Barrick yawahonga wabunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barrick yawahonga wabunge?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Aug 9, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Barrick yawakodia wabunge ndege kwenda Nyamongo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 08 August 2011 21:02 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira.James Lembeli

  Waandishi Wetu, Tarime, Dodoma na Dar
  HATUA ya uongozi wa mgodi wa North Mara Barrick uliopo Nyamongo, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara kukodi ndege tatu ndogo kwa ajili ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwenda mgodini hapo, imezua malalamiko huku baadhi ya wananchi wakidai kwamba kitendo hicho huenda kikashawishi mtizamo wa kamati hiyo.

  Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli jana ilifanya ziara ya siku moja mgodini Nyamongo ikitokea mjini Dodoma, ziara ambayo kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo yake iliyoyatoa mwaka jana kuhusu athari za mazingira zilizosababisha baadhi ya wakazi wanaouzunguka kupata athari za kiafya.

  Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alikuwa amealikwa kuambatana na kamati hiyo, lakini safari yake iliishia Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma baada ya kubaini kwamba ndege husika zilikuwa zimekodiwa na kampuni ya Barrick.

  "Kweli mimi nipo Dodoma, nimerudia pale Airport (Uwanja wa Ndege), siwezi kwenda kuwasaliti wananchi wangu wa Tarime, maana kama tunakwenda kuwakagua Barrick halafu tupande ndege za Barrick sidhani kama tutatenda haki," alisema Nyangwine alipozungumza na gazeti hili kwa simu na kuongeza:

  "Barrick ndiyo (kampuni) inayotuhumiwa na wapiga kura wangu kwa kuwanyanyasa kwa kutowalipa baadhi yao fidia za mali zao hadi sasa mbali na kuhamishwa maeneo yao, kumekuwa na madhara makubwa kwa wananchi kutokana na matumizi ya maji yenye kemikali za sumu kutoka mgodini na maji hayo yanaingia Mto Tigite na kuleta madhara pia kwa wanyama, halafu nipande ndege yao! Haiwezekani."

  Msimamo wa Nyangwine unafanana na ule ambao umewahi kutolewa na Lembeli katika moja ya vikao vya Bunge mwaka 2009, akisema kwamba amekataa kupanda ndege za kampuni hiyo kwani huweka gharama za safari hizo kama sehemu ya huduma inazotoa kwa jamii.

  Lakini jana, Lembeli aliwaongoza wabunge wenzake kupanda ndege za Barrick ambazo zilitua Dodoma majira ya asubuhi na ujumbe wa baadhi ya wakuu wa kampuni hiyo, walioongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Deo Mwanyika kisha kuruka kuelekea Nyamongo.

  "Kilichonishtua ni kumwona yule bwana Mwanyika na hapo nilimwuliza Mwenyekiti (Lembeli) kwamba hii siyo rushwa? Lakini yeye akanijibu kwamba siyo rushwa kwa sababu ni jambo ambalo limefanyika kwa uwazi, lakini mimi nikaona kwamba siwezi kwenda na kamati hiyo kwa sababu hapo hakuna uhuru wa kufanya kazi," alisema Nyangwine.

  Alisema wananchi wake wasingemwelewa iwapo wangeshuhudia akishuka kutoka kwenye ndege ya Barrick wakati ni siku chache tu zilizopita alilalamika bungeni kuhusu madhara na unyanyasaji unaofanywa na kampuni hiyo dhidi ya wananchi.

  "Serikali hii ina uwezo wa kuwasafirisha wabunge wa kamati yoyote ile kama kuna suala lenye mgogoro au utata ili kubaini ukweli, sasa hii ya kuchukuliwa kwa ndege ya watuhumiwa haki haitatendeka ndiyo maana nimeona nisipande ndege hiyo ningelijua mapema ningekwenda huko jimboni kwangu wangenikuta hukohuko," alisema Nyangwine.

  Ofisi ya Bunge
  Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema jana kwamba ziara ya kamati hiyo ilipata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kampuni ya Barrick iligharamia kila kitu katika ziara hiyo.

  Hata hivyo, alisema hakuwa akifahamu idadi ya wabunge waliokwenda lakini taarifa ambazo Mwananchi lilizipata zilisema kuwa walikuwa zaidi ya 20, wakiwamo, Lembeli, Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkader Shah na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa.

  Wengine ni Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo na Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Buchosa (CCM), Dk Charles Tizeba, Mbunge wa Kikwajuni (CCM), Hamad Yusuff Masauni na Mbunge wa Longido (CCM), Mike Lekule Laizer.
  Joel alisema Spika aliridhia ziara hiyo kugharamiwa na Barrick na kwamba suala la wabunge kukubali au kutokubali kushawishiwa katika uendaji wao litategemea msimamo wao wenyewe kama kamati.

  "Kwa kawaida ziara za wabunge na Kamati za Bunge hugharamiwa na Ofisi ya Bunge, lakini ni kwa zile tu ambazo zipo kwenye kalenda na ratiba ya mwaka, sasa hii ya kwenda Nyamongo haipo kwenye utaratibu huo hivyo haikuwa rahisi kugharamiwa na Ofisi za Bunge, ndiyo maana waliomba kwa Spika ili Barrick wagharamie naye aliwaruhusu," alisema Joel.

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Barrick, Teweli Teweli alisema ilikuwa ni lazima kwa Barrick kugharamia ziara ya Kamati hiyo ya Bunge kutokana na asili ya kazi waliyokuwa wamekwenda kuifanya mgodini hapo.

  Teweli alisema kwa kuwa Barrick walikuwa wakituhumiwa kwa uharibifu wa mazingira, taratibu za kisheria zinawalazimisha kugharamia mchakato mzima wa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na taasisi mbalimbali za Serikali na Bunge na kwamba ziara ya jana inaangukia chini ya utaratibu huo.

  Mgodini Nyamongo
  Katika Mgodi wa Nyamongo, wenyeviti wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo wa Nyamongo, jana walizuiwa kuingia ndani ya mgodi huo walipokuwa wakitaka kwenda kushiriki katika mazungumzo baina ya uongozi wa Barrick na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge.

  Miongoni mwa waliofungiwa nje ya lango kuu la kuingia mgodini hapo ni Elisha Nyamhanga wa Kijiji cha Nyangoto, Omtanzania Omtima wa Kijiji cha Kewanja na Daudi Itembe wa Kijiji cha Matongo.

  Februari, mwaka jana kamati hiyo chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Job Ndugai ilifanya uchunguzi wa taarifa za athari za sumu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mgodi huo na kutoa taarifa inayoweka wazi kwamba kulikuwa na udhaifu katika ufuatiliaji wa sakata hilo.

  Kamati hiyo katika maazimo yake iliiagiza Serikali ichukue hatua za haraka kulichunguza suala hilo na kutoa malipo ya fidia kwa waathirika, huku baadhi ya wabunge waliochangia taarifa hiyo wakitaka kuwekwa kwa taratibu za kisheria za kukagua migodi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  huu uozo sijui utaendelea hadi lini..............................hivi unapopokea ugali kutoka kwa mtu unayeenda kukagua utendaji wake hivi yule raia si ataona hutamtendea haki?
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sijui hapo sheria zinasemaje.... nadhani auditors watatushauri vizuri zaidi
   
 4. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,388
  Likes Received: 10,555
  Trophy Points: 280
  mimi napita nitarudi baadae
   
Loading...