Barbra aachie ngazi Simba kwa maslahi ya timu, wapigaji wengi ndani ya timu wanamhujumu

Mwishokambi

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
305
1,166
Mimi naijua Simba, sijaanza kushabikia Leo wala jana, nmeanza kwenda uwanjani kuangalia Simba enzi za akina Aston Padon, Juma Limonga, Sunday Juma, Mosses Mkandawile, Omary Hussein Kevin keegan.

Simba imeshazoea kuwa kama kuna mtu ndani ya uongozi hawamtaki basi wanahujumu timu ili mambo yao yafanikiwe.

CEO amebana sana mianya ya upigaji ndani ya timu, mambo ya kuchezea hela bila utaratibu hakubaliani nayo, wajanja wanataka fungu kubwa la kamati ya ufundi jambo ambalo CEO Barbra hakubaliani nayo, sasa kinachofanyika ni kumkalia vikao vya majungu ili aharibikiwe aonekane amefeli, Simba imemuachia timu yeye tena kwenye gemu ngumu dhidi ya yanga, wamejisemea, Ngoja tumuache tuone atafanya nn, ndicho kilichotokea jana dhidi ya yanga, akina Kaduguda waligoma kwenda kumsaidia kwa madai hawakubaliani na baadhi ya mambo ndani ya timu.

Simba ikiwa na Hassan Hassanoo, Kassim Dewji, Dalali, Magori, na baadhi ya wazee haiwezi kufungwa na Yanga isipokuwa hujuma zinafanyika ili Barbra aondoke.Ndio maana namshauri Mo Dewji asiweke hela yake hiyo B 20, wajinga wajinga wengi pale klabuni kwetu.

Namshauri Barbra aachie ngazi ili Simba isonge mbele, kuna watu wanauza ishu ndani ya timu ili kumchafulia utendaji wake.
 
Hakuna hujuma wala uchawi, tukubali tu kwamba huu msimu wenzetu Yanga wamekuwa bora ndani na nje ya uwanja

Simba tumedrop ktk ubora wetu kulinganisha na misimu MINNE mfululizo tuliyotawala ndio maana hata tuliondolewa CAF champions lg hatua ya mtoano na wale Jwaneng na huku ktk ligi yetu tumeachwa gap kubwa na Yanga

Pia naona Simba tulibugi ktk replacement ya mwalimu Didier Gómez na kumleta Pablo, bado naona Gómez yupo bora sn kuliko hata Pablo
 
Hamkufanya replacement ya Bashite nayo imechangia kwa kiasi fulani.
 
Hakuna hujuma wala uchawi, tukubali tu kwamba huu msimu wenzetu Yanga wamekuwa bora ndani na nje ya uwanja...
Hapana walichokifanya Yanga ni kumaintain tu walipokuwepo toka msimu uliopita ila Simba ndiyo wameporomoka kutoka walipokuwa.

Mfano magoli tu Yanga wamefunga magoli machache kuliko waliyofunga msimu uliopita.

Simba msimu hajafikia hata Magoli waliyofunga Kagere, Bocco na Mugalu combined hapo hujazungumzia magoli ya Luis na Chama plus Dilunga na wengine.

Kimsingi Simba Msimu huu hata wangefunga robo tatu tu ya magoli waliyofunga last season wangechukua ubingwa tena easy tu.
 
Hiyo timu amehongwa ni kama yake kwasasa kwahyo msimbugudhi lasivyo mtaondoka nyie kama alivyoondoka Manara
 
Kwahiyo aachie ngazi ili upigaji uendelee?wewe ni mmoja wa hao wapigaji
Mm naijua Simba, sijaanza kushabikia Leo wala jana, nmeanza kwenda uwanjani kuangalia Simba enzi za akina Aston Padon, Juma Limonga, Sunday Juma, Mosses Mkandawile, Omary Hussein Kevin keegan.

Simba imeshazoea kuwa kama kuna mtu ndani ya uongozi hawamtaki basi wanahujumu timu ili mambo yao yafanikiwe.

CEO amebana sana mianya ya upigaji ndani ya timu, mambo ya kuchezea hela bila utaratibu hakubaliani nayo, wajanja wanataka fungu kubwa la kamati ya ufundi jambo ambalo CEO Barbra hakubaliani nayo, sasa kinachofanyika ni kumkalia vikao vya majungu ili aharibikiwe aonekane amefeli, Simba imemuachia timu yeye tena kwenye gemu ngumu dhidi ya yanga, wamejisemea, Ngoja tumuache tuone atafanya nn, ndicho kilichotokea jana dhidi ya yanga, akina Kaduguda waligoma kwenda kumsaidia kwa madai hawakubaliani na baadhi ya mambo ndani ya timu.

Simba ikiwa na Hassan Hassanoo, Kassim Dewji, Dalali, Magori, na baadhi ya wazee haiwez kufungwa na Yanga isipokuwa hujuma zinafanyika ili Barbra aondoke.Ndio maana namshauri Mo Dewji asiweke hela yake hiyo B 20, wajinga wajinga wengi pale klabuni kwetu.

Namshauri Barbra aachie ngazi ili Simba isonge mbele, kuna watu wanauza ishu ndani ya timu ili kumchafulia utendaji wake.
 
Hapana walichokifanya Yanga ni kumaintain tu walipokuwepo toka msimu uliopita ila Simba ndiyo wameporomoka kutoka walipokuwa.

Wachezaji wengi wa Yanga ni wapya. Mfano kati ya walionza jana, saba ni wapya wamesajiliwa msimu.
 
Barbra yupo pale Simba kulinda na kuzisimamia pesa za MO. Atapoondoka ujue na MO anaacha kuidhamini klabu.
 
Barbra haondoki Simba SC, full stop.

Hawezi kuondoka halafu hao wapigaji uliodai wapo watambe, huo utakuwa ni uzuzu.
 
Hapo mwisho umeongea utumbo. Haiwezi kufungwa na Yanga?. Kwani ni mara ya kwanza managongwa na Yanga?. Miaka yote mnavyogongwa hao wanakuwa hawapo?.
 
Shabiki wa Simba asiyejielewa wewe,yani unasisitiza kabisa Babra aondoke ili watu wapige hela!
Simba na Babra,Babra na Simba forever.
 
Yaani huyu jamaa anataka Barbra aondoke ili wapigaji waendeleze upigaji! Huyu huenda ni miongoni mwa hao wapigji.
Hatuwezi kuendeleza soka kwa kuishi kwa mazoea, tena mazoea yenyewe ya hovyo kama haya ya wizi wa mali za klabu.
 
Akitoka Aunt Barbara sitakaa niichangie simba chochote na uanachama naacha. Puuuumbuuuyafisi.
 
Back
Top Bottom