Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
Mh. Mbowe,
Kila mtanzania anafahamu kwamba unatamani sana kuwa rais. Kumbuka mwaka 2010 kabla ya CHADEMA kumsimamisha Dr. Slaa kuwa mgombea wa urais, vijana wachache sana walikiunga cchadema mkono. Lakini baada ya kumsimamisha Dr. Salaa, Tanzania ililipuka kwa shangwe na nderemo. Muda unavyokwenda ndivyo CHADEMA inavyozidi kupaa kwani Dr. Slaa anaaminika kwa machungu aliyonayo kwa taifa letu. Dr. Slaa ndiye Nyerere aliyebaki katika hii taifa
Nikiwa mwana CCM anayeiombea mema CHADEMA, na ambaye anajitayarisha kujiunga na ukombozi kabla ya 2015, nakusihi usijaribu kugombea urais 2015. Endeleeni kujenga chama, mwacheni Dr. Slaa agombee. Waambie mamluki kama Zitto na Shibuda wana CCM wenzangu watulie. Wewe bado kijana, tulia mwachie Dr. Slaa alikomboe taifa. Kwani yeye ndio mhimili wa upinzani hapa nchini. Mkifanya kosa kukurupuka na mambo ya urais kama mwana CCM Zitto, utashangaa CHADEMA itakavyo pukutika. Gombea Urais 2020 au 2025
Kuna kundi la vijana mahiri na wataalamu wa hali ya juu Ulaya na marekani ambao wanajipanga kuisaidia CHADEMA ikiwa Dr. Slaa atasimamishwa. Na watu kama Samwel Sitta wanaodahi kwamba CHADEMA haina watu wanaoweza kuongoza serikali, watashangaa mfuriko wa vijana toka Marekani na ulaya pamoja na waliopo nyumbani wakiongozwa na wewe pamoja na Dr. slaa watakavyoibadilisha sura ya Tanzania. Endeleza harakati bila kukiangalia kiti cha urais. waache wakina zitto waendelezo ndoto na tamaa zao za kibinafsi na za madaraka
NB: Kuna siri nzito nitawamwagieni humu siku chache zijazo. Ila kwa sasa, kuweni makini na January Makamba pamoja na Zitto. Kuna mpango maalum wa kuwatumia kukimaliza CHADEMA