Zamazamani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2008
- 1,859
- 763
pole sana ndugu, sasa unaonaje nikukaribishe kwenye benki yangu ufungue akaunti pia na NGO yako tutaifungulia akaunti unaonaje, nitafurahi saana kukuona mdau na hutajuta kamwe, hao barclays wamejichokea sana na pia wamepigwa wizi wa kufa m2 karibu mkuu, nitafurahi saana ukija
Mkuu benki ziko nyingi na zingine wala hazichukui muda kiasi hicho kufungua ama kufunga account. Au una agenda iliyofichika ambayo nao Barclays wameishtukia na wanaifanyia kazi? Watchout!
Hakuna chochote kilichojificha...wengi watashuhudia humu....ile ya NGO tunajaribu kufungua pale Access Bank lakini bado ngumu sana..miyeyusho mingi......pale tawi la lumumba tumechemsha ...baada ya ku submit documents zote walizohitaji ,na usumbufu mwingi hakieleweki kinachoendelea...tunajaribu tawi la kijitonyama sasa!!!!niambie benki gani tofauti??
Mmeshajaribu kufungua accunt kwenye bank ngapi mpaka sasa?
Kama mmewapa documents ZOTE wanazotaka, usumbufu mwingine ni upi huo mkuu?
Jamani...
Sijui tatizo kama ni langu na watu walio karibu yangu..au ni vipi....kwa kweli huduma za benki za Barclays zinanitia kichefuchefu mno....nimejaribu kufungua akaunti personal sasa yapata mwezi wa tatu haijawezekana.......tena baada ya kuchoshwa na tawi la Ubungo plaza ..nikatoa kitu kidogo ...huduma iende spidi ikawa hola(mhusika jina ninalo)..nikajaribu tena tawi la pale Sea Cliff...usumbufu nilioupata nimenyoosha mikono...kama haitoshi ikatokea NGO ninayojishughulisha nayo imepewa msaada wa hela (cheque) na sababu hatukuwa na akaunti tuka jaribu kufungua akaunti pale Barclays downtown....tangu December 2009 mpaka leo...leta hiki,leta kile, haukuleta kile, sasa ulete kile.,baada ya wiki uje mambo yatakuwa tayari....ukienda unakuta kimtu kingine kabisa kinakwambia ulisahau kuleta kile...basi..stori goes on and on!!!!...kutwa kuchwa....sometimes simu wanapiga lakini hakuna kinachoendelea...baada ya kuchoshwa nikawa nalalamika mbele ya watu wachache,...kumbe nao yamewakuta kama haya....nimeambiwa nisithubutu tena...ndivyo walivyo....kumbe hata hatua ya kufungua matawi mengi ni very hopeless move ,sasa nimekubali....sina uhakika kama uongozi unayajua haya...nimewanyooshea mikono...tunajiuliza hivi na nchi nyingine wapo hopeless hivi hivi????nimenawa...
Barclays siku hizi kimeo hawafai kabisaa
Nenda Azania Bank, Akiba commercial,Stanbic hata Exim bank si wabaya
Ninacholalamikia mimi ni utaratibu mbovu wa wahusika wa Barclays...haiwezekani kila mtu ndani ya benki hiyohiyo anamahitaji tofauti...yaani unasubmit documents zote wanazohitaji then anakwambia sasa mambo safi akaunti itafunguliwa....then ukienda baada ya siku tatu...unamkuta mwingine anakueleza hadithi nyingine...mchezo ndiyo huo.huo..kama kuna mapungufu ya msingi kwa nini wasiseme mwanzoni??? kipi kipya hapo???Anyways... mbona hata wenyewe baadhi yao wanakubali kuwa benki yao ni ya kichovu?? ...si neno najaribu sehemu nyingine ....Mimi siwaluamu Barclays. Haya yote ni matokeo ya watu kutukuwa waaminifu. Barclays wameibiwa sana na watu, kampuni feki na NGO feki wakishirikiana na wafanyakazi.
Siku hizi wame waangalifu sana katika kufungua accounts na kutoa mikopo.