Barclays TZ...The hopeless,nimewanyooshea mikono!

Zamazamani

JF-Expert Member
Jun 13, 2008
1,856
762
Jamani...

Sijui tatizo kama ni langu na watu walio karibu yangu..au ni vipi....kwa kweli huduma za benki za Barclays zinanitia kichefuchefu mno....

Nimejaribu kufungua akaunti personal sasa yapata mwezi wa tatu haijawezekana.... tena baada ya kuchoshwa na tawi la Ubungo plaza ..nikatoa kitu kidogo ...huduma iende spidi ikawa hola (mhusika jina ninalo)..nikajaribu tena tawi la pale Sea Cliff...usumbufu nilioupata nimenyoosha mikono...

Kama haitoshi ikatokea NGO ninayojishughulisha nayo imepewa msaada wa hela (cheque) na sababu hatukuwa na akaunti tuka jaribu kufungua akaunti pale Barclays downtown....tangu December 2009 mpaka leo...leta hiki, leta kile, haukuleta kile, sasa ulete kile, baada ya wiki uje mambo yatakuwa tayari... ukienda unakuta kimtu kingine kabisa kinakwambia ulisahau kuleta kile... basi..stori goes on and on!!!!...kutwa kuchwa.... sometimes simu wanapiga lakini hakuna kinachoendelea...

Baada ya kuchoshwa nikawa nalalamika mbele ya watu wachache,... kumbe nao yamewakuta kama haya.... nimeambiwa nisithubutu tena...ndivyo walivyo....kumbe hata hatua ya kufungua matawi mengi ni very hopeless move sasa nimekubali....sina uhakika kama uongozi unayajua haya... nimewanyooshea mikono...tunajiuliza hivi na nchi nyingine wapo hopeless hivi hivi? nimenawa...
 
pole sana ndugu, sasa unaonaje nikukaribishe kwenye benki yangu ufungue akaunti pia na NGO yako tutaifungulia akaunti unaonaje, nitafurahi saana kukuona mdau na hutajuta kamwe, hao barclays wamejichokea sana na pia wamepigwa wizi wa kufa m2 karibu mkuu, nitafurahi saana ukija
 
pia mkuu katika ulimwengu huu wa biashara ya benki huitakiwi kutoa kitu kidogo ili uhudumiwe hiyo kwa sasa imekufa haipo usipate tabu
 
Mkuu Mbona Benk zipo nyingi tu!

Nenda Benki M mambo chap chap! au jaribu Dar es Salaam Community Bank pia kuna Benki ya akina Mama na nyinginezo kibao!
 
Mkuu benki ziko nyingi na zingine wala hazichukui muda kiasi hicho kufungua ama kufunga account. Au una agenda iliyofichika ambayo nao Barclays wameishtukia na wanaifanyia kazi? Watchout!
 
Niliwahi kufungua account tawi lao la post then nikasafiri nje ya nchi. Nikiwa safarini, nikawa nawapigia simu kucheck progress ipoje lkn cha achabu nikaambiwa ati hakuna kumbukumbuku zangu pale na wala hawajawi kupokea application yenye jina langu! - yaani mpaka meneja wa atwi aliniambia huu ujinga Nilichoka kabisa

Baada kama ya miezi minne hivi, wakanitumia email with account numbers.

Mpaka leo nimeacha pesa ya kutunza account tu - nina wasiwasi nao wale wahuni
 
pole sana ndugu, sasa unaonaje nikukaribishe kwenye benki yangu ufungue akaunti pia na NGO yako tutaifungulia akaunti unaonaje, nitafurahi saana kukuona mdau na hutajuta kamwe, hao barclays wamejichokea sana na pia wamepigwa wizi wa kufa m2 karibu mkuu, nitafurahi saana ukija

...kwa mfano benki gani ambayo iko serious??? ...sitaki kusikia CRDB wala ACCESS Bank sababu ni headache tupu nazo...
 
Mkuu benki ziko nyingi na zingine wala hazichukui muda kiasi hicho kufungua ama kufunga account. Au una agenda iliyofichika ambayo nao Barclays wameishtukia na wanaifanyia kazi? Watchout!

Hakuna chochote kilichojificha...wengi watashuhudia humu....ile ya NGO tunajaribu kufungua pale Access Bank lakini bado ngumu sana..miyeyusho mingi......pale tawi la lumumba tumechemsha ...baada ya ku submit documents zote walizohitaji ,na usumbufu mwingi hakieleweki kinachoendelea...tunajaribu tawi la kijitonyama sasa!!!!niambie benki gani tofauti??
 
Hakuna chochote kilichojificha...wengi watashuhudia humu....ile ya NGO tunajaribu kufungua pale Access Bank lakini bado ngumu sana..miyeyusho mingi......pale tawi la lumumba tumechemsha ...baada ya ku submit documents zote walizohitaji ,na usumbufu mwingi hakieleweki kinachoendelea...tunajaribu tawi la kijitonyama sasa!!!!niambie benki gani tofauti??

Mmeshajaribu kufungua accunt kwenye bank ngapi mpaka sasa?

Kama mmewapa documents ZOTE wanazotaka, usumbufu mwingine ni upi huo mkuu?
 
Mmeshajaribu kufungua accunt kwenye bank ngapi mpaka sasa?

Kama mmewapa documents ZOTE wanazotaka, usumbufu mwingine ni upi huo mkuu?

Ninatilia mashaka malalamiko ya Zamanizamani. Kama hiyo NGO yake anajaribu kuifungulia benki akaunti halafu benki zinamzungusha, inawezekana akawa hatimilizi masharti yanayotakiwa! Haiwezekani benki zote zikatae kukufungulia akaunti!
 
Stanbic na Azania ni bank nzuri sana na kufungua Acc ni siku moja kama ukiwa na kila kitu, haya mambo ya kibenki hayahitaji mafafa, tafuta karatasi za ukweli sidhani kama utasumbuka
 
Mimi siwaluamu Barclays. Haya yote ni matokeo ya watu kutukuwa waaminifu. Barclays wameibiwa sana na watu, kampuni feki na NGO feki wakishirikiana na wafanyakazi.
Siku hizi wame waangalifu sana katika kufungua accounts na kutoa mikopo.
 
Jamani...
Sijui tatizo kama ni langu na watu walio karibu yangu..au ni vipi....kwa kweli huduma za benki za Barclays zinanitia kichefuchefu mno....nimejaribu kufungua akaunti personal sasa yapata mwezi wa tatu haijawezekana.......tena baada ya kuchoshwa na tawi la Ubungo plaza ..nikatoa kitu kidogo ...huduma iende spidi ikawa hola(mhusika jina ninalo)..nikajaribu tena tawi la pale Sea Cliff...usumbufu nilioupata nimenyoosha mikono...kama haitoshi ikatokea NGO ninayojishughulisha nayo imepewa msaada wa hela (cheque) na sababu hatukuwa na akaunti tuka jaribu kufungua akaunti pale Barclays downtown....tangu December 2009 mpaka leo...leta hiki,leta kile, haukuleta kile, sasa ulete kile.,baada ya wiki uje mambo yatakuwa tayari....ukienda unakuta kimtu kingine kabisa kinakwambia ulisahau kuleta kile...basi..stori goes on and on!!!!...kutwa kuchwa....sometimes simu wanapiga lakini hakuna kinachoendelea...baada ya kuchoshwa nikawa nalalamika mbele ya watu wachache,...kumbe nao yamewakuta kama haya....nimeambiwa nisithubutu tena...ndivyo walivyo....kumbe hata hatua ya kufungua matawi mengi ni very hopeless move ,sasa nimekubali....sina uhakika kama uongozi unayajua haya...nimewanyooshea mikono...tunajiuliza hivi na nchi nyingine wapo hopeless hivi hivi????nimenawa...


Why Barclays? benki zingine huzioni kafunguwe akiba comercial?
 
Barclays siku hizi kimeo hawafai kabisaa


Sio Kimeo Jamaa ndio KImeo kwani Bank ina utaratibu wake wakikwambia kalete hiki nenda sasa wewe Record zako watawekaje Kwani ulienda bila ya Barua ya Mwenyekiti passport size za miaka ya nyuma na wewe unataka kufungua NGO inautaratibu wake kwani kuna Management sasa wewe ndio unataka kufungua mwenyewe hiyo sahau hata uende Bank yoyote ile mimi Ninachojua Barclays ni Bank ya Uhakika ukifika pale Ulizia Ofisa mmoja anaitwa Henry yeye ni investigation atakusaidia vilivyo. bye
 
Nenda Azania Bank, Akiba commercial,Stanbic hata Exim bank si wabaya

Wengine ni Stanchat, TPB, TWB, DCB, Access, CBA, BOA, CRDB, NMB, NBC, City bank, FBME bank, Bank M, DTB, KCB, Mkombozi bank, du the list is long see http://www.bot-tz.org/BankingSupervision/RegisteredBanks.asp

Achana na hao wachovu nenda kwa akufaaye. Sisi wengine tuko mstarini kwenye 'benki yetu' tunangoja ATM na cashier tupate hela na hatujali urefu wa mstari.... tumeridhika na hali hatuna mpango wa kuhama!
 
Mimi siwaluamu Barclays. Haya yote ni matokeo ya watu kutukuwa waaminifu. Barclays wameibiwa sana na watu, kampuni feki na NGO feki wakishirikiana na wafanyakazi.
Siku hizi wame waangalifu sana katika kufungua accounts na kutoa mikopo.
Ninacholalamikia mimi ni utaratibu mbovu wa wahusika wa Barclays...haiwezekani kila mtu ndani ya benki hiyohiyo anamahitaji tofauti...yaani unasubmit documents zote wanazohitaji then anakwambia sasa mambo safi akaunti itafunguliwa....then ukienda baada ya siku tatu...unamkuta mwingine anakueleza hadithi nyingine...mchezo ndiyo huo.huo..kama kuna mapungufu ya msingi kwa nini wasiseme mwanzoni??? kipi kipya hapo???Anyways... mbona hata wenyewe baadhi yao wanakubali kuwa benki yao ni ya kichovu?? ...si neno najaribu sehemu nyingine ....
 
Mtoa mada nadhani umesahau kuwa unapofungua account "Taratibu na Masharti huzingatiwa"...hapa wanamaanisha taratibu na masharti ya kibenki!! Nakushangaa kwa nini unatoa kitu kidogo ili kufungua account, kama umekamiisha kila kitu, ninao uhakika, umetoa documents zinazotakiwa, umepata wadhamini, una barua ya mtendaji, kitambulisho halali n.k process ni siku moja tu ndugu yangu! Na pia nashangaa NGO yako umeifunguaje haina akaunti?? Nadhani hapo kuna maswali ya kujiuliza....ndiyo maana kumetokea hizi kasoro!! Kila mtu anaishtukia NGO yako ati!! Kwa nini usiende CRDB, ACM, SCB, NBC, NMB etc?? Maana baada ya kuona unasumbuliwa huko Barclays ungeenda zako kwingine basi...ulikuwa na ulazima gani kung'angana na Barclays?? Miezi mitatu bado umo tu?..Tena kwenye ulimwengu huu ambao mabenki yanawafuata watu hadi majumbani?? You are not serious....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom