirudishe salama nyumbani. Naomba mkono wako unitangulie. Amin” Erick alijikuta akisali huku ndege ikianza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Saddam uliokuwa katika jiji a Baghdad.
Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege wakaanza kuteremka, Erick akaanza kuyapitisha macho yake katika baadhi ya maghorofa yaliyokuwa yamejengwa katika jiji hilo ambalo alikuwa akilisikia tu katika vyombo mbalimbali vya habari, Baghdad.
Majengo hayakuwa yakivutia sana kama yale ambayo aliyaona nchini Marekani, Uingereza, Uholanzi na nchi nyingine za Ulaya. Idadi kubwa ya watu ilikuwa ikionekana vizuri machoni mwake huku idadi hiyo wengi wao wakiwa wamevaa kanzu na vilemba vichwani.
Erick akaanza kuelekea nje ya jengo la uwanja huo, kijana mmoja ambaye alishika bango lililoandikwa jina lake lilikuwa likionekana vizuri machoni mwake. Kwa hatua fupifupi zilizojaa haraka, Erick akaanza kumsogelea kijana yule ambaye akampeleka moja kwa moja mpaka katika teksi iliyokuwa nje.
“Welcome to Baghdad City” Kijana yule ambaye alikuwa akindesha gari alimkaribisha kwa kutmia kingereza kilichojaa lafudhi ya kiarabu.
“Thank you” Erick aliitikia huku macho yake yakiangalia nje.
Gari lilikuwa likitembea kwa mwendo wa taratibu sana, idadi kubwa ya watu wengi ambao walikuwa wakiandamana mitaani huku wakiwa na mabango ndio ambao walisababisha foleni kubwa ya magari. Erick alibaki akiwaangalia waandamanaji wale pamoja na kuyasoma baadhi ya mabango ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya Kingereza.
Hadi kufikia hatua hiyo tayari Erick akaonekana kuanza kuogopa. Waandamanaji ambao walikuwa wameshika mabango ya kumkataa rais wa nchi hiyo bado walikuwa wakiendelea kuandamana huku mikononi wakiwa wameshika picha za rais huyo.
Ingawa mabomu ya machozi yalikuwa yakipigwa lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeonekana kuogopa na kurudisha mguu wake nyuma, wote walikuwa wakisonga mbele kuwasogelea mapolisi ambao walionekana kuwa na hasira muda wote.
Sala za Erick za kumuomba Mungu zikaanza tena. Alitamani waandamaji wale wasogee pembeni kwa ajili ya kulipisha gari lao lipite. Walichukua dakika kumi mpaka kuwapita waandamaji wale na baada ya kipindi kichache wakafika nje ya hoteli moja iliyoitwa Majifallus.
“This is the hotel I was told to take you to (Hii ndiyo hoteli niliyoambiwa nikulete)” Kijana yule alimwambia Erck.
Erick akaufungua mlango na kushuka garini na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo la hoteli ile. Moja kwa moja akaanza kupiga hatua kuelekea sehemu ya mapokezi. Kila kitu alikikuta kikiwa kimewekwa tayari kwa ajili yake.
“Thank you” Erick alimwabia dada wa pale mapokezi huku akiupokea ufunguo.
Erick akaanza kupiga hatua kuzifuata ngazi za kuelekea katika ghorofa za juu. Wasiwasi bado ulikuwa ukiendelea kutawala moyoni mwa Erick, fujo ambazo alikuwa akizisoma katika magazeti hasa za maandamano tayari zilikuwa zimekwishaonekana.
Huku Erick akiendelea kupandisha ngazi, akashtukia akishikwa bega kwa nyuma. Akageuka na macho yake kugongana na macho ya mtu ambaye wala hakuwa mgeni machoni mwake. Kwa haraka haraka akavuta kumbukumbu juu ya mtu yule kama alikwishawahi kumuona kabla.
“Erick....” Mwanaume yule aliita.
“Brian..”
Wote, huku wakionekana kuwa na furaha wakaanza kuelekea katika ghorofa ya juu. Maswali mfululizo yalikuwa yakimjia Erick, hakuwa akifahamu sababu ambayo ilimleta Brian nchini Iraq, kila alipotaka kumuuliza, alisita kufanya hivyo.
“Nilikuona tangu uwanja wa ndege, kila nilipojaribu kukuita, haukugeuka” Brian alimwambia Erick.
“Ulijua kama nilikuwa naingia hapa leo hii?”
“Ndio. Nilipewa taarifa na mkurugenzi wa CNN, Bwana Swan” Brian alijibu.
“Umekuja kufanya nini huku?”
“Kufanya kazi pamoja nawe. Natamani kujifunza mambo mengi kutoka kwako” Brian alijibu.
“Na vipi kuhusu kazini kwako? Hauoni kama utatumia muda mrefu kuwa huku?”
“Hilo si tatizo. Nimeomba ruhusa. Waliniruhusu kwa sababu tu nilikuwa nakuja kufanya kazi na mmoja wa waandishi aliyetumwa na shirika la CNN” Brian alijibu.
Ukaribu wao ukaonekana kuanza kurudi kwa mara ya pili. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye walikuwa wamemzoea nchini Iraq zaidi ya kuzoeana wenyewe kwa wenyewe. Ukaribu wao ukazidi kuongezeka kila siku, wakawa wakitoka pamoja na kwenda kufanya kazi pamoja mitaani, waliandika kila kitu ambacho walikiona kufaa kuandikwa katika vitabu vyao vidogo.
“Nimefurahi kukutana nanyi. Mimi ni Mchungaji Joseph Terence wa kanisa la Salvation jijini New York. Huyu ni mke wangu, anaitwa Mary” Mwanaume mmoja alevalia suti alijitambulisha mbele yao.
“Bwana Asifiwe” Mary alisalimia.
“Amen” Wote wakajikuta wakiitikia.
“Tumekuja hapa kwa kazi moja tu, tumekuja kufungua kanisa hapa Baghdad. Nafikiri kazi hii tutaifanya kesho pamoja na mke wangu” Mchungaji Joseph aliwaambia.
***
Uongozi wa rais Yassin Idrisour ulikuwa ukiwakasirisha wananchi wote wa Iraq. Vita ambavyo vilikuwa vimetokea katika miaka kadhaa ya nyuma dhidi ya Wamarekani na Waingereza bado viliwaacha katika maumivu makali, maumivu ambayo hayakuwa na dalili yoyote ya kupona.
Kila raia wa Iraq alikuwa akiwachukia Wamarekani na Waingereza kuliko mtu yeyote duniani, walitamani mataifa ya Marekani na Marekani yapotee ili nchi hizo zisiweze kuonekana katika uso wa dunia hii. Wanajeshi mbalimbali wa Kimarekani na Uingereza ambao walikuwa nchini Iraq kwa ajili ya kulinda amani walikuwa wakiuawa kila siku.
Mauaji ya siri siri dhidi ya Wamarekani na Waingereza bado yalikuwa yakiendelea kila siku. Waandishi wa habari na watalii kutoka katika nchi hizo walikuwa wakikamatwa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alijua mahali ambako watu hao walipokuwa wakipelekwa, wapelelezi wa Kimarekani wa F.B.I na wale wa Uingereza walijitahidi kupeleleza lakini hawakuwa na jibu lolote katika upelelezi wao.
Nchi ya Iraq ikaonekana kuwa chungu. Japokuwa mauaji yalikuwa yakishamiri nchini Iraq lakini Wamarekani na Waingereza hawakukoma kabisa kuingia ndani ya nchi hiyo iliyoonekana kujaa damu.
Rais Yassin alionekana kuwa kama kibaraka wa nchi hizo, kila siku alikuwa akiwatetea. Alipokuwa akiongea na vyombo mbalimbali vya habari nchini Iraq, alizidi kuutetea uwepo wa Wamarekani nchi humo, uwepo ambao aliutetea kwamba ulikuwa ni wa kuhakikisha amani nchini humo.
Kila siku Wananchi wa Iraq walikuwa wakiandamana kutaka rais huyo atoke madarakani, hawakumtaka rais ambaye alionekana kuwa karibu na Wamarekani ambao walikuwa wamewapa vidonda visivyokuwa na uhakika wa kupona mioyoni mwao.
Waliwapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao wa karibu katika vita ambavyo vilikuwa vya kumtafuta gaidi ambaye alikuwa ameitikisa dunia katika kipindi hicho, Allabdullah Massoud. Uwepo wa Mmarekani ukaonekana kuwa ghadhabu katika maisha ya kila mwananchi wa Kimarekani.
Ingawa Wamarekani wakishirikiana na Waingereza walijitahidi kuijenga nchi hiyo lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na upendo na Wamarekani hao. Chuki dhidi ya Wamarekani ilikuwa ikiongezeka kila siku, mtoto alipokuwa akikua, alijikuta akiwachukia Wamarekani pasipo sababu yoyote ile.
Watu walipigwa na mabomu ya machozi mitaani huku wengine wakipigwa na risasi za moto lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kupiga hatua kurudi nyuma katika maandamano ambayo walikuwa wakiyafanya kila siku.
Walionekana kuwa radhi kupoteza maisha yao katika maandamano hayo lakini ili mradi Wamarekani hao waondoke nchini humo. Mabango yaliyokuwa yakimtaka rais wa nchi hiyo atoke madarakani bado yalikuwa yakionekana katika kila makundi ya maandamano nchini Iraq.
“Ni lazima tuwaue Wamarekani wote waliokuwa wamepanga katika hoteli nchini hapa” Baadhi ya Waarabu ambao mara kwa mara walikuwa wakionekana kuwachukia Wamarekani walisema.
Msako wa Wamarekani ukaanza kufanyika kimyakimya. Hawakutaka taarifa hizi zijulikane na mtu yeyote ambaye alikuwa nje ya kundi hilo lililopewa kazi ya kuwamaliza Wamarekani. Wamarekani ambao walikuwa katika hoteli katika miji mingine walitekwa.
Kazi ya kuwateka Wamarekani waliokuwa wakiishi katika hoteli zilizokuwa ndani ya jiji la Baghdad ikaanza mara moja. Waarabu wakaanza kuingia katika kila hoteli na kuanza kuwatafuta Wamarekani. Wamarekani wengi walikamatwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana.
Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Iraq kilifanyika kimyakimya. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifahamu juu ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo. Kila siku Wamarekani walikuwa wakitekwa na kupelekwa katika sehemu zisizojlikana kabisa.
“Hoteli zote tumemaliza mkuu. Tumewapata Wamarekani mia nane” Bhazir alimwambia kiongozi wao, Ashraf
“Mmekwenda katika kila hoteli?” Ashraf aliuliza.
“Ndio Mkuu”
“Na hapa Baghdad, mmemaliza hoteli zote?”
Bhazir hakutoa jibu lolote lile, alikaa kimya kwa muda huku akionekana kufikiria kitu. Baada ya sekunde kadhaa, akauinua uso wake na kumwangalia kiongozi wake.
“Kuna hoteli moja hatukuingia” Bhazir alijibu.
“Hoteli gani?”
“Majifallus Hotel”
“Kwa nini?”
“Kuna ulinzi mkubwa mkuu”
“Hata kama kuna ulinzi, hakikisheni mnakwenda na kuwateka Wamarekani wote. Kama mkiona mnashindwa, tumieni bunduki” Kiongozi yule alisema.
Kwa haraka sana pasipo hata kupoteza muda wowote ule, Bhazir akatoka ndani ya chumba kile na moja kwa moja kuanza kupiga hatua kuelekea nje. Akawachukua vijana kumi waliokuwa na bunduki mikononi mwao na kuanza kelekea katika hoteli ya Majifallus.
“Kama kuna yeyote atakataa, tumuueni huko huko hotelini. Mmenielewa?”
“Ndio” Vijana wale waliitikia huku wakiwa wamebakisha hatua themanini kuingia ndani ya eneo la hoteli ile aliyopanga Erick, Brian, mchungaji Joshua na mkewe.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 3
WHATSAPP: 0758860093

Kelele zilianza kusikika kutoka katika vyumba vya jirani. Erick akakurupuka kutoka kitandani kama mtu ambaye alikuwa ameota ndoto mbaya na ya kutisha. Akainuka na moja kwa moja kuwasha taa na kisha kuangalia saa kubwa ya ukutani.
Saa ilimuonyeshea kuwa ilikuwa saa tatu usiku. Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani mwake kuhusiana na kelele zile alizokuwa amezisikia. Erick akapuuzia kwa kudhani kuwa kelele zile zilitoka nje ya hoteli ile, akazima taa na kuanza kupiga hatua kuelekea kitandani.
Hata kabla hajafika kitandani, kelele zile zikaanza kusikika tena. Erick akasimama kwa muda, tayari alionekana kuhisi hali ya hatari ikiwa imeanza kutokea ndani ya hoteli hiyo. Akapiga hatua kuufuata mlango wa chumba kile na kuufungua.
Erick hakuamini macho yake, Wamarekani wengi ambao walikuwa ndani ya hoteli ile walianza kuvutwa na kupelekwa nje na watu ambao walikuwa wameshika bunduki mikononi mwao. Erick akaanza kutetemeka, hali ile ikaonekana kumuogopesha kupita kiasi.
Jina la kwanza ambalo lilimjia kichwani kwa wakati huo lilikuwa Brian, Mmarekani ambaye alikuwa rafiki yake. Hakuelewa kama katika kipindi hicho Brian alikuwa salama au na yeye alikuwa amekwishachukuliwa na Waarabu wale ambao walionekana kuwa na hasira.
Erick akaupiga moyo konde, akaufungua mlango kwa mara nyingine na kuanza kupiga hatua kuelekea katika chumba alichokuwa akikaa Brian. Mlango ulikuwa umevunjwa, Erick akapiga hatua na kuingia ndani.
Kila kitu kilikuwa shaghalabaghala. Akaanza kuliita jina la Brian, aliliita zaidi na zaidi lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeitikia. Wasiwasi zaidi ukazidi kumkamata Erick, tayari akili yake ikamwambia kuwa Brian alikuwa amechukuliwa na Waarabu wale walioingia katika hoteli ile katika kipindi kichache kilichopita.
“Erick... Erick...” Erick alisikia akiitwa nyuma ya kabati.
Kwa haraka sana Erick akaanza kupiga hatua kuelekea kule ambako alisikia akiitwa. Brian alikuwa amejificha huku uso wake ukionekana kuwa na hofu tele.
“Vipi?” Erick aliuliza.
“Tuondoke. Kuna kitu nimekijua, ila nitataka kukijua zaidi” Brian alimwambia Erick.
“Kitu gani?” Erick alimuuliza Brian.
“Kitu kimoja ambacho kila Mmarekani na Muingereza anahitaji kukifahamu” Brian alimwambia Erick
Erick hakuongea kitu chochote kile, alibaki kimya akimwangalia Brian. Hali ilionekana kutokuwa na usalama wowote mahali hapo lakini baada ya kuona hali imekuwa shwari, wakatoka nje. Michirizi ya damu ilionekana ukutani, hawakuelewa kama michirizi ile ilisababishwa kwa mtu yeyote kupigwa na risasi au kipigo.
Hawakutaka kupoteza muda kujiuliza maswali ambayo wala hayakuwa na majibu yoyote, wakaendelea kupiga hatua kuelekea nje ya hoteli ile kwa kuanza kushusha ngazi. Erick alibaki akimshangaa Brian. Hakuelewa sababu iliyomfanya Brian kufanya kitendo kama kile ambacho kilikuwa ni hatari kwake.
“Mbona tunakwenda chini? Haujui kama kuna hatari huko, hasa kwako” Erick alimuuliza Brian ambaye alionekana kutokusikia.
Wakashuka chini hadi katika ghorofa ya kwanza. Mlinzi alikuwa amefungwa kamba huku watu wengine waliokuwa katika hoteli ile wakiwa wamelala kifudifudi. Erick na Brian walizidi kutembea kuelekea nje.
Wakaanza kuangalia katika kila upande, magari mawili yaliyokuwa yamebeba Wamarekani na Waingereza kadhaa yalikuwa yameanza kuondoka kuelekea katika Mji wa Al Aziziyah uliokuwa upande wa kusini mwa nchi ya Iraq. Kwa harakaharaka Brian na Erick wakaanza kuifuata teksi moja ya kukodi iliyokuwa mahali hapo na kuingia ndani.
“Mnakwenda wapi?” Dereva wa ile teksi aliwauliza.
“Yafuate magari yale” Brian alimwambia.
“Yale mawili yaliyowabeba Wamarekani?”
“Ndiyo”
“Hapana. Siwezi kufanya hivyo. Hii ni hatari kubwa sana. Nikifanya hivyo halafu wakagundua, nitauawa” Dereva yule aliwaambia huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikiongea.
Brian akakaa kimya kwa muda, alimwangalia Erick katika ishara ya kutaka kufahamu ni kitu gani walichotakiwa kufanya kwa wakati huo ili kumshawishi dereva yule afanye kama kile walichotaka akifanye.
Neno fedha ndilo ambalo lilimjia Brian kichwani. Kwa harakaharaka akaifungua pochi yake na kutoa noti mbili za dola mia moja na kumgawia dereva yule. Dereva hakuyaamini macho yake, aliziangalia fedha zile mara mbilimbili, kiasi kile kilionekana kuwa kikubwa ambacho ungeonekana kichaa kama ungekikataa.
“Ulisema magari yale mawili?” Dereva aliuliza huku akiwasha gari.
“Ndiyo. Fanya haraka kabla hayajatuacha sana” Brian alimwambia dereva ambaye akaanza kuliondoa gari lile na kuyafuata magari yale mawili.
Magari yale yaliendelea kuelekea katika upande Kusini Mashariki ambapo kulikuwa na Mji wa Wasit. Mwendo wa magari yale ulikuwa ni wa kasi kupita kawaida, barabara haikuwa ya lami, ilikuwa ni barabara ya vumbi ambayo haikuonekana kuwa na uimara mkubwa sana. Alichokitaka Brian mahali hapo ni kuendelea kuyafuata magari yale huku taa za gari lile lao zikiwa zimezimwa kwani hawakutaka watu wale wajue kama walikuwa wakiwafuatilia.
Safari iliendelea kwa zaidi ya saa moja na ndipo magari yale yakaanza kuingia katika Mji wa Wasit, mji ambao ulikuwa maarufu kwa ajili ya uchimbaji wa mafuta nchini humo. Hali ya hewa katika kipindi hicho ilikuwa ni joto kali sana ambalo lilionekana kuwa zaidi ya lile ambalo lilikuwa likipatikana ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Magari yale yakaanza kuingia katika barabara moja ambayo nayo ilikuwa ni ya vumbi na kisha kuendelea na safari kana kwamba walikuwa wakitaka kuelekea katika Mji wa Thawra, mji ambao ulikuwa maarufu sana kwa upatikanaji wa ngamia.
Baada ya mwendo fulani, magari yale yakaanza kuingia katika eneo la nyumba fulani ambayo ilionekana kuukuu. Brian na Erick hawakutaka kuendelea mbele, walichomwambia dereva ni kuwashusha na kisha kujua mambo yake.
“Kuna hoteli hapa?” Brian alimuuliza dereva.
“Mbali sana kutoka mahali hapa. Mtahitaji mwendo wa dakika kumi kwa miguu” Dereva yule aliwajibu.
“Hakuna shida. Unaweza kwenda” Brian alimwambia dereva yule ambaye aliondoka mahali pale.
Waliendelea kusimama mahali pale kwa muda fulani huku wakiangalia katika kila kona mahali pale. Sehemu ile ilikuwa imetawaliwa na giza huku mwanga ukionekana kwa mbali kutoka katika lile jumba kubwa na bovu ambalo magari yale mawaili yalikuwa yameingizwa ndani.
Hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya kwa wakati huo, hawakujua kama walitakiwa kwenda moja kwa moja ndani ya jumba lile au walitakiwa kubaki kule nje. Bado swali lilikuwa likiendelea kuwa kichwani mwa Erick, hakujua sababu ambayo iliwapelekea kuyafuatilia magari yale ambayo yalikuwa yamewabeba wazungu wale.
Walisimama kwa muda mahali pale mpaka pale ambapo Brian akashauri kitu kimoja cha hatari kifanyike mahali pale, kuelekea ndani ya jumba lile. Ushauri ule ulionekana kuwa wa hatari sana ambao haukutakiwa kushauri mahali pale, wangeweza vipi kwenda kule na wakati katika kipindi hicho Waarabu walionekana kuwa na hasira kubwa na wazungu? Katika kila swali ambalo Erick alikuwa akijiuliza mahali pale alikosa jibu.
Brian hakuonekana kuogopa hata kidogo, dhamira yake kwa wakati huo ilikuwa ni kuingia ndani ya lile jumba na kisha kujionea kile ambacho kiikuwa kikiendelea ndani ya jumba lile. Kwa wakati huo alitaka kufahamu kitu kimoja tu kwamba Wamarekani na Waingereza walikuwa wakipelekwa kule ndani kufanya nini. Kadri ambavyo Erick alishauri kutokwenda ndani ya jumba lile, Brian alionekana kupinga sana, alichokuwa akikitaka yeye ni kwenda ndani ya jumba lile.
“Haiwezekani kwenda hivi! Tunaweza kukamatwa” Erick alimwambia Brian.
“Unaogopa nini sasa? Wewe ni mwandishi wa habari. Nakuhakikishia kwamba kama tutafanikiwa katika kujua kila kitu kinachofanyika ndani ya jumba lile, tutapata fedha nyingi sana” Brian alimwambia Erick.
“Na kama tukikamatwa hauoni kama litakuwa tatizo ambalo litaweza kusababisha kuuawa?” Erick alimuuliza Brian.
“Kufa kwa sababu ya kupata kitu fulani si tatizo. Haiwezekani kuwa na tatizo kabisa kama utakufa huku ukijaribu kufanya kitu fulani” Brian alimwambia Erick.
Bado malumbano yalikuwa yakiendelea mahali hapo. Kitu alichokuwa akikitaka Brian ni kwenda kuingia ndani ya jumba lile lakini kwa Erick kila kitu kilionekana kuwa tofauti sana. Hakutaka kabisa kuingia ndani ya jumba lile kwani alijua kwa vyovyote vile wangeweza kuonekana na mwisho wa siku kukamatwa na kuuawa.
Bado waliendelea na malumbano mpaka pale Erick aliposhauri kwamba ilikuwa ni lazima kwenda katika nyumba yoyote mahali hapo na kutafuta kanzu pamoja na vilemba kwa ajili ya kuvaa ili wasiweze kugundulika mara moja mara watakapoamua kuingia ndani ya jumba lile. Ushauri huo ukapitishwa na pande zote mbili, wakaanza kuondoka kuelekea katika nyumba ambazo zilikuwa zikionekana kwa mbali sana kutokana na taa ambazo zilikuwa zimewashwa ndani ya nyumba hizo.
Walipozifikia wakaanza kuzunguka huku na kule na hatimae kuyaona baadhi ya mavazi ambayo yalikuwa yameanikwa kwenye kamba nje ya nyumba moja. Walichokifanya ni kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata mpaka pale ambapo walipoifikia kamba ile na kisha kuchukua nguo ambazo walikuwa wakizihitaji na kuondoka mahali hapo.
Walipofika umbali fulani wakazivaa kanzu zile na kisha kuanza kulifuata jumba lile huku kwa mbali zikisikika sauti za Wamarekani wakipiga kelele huku wakitukana ovyo. Katika kipindi hicho wakajivika ujasiri, moja kwa moja wakaanza kupiga hatua kulifuata jumba lile ambalo baada ya kuufikia mlango wa kuingia ndani, wakaanza kuingia.
*****
Wote wakaanza kuingia ndani ya jumba lile huku kwa mavazi ambayo walikuwa wameyavaa yakiwafanya kuonekana kuwa kama waarabu ambao walikuwa wakiingia ndani ya jumba hilo. Hakukuwa na mwanga mkubwa ndani ya jumba hilo japokuwa kulikuwa na taa ambazo hazikuwa zikitoa mwanga mkubwa.
Wakaanza kuangalia huku na kule, idadi ya waarabu haikuwa kubwa sana ingawa kila mwarabu ambaye alikuwa mahali hapo alionekana kuwa na jambia pamoja na magobore makubwa huku kanzu zao pamoja na vilemba vikiwa mwilini mwao.
Brian na Erick wakaanza kupiga hatua kuelekea juu ya ghorofa la jumba hilo kwa kutumia ngazi ambazo zilionekana kuchoka sana. Mwendo wao ulikuwa ni wa kawaida sana lakini Erick alikuwa akionekana kuwa na hofu kupita kawaida. Kelele zile za wala wazungu bado zilikuwa zikiendelea kusikika ndani ya jumba lile.
Vyumba vingi vilikuwa vikionekana ndani ya jumba lile hali ambayo ikawa ngumu sana kujua vile vyumba ambavyo vilikuwa vikisikika kelele zile. Hawakusimama, wakaendelea kusonga mbele zaidi na zaidi mpaka walipofika katika mlango ambao ulikuwa ni wa mwisho ndani ya jumba hilo. Walichokifanya ni kuufungua mlango huo na kisha kuingia ndani.
Picha ambayo walikutana nayo ndani ya jumba lile ikaoneonekana kuwaogopesha kupita kawaida. Wazungu wote ambao walikuwa ndani ya chumba kile kikubwa walikuwa wamevuliwa nguo huku wakichapwa mijeredi hali ambayo ilionekana kuwa kama adhabu ya wao kuingia ndani ya nchi ile ambayo haikuwa na mapenzi na Wamarekani wala Waingereza.
Kelele zile ndizo ambazo zilikuwa zikisikika kwa sauti ya juu sana katika usiku huo. Erick akazidi kutetemeka zaidi, picha ile ikamtia hofu kupita kawaida. Mwili wake ukaanza kutokwa na jasho jembamba hali ambayo ilimfanya kutamani kutoka ndani ya chumba kile.
“Let get out of here (Tuondoke mahali hapa)” Erick alimwambia Brian.
“Let’s wait (Tungoje kwanza)” Brian alimwambia Erick.
Bado walikuwa wakiendelea kuangalia kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali pale. Waarabu wale walionekana kuwa na hasira kupita kawaida. Bado walikuwa wakiendelea kuwachapa huku wakiongea maneno mengi yaliyojaa kejeli.
“Lets save them (Tuwaokoe)” Erick alishauri huku akionekana kuumia juu ya kile ambacho kilikuwa kikitokea.
“No! We have no guns (Hapana. Hatuna bunduki)” Brian alimwambia Erick.
Hawakutaka kuendelea kusimama mahali pale, walichokifanya ni kuanza kutembea tembea ndani ya jumba lile. Waarabu hawakuonekana kuwatambua kabisa, kwanza ilitokana na mwanga hafifu ambao ulikuwepo mahali pale lakini kubwa zaidi ilitokana na kanzu pamoja na vilemba ambavyo walikuwa wamevivaa huku asilimia kubwa ya uso wao ukiwa umezibwa.
Walipokaa ndani ya chumba kile kwa muda fulani, hapo hapo wakatoka na kisha kuanza kuelekea katika chumba kingine. Huko hali ilionekana kuwa kama ile iliyokuwa kule. Wamarekani wengi pamoja na Waingereza walikuwa wametekwa na kuwekwa ndani ya chumba hicho. Haikujalisha kama ulikuwa mwanaume au mwanamke, wote walikuwa watupu kabisa.
Mijeredi bado ilikuwa ikiendelea mahali hapo huku picha kubwa ya gaidi la kimataifa ambalo lilikuwa likitafutwa sana na Wamarekani, Yousouf ikiwa mbele kabisa ya kila chumba ndani ya jumba lile. Vyumba vile vilionekana kuwa vyumba vilivyojaa maumivu makali, wazungu wengi walikuwa wakiuawa ndani ya vyumba vile.
Vyakula havikuwa vikiletwa ndani ya vyumba vile na kama vilikuwa vikiletwa basi vilikuwa vidogo sana tena huku vikiwa haviwatoshi kabisa. Lengo kubwa la kuwateka watu hao lilikuwa ni moja tu, kuwaua kwa maumivu makali, yaani mtu kufa huku akijiona kwamba alikuwa anakufa.
Lengo la waarabu lile lilikuwa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, wazungu wengi walikuwa wakifa kila siku jambo ambalo lilionekana kumtsha kila mtu. Hakukuwa na taarifa yoyte ile ambayo ilikuwa ikijulikana hasa juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya jumba lile. Kila kilichokuwa kikiendelea ndani ya jumba lile kilionekana kuwa siri kubwa.
Wamarekani na Waingereza hawakutaka kukata tamaa, mara kwa mara walikuwa wakiwatuma wapelelezi wao kuelekea katika nchi ya Iraq hasa katika jiji lile la Baghdad kwa ajili ya kuangakile na kujua kile ambacho kilikuwa kikitokea lakini mwisho wa siku hata wapelelezi wale walikuwa wakikamatwa na kuuawa jambo ambalo liliwafanya kutokujua ni mahali gani Wamarekani na Waingereza walipokuwa wakipelekwa.
Brian na Erick hawakutaka kuendelea kukaa ndani ya chumba kile, kitu ambacho walikuwa wamekipanga mahali hapo ni kuodoka na kuelekea mjini ambapo huko wangefanya mawasiliano na jeshi la Marekani na kisha kuwaambia kile ambacho kilikuwa kimeendelea nchini Marekani.
Erick akaonekana kushangaa, alijua fika kwamba kama taarifa ile wangeitoa katika jeshi la nchini Marekani basi nao wasingeweza kukaa ndani ya nchi ile jambo ambalo lingewafanya kuondoka na kuelekea Marekani huku akiwa hajaifanya hata ile kazi ambayo aliambiwa kuifanya nchini Iraq.
“We don’t have to tell them (Haitupasi kuwaambia)” Erick alimwambia Brian ambaye alionekana kushtuka.
“Why? (Kwa nini?)”
“We are Journalist, right? (Sisi ni waandishi wa habari, sawa?)” Erick aliuliza.
“Right (Sawa)
“We have to proceed with our works that brought us in here (Inatupasa tuendelee na kazi yetu ambayo ilituleta mahali hapa)” Erick alimwambia Brian.
“Which work? (Kazi gani?)” Brian aliuliza.
“To write down what we suppose to write (Kuandika kila kitu tunachotakiwa kukiandika)” Erick alijibu.
“This is the one. Trust me Erick, you are here because they want you to give them feedback about what the hell is going on in here. Journalists were taken to Iraq but they did not succeed. We have to see what is going on here, then we are going back to home (Hiki ndicho chenyewe. Niamini Erick, upo hapa kwa sababu wanataka uwaambie kile kinachoendelea mahali hapa. Waandishi wengi wa habari waliletwa Iraq lakini hawakufanikiwa. Tukiona kile kinachoendelea mahali hapa, kwa hiyo ni lazima turudi nyumbani)” Brian alimwambia Erick.
“They? Who are they?” (Wao? Wao wakina nani?)
“Americans” (Wamarekani)
Hakukuwa na sababu ya kuendelea kuongea mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuondoka huku wakionekana kutembea kwa mwendo wa kasi. Lengo lao kwa wakati huo lilikuwa ni kufika mjini ambapo hapo wangeelekea hotelini na kisha kupiga simu nchini Marekani na kuwaambia kile ambacho kilikuwa kinaendelea.
Wakashuka ngazi kwa haraka sana na kisha kuzidi kutembea kwa kasi kupita kawaida. Kitendo kile cha kutembea kwa haraka na ndicho ambacho kikawafanya hata waarabu wengine kuanza kuwatilia mashaka. Huku wakiwa wameufikia mlango wa kutokea nje ya jumba lile, wakaamriwa kusimama lakini hakufanya kile ambacho waliambiwa kukifanya, wakaanza kukimbia jambo ambalo likawafanya waarabu kuanza kuwamiminia risasi ambazo ziliishia kugonga ukutani.
Milio ile ya risasi ndio ambayo ilionekana kuwashtua waarabu wengine na kutoka hapo nje. Hakukuwa na kitu cha kusubiri, walichokifanya ni kuzishika bunduki zao vizuri na kisha kuanza kuwafukuza huku wakiendelea kuwamiminia risasi mfululizo.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 4
WHATSAPP: 0758860093

Erick na Brian walikuwa wakikimbia kwa mwendo wa kasi kuelekea wasipoafahamu, milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika masikioni mwao hali ambayo iliifanya kuongeza kasi zaidi na zaidi. Erick alikuwa akikimbia huku akiogopa kupita kiasi, risasi ambazo zilikuwa zikipiga ardhini zilikuwa zikimfanya kuona kwamba mwisho wake ulikuwa ukikaribia.
Walikuwa wakikimbia kwa umbali mrefu huku kukiwa hakuna hata nyumba iliyoonekana, hali ya jangwa iliyokuwepo katika eneo lile iliwapa tabu kupita kawaida. Walikimbia kwa muda wa dakika kumi na ndipo wakafanikiwa kuiona nyumba moja ambapo wakaifuata na kuingia ndani.
Ngamia waliokuwa wamefungwa nje ya nyumba ile wakaanza kupiga kelele mpaka wale Waarabu wale walipofika na kugundua kwamba watu wao waliokuwa wakiwakimbiza walikuwa wameingia ndani ya nyumba ile. Wakaufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ile na kuanza kuwatafuta.
Walizunguka katika eneo la nyumba nzima huku wakiwatafuta watu hao. Japokuwa wenyeji walikuwa wameamka na kuanza kuwashangaa lakini hakukuwa na mtu aliywaongelesha, walipoona kwamba wamewakosa, wakawageukia wenyeji wale.
“Wapo wapi?” Mwanaume mmoja aliuliza kwa sauti iliyojaa ukali.
“Wakina nani?”
“Wale tuliokuwa tukiwakimbiza” Mwanaume yule alijibu.
“Mmmh! Mbona hatujaona mtu humu.”
“Unasemaje?”
“Hatujaona mtu humu. Watakuwa wamepita katika mlango ule pale wa kwenda nje upande wa pili” Mwanaume yule alisema hali iliyowafanya Waarabu wale kuufungua mlango ule.
Macho yao akatua katika ukuta uliokuwa nyuma ya nyumba ile, walipouangalia vizuri ukuta ule, wakaona mikwaruzo ambayo moja kwa moja wakajua kwamba watu waliokuwa wamewafukuza walikuwa wamepanda ukuta na kutokea upande wa pili.
Hawakutaka kuendelea kubaki mahali pale, walichokifanya ni kuanza kuupanda ukuta ule na kutokea upande wa pili. Wakaanza kuangalia katika kila kona lakini hawakuweza kumuona mtu yeyote yule zaidi ya alama za viatu zilizoonyesha kwamba walikuwa wamekimbilia upande wa mashariki.
Wakaanza kuzifuata zile alama za viatu kule kulipoelekea, japokuwa walikuwa wamejitahidi sana kuwatafuta lakini hawakuweza kuwapata jambo liliowachanganya sana.
“Ni lazima tuwapate” Mwarabu mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi aliwaambia wenzake na kisha kutawanyika.
Tayari akili yao kwa wakati huo ilikwishajua kwamba ni lazima watu wale waliokuwa wameona kila kilichoendelea ndani ya jumba lile wangeweza kwenda kutoa siri kwa Wamarekani ambao wangekuja mahali pale na kuwakomboa Wazungu wengine waliokuwa ndani ya jengo lile.
*****
Erick na Brian walitokea upande wa pili wa nyumba ile na kukutana na ukuta, walichokifanya, tena huku wakiwa katika kasi ya ajabu wakauparamia ukuta ule, wakarukia upande wa pili na kuendelea kukimbia mbele zaidi. Hawakutaka kukamatwa na kutiwa mikononi mwa Waarabu wale walioonekana kuwa na hasira mno.
Walizidi kukimbia zaidi mpaka kuzifikia nyumba zaidi ya ishirini zilizokuwa zimejengwa katika eneo moja, wakaanza kutembea kwa mwendo wa harakaharaka kuzifuata, baada ya kuzifikia, wakaingia ndani.
Walikuwa wakihema kupita kawaida jambo lililowafanya watu waliokuwa ndani ya nyumba ile kuwasogelea na kuanza kuzungumza nao. Bado Brian alionekana kumshangaza sana Erick, alikuwa akiongea na Waarabu wale kwa lugha ya Kiarabu iliyoonekana kuzoeleka sana mdomoni mwake.
Baada ya kuongea na wale watu kwa muda wa dakika moja, wakawachukua na kisha kuwapeleka chumbani kwa ajili ya kupumzika. Bado Erick alionekana kumshangaa Brian kwa kile kitendo chake cha kuongea lugha ya Kiarabu kwa ufasaha kwa umahiri mkubwa namba ile.
“Why do you look me that way?” (Kwa nini unaniangalia hivyo?) Brian alimuuliza Erick
“Where did you learn to speek Arabic?” (Umejifunza wapi lugha ya Kiarabu?) Erick aliuliza.
“I learned at school. We had an arabian teacher who always taught us how to speek arabic” (Nilijifunza shuleni. Tulikuwa na mwalimu wa Kiarabu ambaye mara kwa mara alikuwa akitufundisha kuzungumza Kiarabu) Brian alimwambia Erick.
Siku hiyo walikuwa wakiongea mambo mengi ambayo walipaswa kuogea kwa wakati huo. Muda ulizidi kusogea zaidi na zaidi mpaka kufikia saa kumi alfajiri muda ambao adhana ikaanza kusikika masikioni mwao. Sauti za milango ambayo ilikuwa ikifunguliwa ikaanza kusikika kuonyesha kwamba watu walitakiwa kuwa msikitini kwa wakati huo, msikiti ambao haukuwa mbali kutoka hapo walipokuwa.
Katika kipindi chote walikuwa macho, usingizi, kwao haukupatikana kabisa. Huku watu wakiendelea kutoka nje ya vyumba vyao kwa ajili ya kuelekea msikitini, mara sauti za watu ambao hawakuonekana kuwa wa amani zikaanza kusikika kutoka masikioni mwao jambo ambalo likawafanya kushtuka kupita kawaida.
Hawakutaka kujiuliza maswali zaidi, tayari walijua kwamba wale watu ambao walikuwa wamewakimbia ndiyo waliokuwa wamekuja mahali hapo. Wote wakaonekana kuingiwa na wasiwasi kupita kawaida, tayari wakaona kwamba walikuwa wameingizwa mikononi mwa Waarabu wale ambao walikuwa wakiwasaka kama lulu kwa ajili ya kuficha siri zao za kuwateka Wamarekani na Waingereza wengi katika jiji hilo la Baghdad.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza Erick.
“Lets run” (Tukimbie)
“What?” (Nini?)
“Leave it to me. You have to do what I ask you to do, right?” (Niachie mimi. Unatakiwa kufanya kile ninachotaka ukifanye. Sawa?) aliuliza Brian.
“Right” Erick alisema huku watu wale wakisikika wakiongea kwa nje na Waarabu wengine ambao walikuwa wameamka kwa ajili ya kwenda kumswali msikitini.
*****
Mchungaji Joshua na mkewe, Mary walikuwa kwenye maumivu makali, mijeredi waliyokuwa wamechapwa na Waarabu wale iliwaacha wakiwa kwenye maumivu makali. Walikuwa uchi wa mnyama. Muda wote walikuwa wakilia tu huku mchungaji Joshua akijitahidi kumbembeleza mkewe ambaye alikuwa akiugulia kwenye maumivu makali zaidi yake.
Hakukuwa na tumaini lolote ambalo walikuwa wakilitumainia kwa wakati huo zaidi ya kumuomba Mungu awaokoe kutoka katika mikono ya Waarabu wale waliokuwa na roho iliyojaa ukatili kupita kawaida. Kila alipokuwa akiyapitisha macho yake kwa Wazungu wengine arobaini ambao walikuwa katika chumba kile, moyo wake ulikuwa kwenye masikitiko makubwa.
Muda wote alikuwa akimshika mke wake mkono huku akimuomba Mungu wake kimoyomoyo afanye muujiza utakaowafanya kutoka salama katika mikono ya Waarabu wale. Ingawa walikuwa wametekwa na kufungiwa ndani ya chumba kile kilichojaa mateso lakini kamwe hakutaka kuusitisha mpango wake wa kufungua kanisa ambao ulikuwa umewafanya kuja nchini Iraq ndani ya Jiji la Baghdad.
Mipango yake ya kuanzisha kanisa bado ilikuwa moyoni mwake kwa wakati huo, makanisa machache ambayo yalikuwa yakipatikana ndani ya Jiji la Baghdad yalionekana kutokutosha kabisa. Sala zake bado zilikuwa zikizidi kuendelea zaidi na zaidi huku wakati mwingine akisimama mbele ya Wazungu wenzake na kuwaambia juu ya imani kubwa ambayo alikuwa nayo moyoni mwake kwamba ilikuwa ni lazima waokolewe mahali hapo na kurudi nyumbani kwao, nchini Marekani na Uingereza.
Katika kipindi ambacho Erick na Brian kuingia ndani ya chumba kile, mchungaji Joshua akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi kutokana na watu wale kumuangalia sana. Kitendo kile tayari kilikuwa kimemfanya kuwa na mashaka zaidi moyoni mwake. Hakuwatambua kwamba wale walikuwa Erick na Brian ambao walikuja ndani ya jumba lile na kuangalia kila kilichokuwa kikiendelea mahali pale.
Mpaka Erick na Brian wanaondoka mahali hapo, mchungani Joshua alikuwa na wasiwasi mwingi. Ni ndani ya sekunde chache baada ya Erick na Brian kuondoka ndani ya chumba hicho ndicho kipindi ambacho milio ya risasi ikaanza kusikika nje.
Kelele zikaanza kusikika ndani ya chumba hicho, kila mtu kwa wakati huo akaonekana kukiogopa kifo, milio ya risasi ambayo ilikuwa ikisikika ilikuwa imeinua hofu kubwa mioyoni mwao. Baada ya dakika kadhaa, kundi la Waarabu watatu wakaingia ndani ya chumba kile huku nyuso zao zikiwa katika hali ya hasira kupita kawaida.
Walichokifanya mahali hapo ni kuanza kuwahesabu watu wote waliokuwa ndani ya chumba kile. Kitu ambacho walikuwa wamekijua kwa wakati huo ni kwamba wale watu ambao walikuwa wamekimbia walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa mateka ndani ya vyumba vile. Walipomaliza kuwahesabu, wakatoka na kuanza kuelekea katika chumba kingine na kuanza kuwahesabu wengine.
“We are going to leave this room very soon (Tutaondoka ndani ya chumba hiki hivi karibuni)” Mchungaji Joshua aliwaambia wazungu wenzake ambao walikuwa mateka pamoja nao.
“Are we going to leave this place? How? (Tutaondoka mahali hapa? Kivipi?)” Mzungu mmoja aliuliza.
“I don’t know but you have to trust me that we are going to leave this place very soon (Sijui lakini inabidi mniamini kwamba tutaondoka ndani ya chumba hiki hivi karibuni)” Mchungaji Joshua aliwaambia.
Maneno ambayo alikuwa ameyaongea yakaonekana kuinua matumaini ndani ya mioyo ya wazungu wale lakini swali lilikuwa moja tu kichwani mwao kwamba ni kwa namna gani wangeweza kuondoka ndani ya chumba kile ambacho hakikuwa chumba cha amani kabisa katika maisha yao. Kitu ambacho walitakiwa kukifanya kwa wakati huo ni kuamuamini mchungaji Joshua maneno ambayo alikuwa amewaambia.
Baada ya dakika kumi, Waarabu nane wakaingia ndani ya chumba hicho na kuanza kuwaangalia mateka wote. Kwa wakati huu walikuwa wameingia kitofauti sana, mikononi hawakuwa na bunduki kama ambavyo walivyokuwa wakiingia katika kipindi cha nyuma, katika kipindi hiki walikuwa na majambia pamoja mapanga huku wengine wakiwa na visu.
Ukiachilia silaha hizo, kulikuwa na mwarabu mwingine ambaye alikuwa ameshika kamera pamoja na vifaa vingine ambavyo vilikuwa vikitumika katika upigaji picha. Tayari akili yao ilikuwa imepata majibu juu ya kitu kile ambacho kingekwenda kutokea mahali hapo, kuchinjwa kama wanyama huku picha za video zikichukuliwa.
Baadhi ya wazungu wanne wakainuliwa na kisha kuvalishwa vitambaa vyeusi usoni mwao na kuanza kupelekwa nje ya chumba kile. Kila mtu kwa wakati huo alikuwa akipiga kelele za kutaka watu hao waachiwe lakini Waarabu wale hawakuonekana kujali kabisa, walichokuwa wakikitaka ni kuondoka na wazungu hao na kufanya kile ambacho walikuwa wakitaka kukifanya.
“They are going to slaught them (Wanakwenda kuwachinja)” Mwanaume mmoja alisema huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Please! Lets pray for them (Tafadhali! Tuwaombeeni)” Mchungaji Joshua alisema na kisha wote kwa pamoja ndani ya chumba kile kushikana mikono na kuanza kuwaombea wale wazungu ambao walikuwa wamechukuliwa na kupelekwa nje, mahali ambapo walijua fika kwamba walikuwa wakielekea kuchinjwa.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 5
WHATSAPP: 0758860093

Kwa harakaharaka Brian akapiga hatua na kuanza kuchungulia nje kupitia mlangoni, Waarabu wanne waliokuwa na bunduki walionekana wakiongea na Waarabu wale ambao walikuwa wakikaa ndani ya ile nyumba. Japokuwa walikuwa wakiongea Kiarabu lakini Brian alikuwa akiwasikia vizuri kabisa, alichokifanya ni kumgeukia Erick na kumwambia kwamba iliwapasa kuondoka mahali hapo.
Wote wakatoka chumbani na kuelekea upande ambao hakukuwa na mtu yeyote. Mwendo wao ulikuwa ni wa harakaharaka sana, hawakutaka kuchelewa, walihitaji kufanya kila kitu kwa kasi kubwa. Walipotokea upande wa pili, wakasikia kwa mbali mlango wa chumba walichokuwa wakikaa ukifunguliwa.
Hapo ndipo walipofanya haraka zaidi. Ngamia kadhaa waliokuwa wamefungwa sehemu mbalimbali katika maeneo hayo walionekana kutaka kuharibu kila kitu mahali hapo. Kwa sababu walikuwa ni wageni na ngamia walikuwa wakifahamu harufu za wenyeji wao, walikuwa wakipiga kelele ambazo zilikuwa zimewashtua Waarabu wale ambao walikuwa ndani.
Kwa mwendo wa kasi wakazidi kukimbia kuelekea katika sehemu iliyokuwa na magari mawili aina ya Land Rover.
Walipoyafikia magari yale, Brian akakipiga kioo kwa kutumia jiwe alilolishika na kioo kuvunjika na kisha kuingia ndani. Muda wote Erick alikuwa akishangaa, mwandishi mwenzake wa habari, Brian alionekana kuwa mtu hatari sana kwa wakati huo, hakujua mambo hayo yote alikuwa amefundishwa wapi.
“Hatuna funguo” Erick alimwambia Brian.
“Subiri. Kazi ndogo sana” Erick alimwambia Brian.
Kwa kasi ya ajabu, Brian akafungua sehemu iliyokuwa katika sehemu ya ufunguo na macho yake kukutana na nyaya mbalimbali zisizopungua kumi. Akaanza kuzichukua yanya moja baada ya nyingine, alipozishika nyaya alizokuwa akizihitaji, akazikata na kuanza kuziunganisha.
Mpaka katika kipindi hicho, Brian akaonekana kuwa komandoo au mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi sana ambayo Edmund hakuwa akiyafahamu.
Waarabu wale waliokuwa ndani wakatoka nje na kuanza kuelekea kule ambapo kulikuwa na magari yale. Brian alifanya vitu kwa haraka sana, mara gari likaanza kushtuka shtuka na hatiame kuwaka. Brian akashikilia uskukani na kisha kuingiza gia na kuliondoa gari mahali hapo katika kasi ambayo ilionekana kumshangaza Erick ambaye alikuwa haamini kile kilichokuwa kikitokea mahali hapo.
“Unanichanganya. Hivi kweli wewe kweli ni mwandishi wa habari?” Erick alimuuliza Brian.
“Utajua tu. Cha kwanza twende hotelini” Brian alimwambia Erick.
“Kufanya nini?”
“Kuchukua begi langu. Kazi inaanzia mahali hapa. Tayari tumechokoza vita na wao, ni lazima tuvimalize hata kabla hatujaelekea nchini Marekani” Brian alimwambia Erick huku akiendesha gari kwa kasi.
“Vita! Tumeanzisha vita?” Erick aliuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo. Hatuna budi kupambana kwa sasa. Unajua kutumia bunduki?” Brian alimuuliza Erick.
“Hapana.”
“Nitakufundisha”
“Mpaka sasa hivi umekwishanichanganya”
“Usichanganyikiwe kwa sasa. Kazi yako kama mwandishi wa habari imekwishaisha. Imebakia kazi yangu tu” Brian alimwambia Erick maneno ambayo yalionekana kumshtua zaidi.
“Bado unanichanganya”
“Usiwe na pupa. Utajua kila kitu. Twende hotelini kuchukua begi langu. Baada ya hapo nitakwambia kila kitu” Brian alimwambia Erick huku tayari wakiwa wanaana kuuacha mji huo wa Wassit uliokuwa katika jiji hilo la Baghdad.
*****
Bado safari ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi. Mwendo ulikuwa ni wa kasi sana kiasi ambacho Erick aliona muda wowote ule walikuwa wakienda kupata ajali. Barabara ilikuwa mbaya, mashimo ambayo yalikuwa barabarani yaliifanya gari lile kudundadunda muda wote wa safari.
Kichwa cha Erick bado kilikuwa kikimfikiria Brian, kitendo cha kujitambulisha kwamba alikuwa mwandishi wa habari huku akiwa amefanya mambo mengi ya hatari kilionekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Maswali yalikuwa yakizidi kumiminika kichwani mwake, alitamani sana kuuliza lakini kwa hali ambayo walikuwa nayo katika kipindi hicho hakuona kama lingekuwa jambo la busara kufanya hivyo.
Baada ya dakika kadhaa wakawa wamekwishafika katika hoteli ya Majfallus. Polisi wengi pamoja na waandishi wa habari walikuwa mahali hapo huku wakiangalia namna hali ilivyokuwa mbaya. Miango mingi ilikuwa imevunjwa, kila mhudumu ndani ya hoteli ile alikuwa akizungumza lake kuhusiana na uvamizi ule ambao ulikuwa umetokea.
Brian na Erick wakateremka kutoka garini na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo la hoteli ile. Polisi waliokuwa mahali pale wakajaribu kumzuia lakini mara baada ya kujitambulisha kwamba walikuwa miongoni mwa wateja waliopanga ndani ya hoteli ile, wakawaruhusu kuingia.
Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika chumba alichokuwa akikaa Brian. Hakukuwa na mlango, mlango ulikuwa umevunjwa kama ambavyo ulivyokuwa katika kipindi kilichopita wakati ambao Waarabu wale walipokuja kuwateka baadhi ya wazungu ambao walikuwa wamepanga ndani ya hoteli ile.
Brian akaanza kulifuata begi lake, alipolifikia, akalichukua na kuliweka kitandani. Muda wote Erick alikuwa kimya akimwangalia tu, bado maswali mengi yalikuwa yakiendelea kumiminika kichwani mwake juu ya Brian ambaye wala hakuwa akieleweka vizuri kwake. Macho yake yakahamia katika begi lile aliloliweka Brian pale kitandani.
Brian akalifungua begi lile, nguo zilikuwa zikionekana kwa juu, akaitoa fulana moja ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiarabu ambayo yalimaanisha ‘TUMUABUDU ALLAH’ na kisha kuivaa. Akazitoa nguo nyingine na macho ya Erick kutua katika bunduki tatu ambazo zilikuwa na vyombo vilivyokuwa na sauti ya kuzuia mlio wa risasi.
Erick akashtuka kupita kawaida, tayari kichwa chake kikatambua kwamba Erick alikuwa mtu hatari sana na wala hakuwa mwandishi wa habari kama ambavyo alijitambulisha kabla. Brian akazitoa bunduki zile zote na kisha kuziweka kiunoni mwake.
“Who are you? (Wewe ni nani?)” Erick aliuliza huku akionekana kuhofia.
“We have no enough time for conversation, we have to leave (Hatuna muda wa kutosha wa mazungumzo, tuondoke)” Brian alimwambia Erick.
Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kwenda kwenye chumba alichopanga Erick na kisha kuchukua begi lake. Katika kila kitu ambacho kilikuwa kikifanyika mahali hapo kilikuwa kikifanyika kwa harakaharaka. Hakukuwa na muda wa kupoteza hata mara moja, tayari maisha yao yalionekana kuwa katika hatari kubwa.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa katika upande wao nchini humo, walitakiwa kujitetea wao kama wao. Wakaanza kutoka nje na kuelekea kule ambapo walikuwa wamelipaki lile gari ambalo walikuja nalo, Brian alipoangalia vizuri katika eneo lile, macho yake yakatua katika gari ambalo alikuwa ameliona kabla ya kufika mahali hapo. Akamsimamisha Erick.
“What is happening? (Nini kinaendelea?)” Erick aliuliza huku akionekana kushtuka.
“They are here (Wapo hapa)”
“I don’t get you. Who is here? (Sijakupa. Nani yupo hapa?)”
“Kindnapers (Watekaji)” Brian alijibu.
Akaanza kuyapeleka macho yake huku na kule, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuweza kuingia ndani ya gari lile, ushauri ambao alikuwa ameutoa mahali hapo ni kuondoka kwa miguu kutafuta sehemu nyingine huku ikiwa imetimia saa sita usiku.
Wakaanza kutembea kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na majengo kadhaa ya ghorofa huku watoto wengi wa mitaani wakionekana katika eneo hilo. Mwendo wao ulikuwa ni wa harakaharaka sana. Walipogeuka nyuma, watu watano walikuwa wakiwafuata huku wakiwa wamevalia kanzu kubwa. Brian akaiinua fulana ile aliyokuwa ameivaa na kisha kuchomoa bunduki na kuishika mkononi mwake.
Hakukuwa na amani kabisa, tayari muda wa vita ukaonekana kuingia. Kutokana na kuwa na idadi kadhaa ya watu katika mitaa ya hapo walipokuwa pamoja na msikiti mkubwa kuliko misikiti yote jijini Baghdad, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alithubutu kupiga risasi. Bado waliendelea kwenda mbele ambapo Brian akamwambia Erick ulikuwa ni wakati wa kukimbia kwa ajili ya kuziokoa roho zao.
Walipoona kwamba wameupita msikiti na kuuacha kwa umbali wa mita mia moja, hapo hapo milio ya risasi ikaanza kusikika. Brian hakuonekana kuwa na wasiwasi kabisa, alizidi kukimbia pamoja na Erick mpaka kufika sehemu ambayo ilikuwa na ghorofa moja na kumwambia Erick asimame nyuma ya ukuta ule.
Brian akaishika bunduki yake na kisha kuanza kumlenga mmoja baada ya mwingine. Kutokana na bunduki zile kuwa na vyombo vya kuzuia mlio wa risasi, wakajikuta mmoja baada ya mwingine wakianguka chini bila kusikika sauti yoyote ambazo zingewafanya kujificha. Ni ndani ya dakika moja, Waarabu wote watano walikuwa chini huku damu zikiwatoka.
“Hivi ni vita. Wewe baki kama mwandishi. Umesikia?” Brian alimuuliza Erick ambaye alijiona kuishi na roho mkononi.
“Sawa” Erick aliitikia huku akitetemeka.
Walipoona kwamba Waarabu wote walikuwa chini, wakatoka kutoka katika sehemu ile na kisha kuanza kuifuata miili ile na kuanza kuiangalia. Damu zilikuwa zimetapakaa katika eneo zima mahali pale. Kila kitu kikaonekana kwenda sawa mahali hapo. Huku wakiwa wanaendelea kuiangalia miili ile, mara wakaanza kusikia sauti za watu ambazo zilikuwa zikiwataka kutokufanya kitu chochote mahali hapo.
Brian alipotaka kugeuka kuona ni walikuwa ni watu gani, milio ya risasi ikasikika na risasi kudhaa kupiga ardhni. Brian akatakiwa kuweka bunduki zake chini na kufanya hivyo.
Huku wakisubiria kuona ni kitu gani wangeambiwa au hata kuziona sura za watu wale waliokuwa nyuma yao, wakashtukia wakipigwa na vitako vya bunduki kichwani mapigo ambayo yaliwafanya kupoteza fahamu bila kujua wale walikuwa wakina nani.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 6
WHATSAPP: 0758860093

Wamarekani na Waingereza walionekana kuchanganyikiwa, hawakuamini kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika nchi mbalimbali za Uarabuni hasa hasa katika nchi ya Iraq tena ndani ya jiji la Baghdad. Wazungu wengi ambao walikuwa wakielekea katika nchi hiyo walikuwa wakipotea katika mazingira ya kutatanisha sana jambo ambalo lilionekana kuhisi kwamba kuna sehemu ambayo walikuwa wakipelekwa.
Kutokana na tukio lile kutokea mara kwa mara, wote kwa pamoja wakaamua kuwatuma wapelelezi ili kujua ni sehemu gani watu hao walipokuwa wakichukuliwa na kupelekwa. Hii ilichukua muda mrefu sana, kwa Waingereza wakaamua kuwatuma wapelelezi wao kutoka katika shirika la kipelelezi la SOCA kwa ajili ya kulifanyia upelelezi jambo hili huku Wamarekani wakiwatumia wapelelezi kutoka katika shirika la FBI na CIA kwa ajili ya kulifanyia upelelezi jambo hilo.
Katika kipindi hicho walikuwa wakihitaji kufahamu kitu kimoja tu, mahali ambapo wenzao walipokuwa wakipelekwa ndani ya jiji hilo. Kitu cha kushangaza ambacho kilikuwa kikitokea ni pale ambapo wapelelezi ambao walikuwa wamewatuma kuuawa kinyama huku wengine wakiwa hawajulikani mahali walipokuwa wakipelekwa.
Jambo hilo lilikuwa likiwauma sana, wapelelezi wengi walikuwa wakichinjwa kama kuku, tena mbele ya kamera jambo ambalo liliibua hofu kubwa sana duniani na watu kuliangalia taifa la Iraq kwa jicho la tatu. Hali ikaonekana kutisha sana nchini Iraq kiasi ambacho kuna wakati Umoja wa Mataifa ukaanza kuingilia kati kwa kuyapeleka majeshi yao nchini humo.
Hali ikaanza kutulia na amani kurudi tena. Wamarekani na Waingereza wakaanza kumiminia nchini humo. Uwepo wao kwa wingi ukaanza kuonekana kuwa kero kwa Waarabu ambao kila siku walikuwa wakitaka nchi yao iachwe mikononi mwao, wasiingiliwe na mtu yeyote yule, na hii ilitokana na visima vingi vya mafuta ambavyo walikuwa navyo.
Ndani ya miezi mitatu ya amani, Waarabu wakaanza kujawa na vinyongo hali ambayo maisha yakarudi na kuwa kama zamani, kuwateka Wamarekani na Waingereza na hata wengine kuwachinja. Hofu zikaanza kuwaingia tena, watu wengi wakakataa kuelekea nchini Iraq.
Kila siku Wamarekani walikuwa wakiumiza vichwa vyao, kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kujua ndugu zao walikuwa wakitekwa na kupelekwa sehemu gani. Hapo ndipo kikao kizito na cha siri cha serikali tena kikiongozwa na rais wa nchi hiyo kikaitishwa. Mkuu wa upelelezi kutoka katika shirika la kipelelezi la FBI alikuwa mmoja wa watu kumi ambao walihudhuria katika kikao hicho.
Mambo mengi yakajadiliwa lakini kubwa zaidi lilikuwa ni kwa jinsi gani wangeweza kufahamu sehemu ambayo ndugu zao walikuwa wakipelekwa. Hapo ndipo uamuzi ukatolewa. Kwanza walitakiwa kumpeleka mpelelezi mwenye umri mdogo kimtazamo pamoja na mwandishi mmoja wa habari ambaye angefanya kazi pamoja na mpelelezi huyo mpaka kujua kila kitu ambacho kilikuwa kikitokea.
Brian Michael ndilo lilikuwa jina ambalo lilikuja vichwani mwao. Walichokifanya ni kumuita na kisha kumpa jukumu kubwa ambalo alitakiwa kulitekeleza kwa haraka sana. Hiyo ilikuwa taarifa mbaya kwa Brian, aliuhisi mwili wake ukitetemeka kwa woga kupita kawaida. Ni kweli kwamba alikuwa akifanya sana kazi ya upelelezi lakini kwa yale ambayo yalikuwa yakitokea nchini Iraq yalikuwa yakimtisha kupita kawaida.
Kila siku alikuwa akiomba Mungu kutokwenda katika nchi ile ambayo ilijaa vitisho sana, sala yake ikaonekana kutokumsaidia, mwisho wa siku alisimama mbele ya rais na kuambiwa kwamba alitakiwa kuelekea nchini Iraq kwa ajili ya kupeleleza mahali ambapo Wamarekani wengi walipokuwa wakipelekwa.
Brian hakubisha japokuwa moyo wake haukupenda kabisa kuelekea kule. Kilichofanyika ni shirika la kipelelezi la FBI kuwasiliana na shirika la habari la CNN na kuwaomba kwamba walikuwa na uhitaji wa mwandishi mmoja wa habari ambaye alikuwa mtu mweusi kwa kazi moja ya kuelekea nchini Iraq. Hapo ndipo mchakato wa kumtafuta mwandishi bora wa habari katika bara la Afrika kufanyika mara moja.
Mshindi, Erick alipopatikana, moja kwa moja akatakiwa kuelekea nchini Baghdad. Walichokifanya ni kumtuma Brian kuanza kuzoeana pamoja na Erick huku akijitambulisha kwamba ni mwandishi kutoka katika shirika la habari la BBC.
Kilichokuwa kikihitajika kwa wakati huo ni urafiki tu. Kama ambavyo ilivyokuwa imepangwa na ndivyo ambavyo ilivyotokea. Brian akaanza taratibu urafiki na Erick kiasi ambacho wakazoeana sana mpaka kuwa pamoja nchini Iraq.
****
Erick akashtuka na kujikuta yupo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na giza kubwa sana, hakuweza kuona kitu chochote mahali hapo kutokana na giza lile ambalo lilikuwepo ndani ya chumba kile. Sakafuni kulikuwa na maji ambayo kwa jinsi yalivyokuwa yakitoa harufu, yalikuwa yakionekana kuwa maji machafu.
Akaanza kupapasa ndani ya chumba kile, harufu ya maji yale yalionekana kuwa kero kubwa puani mwake kiasi ambacho kilimfanya wakati mwingine kujisikia kichefu chefu. Akaanza kutembea ndani ya chumba kile kwa kutumia magoti huku mikono yake ikipapasa sakafuni. Kumbukumbu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea kipindi cha nyuma kikaanza kurudi kichwani mwake.
Hakujua mahali ambapo alikuwepo Brian, kupapasa papasa kule ilikuwa ni kama ishara moja ya kumtafuta Brian mahali pale. Alizidi kupapasa zaidi na zaidi mpaka pale alipougusa mwili wa mwanadamu. Kwanza mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, woga ulikuwa umemshika kupita kawaida.
“Brian….Brian….” Erick alianza kuita kwa sauti ndogo huku akimtingisha kwa kuamini kwamba mtu yule alikuwa Brian.
Hakuitikiwa na mtu yule jambo ambalo likamfaya kuanza kumwagia maji yale yaliyokuwa ndani ya chumba kile. Bado hali haikuwa imebadilika kabisa, mtu yule alionekana kuwa kimya. Alichokifanya Erick ni kuanza kumgusa kifuani kama njia mojawapo ya kusikilizia mapigo yake ya moyo kuona kama yalikuwa yakidunda au la, mapigo ya moyo yalikuwa yamesimama.
Erick akaonekana kuogopa kupita kawaida, hofu ikawa imezidi zaidi moyoni mwake. Akazidi kupapasa zaidi na zaidi mpaka kumfikia mtu mwingine, alipomtingisha zaidi, mtu yule akaamka, alikuwa Brian amba alionekana kuchoka kupita kawaida.
“Erick” Brian aliita kwa sauti iliyoonyesha kama mtu aliyekuwa amepata maumivu fulani.
“Nipo hapa”
“Naomba uniinue” Brian alimwambia Erick huku ambaye akamuinua.
Wote wakakaa chini na kuanza kuongea. Tayari hali ikaonekana kubadilika kwa wakati huo, kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kuondoka ndani ya chumba kile tu. Kwa mbali mwanga ukaanza kuonekana ukipitia mlangoni jambo lililowafanya kugundua kwamba kwa kulikuwa kunaanza kupambazuka.
Mwanga ule ndio ambao uliwafanya kugundua kwamba chumba kile hakikuwa na dirisha hata moja, kilikuwa na mlango mmoja tu ambao ulikuwa na tundu chiini ya mlango ambalo lilikuwa likipitisha hewa. Michirizi ya damu ikaanza kuonekana ukutani huku kukiwa na mikwaruzo ya kila aina. Wote wakaonekana kujua kwamba cumba hicho kilikuwa chumba kilichokuwa na hatari sana.
Walipopitisha macho pembeni yao, kulikuwa na mwili ambao haukuwa na kichwa, ulikuwa umechinjwa. Hofu ikaongezeka zaidi, kwa Erick, akaanza kumkumbuka mke wake, Christina, mpaka kufikia hatua hiyo, aliamini kwamba kilichofuata kilikuwa ni kuchinjwa tu.
Huku mioyo yao ikiwa na hofu, mara mlango ule ukafunguliwa na kisha Waarabusaba kuingia huku wakiwa na bunduki pamoja na visu vilivyoonekana kuwa vikali. Wote wakabebwa juu juu na kupelekwa katika sehemu ambayo ilikuwa na watu wanne tu, watu waliokuwa na visu pamoja na mpiga video kamera huku wale watu ambao walikuwa wamewaleta wakiwa wameondoka mahali hapo.
“Tunachinjwa” Erick alimwambia Brian huku akianza kulia.
“Tumuombe Mungu! Huo ndio msaada ambao umebakia wa kutuondoa mahali hapa” Brian alimwambia Erick na kisha Brian kuchukuliwa na mtu ambaye alivaa kininja na kisha kusimama mbele ya kamera huku kisu kikiwa mkononi mwake. Brian alipoonekana analeta kukuru kakara, vijana wengine wakaja na kumshika miguu yake, akatulizwa huku kijana yule aliyekuwa ameshika kisu akianza kukipeleka kisu shingoni mwa Brian huku Erick akilia kama mtoto.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 7
WHATSAPP: 0758860093

Kisu kilikuwa shingoni mwa Erick ambaye alikuwa akiomba sala ya kimyakimya huku akimtaka Mungu amuokoe kutoka kwa wale vijana ambao walikuwa wamemshika. Huku mwarabu yule akiwa amejiandaa kumchinja, mara milio ya risasi ikaanza kusikika mahali hapo. Mwarabu yule akapigwa risasi na kuanguka chini huku damu zikimtoka kichwani.
Mshika kamera pamoja na Waarabu wengine waliokuwa mahali pale nao wakapigwa risasi mfululizo na kuanguka chini kama mizigo. Brian na Erick wakabaki kwenye mshangao, hawakujua ni mtu gani ambaye alikuwa amewapiga risasi Waarabu wale waliokuwa wamewashikilia mateka huku wakitaka kuwachinja.
Mara msichana mmoja wa kiarabu akatokea mahali hapo, kila mmoja akapigwa na mshtuko mkubwa. Hawakutegemewa kama kungetokea mtu yeyote mahali hapo na kuwaokoa kutoka katika mikono ya Waarabuwale ambao kwao walionekana kuwa watu wenye roho mbaya sana. Msichana yule hakuongea kitu chochote kile alichokifanya ni kuanza kuzikusanya bunduki zilizokuwa mahali pale na kisha kuanza kuwagawia.
“Who are you? (Wewe ni nani?)” Brian alimuuliza msichana yule wa kiarabu.
“There is no need to know me. You have to do what I ask you to do. Am I Understood? (Hakuna uhitaji wa kujua mimi ni nani. Mnachotakiwa kufanya ni kile ambacho nitawataka kukifanya. Nimeeleweka?)” Msichana yule aliwaambia na kuwauliza.
“Underestood (Umeeleweka)” Brian alijibu.
Hapo hapo wote kwa pamoja wakaondoka mahali hapo, hakukuwa na mtu aliyeamini kama kwa wakati huo bado walikuwa wakiendelea kuvuta pumzi ya dunia hii. Mwendo wao ulikuwa ni wa mashaka, bado hawakujiona kuwa na amani mahali hapo, macho yao hayakutulia, muda wote yalikuwa yakiangalia huku na kule kuona kama kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akiwaona.
Miili kadhaa ya Waarabu ilikuwa ikionekana chini huku damu zikiwatoka, tayari waliona kwamba msichana yule ndiye ambaye alikuwa amefanya mauaji ya watu wote waliokuwa ndani ya jumba lile. Waliendelea na safari mpaka kufika nje ambapo wakachukua gari lililokuwa mahali hapo na kisha kuondoka.
Kila mmoja hakujua ni mahali gani ambapo walikuwa wakielekea kwa wakati huo. Walikuwa wakiona wanauacha mji wa Wassit na kuelekea sehemu ambayo ilikuwa na mji wa Dhamir uliokuwa na visima kadhaa vya mafuta. Njia haikuwa nzuri hata mara moja, muda wote ni vumbi tu ndilo ambalo lilikuwa likionekana mahali hapo.
Ukimya ukatawala ndani ya gari, ni sauti ya muungurumo wa gari tu ndio ambao ulikuwa ukisikika mahali hapo. Kila mmoja alikuwa na dukuduku la kutaka kumfahamu msichana huyo ambaye alionekana kuwa na umri mdogo lakini alionekana kuwa mwanamke shujaa ambaye alihitajika kuwekewa uangalifu mkubwa sana.
Japokuwa mioyo yao ilikuwa na maswali mengi lakini kwa wakati huo walikuwa kimya. Sura ya msichana yule ilionyesha dalili zote kwamba kwa kipindi hicho hakutaka kuulizwa swali lolote lile. Gari liliendelea mbele zaidi na zaidi huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi na ndipo wakaanza kuingia katika mji wa Dhamir.
Wakinamama wa kiarabu walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kuchota maji huku madumu makubwa wakiwa wamewabebesha ngamia waliokuwa nao. Safari hiyo ikaishia ndani ya eneo la nyumba moja ambayo ilionekana kama ghorofa lakini lisilokuwa imara kwa sana. Wote wakateremka na kuanza kumfuata msichana yule.
Moja kwa moja msichana yule akaelekea katika chumba ambacho akawataka wote waingie ndani na kutulia huku akiwaandalia chakula na kuwapa maji. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiongea kitu chochote kile, bado walikuwa wamebaki na dukuduku yao ndani ya mioyo yao. Walitumia muda wa nusu saa kumaliza chakula na ndipo maongezi yalipoanza.
“Tunashindwa kuelewa wewe ni nani na unataka nini kutoka kwetu” Brian alimuuliza msichana yule.
“Mimi ninaitwa Yasmin Abdullahman” Msichana yule alijitambulisha.
“Sawa. Kwa nini umeamua kutuokoa?” Brian alimuuliza.
“Kwa sababu nilikuwa nataka kitu kimoja kutoka kwenu” Yasmin aliwaambia.
“Kitu gani?”
“Mumsaidie mdogo wangu ambaye ini lake linamsumbua na hivyo kuteseka kitandani” Yasmin alisema huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga.
“Yaani umetuokoa kwa sababu ya kuokoa maisha ya mdogo wako?” Brian aliuliza huku akishangaa.
“Ndiyo”
“Yupo wapi?”
“Yupo ndani” Yasmin alijibu na hapo hapo kuinuka huku akiomba kumfuata na kisha kusimama karibu na mlango wa kuingia ndani ya chumba kimoja.
Wakayapeleka macho yao kitandani, kijana wa kama miaka kumi na sita alikuwa amelala kitandani. Mwili wake ulionekana kukonda kupita kawaida jambo ambalo likawafanya kugundua kwamba hakuwa na afya ya kutosha. Ugonjwa wa ini ambao ulikuwa ukimsumbua sana ndio ambao ulifikia hata hatua ya kumdhoofisha mwili wake.
“Anaitwa nani?” Brian alimuuliza Yasmin.
“Rahim” Yasmin alimjibu Brian ambaye akaelekea mpaka kitandani pale na kisha kumshika Rahim ambaye alikuwa hoi kitandani.
*****
Maisha yalikuwa magumu sana nchini Iraq, fedha ya nchi hiyo ilikuwa imebanwa kupita kawaida. Maji hayakuwa yakitoka mara kwa mara kama kipindi kilichopita, kutokana na nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zikipatikana katika sehemu yenye jangwa, kila kitu kilionekana kuwa matatizo makubwa.
Matatizo haya yalitokana na machafuko ambayo mara kwa mara yalikuwa yakitokea nchini humo huku baadhi ya wananchi wakimtaka rais wa nchi hiyo, Bwana Yassin aachie ngazi. Uongozi wake ulionekana kuwa mbaya, japokuwa katika kipindi cha nyuma watu walimchagua kuingia madarakani lakini kwa wakati huo alikuwa amebadilika sana.
Mambo mengi ambayo alikuwa ameyaahidi yakaonekana kusahaulika, akajisahau Ikulu na kuamua kufanya mambo yake tu. Hakukumbuka hata siku moja kwamba alikuwa akitakiwa kufanya mambo mengi kwa ajili ya nchi huku akitakiwa kuliwekea utatuzi suala na ukame ambalo lilionekana kuiumiza nchi hiyo kupita kawaida.
Rais Yassin alionekana kujisahau kabisa, maandamano yaliendelea zaidi na zaidi mpaka fujo kutokea mara kwa mara. Vibanda vilichomwa moto huku majengo ya chama chake yakiteketezwa pia kwa moto. Watu walionekana kumkasirikia kupita kawaida. Ingawa waandamanaji walikuwa wakimwagiwa maji ya kuwasha pamoja na kupigwa virungu na mapolisi lakini maandamano hayo hayakuishia, waliendelea kusisitiza msimamo wao huo huo wa kumtaka rais huyo aaachie uongozi hara iwezekanavyo.
Baada ya kipindi fulani, jambo jingine kubwa na baya likaanza kutokea katika nchi hiyo hasa mara baada ya rais huyo kuhusishwa kwamba alikuwa kibaraka wa Wamarekani na Waingereza. Mafuta yalikuwa yakichukuliwa kisiri na wazungu jambo ambalo ikaonekana kuwaletea maumivu makali sana watu wa nchi hiyo pamoja na nchi nyingine jirani za kiarabu kama Syria na Iran.
Waarabu hawakutaka kuona mafuta yao yakichukuliwa na wazungu, watu ambao walikuwa wakiwachukia kupita kawaida. Hali hiyo ndio ikachochea zaidi maandamano mitaani, watu wote ambao walionekana kuwa upande wa rais Yassin walikuwa wakiuawa huku wakati mwingine watu wakiwa wanajitoa mhanga kwa kujilipua katika kundi la watu wa rais Yassin.
Nchi haikutulia hata mara moja, Wamarekani na Waingereza bado walikuwa wakiendelea kupotea katika mazingira ya kutatanisha jambo ambalo lilionekana kumshangaza kila mtu. Nchi ikawa kwenye matatizo makubwa, uchumi ukashuka kwa kiasi kikubwa huku njaa ikianza kuikumbuka nchi hiyo.
Katika kipindi hicho ndicho kilikuwa kipindi cha kupigana hasa na maisha ili kupata fedha ambayo ilikuwa imefichwa. Vijana wengi wakaanza kujiingiza jeshini kwa ajili ya kupata fedha ambazo zilikuwa zikitolewa mara kwa mara kwa wanajeshi. Maisha hayo ya shida ambayo yalikuwa yakiendelea nchini humo ndio ambayo yalimfanya msichana Yasmin kuamua kujiunga na jeshi la nchi hiyo huku mdogo wake, Rahim akiwa mgonjwa kitandani.
Mara ya kwanza kuingia jeshini watu walikuwa wakimshangaa, hawakuamini kama katika kipindi hicho kungetokea na msichana ambaye alikuwa akijiunga na jeshi. Ingawa wanaume wengi walikuwa wakimshangaa lakini Yasmin hakuonekana kujali, alichokijali ni kufanya mazoezi ya nguvu na hatimae mwisho wa siku apewe fedha na kisha kumtibia mdogo wake ambaye alikuwa akiumwa sana.
Mazoezi mazito ya kijeshi yalikuwa yakiendelea zaidi kambini, Yasmin aliendelea kung’angania zaidi. Wanaume wengi wakaonekana kushtuka, Yasmin alionekana kuwa na uwezo kupita wao. Yasmin hakuishia hapo, walipoanza kufundishwa kutumia bunduki, Yasmin alionekana kuwa mtu wa tofauti sana, alikuwa na uwezo mkubwa wa kulenga shabaha.
Mpaka miezi miwili inakatika, Yasmin alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutumia bunduki. Mwili wake haukuwa legelege tena, ulikuwa umekakamaa sana. Fedha ambazo alikuwa akizipata jeshini ndizo ambazo alikuwa akizitumia kumtibia mdogo wake lakini wala hazikusaidia kutokana na matibabu kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha.
Yasmin akakata tamaa, hakuamini kama kungetokea siku ambayo angepata fedha zaidi. Akili yake ikatamani kutaka kufanya jambo jingine la ziada kwa ajili ya kupata fedha na kumtibia mdogo wake, lakini hakuona ni kitu gani alitakiwa kukifanya kwa ajili ya kumuingizia fedha.
Baada ya miezi kadhaa kupita hapo ndipo ambapo Yasmin alipoamua kujiunga na kundi la waasi ambao walikuwa wakiipinga serikali ya rais Yassin ambayo ilikuwa madarakani. Kutoka na kujiunga huko, kidogo kukaonekana kuwa na mafanikio, watu ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kutumia bunduki walikuwa wakilipwa vizuri na kiongozi wao, Kabour Jabrouz ambaye alikuwa akitamani sana nafasi ya uongozi wa nchi hiyo.
Fedha hizo ndizo ambazo alikuwa akizitumia kuendelea kumtibia Rahim ambaye kwa kiasi fulani akaanza kuonyesha mafanikio mwilini mwake . Ile ikaonekana kuwa faraja kwa Yasmin, akajiona kuushinda ugonjwa ule ambao ulikuwa ukimuandama sana mdogo wake wa pekee, Rahim.
Rahim akaanza kupata nguvu, akapata nguvu za kusimama na hata kucheza na wenzake. Baada ya kipindi cha mwezi mmoja, Rahim akaanza kurudi katika hali ile ile jambo ambalo lilikuwa likimuumiza sana Yasmin. Hapo ndipo alipoamua kumfuata kiongozi wao, Jabrouz na kumwambia kwamba alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha, tofauti na mategemeo yake, Jabrouz hakumpa kiasi kile alichokihitaji.
Chuki ya Yasmin juu ya kundi lile pamoja na kiongozi wake ilipoanza kuchipukia moyoni mwake. Hata mpango wa kuwateka Wamarekani na Waingereza ulipoanza, Yasmin hakuonekana kuufurahia. Wazungu wengi walikuwa wakiuawa sana jambo ambalo kwa upande mwingine kama binadamu likaonekana kumuumiza.
Huku kazi zile za kuwateka wazungu zikiendelea, kuna wazo moja ambalo likamjia kichwani mwake. Kitu ambacho alikifahamu kwa wakati huo ni kwamba wazungu wengi walikuwa na fedha na walikuwa radhi kukusaidia endapo tu ungeonyesha msaada kwao kutoka kwako. Hapo ndipo alipoanza mchakato mzima wa kutaka kutafuta wazungu ambao walikuwa wakitekwa na kisha kuwaokoa.
“Kuna watu ambao itabidi wachinjwe leo asubuhi, tena mbele ya kamera na kuutuma mkanda wa video nchini mwao” Jabrouz aliwaambia watu wake mara baada ya kuelezwa juu ya kukamatwa kwa Brian na Erick.
“Watu gani?” Yasmin aliuliza.
“Wamarekani wawili. Mmarekani mweupe na mweusi” Bwana Jabrouz alisema huku akionekana kuwa na hasira.
“Kwa hiyo nifanye nini mkuu?”
“Unatakiwa kwenda kusimamia kila kitu huko. Simamia shughuli yote na kisha kuniletea ripoti pamoja na mkanda huo” Bwana Jabrouz alimwambia yasmin.
“Nitafanya hivyo mkuu” Yasmin alisema huku akipiga saluti.
“Hakikisha kila kitu kinakamilika”
“Ndio mkuu” Yasmin alisema na kupiga tena saluti.
Hapohapo akatakiwa kuondoka kuelekea katika sehemu ambayo watu hao walitakiwa kuchinjwa huku ikiwa imefikia saa kumi na mbili kasoro asubuhi. Yasmin akachukua gari ambalo lilikuwa limeandaliwa kwa ajili ya mizunguko yake ya hapa na pale na kisha kuelekea kule ambapo alikuwa akitakiwa kwenda huku moyo wake ukiwa na furaha, kilioa chake cha miezi yote kikaonekana kuwa mwisho wake siku hiyo.
“Nitawaua wote. Nitaua kwa ajili ya afya ya Rahim” Yasmin alijisemea huku akiikoki vizuri bunduki yake.
*****
Bado Yasmin alikuwa akiendesha gari kwa kasi, bunduki zake alikuwa ameziandaa vizuri kwa ajili ya kufanya mauaji kwa Waarabuambao walikuwa wamewateka Brian na Erick. Kichwa chake kwa wakati huo kiliuwa kikimfikiria mdogo wake, Rahim tu. Alimchukia sana Jabrouz, aliuchukia pia upande ambao alikuwepo kwa muda huo.
Moyoni mwake aliamini kwamba kama Jabrouz angempa kiasi kile cha fedha ambacho alikuwa akikihitaji basi kwa wakati huo tatizo lake lingekuwa linaelekea mwishoni kabisa. Alimchukia sana kwa sababu hakutaka kumsaidia japokuwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kumsaidi. Yasmin alijiona kufanya kazi kubwa sana katika maisha yake pale kazini lakini mwisho wa siku akajiona kama kusalitiwa.
Mawazo yake ya kuwaua wenzake ambao walikuwa wamemshikilia Brian na Erick bado yalikuwa yakiendelea kuwa kichwani mwake. Kadri safari ile ilivyozidi kusonga mbele na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyozidi kumpanda zaidi na zaidi. Bunduki zake alikuwa ameziweka vizuri, mara baada ya kufika akasimamisha gari lake na kuanza kuelekea ndani ya jengo hilo.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na wasiwasi nae, kila mmoja alikuwa akimkaribisha huku akiwa na tabasamu usoni mwake. Katika kipindi hiki Yasmin alionekana kuwa tofauti, hakuwa na sura iliyojaa tabasamu, katika kipindi hiki alikuwa mtu mwenye sura ya tofauti kabisa, sura ambayo ilikuwa ikionekana kuwa na hasira za kufanya jambo lolote baya.
Alichokifanya, akaanza na hao hao waliokuwa wakimpokea kwa nyuso za tabasamu na kisha kuingia ndani. Milio ya risasi haikusikika kabisa kutokana na kuwa na chombo cha kuzuia mlio wa risasi. Kwa kila ambaye alikuwa akimpokea alikuwa akimuua tu. Bado alikuwa akielekea mbele zaidi, damu zilikuwa zikiendelea kumwagika ndani ya jengo lile mpaka pale ambapo aliufikia mlango wa kuingilia katika uwanja mkubwa ambao uliwekwa maalumu kwa ajili ya kuwachinja watu mbalimbali, hasa waandishi wa habari.
Alichokifanya ni kuanza kuangali risasi ndani ya bunduki yake, hakukuwa na risasi hali iliyomfanya kuchukua bunduki kutoka kwa mmoja wa watu ambao alikuwa amewaua na kisha kuufungua mlango ule. Hakutaka kuuliza kitu chochote kile, alichokifanya ni kuanza kuwaua wale watu ambao walikuwa wamewashikilia Brian na Erick.
Hakutaka kuchukua muda mrefu mahali hapo, alipoona kila kitu amemaliza na ndipo akawachukua na kuanza kuondoka nao kuelekea katika nyumba ambayo alikuwa akiishi pamoja na mdogo wake, Rahim ambaye alikuwa mgonjwa kitandani. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikiendelea kumfikiria mdogo wake, kwa jinsi alivyoweza kuwasaidia Brian na Erick, aliamini kwamba nao wangeweza kumsaidi.
“Kwa hiyoyo wewe unataka tumsaidie nini?” Brian alimuuliza Yasmin huku akimwangalia Rahim ambaye alikuwa kitandani.
“Kumuwekea ini jingine”
“Si umpeleke hospitali?”
“Tatizo si kwenda hospitali, tatizo ni kulipa gharama za mtu ambaye atakuwa radhi kutoa ini” Yasmin alimjibu.
“Basi itakupasa kutoa ini lako”
“Hilo ndilo nililolifikiria lakini bado tatizo litakuwa gharama, hawatoi ini bure kuna gharama za kulipia pia” Yasmin alimwambia Brian.
“Kwa hiyo shida yako ni fedha?”
“Ndio” Yasmin alijibu.
Brian akakaa kimya kwa muda huku akimwangalia Yasmin, uso wa Yasmin ulionyesha dhahiri kwamba kwa wakati huo alikuwa akihitaji sana fedha. Brian hakujua ni aina gani ya msaada ambo alitakiwa kumsaidi, hakuwa na fedha katika kipindi hicho, fedha zake zote zilikuwa katika akaunti yake. Kwa kile kitendo alichokifanya Yasmin cha kuwaokoa maisha yao, aliona dhahiri kwamba kumsaidia binti huyo kiasi hicho cha fedha kisingekuwa kinatosha kusema asante.
Wazo jingine likamjia kichwani. Tayari alikuwa na uhakika kwamba Yasmin alikuwa akifahamiana sana na wale watu, kwa hiyo mpaka kipindi hicho alichokuwa akikitaka ni kuomba msaada wa maswali mengi ambayo yalikuwa yakimtatiza kichwani. Ni kweli kwamba alikuwa akiifahamu sehemu ambayo Wamarekani na Waingereza walipokuwa wakipelekwa jijini Baghdad mara baada ya kukamatwa ila alihitaji kuzifahamu sehemu nyingine zaidi.
“Kuna kitu nitahitaji unaisaidie” Brian alimwambia Yasmin.
“Kitu gani?”
“Wamarekani wanapotekwa hupelekwa wapi?” Brian alimuuliza.
“Wengi huwekwa hapa hapa Baghdad ila wengine hupelekwa Karadah, kusini mwa nchi hii ya Iraq” Yasmin alimwambia.
“Kwa nini wanatenganishwa hivyo?”
“Kwa sababu ya usalama tu ila mara nyingi watu ambao hupelekwa huko basi huwa katika hatua za mwisho za kuuawa” Yasmin aliwaambia.
“Ni lazima twende huko. Tena sasa hivi ikiwezekana” Brian alimwambia Yasmin ambaye alionekana kushtuka.
“Twende sasa hivi?”
“Ndio”
“Hapana. Hiyo ni sehemu hatari sana”
“Hata kama. Ni lazima twende huko” Brian alimwambia Yasmin.
“Na vipi kuhusu msaada ninaotaka mnipatie?” Yasmin aliuliza.
“Tukirudi nitakusaidia na mdogo wako kurudi katika hali ya afya njema” Brian alimwambia Yasmin.
“Hapana. Nitakuamini vipi?”
“Kama ulivyotuamini na kuja kutuokoa” Brian alimwambia Yasmin.
Maneno ambayo alikuwa akiongea Brian kwa wakati huo yakaonekana kuwachanganya kupita kawaida, alionekana kuwa king’ang’anizi sana. Hakuijua sehemu hiyo ilikuwa na ulinzi wa namna gani mpaka kufanya kutamani kwenda sehemu hiyo. Kadri Yasmin alipokuwa akizidi kumkataza kwenda kule lakini Brian hakutaka kuelewa kitu chochote kile, alikuwa aking’ang’ania waondoke hapo Wahit na kuelekea Karadah ndani ya jiji hilo hilo la Baghdad.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 8
WHATSAPP: 0758860093

Jabrouz alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kupewa taarifa kwamba watu wake walikuwa wameuawa na wale watu ambao alitegemea kwamba wangechinjwa kutoroka. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka kwa hasira, hakujua ni kwa namna gani watu wale walishindwa kuwadhibiti Brian na Erick mpaka kuwashinda nguvu na hivyo kutoroka kwa kuua watu wengi.
Alichokifanya mahali hapo mara baada ya kupewa taarifa ile ni kuanza kuondoka na kuelekea katika jengo lile. Kila kitu ambacho alikuwa ameambiwa ndicho ambacho alikuwa amekutana nacho huko. Uso wake ukakunjamana kwa hasira, kijasho chembamba kikaoekana kikianza kumtoka huku akikuja ngumi.
Akaawaagiza watu wake wauchukue mkanda wa kamera ambao ulikuwa umechukuliwa video kidogo ungeweza kumpa majibu ya kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Mkanda ukachukuliwa na kisha kukabidhiwa mkononi mwake.
Safari ya kuelekea sehemu ilipokuwa makao yao makuu kuanza. Alipofika hakutaka kuchelewa, akauchukua ule mkanda na kuuweka kwenye deki ya televisheni na kisha kuanza kuuangalia.
Aliona vizuri kabisa katika kipindi kile ambacho Brian alikuwa ameshikwa huku akitaka kuchinjwa. Mara milio ya riasi ikaanza kusikika mahali hapo na watu wote kuuawa pamoja na watu ambao walikuwa wakitaka kumchinja Brian. Mkanda haukukatika, bado ulikuwa ukiendelea kuonyesha. Mara Yasmin akaonekana mahali hapo akimfuata Brian na kuanza kumuinua huku akizikusanya bunduki ambazo zilikuwa mahali hapo.
Jabrouz hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali pale, hakuamini kama mtu ambaye alikuwa amemuamini sana, Yasmin ndiye ambaye alikuwa amefanya jambo kama lile. Kwake, huo ukaonekana kuwa usaliti mkubwa, hakuamini kama Yasmin angeweza kumsaliti kwa namna ile. Alichokifanya huku akionekana kuwa na hasira nyingi, akawaita vijana wake mahali hapo na kuwapa amri moja tu.
“Nataka ndani ya masaa mawili Yasmin awe ameuawa na kichwa chake kiletwe mezani kwangu” Jabrouz aliwaambia watu wake.
“Sawa mkuu” Vijana wale walijibu na kisha kutoka ndani ya nyumba ile na kuanza kuelekea katika nyumba ambayo alikuwa akiishi Yasmin.
Jabrouz akakaa kitini huku akizishika shika ndevu zake, kichwa chake kilikuwa kimechanganyikiwa sana, hakuamini kama kweli Yasmin angekuja kumsaliti kwa namna ile kwani ndiye alikuwa mwanajeshi wake ambaye alikuwa akimuamini kupita kawaida.
“Nitakitaka kichwa chake tu” Jabrouz alijisemea huku akijipiga ngumi pajani mwake.
*****
Magari yalikuwa yakiendeshwa kwa mwendo wa kasi kuelekea katika nyumba ambayo alikuwa akiishi Yasmin. Vichwani mwao kwa wakati huo walikuwa na kitu kimoja tu ambacho kamwe wasingeweza kukisahau kabisa, kumuua Yasmin na kukipeleka kichwa chake katika mikono ya kiongozi wao, Jabrouz. Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida huku wakiziandaa bunduki zao vilivyo.
Watu ambao walikuwa barabarani walipokuwa wakiyaona magari hayo mawili yakija kwa kasi, wakasogea pembeni na kuyaruhusu kupita. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuishangaa sana hali hiyo kwani ilikuwa imekwishazoeleka hasa ndani ya jiji hilo la Baghdad.
“Mlimuelewa mkuu?” Jamaa mmoja aliwauliza wenzake.
“Ndio”
“Alisema nini?”
“Tumuue Yasmin”
“Kingine?”
“Tumpelekee kichwa chake”
“Sawa sawa. Hakuna huruma huku. Mmesikia?”
“Ndio”
Walichukua muda wa dakika kumi na tano na ndipo wakafika ndani ya eneo la nyumba hiyo, kwa kasi ya ajabu tena hata magari hayo hayajasimama, wakarukia chini na kuanza kusogea ndani ya nyumba ile kwa mwendo wa tahadhari kwani walijua fika kwamba Yasmin haku mtu wa kumletea mchezo kabisa. Wakaanza kuufungua mlango na kisha kuingia ndani ya nyumba ile huku wengine wakiwa wameizunguka nyumba ile kwa nje.
Wakaanza kuinia katika kila chumba ndani ya nyumba ile, hakukuwa na mtu yeyote yule. Kila mmoja alionekana kutokuelewa kabisa, walijua fika kwamba Yasmin alikuwa amekwenda nyumbani kwake, sasa kwa nini wakati huo hakuwa huko? Tena mbaya zaidi hata mdogo wake, Rahim hakuwa akionekana kitandani na wakati alikuwa mgonjwa mahututi.
Walichokifanya ni kupiga simu kwa Jabrouz na kumpa taarifa juu ya hali ambayo walikuwa wamekutana nayo ndani ya nyumba ile. Jabrouz akachanganyikiwa, tayari Yasmin akaonekana kumzidi ujanja hadi yeye mwenyewe.
“Mnasemaje?” Sauti ya Jabrouz ilisikika ikiuliza kwa hasira.
“Hayupo”
“Hata mdogo wake?”
“Ndio. Wote hawapo” Jamaa yule alijibu.
“Hakikisheni mnamtafuta na kumkamata. Msipomkamata huku msije kwa sababu naweza nikawaueni kwa kukosa umakini kazini” Jabrouz alisema kwa hasira na kisha kukata simu.
Moja kwa moja wakatoka ndani ya nyumba ile na kuelekea nje. Wakaanza kuangalia huku na kule lakini hakukuwa na dalili za uwepo wa Yasmin mahali pale. Walichokifanya ni kuelekea nyumba ya jirani na kisha kuwauliza. Kutokana na woga ambao walikuwa nao watu hao ambao waliulizwa, wakajikuta wakitoa maelekezo ya kutosha kabisa.
“Wameelekea katika njia hii ya kwenda Karadah”
“Walikuwa wawili au zaidi?”
“Walikuwa wanne ila mdogo wake alikuwa amembeba”
“Sawa. Tunashukuru kwa msaada wao”
Wote wakaingia ndani ya gari, tayari akili zao ziliwaambia kwamba katika kipindi hicho Yasmin alikuwa njiani kuelekea Karadah. Mioyo yao ilikuwa na wasiwasi zaidi, walijua fika kwamba kulikuwa na uwezekano wa Yasmin kuelekea katika kambi yao ya kuwahifadhi mateka iliyokuwa huko Karadah na kisha kuwaua watu waliokuwa huko.
Walichokifanya ni kuwapigia simu watu ambao walikuwa katika kambi hiyo na kuwapa amri kwamba kama Yasmin angefika mahali hapo, auawe kwani hilo ndilo lilikuwa agizo kutoka kwa mkubwa wao, Jabouz ambaye alikuwa na hamu ya kukiona kichwa cha Yasmin kikiletwa mezani kwake.
Waliendelea na safari na baada ya muda wa dakika kumi wakaanza kuingia katika mji mdogo wa Karadah. Machoyao hayakutulia, walikuwa wakiangalia huku na kule kuona kama wangeweza kuliona hata gari ambalo alikuwa akilitumia Yasmin katika mizunguko yake ya kila siku.
“Hebu rudi nyuma” Jamaa ambaye alionekana kuwa kiongozi ambaye alikaa mbele alimwambia dereva ambaye akalisimamisha na kuanza kulirudisha nyuma.
“Lile pale. Gari lake lile pale” Kiongozi yule alisema huku akiichukua bunduki yake.
Wote wakaanza kuteremka chini na kuanza kuelekea katika sehemu ile ambayo ilikuwa na gari lile. Kitu cha kwanza wakaanza kuliangalia gari lile, lilikuwa ni gari ambalo alikuwa akilitumia Yasmin. Wakachungulia ndani ya gari, hawakuona mtu yeyote yule. Vichwa vyao vikajua kwamba Yasmin alikuwa amefika mahali hapo na hivyo kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Walichokifanya ni kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata na kisha kuusukuma mlango ambao ukafunguka na kisha kuingia ndani huku wakitanguliza bunduki zao mbele. Ndani, wakinamama pamoja na watoto wao ndio ambao walikuwa wamekaa huku wakiangalia televisheni. Kila mmoja akaonekana kushtuka, hawakuamini kama kuna watu wangeingia mahali pale huku wakiwa na bunduki mikononi.
“Wako wapi?” Kiongozi yule aliuliza kwa sauti kubwa iliyojaa mikwaruzo.
“Wakina nani?” Mwanamke mmoja aliuliza huku akionekana kuwa na woga.
Hawakutaka kuongea zaidi, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika vyumba vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba watu ambao walikuwa wakiwatafuta walikuwa ndani ya nyumba ile. Waliingia ndani ya chumba kimoja mpaka kingine lakini kote huko hawakuambulia kitu jambo ambalo lilionekana kuwashangaza sana.
“Wako wapi?” Kiongozi yule aliuliza huku akiwa na hasira zaidi.
“Wakina nani?” mwanamke yule aliuliza swali ambalo lilionekana kuwakasirisha zaidi.
Walichokifanya ni kumuinua mwanamke yule na kisha kuanza kuelekea nae nje na kisha kumuonyshea gari lile. Wote ndani walibaki kimya, uwepo wa bunduki mbele ya nyuso zao ulionekana kuwatisha kupita kawaida. Mwanamke yule akaliangalia lile gari, alionekana kushtuka kwani hakujua kama nje ya nyumba ile kungekuwa na gari ambalo lilipakiwa.
“Wako wapi waliokuja na gari hili?” Kiongozi yule aliendelea kuuliza.
“Sijui. Hatujui lolote kuhusiana na gari hili” Mwanamke yule alisema huku woga ukionekana dhahiri usoni mwake.
Jibu ambalo alikuwa amelitoa likaonekana kumkasirisha kila mmoja. Ingwezekana vipi mtu kupaki gari ndani ya uwanja wa nyumba hiyo huku wenye nyumba wakiwa hawasikii kitu chochote kile? Iliwezekana vipi hata muungurumo wa gari hawakuusikia? Kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza mahali pale, walimuona mwanamke yule kuwadanganya kwa kuwaficha kitu fulani.
“kwa hiyo haufahamu kitu chochote kuhusiana na gari hili?” Kiongozi yule alisema huku akiikoki bunduki yake.
“Sifahamu” Mwanamke yule alijibu huku akiapa.
Kiongozi yule akamnyooshea bunduki mwanamke yule huku akimsisitizia kumwambia ukweli juu ya watu ambao walikuwa wamekuja ndani ya eneo la nyumba ile na kulipaki gari lile mahali pale. Japokuwa alikuwa amenyooshewa bunduki lakini mwanamke yule alikuwa akisisitiza kwamba hakuwa amemuona mtu yule ambaye alikuwa amekuja mahali pale na kulipaki gari lile.
“Nakuhesabia mpaka tatu nitataka uniambie wapo wapi” Kiongozi yule alimwambia mwanamke yule ambaye alianza kulia kama mtoto huku akiendelea kusisitiza kwamba hakuwa amemuona mtu ambaye alipaki gari lile ndani ya eneo la nyumba yake.
“Moja” kiongozi yule alianza kuhesabu lakini mwanamke yule aliendelea kusisitiza kwamba hakumuona mtu aliyepaki gari lile mahali pale.
“Mbili” Kiongozi aliendelea.
“tat….” Kiongozi alisema na mara ghafla milio ya risasi ikaanza kusikika mahali pale.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 9
WHATSAPP: 0758860093

Brian hakuonekana kuwa muelewa hata kidogo, bado alikuwa aking’ang’ania waelekee Karadah kwa ajili ya kuangalia sehemu ambazo wazungu walikuwa wamehifadhiwa.
Hakukuwa na mtu aliyekuwa na nguvu za kumzuia kwani jambo lile ndilo ambalo alikuwa akilitaka litokee kwa wakati huo. Japokuwa Yasmin alikuwa aking’ang’ania zaidi na zadi kwamba sehemu ile ilikuwa ni ya hatari, mwisho wa siku akakubaliana nae na kisha kuanza kuelekea Karadah.
Alichokifanya Yasmin ni kumbeba mdogo wake, Rahim na kuanza kuondoka ndani ya chumba kile na kutoka nje. Muda wote macho yao yalikuwa yakiangalia huku na kule, hawakuwa na amani kabisa, walikuwa wakifahamu fika kwamba kwa wakati huo walikuwa wakitafutwa sana na Waarabu ambao walikuwa wakitaka kuwaua.
Mara baada ya kufika nje ya nyumba ile, wote wakaingia garini na Yasmin kushikilia usukani na kisha kuanza safari ya kuelekea Karadah. Watu waliokuwa pembeni ya eneo lile wakabaki wakiwashangaa tu, hawakuelewa mahali ambapo Yasmin alikuwa amewatoa watu wale ambao walionekana kuwa wageni machoni mwao.
Vumbi jingi likatimka mahali hapo, Yasmin akalitoa gari katika eneo hilo kwa mwendo wa kasi ambao ulimshangaza kila mtu. Ndani ya gari, Yasmin alionekana kuwa na wasiwasi juu ya maisha yake, maisha ya Brian na Erick, aliitambua vizuri sana kambi iliyokuwa Karadah, ilikuwa moja ya kambi ambayo haikuhitaji kuletewa masihala hata kidogo.
Mara baada ya dakika kadhaa wakawa wamekwishafika katika mji wa Karadah. Alichokifanya Yasmin ni kulipeleka gari lile katika eneo la nyumba moja na kisha kulipaki.
Wote wakateremka garini huku Yasmin akimchukua mdogo wake na kumbeba. Brian na Erick walidhani kwamba ndani ya nyumba hiyo ndio ambayo walitakiwa kuingia, lakini kitu cha ajabu wakashangaa kumuona Yasmin akianza kuelekea sehemu nyingine.
“Unakwenda wapi?” Brian alimuuliza Yasmin ambaye alikuwa akizidi kuondoka bila kujibu kitu chochote kile.
Walichokifanya ni kuanza kumfuata Yasmin ambaye safari yake iliishia katika geti moja la hoteli ambayo wala haikuwa mbali kutoka katika nyumba ile waliyokuwa wamepanga. Moja kwa moja Yasmin akamfuata dada aliyekuwa mapokezini na kuanza kuongea nae, alipomaliza, akauingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi fulani cha fedha na kumkabidhi.
Hawakutakiwa kubaki mahali hapo, wakaanza kuondoka kuelekea katika chumba ambacho Yasmin alikuwa amepewa. Dada wa pale mapokezini hakutakiwa kwenda pamoja nao, kwa sababu namba zilikuwa milangoni, wakaona ingekuwa vizuri kama wangekwenda wenyewe.
Wakapandisha ghorofa ya kwanza mpaka ya pili na kisha kuanza kukitafuta chumba namba ishirini walichokuwa wamepangiwa, walipoingia ndani ya chumba hicho, Yasmin akamlaza Rahim kitandani na kuelekea dirishani. Macho yake akayapeleka katika gari lao ambalo walikuwa wameliacha upande wa pili katika nyumba ambayo wala haikuwa mbali kutoka pale walipokuwa.
“Vipi” Brian aliuliza huku akimfuata.
“Najaribu kuliangalia gari letu. Kama kweli tunatafutwa, wanaweza wakaja” Yasmin alimwambia Brian.
Brian akasogea pale dirishani na kisha nae kuanza kuangalia nje, gari lile lilikuwa palepale huku kukiwa hakuna dalili za kuonyesha kama watu ambao walikuwa ndani ya nyumba ile walifahamu kama kulikuwa na gari ambalo lilikuwa limekiwa nje ya nyumba yao. Wala hazikupita dakika nyingi, magari mawili yakaonekana yakipita mahali hapo na kisha kusimamishwa na kuanza kurudishwa nyuma.
Waarabu nane ambao walikuwa na bunduki mikononi mwao wakateremka na kuanza kulifuata gari lile na kuchungulia ndani, walipoona hakukuwa na mtu wakaanza kuingia ndani ya nyumba ile.
Walikaa kwa sekunde kadhaa na kisha kutoka na mwanamke mmoja ambaye jamaa mmoja aliyeonekana kuwa kiongozi akionekana kumlazimisha mwanamke yule kusema kitu fulani.
Waliendelea kumwangalia zaidi na zaidi, mwanamke yule alikuwa akilia kama mtoto hasa mara baada ya kuona amenyooshewa bunduki.
Alichokifanya Yasmin, akachukua bunduki yake na kisha kuwaelekezea waarabu wale ambao walikuwa wakimwangalia mwanamke yule huku wakionekana kuwa na hasira.
“Utaweza kumpiga risasi kweli?” Brian alimuuliza Yasmin.
“Usijali. Shabaha niliyo nayo ni kubwa sana” Yasmin alijibu.
Brian hakutaka kubaki hivi hivi, nae akachomoabunduki yake kutoka kiunoni na kuwalekezea vijana wale. Kila mmoja alikuwa amejiandaa kuwafyatulia risasi.
Baada ya sekunde chache, wakaanza kuwafyatulia risasi waarabu wale. Hakukuwa na risasi yoyote ambayo ilimkosa mtu yeyote, zote ambazo zilizokuwa zimefyatuliwa zilikuwa zimeingia katika miili yao na kuanguka.
Waarabu wote walikuwa chini, wengine walikuwa wakirusha rusha migu na mikono yao huku na kule na wengine wakiwa wametulia kabisa. Walipoona kwamba kazi yao imekamilika, wakatoka dirishani pale na kisha kushusha pazia.
Watu wakaanza kujaa katika eneo lile na kisha kuanza kuiangalia miili ile ya watu wale, kila mmoja alishindwa kufahamu sehemu ambayo risasi zile zilikuwa zimetoka japokuwa kuna kipindi walikuwa wamesikia milio ya risasi.
*****
Waliendelea kukaa ndani ya chumba kile hotelini kwa takribani dakika kumi huku Brian akiwapigia simu wakuu wake wa kitengo cha upelelezi cha F.B.I na kuwaambia kuhusu kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Iraq hasa ndani ya jiji hilo la Baghdad.
Kila taarifa ambayo alikuwa ameitoa mahali hapo ilikuwa ikilingana sawa sawa na kila kilichokuwa kikiendelea.
Katika kipindi chote hicho Yasmin alikuwa akimwangalia mdogo wake, rahim ambaye alikuwa kimya kitandani, moyo wake ulikuwa ukimuuma sana, hakuamini kama mpaka katika kipindi hicho alikuwa amekosa fedha za kuweza kumtibia mdogo wake ili arudiwe katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa zamani kabla ya ugonjwa ule kumshika.
Waliendelea kukaa zaidi na ndipo miungurumo ya magari ikaanza kusikika nje, wakasimama na kisha kufungua kidogo pazia na kuanza kuangalia nje. Magari mawili ya polisi yalikuwa yamepaki katika eneo lile ambalo lilikuwa na miili ile na kisha kuanza kuipakiza ndani ya magari ambayo walikuwa wamekuja nayo mahali pale.
Baada ya dakika kadhaa kuipakiza miili ile, wakaingia garini na kisha kuondoka mahali hapo huku wakiwa wamechukua maelezo ya kutosha kutoka kwa watu ambao walikuwa wakiishi ndani ya nyumba ile pamoja na majirani. Hali ilipoonekana kuwa kimya, Brian akaanza tena kulalamika kwamba iliwapasa kuelekea katika sehemu ambayo wazungu walikuwa wakitekwa na kuhifadhiwa hapo Karadah.
“Ni lazima twende huko” Brian aliwaambia.
“Lakini mbona unakuwa kama si muelewa?” Yasmin alimuuliza huku akionekana kukasirika.
“Kama sehemu yenyewe ni ya hatari, haina budi ukabadilisha mawazo yako” Erick aliingilia na kumwambia Brian.
Katika kila kitu ambacho kiliongelewa mahali hapo kikaonekana kutokueleweka kwa Brian, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuelekea katika kambi ya mateka iliyokuwa hapo Karadah.
Malumbano yakaendelea zaidi na zaidi lakini mwisho wa yote, Brian akaonekana kushinda na hivyo wote kujiandaa na safari hiyo ya hatari ya kwenda katika kambi hiyo.
Hawakutaka kwenda huko pamoja na Rahim, walitakiwa kumuacha ndani ya chumba kile na kisha wao kutoka nje. Brian akachukua simu yake na kisha kuanza kupiga katika kitengo cha upelelezi cha F. B. I na kisha kuanza kuwaambia kwamba ilikuwa ni lazima wafike Karadah haraka iwezekanvyo.
“Hivi kuna ulazima wa mimi kwenda huko? Naona kama ningebaki na mgonjwa” Erick aliuliza.
“Umuhimu wako upo. Tena mkubwa sana hata zaidi ya Yasmin” Brian alijibu.
“Kuna umuhimu gani sasa wa mimi kuwa huko?”
“Kwa ajili ya kuandika habari. Itakupasa kuandika kila utakachokiona” Brian alimjibu Erick.
Erick akabaki kimya, moyo wake haukujisikia amani kabisa, maisha ambayo alikuwa akipitia katika jiji la Baghdad yalionekana kuwa maisha ambayo yalijaa vitisho vikubwa sana. Alitamani kumkatalia Brian kwenda kule walipokuwa wakielekea lakini kwake likaonekana kuwa jambo gumu sana kwani angeonekana kuwa msaliti mkubwa.
Walitembea kwa mwendo wa dakika arobaini na tano na ndipo kwa mbali mbele yao kukaonekana kuwa na jengo kubwa. Alichokifanya Brian ni kupiga tena simu na kisha kutoa maelekezo juu ya mahali ambapo walitakiwa kufika mara baada ya kuingia nchini Iraq. Wakaanza kupiga hatua kuelekea katika jengo lile huku wakijificha ficha.
“Tutaingia salama na kutoka salama” Brian aliwaambia wenzake huku wakizianaa bunduki zake.
“Ila lengo kubwa la kwenda mule ndani ni nini hasa?” Erick aliuliza.
“Kuwaokoa wenzetu na kisha kuondoka nao” Brian alijibu.
“Je tukishindwa kuwaokoa?”
“Basi tutakufa” Brian alimjibu Erick ambaye woga aliokuwa nao ukizidi kuongezeka.
Kwake, Brian alionekana kuwa mtu wa tofauti kabisa, mtu ambaye hakuwa akiogopa kufa hata mara moja. Muda wote Brian alikuwa akionekana kujiamini kupita kawaida, kwake kifo wala hakuonekana kukijali sana, moyoni aliamini kitu kimoja tu kwamba kila nafsi duniani ingeonja mauti.

Je nini kitaendelea?
 
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
HADITHI: BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD 10
WHATSAPP: 0758860093

Taarifa zilikuwa zimetolewa ndani ya shirika la kipelelezi la kijasusi la F.B.I lililokuwa nchini Marekani. Taarifa ile ilionekana kumfurahisha kila mmoja, kujulikana kwa mahali ambapo wazungu walipokuwa wakipelekwa nchini Iraq ndani ya jiji la Baghdad zilionekana kuwafurahisha sana.
Kwa haraka haraka maandalizi yakaanza kufanyika, hawakutakiwa watu kutoka nchini Marekani ndio waelekee huko bali Wamarekani ambao walikuwa nchini Iraq ndio ambao walitakiwa kwenda huko. Simu zikapigwa na kila kitu kuelezwa, hakukuwa na mtu wa kupinga na kwa sababu watekaji walikuwa wakitumia silaha, wanajeshi wa Marekani ndio ambao walitakiwa kutumia bunduki katika kufanya uvamizi ndani ya maeneo hayo na kisha kuanza kuua huku lengo kubwa likiwa ni kutaka kuwaokoa watu wao.
Hakukuwa na muda wa kuchelewa, simu ambazo zilikuwa zimepigwa kwa wanajeshi ambao walikuwa nchini Iraq ndizo ambazo ziliwafanya kufanya haraka haraka kwa ajili ya kwenda kufaya uvamizi katika sehemu hizo ambazo walikuwa wameelekezwa na Brian ambaye alikuwa huko.
Wanajeshi wale wakatoka katika vituo vyao vilivyokuwa hapo Baghdad na kwenda katika mji wa Wassit ambao ulikuwa kaskazini mwa jiji hilo. Mwendo wa magari yao ulikuwa ni wa kasi kupita kawaida, hawakutaka kuchelewa hata mara moja. Kila kitu ambacho walikuwa wakitaka kukifanya mahali hapo walikuwa wakikifanya kwa haraka haraka.
Raia wakajua kulikuwa na kitu ambacho kilitokea, haikuwa mara zote ambazo wanajeshi wa Marekani walikuwa wakiendesha gari kwa mwendo wa kasi namna ile. Watu wakajiweka pembeni na kisha kuyaangalia magari yale ambayo yalikuwa yakikimbia kupita kawaida.
Mara baaba ya kufika katika mji mdogo wa Wassit, hapo hapo wakateremka na kuanza kuelekea katika nyumba ambayo walikuwa wameelekezwa Kwa kutumia darubini ambazo walikuwa nazo waliweza kuwaona baadhi ya waarabu wakitembea tembea ndani ya jumba lile huku wakiwa na bunduki mikononi mwao.
Mkuu wa kikosi kile akanyoosha mkono wake juu na kisha kuvikunja vidole vyote na kuviacha viwili vikiwa vimesimama na kuvipeleka mbele na nyuma hali iliyomaanisha kwamba wanajeshi wawili tu ndio ambao walitakiwa kusogea mbele zaidi. Kama alivyotoa ishara ile na ndivyo ilivyokuwa, wanajeshi wawili wakaanza kusogea mbele zaidi kuifuata jengo lile na kisha wengine kufuata.
Hawakuwa na muda wa kuchelewa, hapo hapo risasi zikaanza kusikika na waarabu wengi kuanguka chini. Kelele ziliendelea kusikika kutoka katika vyumba ambavyo mateka walipokuwa ndani ya jengo hilo. Waarabu wakaonekana kumalizika kupita kawaida, uvamizi ambao walikuwa wameutumia wamarekani katika kipindi hicho ulionekana kuwa uvamizi wa kushtukiza sana ambao uliwafanya waarabu wengi kuuawa kwa sababu ya kukosa maandalizi ya uvamizi ule.
“Damu zilikuwa zimetapakaa katika jengo zima, moja kwa moja wanajeshi wale wa Kimarekani wakaanza kuingia ndani zaidi katika jengo lile. Bado walikuwa wakiendelea kuua zaidi na zaidi mpaka walipovifikia vyumba vile na kisha kuwatoa watu wao ambao walionekana kuwa katika hali isiyo ya kawaida, miili yao ilikuwa imeanza kukosa nguvu.
“Kuna wengine?” Mwanajeshi mmoja aliuliza.
“Ndio. Kuna jengo moja lipo Karadah”
“Twendeni sasa hivi”
“Hapana. Kuna wenzetu washakwenda huko”
****
Bado Brian, Erick na Yasmin walikuwa wakiendelea kulisogelea lile jumba kwa tahadhari kubwa sana. Walikuwa makini kuliko katika kipindi chochote kile. Erick alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa lakini kwa Brian hali ilionekana kutokuwa ya wasiwasi kabisa. Kwake, aliamini kwamba roho ya binadamu ilikuwa ni lazima ionje mauti hata kama kuna kitu gani kitatokea.
Waarabu waliokuwa na bunduki walikuwa wakionekana nje ya jengo lile, walichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kuwalenga na risasi. Kila risasi ambayo ilikuwa ikitoka mahali hapo, haikupotea, ilikuwa ikimuingia mtu mmoja. Waliendelea kuwapiga risasi na ndipo kuanza kukimbia kwa kasi kulifuata geti la jumba lile na kuingia ndani.
Hakukuwa na mtu yeyote katika eneo la nyumba ile jambo ambalo kila mmoja akabaki akishangaa, haikuwezekana kutokuwa na mtu yeyote yule, hiyo ilimaanisha kwamba wale walinzi ambao walikuwa wamewaua pale getini ndio walikuwa watu pekee ndani ya jengo lile? Kila walipokuwa wakijiuliza mahali hapo walikosa jibu.
Hawakutaka kuendelea kujiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu, walichoamua kwa wakati huo ni kusonga mbele tu. Wakaanza kupandisha ngazi huku bunduki zao zikiwa tayari kwa kitu chochote kile ambacho kingetokea mahali hapo. Ukimya ulikuwa umetawala kupita kawaida, hakukuonekana kuwa na mtu yeyote yule jambo ambalo lilionekana kumshangaza hata Yasmin mwenyewe.
Wakaufikia mlango wa chumba kimoja na kuufungua na kisha kuingia ndani. Chumba kilikuwa kikubwa sana ambacho kilikuwa na mateka wengi sana. Jambo la ajabu ambalo lilionekana kuwashangaza, mateka wote walikuwa kimya jambo ambalo halikuwa la kawaida. Huku wakiangalia kwa nyuso zilizojaa maswali, mara kundi la waaarabu ambalo lilikuwa limejificha katika kila kona ndani ya jumba lile likaibuka na kuwaweka chini ya ulinzi.
Kwa kila tukio ambalo lilikuwa likionekana mahali hapo lilikuwa ni kama filamu ya maigizo ambazo mara kwa mara zilikuwa zikichezwa nchini Marekani. Idadi ya waarabu ilikuwa kubwa sana jambo ambalo likawafanya kuziachia bunduki zao na kisha kunyanyua mikono yao juu. Hawakuwa na jinsi, walifika mahali hapo kwa ajili ya kuokoa mateka lakini mwisho wa siku nao wakajikuta wakiwa mateka.
Bunduki zao zikachukuliwa na kisha kufungwa kamba na kutolewa nje katika uwanja mkubwa wa jumba lile. Kwa haraka sana bila kupoteza muda simu ikapigwa kwa Jabrouz ambaye ndani ya dakika tano akafika mahali hapo huku uso wake ukionekana kuwa na tabasamu. Akaanza kupiga hatua kuwafuata, alipowafikia, akaanza kumpiga vibao Yasmin kitendo ambacho kilimuuma sana Brian.
“Nahitaji vichwa vyao wote watatu” Jabrouz huku akionekana kukasirika. Hakukuwa na sababu ya kusubiri, mkuu alikuwa amekwishaongea kitu kimoja ambacho kilitakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka sana. Wote wakachukuliwa huku wakiwa wamefungwa kamba kwa nyuma. Muda wote Erick alikuwa akilia, hakuamini kama mwisho wake ungekuwa namna ile, kuchinjwa nchini Iraq ndani ya jiji kubwa la Baghdad.
“Anza na Yasmin” Jabrouz alitoa amri.
Kila klichoongelewa hapo ndicho ambacho kikafanyika, Yasmin akalazwa kifudifudi na kisha mwanaume aliyekuwa na kisu kikali kukaa juu ya mgongo wake. Yasmin alikuwa akipiga kelele za kuomba msamaha lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kujali. Wanaume watatu ambao walikuwa wamemshika miguu yake walikuwa wamemshika vilivyo, kisu kikaanza kupitishwa shingoni mwake, damu zikaanza kutoa. Ndani ya sekunde ishirini tu, kichwa kilikuwa kipo mkononi mwa mchinjaji.
Ile ilionekana kuwa kama ndoto moja kubwa na ya kutisha ambayo Erick hakudhani kama alikwishawahi kuiota. Kuliona tukio la mtu akichinjwa mbele ya macho yake lilionekana kumuogopesha kupita kawaida. Akabaki akitetemeka tu. Mwili wa Yasmin ulikuwa ukijirusha jirusha pale chini huku damu zikitapakaa mahali pale.
Mtu ambaye alifuata kwa wakati huu alikuwa Brian. Brian alionekana kutokuhofia kitu chochote kile. Hata alipolazwa kifudifudi na kisha kukaliwa juu huku akishikwa na watu wawili kwa juu, hakuleta usumbufu wowote ule. Mwanaume yule ambaye alikuwa na kisu mkononi akamkalia kwa juu na kisha kukipeleka kisu kile shingoni mwa Brian.
Kama kawaida yake, kisu kile kikaanza kuikata shingo yake, damu zilikwishaanza kuonekana. Mara ghafla katika hali ambayo hakukuwa na mtu ambaye aliifikiria, risasi zikaanza kusikika mahali hapo huku mchinjaji akiwa mtu wa kwanza kupigwa risasi ya kichwa. Kila mmoja akaonekana kuchanganyikiwa, hawakuwaona wapigaji, mapigano yakaanzia hapo.
Ilikuwa ni vita kubwa, Erick alikuwa amelala chini huku akimwangalia Brian ambaye muda wote alikuwa akitabasamu huku akitokwa na damu shingoni mwake kutokana na kisu kumkata kidogo. Wamarekani ambao walikuwa wamevamia mahali hapo walionekana kujiandaa na vita.Risasi zilipigwa mfululizo na ndani ya nusu saa, hakukuwa na mwarabu yeyote ambaye alikuwa hai, wote walikuwa wamepigwa risasi na kufa akiwepo Jabrouz, mkuu wa jeshi la waasi nchini Iraq.
“How do you feel? (Unajisikiaje?)” Mwanajeshi mmoja ambaye alikuwa akiongoza kikosi hicho cha uvamizi ailimuuliza Brian.
“Take me to the hospital (Nipelekeni hospitalini)” Brian aliogea kwa shida.
Kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea jijini Baghdad kikaonekana kuwa historia ndefu ambayo ilijaa vitisho vikubwa katika maisha yake. Mateka wote ambao walikuwa wametekwa wakaokolewa na yale majumba mawili kati ya lile la Wassit na Karadh kufungwa kabisa. Brian na Erick wakarudi nchini Marekani huku wakiwa pamoja na Rahim ambaye walimuona kutokuwa na msaada kabisa.
Baada ya kufika nchini Marekani, matibabu ya ini la Rahim yakafanyika na uwekewa ini jingine kitu ambacho kilimrudishia afya njema maishani mwake na Brian kuamua kukaa nae kama shukrani kwa dada yake, Yasmin ambaye alikuwa amewaokoa jijini Baghdad.
Baada ya kurudi nchini tanzania ambako alipokelewa kwa shangwe, Erick akaandika kitabu ambacho kilikuwa kimeelezea kwa kina maisha ambayo alipitia nchini Iraq ndani ya jiji la Baghdad na kukiita BARUA NDEFU KUTOKA BAGHDAD. Kitabu hicho kilichokuwa kimeandikwa kwa lugha tano kilikuwa kimedhaminiwa na mashirika makubwa na kuuzwa duniani kote.
Kilikuwa kitabu ambacho kiliwafumbua macho watu wengi, kilikuwa ni kitabu ambacho kiliwaogopesha sana watu waliokuwa wamekisoma. Ndani ya mwezi mmoja tu, tayari Erick alikuwa ameuza zaidi ya kopi milioni tano duniani kote jambo ambalo lilimfanya kuingiza kiasi kikubwa maishani na kuwa mtu mwenye fedha nyingi ambazo aliamua kufungulia miladi mbalimbali.
Kitabu kile hakikuishia hapo, bado kilikuwa kikizidi kununuliwa zaidi na zaidi na kumuingizia fedha sana ambazo nyingine aliamua kumgawia Brian pamoja na kuendeleza maisha ya Rahim aliyekuwa akiishi nchini Marekani.
Baada ya miezi kadhaa kupita, mke wake, Christina akajifungua mtoto wa kiume ambaye aliamua kumpa jina la Brian, kumbukumbu ya rafiki yake ambaye alikuwa amesaidiana nae kwa kila kitu nchini Iraq ndani ya jijila Baghdad.

MWISHO.
 
Back
Top Bottom