Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,997
- 3,933
Kasim Majaliwa,
Waziri Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
S.L.P 980, Ofisi ya Waziri Mkuu,
DODOMA, TANZANIA
YAH; BODI YA MIKOPO NA MAKATO YA ASILIMIA 15 KUFUATIA SHERIA YA MWAKA 2016 PAMOJA NA TOZO YA ASILIMIA 6 AMBAYO BODI IMESHINDWA KUITOLEA UFAFANUZI SAHIHI JUU YA UTEKELEZAJI WAKE
Tafadhali rejea kichwa cha habari.
Malalamiko ya wanufaika juu ya makato ya asilimia 15 na ongezeko la thamani ya asilimia 6 iliyoanzishwa kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo na kwamba kila mwaka kutakuwa na ongezeko la asilimia 6.
Aidha, baada ya Bodi ya Mikopo kuombwa kutoa ufafanuzi wa makato pamoja na ongezeko la asilimia 6 kila mwaka, Bodi ilijibu kupitia tamko lake kwa umma tarehe 6, Juni 2019 kama ifuatavyo;
(b)-ii; Kutamka kuwa Mnufaika aliyeajiriwa atakatwa asilimia 15 ya mshahara ghafi kwa ajili ya marejesho kwa HESLB. Awali, Sheria iliipa Serikali(Bodi) mamlaka ya kupanga kiwango cha makato. Tozo ya asilimia VRF (6%) ipo ndani ya makato ya asilimia 15. Rejea tamko hilo sambamba na barua hii.
Inashangaza kuona kwamba ongezo la asilimia 6 lipo ndani ya makato ya asilimia 15 ya kila mwezi lakini bado kila mwaka deni linaendelea kuongezeka kwa asilimia 6 kwenye salio lililobaki yaani outstanding loan Balance. Kwa maana nyingine, Bodi inakata tozo la asilimia sita mara mbili kinyume na sheria.
Kwa mfano daktari aliyesoma Tanzania katika chuo cha Bugando mwenye deni la shilingi milioni 30;
Kwa mshahara ghafi wa shilingi 1,500,000, makato ya Bodi yatakuwa 225,000/mwezi (Asilimia 15 ambayo ilielezwa kwamba ndani yake kuna tozo ya asilimia 6); Hivyo kwa muda wa miezi 12, mnufaika atalipa jumla ya shilingi 2,700,000. Deni linalotakiwa kubaki kwa mwaka unaopindukia ni shilingi 27,300,000, lakini kwa kuwa kuna tozo la asilimia 6, deni hilo litakuwa shilingi 28,938,000 ambalo ndio mnufaika ataendelea nalo.
Aidha mawasiliano yalifanyika na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo yakimshauri kupitia upya kikokoto kinachotumika katika utekelezaji wa makato. Hakukuwa na mrejesho.
Kwa maelezo hapo juu, tunaomba na kushauri ofisi yako juu ya yafuatayo;
· Serikali ipitie upya sheria ya mwaka 2012/2013 yenye incremental ya asilimia 6
· Serikali iangalie namna ya kupunguza makato ya asilimia 15
· Uchunguzi ufanyike juu ya tozo ya asilimia 6 inayokatwa mara mbili
· Bodi ihakikishe kwamba wafanyakazi wote wa sekta binafsi wanafikiwa; na wale ambao hawakurudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yao. Bodi iwasiliane na balozi za Tanzania kuwatambua na kuwatengenezea mfumo wa urejeshaji wakiwa huko nje. Kuna udhaifu katika utendaji wa Bodi ya Mikopo na makato yasiyokuwa na ufafanuzi sahihi, pia kuna kiasi kikubwa cha fedha wanashindwa kukusanya kutokana mapungufu ya mifumo yake. Matokeo ni nguvu nyingi hutumika kwa watumishi wa umma ili kufikia malengo ya makusanyo.
Asante.
Nakala; John Pombe Magufuli,
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
S.L.P 1102, CHAMWINO
40400 DODOMA
View attachment 1406572View attachment 1406574View attachment 1406575