Bariadi, Simiyu: Wanne wafariki papo hapo baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Watu wanne wamefariki papo hapo baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana usiku huu 12.7.2022, eneo la Nyaumata nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu. Kamanda wa Polisi Mkoa Simiyu, Blasius Chatanda ameiambia STV kuwa ajali hiyo imehusisha magari madogo ya abiria.

RPC mkoa wa Simiyu amethibitisha vifo hivyo na kusema "Nimefika eneo la ajali nimeona waliofariki wote ni wanaume. Gari moja mchomoko lilikuwa likitokea Lamadi na lingine Bariadi. Dereva aliyekuwa akitoka Lamadi aliova-take ndipo akakutana na mwenzake. Chanzo ni mwendo kasi. Madereva wamejeruhiwa na wapo chini ya ulinzi,"

20220712_232929.jpg
 
Hii barabara ya Lamadi mpaka Mwigumbi kupitia Bariadi na Maswa ni mkeka usio na magari hivyo inakuwa na kujiamini upo peke yako umakini unapotea.
 
Hii barabara ya Lamadi mpaka Mwigumbi kupitia Bariadi na Maswa ni mkeka usio na magari hivyo inakuwa na kujiamini upo peke yako umakini unapotea.
Mkuu naomba unifahamishe, hivi toka Mwigumbi to Bariadi via Maswa walishatandika "mkeka"?
 
Back
Top Bottom