Habari zenu wakuu, natumaini mpo njema kiafya mpaka muda huu mnasoma uzi huu.
Naenda direct kwenye lengo la uzi huu, juzi nilinunua bidhaa (kifaa cha umeme) yenye thamani ya TZS. 520,000/= lakini leo nilipojaribu ku-scan barcode kwenye box lake haileti information zozote, nimepata wasiwasi kuwa huenda ni bidhaa feki kwasababu kama wameweka barcode basi zilipaswa kuwa na information. Nataka kumrudishia muuzaji na kudai fedha zangu, nina risiti na alinipa Guarantee ya miezi 6 kwa mkataba wa maneno nikiwa na shahidi mmoja.
Maswali ninayojiuliza ni;
Je, bidhaa hii ni feki?
Kwanini kuwe na barcode zisizofanya kazi, au ni zuga tu?
Je, bidhaa ni imara ila ina barcode feki?
Naombeni msaada kwa hili kwa wale wenye ujuzi na haya mambo.