Bariki ndoa na si kufunga ndoa

Cobra70

Senior Member
Jan 2, 2020
167
363
Ndoa ni nadhiri au maagano mnaojiapiza mbele ya Mungu yaani kwamba mume na mke mtavumiliana kwenye raha na shida. Katika karne hizi vijana mnafunga ndoa kama sanaa za maonesho tu baada ya hapo ni usimbe na umalaya kwenda mbele.

Huwezi ukamfahamu mtu tabia yake vizuri ndani ya miezi, mwaka au miaka miwili ukasema huyo ni mke au mume.

Ndio maana mataifa ya magharibi yaliotuletea dini ya kikristo utasikia mtu amefunga ndoa na mpz wake wa zamani mala nyingine tayari walishazaa hata watoto watatu au wameishi zaidi ya miaka kumi lengo ni kujuana vema na kila mmoja kuridhika na mwenzake na kuepusha kuingia maagano ya kimungu bila ya kujiandaa na kujiridhisha.

Vijana acheni kukurupuka.
 
Tatizo mnaoa wake ambao sio wenu
Yaan unaoa mke wa mwenzako
Mke mwema anatoka kwa Bwana Sasa wewe utopolo unaoa kwa kuangalia matako na shape

Hutaki kumshirikisha Mungu akupe wako
 
Mimi nimeshatest japo nimezaa lakini nimebaini hanifai kabisa, Nina appointment na mashine mpya nayo sitajiingiza kichwakichwa.
 
Mkipendana, kitendo cha kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto, Mungu ameshabariki hilo tendo. Mengine ni ya nini? Ila kiserikali inabidi muwe na cheti cha kuhalalisha hiyo ndoa. Chapchap bomani mambo yameisha. Bomani hutaulizwa kama unashiriki jumuiya au zaka.
 
Ndoa ni nadhiri(makubaliano) baina ya wawili, ile inayofanyika msikitini au kanisani ni kuja kutangazia umma kuhusu makubalino yenu na kupata kibali cha kuishi pamoja kulingana na dini husika ili isiwe uzinifu.

Sasa swala la kuchukuana kwanza halafu baadae ndoa ndio ije kubarikiwa si itakua uzinifu mkuu
 
Maana watu wamezidisha utani hata kwa vitu ambavyo haviitaji utani! Kwann uape kuishi hadi kufa na mmeo au mkeo mwisho wa siku unamuacha kwa kutoa kasoro kedekede! Mungu hadhiakiwi aisee.
 
Back
Top Bottom