Wakuu nimejaribu kutafuta mwelekeo wa hili jambo inaonekana liko vibaya kiutendaji.
Wapo waliouliza maswali mazuri hapa kwenye jukwaa ambayo nami ningependa niongeze kidogo.
1. Hivi hatuna Kamati za kitaalamu kwenye hizi Wizara ambazo zinashughulikia mambo kama haya? Sidhani ni jambo zuri sana Singh kwenda kumwona Gavana na kukubaliana naye kuwa a-release fedha ya mgogoro kama hiyo.
2. Je AG anayo nguvu ya yeye mwenyewe ya kuelekeza malipo kama haya yafanyike bila hata kuonyesha dondoo za kikao kilichoamua jambo kama hilo. Ikiwa na majina ya waliokaa kikao? Je mtu mmoja si ataweza kuuza nchi kwa mapango kama huu?
3. Kwanini huu uamuzi ulipochukuliwa na hata barua zenyewe zinaonyehsa, wahusika wakuu TANESCO hawakuhusishwa hapo mwishoni? Kwanini sioni Meneja Mkuu wa TANESCO akipewa nakala? Au hata akitajwa kuwa alikuwepo kwenye kikao chochote kilichofikia maamuzi hayo? Huu si uongozi na utendaji wa kudharauliana?
4. Kwanini sioni mahali ambapo TRA imetajwa kwamba katika kuuzwa kwa hisa za Mechmar na VIP, na PAP kuwa mmiliki wa share nyingi kuwa TRA ilikusanya kodi stahili kutoka kwenye mkataba wa mauziano?
5. Kwanini sijaona mahali AG ameipa taarifa TRA kuhusu mauziano hayo na kwamba ni kiasi gani ili TRA waweze kuokokotoa kiwango cha kodi stahili?
Hayo tu ndiyo nataka majibu yake kwa sasa.
Asanteni kwa michango yenu inaelimisha sana.