hewizet
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 2,518
- 1,659
samahani kidogo umesemaje eti??CAG ni ofisi katika mtu na sio mtu katika ofisi.
python.
samahani kidogo umesemaje eti??CAG ni ofisi katika mtu na sio mtu katika ofisi.
Tupe sababu za msingi,usiishie kutamka tu.Tanzania nzima INA professor mmoja tu, Prof Assad. Wengine wote ni miyeyusho
Nina Uhuru kamili wa kuandika nitakacho ili mradi sivunji sheria, huna mamlaka yoyote ya kunipangia cha kuandikaType sababu za msingi,usiishie kutamka tu.
Kwani lazima ujibu huku si ungejiandikiaKwani hauna anuani ya Speaker hadi barua uitume humu? Kama hafiki humu ataisoma vipi
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli una uhuru wa kuañdika unachotaka ilimradi huvunji sheria,lakini as a great thinker unapaswa kutupa cream,sio whey.Nina Uhuru kamili wa kuandika nitakacho ili mradi sivunji sheria, huna mamlaka yoyote ya kunipangia cha kuandika
Umesahau mkuu, kuna na leprofeseriii Lipumba.Tanzania nzima INA professor mmoja tu, Prof Assad. Wengine wote ni miyeyusho
Shukrani Kaka yangu Mayalla! Shukrani sanaDu Mkuu Nondo ni nondo kweli, dogo unatisha!.
Naunga mkono hoja 100/100
P
Kwani hauna anuani ya Speaker hadi barua uitume humu? Kama hafiki humu ataisoma vipi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee kwa maneno yako haya nakupa KONGOLE,ni maneno kuntu,maneno yaliyoenda shule.Nondo wewe bado ni kijana mdogo ,ila nadhani umewazidi akili ,watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 50.
Kila nikikaa swali linanijia kichwani ,kwa nini tumefika hapa?
Ina maana maisha yetu yako mikononi mwa watu wachache kiasi hiki?
Hii mamraka ya kufanya ruling juu ya maisha yetu nani kawapa hawa watu?.
Ina maana wao wana roho ngumu kiasi gani ,wasiuogope uma wote huu?
Wana uhakika gani kuwa wana nguvu ya kutosha kuutuliza uma uliokasirika?
Wanadamu wenye busara waliweka katiba na sheria ili ziwe miongozo ya maisha yetu hapa duniani. Sheria hizi zimewalazimisha wanadamu waheshimu haki na utu wa wenzao bila wao kupenda.
Ikiwa binadamu mwenzetu ataamua kwa makusudi kabisa kudhalau katiba na sheria ,nadhani jibu ni rahisi kabisa ,kwamba huyu sasa si binadamu mwezetu ,ameukimbia ubindamu na kuvaa unyama. Na kwa mjibu wa vitabu vya dini sisi binadamu tumepewa mamraka ya kutawala wanyama. Sisi hatuwezi kutawaliwa na wanyama.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru mkuuMzee kwa maneno yako haya nakupa KONGOLE,ni maneno kuntu,maneno yaliyoenda shule.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe umesoma mjulishe Mgogo mwenzio maana yaliyomo ndani ya barua ni kweli kabisa.Kwani hauna anuani ya Speaker hadi barua uitume humu? Kama hafiki humu ataisoma vipi
Sent using Jamii Forums mobile app
For your information, this is a cloistered move, the bigman is behind everything you see/hear. Nonsense.
Kumbe Nondo ana hoja zinazo sound kama hizi,ningewashauri wabunge wetu wamushauri spika atekeleze maswala ya katiba kuhusu CAG
Nakala kwa mwigulu nchema, aone nondo za Abdul Nondo aliye sema amejiteka!Mh.Ndugai,pole na majukumu ya kila siku.
Mimi ni miongoni mwa raia wanaotafakari bila kupata majibu juu ya maamuzi ya bunge lako la kutofanya kazi na CAG
Mh.Spika sitaki kusema kati yako wewe na CAG nani mkubwa kwa mwenzia au nani ana nguvu kisheria,wewe umepewa mamlaka na sheria ya bunge ,yeye amepewa mamlaka ,kinga na katiba na sheria ya ukaguzi wa umma ya 2008 .
Maana nakumbuka ulisema wewe ndiye BOSS wake lakini jambo la kushangaza Bunge kukuondoa wewe kama ni spika ni vyepesi kuliko kuondolewa CAG Assad njia ya kumuondoa ni ndefu mno,leo hii Bunge limekataa kufanya nae kazi Ila bado yupo ofisi.
Mh.Spika jana umesema umesitisha kufanya kazi na Assad sio ofisi ya CAG ,Mh.Spika hoja sio Assad Bunge halijawahi fanya kazi na Asad ,ila Bunge hufanya kazi na CAG . Mgogoro uliopo sio Ndugai na Assad , mgogoro uliopo ni Assad kama CAG na Ndugai kama Spika wa bunge , mgogoro huu ni wa kiofisi ,ofisi ya Bunge na Ofisi ya CAG ,hivyo ukikataa fanya kazi na CAG Assad umekataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG Assad ,nakumbuka CAG hana Naibu .Kinga ya ofisi ya CAG ipo kikatiba kupitia CAG.Ofisi haiwezi kufanya kazi na kuwa na kinga bila CAG,hakuna ofisi ya CAG bila CAG.
Mh.Spika nadhani unamtega Mh.Rais kuwa kisheria sasa anapaswa kuunda tume ya uchunguzi dhidi ya CAG juu ya shutma zako,Mh.Spika hilo sio jambo rahisi sababu shutma dhidi ya CAG zinapaswa kuwa za kikatiba ibara ya 144 (2) ,kama ameshindwa tekeleza majukumu yake, kama amevunja na ameenda kinyume na sheria ya maadili ya watumishi wa umma.
Mh.Spika shutma zako dhidi ya CAG zinaangukia wapi katika sababu hapo juu za kumuondoa?,labda utasema ni kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma .Na je, kusema Bunge ni dhaifu ni kuvunja sheria ya maadili ya viongozi?
Kwa tafsiri nyepesi tume hii kama itaundwa haitakuwa na shutma za kikatiba zakuchunguza ,zaidi ya shutma zako za neno "DHAIFU" .
Mh.Spika yaani Mh.Rais aunde
tume yenye majaji wa mahakama kuu ya ndani na ya nje kutoka nchi ya jumuiya ya madola (Commonwealth) waje kufanya uchunguzi wa shutma dhidi ya CAG kwa kutamka tuu neno dhaifu ?,hakika omba Mungu Mh.Rais asiunde tume hiyo kwa hekma zake kwani itadhihirisha zaidi ya udhaifu wako na namna ambavyo Bunge halina mamlaka ya kumuwajibisha CAG.
Mh.Spika unajua kuwa Spika wa bunge la India (Congress leader) Mr.Kapil Sabal aliibua hoja dhidi ya CAG 2019 February ni pale tuu kulipokuwa na maslahi ya taifa Bunge lao lilimtikisa CAG Rajiv Mehrish kipindi cha utoaji wa taarifa ya kashfa ya rushwa itwayo *Rafale Jet deal* kusema hapaswi kuichunguza kashfa hiyo sababu na yeye alikuwepo katika timu ya mashauriano ya ununuzi wa ndege hizo za Rafale Jets nchini ufaransa akiwa katibu wa fedha wa wizara.
Ni tofauti na wewe una mtikisa CAG kwa kusema Bunge ni dhaifu ,nina maana una mtikisa CAG kwa sababu ndogo sana zaidi yote umepata CAG mzuri, mnyenyekevu,pole,mwenye hofu ya Mungu ,muwazi hakika ungemtumia ungelipa heshima Bunge kupitia uangalizi imara wa fedha za umma (Strong parliamentary oversight of public financial management).
Mh.Spika unafahamu fika kuwa kinga ya CAG ni kwasababu ya unyeti wa majukumu yake ili afanye kazi kwa uhuru,kwa utulivu ,bila kuingiliwa na kutikiswa sababu anafanya kazi ya kukagua matumizi ya kodi na fedha za watanzania hadi katika ofisi na idara za mapapa bila kumpa kinga hiyo angefanya kazi kwa hofu ,uoga,kujipendekeza,kuficha madudu kuhofia kuondolewa ndio maana akapewa kinga na hana maslahi yeyote ya kuajiriwa akimaliza kuhudumu katika nafasi hiyo. Ila umeamua kumtikisa bila kujua kuwa athari zitakazo patikana sio kwa Assad au CAG na wala sio kwa Ndugai au spika ni kwa umma wa watanzania.
Mh.Spika unafahamu fika kuwa Bunge (Legislature ) ndio moyo wa mchakato wa uangalizi matumizi ya fedha za umma (Public financial management) kupitia ofisi ya mkaguzi (SAI-Supreme auditor institution ) na PAC ila hujaona umuhimu wa kusimamia kikamilifu uangalizi wa fedha za umma (oversight) badala yake umeamua kumtikisa CAG ,pamoja na kinga zake zote alizonazo kikatiba umeamua kumtikisa kwa makusudi.
Mapendekezo yangu.
1.Mh.Rais asiunde tume yeyote kama njia ya utatuzi wa mgogoro huu sababu hakuna kosa la kikatiba wala la kosa maadili ya uongozi wa umma lililofanywa na CAG ,hivyo tume haina cha kuchunguza sababu makosa au sababu za kuundwa kwa tume yameoneshwa katika katiba ibara ya 144.
2. Bunge litengue maamuzi yake ya kutofanya kazi na CAG sababu maazio yake hayatekelezeki,sababu anayepaswa kupeleka report Bungeni kisheria ni Rais na sio CAG ,Je,Bunge litagomea Report ya CAG kutoka kwa Rais ? au ni Rais ndio hatopeleka Report ya CAG Bungeni ? ! Yote mawili yakifanyika itakuwa ni kinyume cha sheria.
Shukrani yangu ni hayo.
Abdul Nondo
abdulnondo10@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata sumu ya panya itamfaa. Kilangila.unfortunately there is no vaccine against stupidity, ningekupa