Barua Kwa Rais Kikwete Kuhusu Mtwara

Barua Kwa Rais Kikwete Kuhusu Mtwara

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Mheshimiwa Rais,

Najua uko bize ofisini kwako ukiendelea kutekeleza majukumu uliyopewa na Watanzania tangu 2010. Au pengine uko nchi fulani ukitembea huku na kule kuaangalia hili na lile ambalo wenzetu hao wameweza kulijenga. Au labda, kwa sababu leo ni wikiendi, uko katika ukumbi mmojawapo wa starehe hapo Magogoni ukipata kinywaji pamoja na wasaidizi wako.

Mheshimiwa Rais, najua unafika Jamii Forums mara kadhaa. Ama, kama wewe binafsi hufiki humu, wasaidizi wako wataisoma barua hii na kukufikishia ujumbe wangu. Ujumbe wangu waweza usitofautiane sana na jumbe nyingi zilizojaa vilio na machozi, ambavyo hata hivyo hukuvijali sana. Hata hivyo ujumbe huu ni wa muhimu kwako hasa kwa sababu unahusu wewe, pamoja na serikali yako kwa ujumla. Waweza kuupuuza kama ulivyozoea, ila tambua kuwa utakapoupuuza ujumbe huu, kuna siku utaukumbuka maana kwa hakika hali ya nchi si shwari.

Mheshimiwa Rais, matatizo yanapozidi, mioyo ya watu huota sugu. Kuna matukio kadhaa ambayo yameshatokea katika nchi yetu. Sitaki kuzungumzia ya nyuma ila nakukumbusha tu kuwa kuna mauaji ya watu watatu kule Arusha, mtu mmoja kule Morogoro, mwandishi wa habari kule Iringa, mtu mwingine kule Arumeru Mashariki, mtu mwingine kule Singida, na maeneo mengine mengi. Nikukumbushe pia mabomu ya Mbagala na Gongolamboto mwaka 2009 na 2011 ambayo yaligharimu maisha ya Watanzania wengi, na wengi kuachwa vilema. Nikukumbushe pia habari za machafuko ya Zanzibar na kuchomwa kwa makanisa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Rais, hayo yote ni tisa; kumi ni suala la gesi ambalo hadi sasa tumejulishwa kuwa wamefariki watu saba na wengine kujeruhiwa. Vilevile huko Morogoro na kuna mapigano ya wakulima na wafugaji, na huko Kariakoo kuna machafuko ya Machinga na Migambo.

Yote haya yanatokea na wewe uko kimya, sijui kwa nini. Umeshakuwa utamaduni wako kukaa kimya pale mambo yaanzapo na hatimaye kuibuka mwishoni mambo yakiwa yameshaharibika. Sijajua vizuri ni nani wanakushauri kufanya hivyo, kukaa kimya, ila nikujulishe tu kuwa wakushaurio wanakushauri vibaya.

Mheshimiwa, hali ya nchi iko tete sana hadi sasa. Hili swala linahitaji hatua madhubuti, si za wasaidizi wako tena, si za Mawaziri wako tena, bali wewe mwenyewe. Kutokuridhishwa na utendaji wako kumeenea kila mahali. Watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume, wanalalamika; watu wameshindwa kujua nchi unaipeleka wapi. Kumekuwa na matumizi ya silaha kwa kiasi kikubwa sana. Hali inatisha.

Mheshimiwa Rais, cheche ndogo yaweza kuutafuna msitu mkubwa, hasa msitu wenye nyasi kavu. Tanzania imekabiliwa na matatizo mengi ya huduma za afya, elimu, umeme, barabara, kupanda kwa bei za vyakula, n.k. Kwa ujumla, haya yote yanaifanya Tanzania iwe kama msitu wenye nyasi kavu. Zinapotokea cheche za moto kila upande wa msitu huu, kwa hakika msitu huu utateketea. Msitu huu utakapoteketea, wewe ndiwe utakayeingia matatani zaidi. Kwa hakika, kilichowakuta wakina Ben Ali, Hussein Mubarak na wengine wengi, kinainyemelea nyumba yako.

Mheshimiwa Rais, najua walishakutahadharisha wengi, ila nami niongezee. Suala la Mtwara si la kunyamaziwa hivyo. Nakuhakikishia, badala ya kuvuna gesi Mtwara, utavuna damu, ikiwa hutachukua hatua za haraka. Watu wamechoshwa na unyonyaji wanaofanyiwa. Watu wameota sugu mioyoni mwao. Watu wameshindwa kusubiri, watu wanataka mabadiliko. Watu wanataka wasikilizwe, watu wanataka watambuliwe, watu wanataka waheshimiwe.

Mheshimiwa, ni kweli wewe una majeshi, una askari, una silaha. Lakini wananchi wana mioyo ya ujasiri, wana umoja, wana ndoto, wana hoja; hizo ndizo silaha zao ambazo kamwe majeshi na silaha haviwezi kuzishinda. Ndio maana hadi sasa watu wamekufa huko Mtwara. Watanzania wameshafikia hatua hiyo, wako tayari kufa kwa ajili ya haki. Na kama huchukui hatua za haraka za kutekeleza maoni ya Wananchi wa Mtwara, tegemea vifo vingi zaidi.

Waswahili walisema, mzarau mwiba mguuni huota tende. Naona unapuuzia huu mwiba. Tambua kuwa, mwiba unatakiwa uutoe mapema. Usipoutoa mapema, hakika, utaota tende, hakika utaozesha mguu mzima, na mwisho wake, utaupoteza mguu wako au hata mwili mzima. Kamwe, huwezi kukabiliana na madai ya wananchi kwa kuwaonyesha una majeshi makubwa kiasi gani; wala si kwa kuwaonyesha una silaha kiasi gani; wala si kwa kuwaonyesha wewe ni mwamba kiasi gani. Madai ya wananchi yanatakiwa yafafanuliwe kwa hoja na si vioja, kwa uongofu na si hofu, kwa utashi na si matusi. Watu wanapolia hadi machozi yanapowakauka, na bado wasione kusikika kwa vilio vyao, mwisho wanaamua kuzitoa damu zao, na hizo zitokapo hata wewe hutakuwa salama.

Mheshimiwa, migomo na maandamano vinapokuwa sehemu ya maisha ya wananchi, matatizo yao yasipotatuliwa hadi wagome na kuandamana, tunazalisha kizazi kikaidi, kisichoogopa silaha, kisichoogopa majeshi, kizazi kisichouogopa uongozi. Hya yakishatokea (na yameanza kutokea) nchi itaingia vitani, nchi itakuwa machafukoni, nchi haitatawalika. Tatua matatizo ya wananchi yangali machanga; udongo uwahi ungali maji. Juzi ilikuwa Arusha, leo ni Mtwara, kesho itakuwa Mwanza na Kigoma, keshokutwa Tanga na Pwani; mwisho itakuwa nchi nzima. Matokeo yake utatafuta pa kukimbilia wala hutapaona kamwe.

Tafadhali ipokee barua yangu.
 
Katika miaka 10 ya Rais huyu dhaifu sijawahi kusikia akitoa maamuzi maguzi magumu au kuamua kitu km amiri jeshi mkuu kwa serikali yake au wananchi wake, always maamuzi yake naweza kuyafananisha na dada zetu....ni yuko kama pambo tu Ikulu...hiyo barua ataipa na ataipuuza coz hana jibu sijui hiyo elimu yake ni ya UDSM kweli au ni kaipata chuo cha jeshi? watanzania tumeamka si wale wa zamani tena...dadavua pls
 
Uliyosema ni kweli kabisa. Ila mwisho wa kupuuzia kwake ni majuto. Ngoja tu aendelee kpuuzia
 
Ni ushauri mzuri sana lakini unatolewa kwa mtu ambaye ni kiziwi, kipofu, dhaifu na mshirikina!!! Hautafanyiwa kazi kwa namna yoyote ile!!!!!!! Tusubiri tu umwagaji damu!!!
 
Mwenzio huwa hana muda wa kusoma. Laiti ungeandika tanzia au kumwalika kwenye kufungua kanda ya muziki ungemuona right away. Hata watu wake wanaotumia kodi zetu huwa hawana muda wa kusoma zaidi ya kuzurura kila wapatapo fursa wakiandamana na bwana na bi mkubwa. Ulimbukeni mwingine bwana!
 
Barua ina point lakini sio utani, kumwandikia mheshimiwa hiyo barua ni kama hii picha hapa chini.
attachment.php
 
Attachments

  • gitaa.jpg
    gitaa.jpg
    57.6 KB · Views: 1,079
huyu rais unayemwandikia yupo bize kukusanya mali zaidi, asichojua ni kuwa hata hizo mali anweza akakosa zote iwapo hali ya amani itavunjika. ni bora akawa maskini kuliko anachokifanya sasa kupitia kwa Riziwani. hizo mali wajutia. na huo ndo ukimya wake.
 
Nakupa 5,big up umeandika barua nzuri naamini rais wetu ni msikilizaji na muelewa atalifanyia kazi.
 
Umefanya la maana kabisa. Tusiogope kusema au kutoa ushauri na maoni tukiofia kwamba hayatamfikia au hatayafanyia kazi, kuna siku mambo yatamuwia magumu aanze kuutafuta ushauri huo na hataupata popote. Lakini mtoa ujumbe tayari utakuwa ushakamilisha jukumu lako muhimu la kutoa maoni. Hata mtoto akiwa mkaidi kivipi mzazi haachi hata siku moja kumkanya na kumshauri. Ushauri hutolewa bure siku zote na ubaki kwa mpokeaji kuufanyia kazi au kuupuuza..
 
Alishaandikiwa barua nyingi sana umetimiza wajibu tu kama ulivyosema yakimkuta

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nakushangaa unaandika barua yako ndefu na nzuri lakini bahati mbaya sana Tz haina Rais sasa siju nani ataisoma barua yako
 
Bershaza huo. Utawala wako umepimwa umeonekana........tusubiri utabili
 
Ni ushauri mzuri sana lakini unatolewa kwa mtu ambaye ni kiziwi, kipofu, dhaifu na mshirikina!!! Hautafanyiwa kazi kwa namna yoyote ile!!!!!!! Tusubiri tu umwagaji damu!!!

Hivi huyu jamaa Kikwete ana akili gani jamani? Tumempa madaraka sie wenyewe yeye anatugeuka na kutusanifu kila kukicha. Kwa wale wanaomfuatilia tu naombeni mniambie ni jambo gani la maana alilolifanya katika miaka yake 8 ya utawala?
 
Nakushangaa unaandika barua yako ndefu na nzuri lakini bahati mbaya sana Tz haina Rais sasa siju nani ataisoma barua yako

Ni kweli Lubua amechukua muda na kuwasilisha vizuri tatizo anayeandikiwa hana washauri zaidi ya kundi la marafiki .
Watu wa Mtwara wanaweza kuwa na hoja ya msingi. Ila kuzuia Bomba la gesi lisijengwe sio njia sahihi. Kwani ni kuanza hoja kwa kutumia nguvu.
Serikali inawezekana haikutoa elimu ya kutosha kuhusu kuvuna Gesi Huko Mtwara . Kinachotakiwa ni viongozi wa serikali huko Mtwara kudai kulipwa kama wanavyolipwa kwenye maeneo wanakoiba madini.

Tatizo tunavuna gesi kwa kutumia sera na sheria za Petroli. Jakaya take your time out toa ufafanuzi na kuwapa matumaini watu wa Mtwara but hawapaswi kuweka masharti. Kuzuia serikali kusafirisha gesi kwenda Dar is just another form of modern barbarism. Hawana hati miliki ya Mali asili. Kwa mujibu wa sheria zilizopo serikali ndiyo yenye miliki kwa niaba ya Watanzania na kusema Mtwara kwanza it's totally wrong.

Angekuwa kapewa mwekezaji then kungekuwepo na hoja. Wale wasiojua historia Mtwara and Lindi wamekuwa wakipatiwa umeme wa Ruzuku kwa miaka mingi so hawajawahi kuonewa. Hata Leo hii wanapata umeme wa uhakika kuliko sehemu yoyote ile ya Jamhuri ya Tanzania .

Tuwe waungwana kwani serikali inawajali sana. Sasa ukiwa na shamba la machungwa kule Muheza na soko la uhakika liko Dar ni lazima machungwa yaende Huko. Hivyo hivyo kuna soko kubwa la gesi Dar na la uhakika. Ni uendawazimu kulazimisha watumiaji wa uhakika walioko Dar wahamishiwe Mtwara.

Serikali inapaswa kuharakisha ujenzi wa mabomba ya gesi na kupelaka sokoni na kule ambako hakuna Bomba watumie LNG haraka sambamba na kuendelea na mjadala au mazungumzo na watu walioko Mtwara bila masharti yoyote.Tanzania is not yet a failed state kwa hiyo sheria zilizopo ni lazima tuziheshimu na kuendelea kutii bila kulazimishawa irrespective of who is the tenant of Magogoni period. We are polarized on a number of issues but the bottom line is to rescue the power sector from the current predicament.
 
Katika miaka 10 ya Rais huyu dhaifu sijawahi kusikia akitoa maamuzi maguzi magumu au kuamua kitu km amiri jeshi mkuu kwa serikali yake au wananchi wake, always maamuzi yake naweza kuyafananisha na dada zetu....ni yuko kama pambo tu Ikulu...hiyo barua ataipa na ataipuuza coz hana jibu sijui hiyo elimu yake ni ya UDSM kweli au ni kaipata chuo cha jeshi? watanzania tumeamka si wale wa zamani tena...dadavua pls

Wana macho lakini hayaoni, wana Masikio lakini hayasikii. Wewe ni mmoja wao.
 
Ni kweli Lubua amechukua muda na kuwasilisha vizuri tatizo anayeandikiwa hana washauri zaidi ya kundi la marafiki .
Watu wa Mtwara wanaweza kuwa na hoja ya msingi. Ila kuzuia Bomba la gesi lisijengwe sio njia sahihi. Kwani ni kuanza hoja kwa kutumia nguvu.
Serikali inawezekana haikutoa elimu ya kutosha kuhusu kuvuna Gesi Huko Mtwara . Kinachotakiwa ni viongozi wa serikali huko Mtwara kudai kulipwa kama wanavyolipwa kwenye maeneo wanakoiba madini.

Tatizo tunavuna gesi kwa kutumia sera na sheria za Petroli. Jakaya take your time out toa ufafanuzi na kuwapa matumaini watu wa Mtwara but hawapaswi kuweka masharti. Kuzuia serikali kusafirisha gesi kwenda Dar is just another form of modern barbarism. Hawana hati miliki ya Mali asili. Kwa mujibu wa sheria zilizopo serikali ndiyo yenye miliki kwa niaba ya Watanzania na kusema Mtwara kwanza it's totally wrong.

Angekuwa kapewa mwekezaji then kungekuwepo na hoja. Wale wasiojua historia Mtwara and Lindi wamekuwa wakipatiwa umeme wa Ruzuku kwa miaka mingi so hawajawahi kuonewa. Hata Leo hii wanapata umeme wa uhakika kuliko sehemu yoyote ile ya Jamhuri ya Tanzania .

Tuwe waungwana kwani serikali inawajali sana. Sasa ukiwa na shamba la machungwa kule Muheza na soko la uhakika liko Dar ni lazima machungwa yaende Huko. Hivyo hivyo kuna soko kubwa la gesi Dar na la uhakika. Ni uendawazimu kulazimisha watumiaji wa uhakika walioko Dar wahamishiwe Mtwara.

Serikali inapaswa kuharakisha ujenzi wa mabomba ya gesi na kupelaka sokoni na kule ambako hakuna Bomba watumie LNG haraka sambamba na kuendelea na mjadala au mazungumzo na watu walioko Mtwara bila masharti yoyote.Tanzania is not yet a failed state kwa hiyo sheria zilizopo ni lazima tuziheshimu na kuendelea kutii bila kulazimishawa irrespective of who is the tenant of Magogoni period. We are polarized on a number of issues but the bottom line is to rescue the power sector from the current predicament.

Nilitaka nisikujibu ila haya, nakujibu:-
1. Bomba hallina faida kwa kuwa Pwani yote hadi Tanga Kuna Gas ya kutosha hata Dar yenyewe ina Gas, je ikigunduliwa ni ninimustakabali wa hilo Bomba? Kama sio White Elephant?

2. Wana Mtwara hawako tayari kuona mikataba ya kimadini madini inatumika kwenye Gas, Terms na condition zqa gas lazima ziwe tofauti kwani wameshuhudia za huko ziki fail na kushindwa kuwanufaisha wannachi na sasa lazima mambo yawe tofauti.
3. Serekali yako ya kijambazi kama inavyotaka kujenga bomba ka miezi 18 sasa tunataka tuonew Hospitali ya rufaa, Hispitali za mikoa, Wilaya, na zahanati zikiborehswa au kujengwa ndani ya muda huohuo.
4. Wanataka waone Elimu ikiboreshwa na hili ni kwa ujenzi wa shule bora na sio hizi za sasa watu wanasoima kwa kukaa chini ya miti na kwenye matofali , wanataka Pre primary, primary, secondary, Vyuo vikuu, Vyuo vya Ufundi vikijengwa na bila kusahahu nazimhgira bora kwa walimu na wakufunzi wao.
5. Wanataka kuona Huduma ya maji na Umeme. Kuwafikia wanachi wote kuanzia mjini hadi vijijini.
6. Wanataka kuona Viwanda vikifufuliwa na kuboreshwa kwa ajili ya ajira na maendeleo kiujumla.
7. Wanataka kuona Bandari ya Mtwara ikijengwa sambaba na Reli kwenda Dar, kwenda Rukwa na soingea mpaka mpakani mwa nchi jirani za malawi na zambia na hata kongo pia.
8. Wanataka kuona barabara zinaboreswaha na kujengwa kiuwakika na zewnye ubora.
9. Wanataka kuona huduma ya usafiri na usafirishaji kupitia bahari ikirudi na kuboreshwa.
Na mwngine mengi muuende mkawasikilize huko.

Na sio kuja humu kuleta kejeli na vituko, na pia kumukeni wakati ni huu na hawapo tayari kufanywa mazuzu kama mulivyo wafanya wasukuma, wakurya, wamasai na wengineo huko.
 
Back
Top Bottom