Siku moja mfanyakazi wa Posta
akiwa katika kazi yake ya kupanga
barua alikuta barua moja
imeandikwa "Kwenda kwa
Mwenyezi Mungu". Akashangaa
lakini kwa udadisi akaamua
kuifungua. Ilikuwa imeandikwa:
"Ee Mungu, mimi ni mwanamke
mjane, kikongwe wa miaka 85.
Jana wakati natoka hospitalini
niliibiwa pochi yangu ambayo ndani
yake ilikuwa na akiba yangu ya
muda mrefu sana ya shilingi laki 1.
Kama unavyojua nilikuwa na
mpango wa kuwaalika kina bibi na
wazee wenzangu kwa sherehe ya
kutimiza miaka 85. Hapa nilipo
sijui nitafanya nini. Mimi nimemua
kukuachia wewe kila jambo kwa
sababu sina tena tumaini. Watoto
sina, wajukuu sina, shida tupu,
sina anayenijali na kibaka naye
umeacha hadi akaniibia. Nimeona
tu niandike kukueleza jinsi gani
moyo wangu umeamia. Nisamehe
kama nimekosa. Naomba msaada
wako. Ni mimi mja wako,
Mwagito."
Jamaa aliyekuwa anaisoma
akaguswa sana moyoni,
akawakusanya wafanyakazi wenzake
wakachanga hela ikafika 96,000
wakaituma kwa yule bibi siku ile
ile. Wakawa wana furaha kwamba
wamefanya jambo jema. Siku
zikapita na baada ya mwezi jamaa
akaona tena barua toka kwa yule
yule bibi ikiwa imeandikwa
"Kwenda kwa Mwenyezi Mungu".
Akawakusanya wafanyakazi wenzake
wote akaifungua wakaanza
kuisoma.
"Ee Mungu, sijui nikushukuru vipi
kwa maajabu uliyonitendea.
Nilifanya sherehe nzuri na wazee
wenzangu na nashukuru kwa
kuniwezesha kufurahia siku hizi za
mwisho katika uzee wangu huu na
nimetoa ushuhuda kwa marafiki
zangu juu ya matendo yako
makuu. Hata hivyo hela ilikasoro
shilingi 4,000. Nadhani wizi huo ni
kazi ya wafanyakazi wa Posta
maana ni wezi, walafi na wasio na
huruma hata kidogo., Ni mimi mja
wako Mwagito."
akiwa katika kazi yake ya kupanga
barua alikuta barua moja
imeandikwa "Kwenda kwa
Mwenyezi Mungu". Akashangaa
lakini kwa udadisi akaamua
kuifungua. Ilikuwa imeandikwa:
"Ee Mungu, mimi ni mwanamke
mjane, kikongwe wa miaka 85.
Jana wakati natoka hospitalini
niliibiwa pochi yangu ambayo ndani
yake ilikuwa na akiba yangu ya
muda mrefu sana ya shilingi laki 1.
Kama unavyojua nilikuwa na
mpango wa kuwaalika kina bibi na
wazee wenzangu kwa sherehe ya
kutimiza miaka 85. Hapa nilipo
sijui nitafanya nini. Mimi nimemua
kukuachia wewe kila jambo kwa
sababu sina tena tumaini. Watoto
sina, wajukuu sina, shida tupu,
sina anayenijali na kibaka naye
umeacha hadi akaniibia. Nimeona
tu niandike kukueleza jinsi gani
moyo wangu umeamia. Nisamehe
kama nimekosa. Naomba msaada
wako. Ni mimi mja wako,
Mwagito."
Jamaa aliyekuwa anaisoma
akaguswa sana moyoni,
akawakusanya wafanyakazi wenzake
wakachanga hela ikafika 96,000
wakaituma kwa yule bibi siku ile
ile. Wakawa wana furaha kwamba
wamefanya jambo jema. Siku
zikapita na baada ya mwezi jamaa
akaona tena barua toka kwa yule
yule bibi ikiwa imeandikwa
"Kwenda kwa Mwenyezi Mungu".
Akawakusanya wafanyakazi wenzake
wote akaifungua wakaanza
kuisoma.
"Ee Mungu, sijui nikushukuru vipi
kwa maajabu uliyonitendea.
Nilifanya sherehe nzuri na wazee
wenzangu na nashukuru kwa
kuniwezesha kufurahia siku hizi za
mwisho katika uzee wangu huu na
nimetoa ushuhuda kwa marafiki
zangu juu ya matendo yako
makuu. Hata hivyo hela ilikasoro
shilingi 4,000. Nadhani wizi huo ni
kazi ya wafanyakazi wa Posta
maana ni wezi, walafi na wasio na
huruma hata kidogo., Ni mimi mja
wako Mwagito."