Baraza la Vijana CHADEMA latangaza Uchaguzi wake wa Marudio

Nauliza hivi! hiivi,kuwa uchaguzi wa mwenyekiti unaanyika lini? kipi bora mwenyekiti au kiognozi wa vijana? kwa nini wazee wasimweke tu huyo wanaemtaka??

nitauliza mpaka nijue uchaguzi wa mnweyekiti ni lini!

Mwenyekiti gani tena wa CCM taifa hata mimi sijawahi kusikia uchaguzi huo nasikia ukiwa rais tu tayari umeukwaa uenyekiti
 
Luteni, Na wewe una sababu za kitoto kwelikweli. Huo uchaguzi ulifanyikia wapi ambapo usiku unakimbiwa? Si ukubali tu kuwa wenye chama walimzima mshikaji wake Zitto?

Jamaa hawana mchezo ukileta za kuleta unakwenda na maji haingii mdudu mtu mle full bullet proof
 
Mwenyekiti gani tena wa CCM taifa hata mimi sijawahi kusikia uchaguzi huo nasikia ukiwa rais tu tayari umeukwaa uenyekiti

Thanks for that excuse, so you are copying and implementing CCM standard??
 
Thanks for that excuse, so you are copying and implementing CCM standard??

The best way to innovate is to understand thoroughly the existing establishment, picking up what is useful and letting go all its nonsense. At times you might be considered copying and pasting the prevailling status, while infact advancing towards total coverage.

Otherwise you might produce a weakest adventure of all times. Innovation is all about filling the gaps left by the existing structure, solving the problems it couldn't solve, answering questions it knew not the answers to. How then would you do this without knowing any fruitful thing left within it, probably left to rust and perish.

Any newly established party in Tanzania has no way but to somehow copy some bits of the Legend CCM and innovate there after.
 
Kijichama fisadi! Chadema wanafanya ufisadi ktk uchaguzi mdogo wa vijana na wanashindwa ku control kura mpaka zinaibiwa, uchaguzi unarudiwarudiwa kweli hiki ni chama kinaweza kuendesha nchi? chadema ni kichekesho !!

Say no to CHADEMA, wanashindwa kusimamia uchaguzi wa vijana wao! wataweza nini?
katika zama hizi za mapambano ya kisiasa , hutazamii kuwa CHADEMA ni kijichama fisadi....mawazo dhaifu hutolewa na mtu dhaifu, hekima ni zawadi kwa wachache na wasio nayo utawatambua kwa mawazo yao dhalili, waoga kufikiri mambo mazito ni mabingwa wa matusi hivyo ndivyo viashiria vya watu wa hovyohovyo.
 
The best way to innovate is to understand thoroughly the existing establishment, picking up what is useful and letting go all its nonsense. At times you might be considered copying and pasting the prevailling status, while infact advancing towards total coverage.

Otherwise you might produce a weakest adventure of all times. Innovation is all about filling the gaps left by the existing structure, solving the problems it couldn't solve, answering questions it knew not the answers to. How then would you do this without knowing any fruitful thing left within it, probably left to rust and perish.

Any newly established party in Tanzania has no way but to somehow copy some bits of the Legend CCM and innovate there after.

He said that they will never bother to elect chairman since CCM is not electing chairman, is this filling gaps so that you can innovate the best one?
 
mimi nafikiri uchaguzi wowote ule lazima uwe fair na uwe wazi, the last tatizo lililojitokeza ni kwamba final results ilionyesha kuwa kura zilizidi watu waliopiga au waliokuwepo so kwa vigezo hivo ungempa ushindi aliyeshinda ina maana the whole election isingekuwa na legitimacy yoyote ile. Mimi nafikiri ni jambo la busara na lilikuwa jambo la busara kufuta matokeo na kwenda kwenye episode nyingine ambayo ni ya marudio.

Hii inaonyesh kupevuka na pia inaonyesha the integrity democrasy ndani ya chama, ni mfano wa kuigwa.

Demokrasia na CHADEMA? Labda mwenzetu uko usingizini unaota, kama CHADEMA kungelikuwa na demokrasia, leo mwenyekiti wenu angelikuwa Zitto na huo uchaguzi wa vijana usingerudiwa.

Teueni tu wale ambao wenye CHAMA wanawataka, kuna haja gani ya kudanganya wananchi kwa demokrasia ambayo hamuikubali?

Hata mwenyekiti wanawake nao ulikuwa mizengwe tupu. Hicho ndio chama mbadala kweli?
 
Ndugu yangu hatuko hapa katika kutukanana ama kubishana..tuko hapa katika kupashana habari na si vingenevyo..wewe kama unayako ishia zako..UMEFULIA.Teh teh teh.Vipi umemaliza kufanya mikatano yako ya hadhara?

Majibu yako sawa na jina lako, umeanza jazba badala ya kujibu maswali na utata, udhaifu unao kabili chama chako cha Chadema.

JF tupo si kwakupeana habari pekee bali pia kudadisi habari, mtunachtaka kuelewa hapa ni vipi chadema wameshindwa kusimamia uchaguzi wa vijana wake, as result, matokeo yamejaa fraud, corruption na uchafu wote.

swali kama chama chako kimeshindwa kusimamamia uchaguzi wa watu wacheche, watawezaje kulisimamia li nchi kubwa kama la tanzania? hakuna matusi hapo unatakiwa kujibu acha sensitivity zako za ajabu!!
 
katika zama hizi za mapambano ya kisiasa , hutazamii kuwa CHADEMA ni kijichama fisadi....mawazo dhaifu hutolewa na mtu dhaifu, hekima ni zawadi kwa wachache na wasio nayo utawatambua kwa mawazo yao dhalili, waoga kufikiri mambo mazito ni mabingwa wa matusi hivyo ndivyo viashiria vya watu wa hovyohovyo.

Jibu maswali acha kuleta ngonjera !!1
 
Bull,Butola Kubwajinga na Waberoya
Naona wengine hapa hamjazungumza siku nyingi na mmepata pa kusemea..Binafsi sina muda wa kubaishana na watu kama ninyi mlioko kazini saa hizi kwasasabu manzozijua ninyi.Nimeirusha hii thread ili watu wahabarike na sio jukwaa la malumbano yasiyokuwa na mashiko..kama mnataka malumbano basi anzisheni thread zenu sio kudandia kwa wenzenu ebo!shit...mkiendeka for sure natuma PM kwa wahusika waifunge thread hii..
 
Demokrasia na CHADEMA? Labda mwenzetu uko usingizini unaota, kama CHADEMA kungelikuwa na demokrasia, leo mwenyekiti wenu angelikuwa Zitto na huo uchaguzi wa vijana usingerudiwa.

Teueni tu wale ambao wenye CHAMA wanawataka, kuna haja gani ya kudanganya wananchi kwa demokrasia ambayo hamuikubali?

Hata mwenyekiti wanawake nao ulikuwa mizengwe tupu. Hicho ndio chama mbadala kweli?

Kwani demokrasia ni kuchaguliwa Zitto tu hata angeshiriki unajuaje angeshinda demokrasia si kuchagua viongozi tu hata kujiunga na chadema ni demokras pia haulazimishwi
 
Bull,Butola Kubwajinga na Waberoya
Naona wengine hapa hamjazungumza siku nyingi na mmepata pa kusemea..Binafsi sina muda wa kubaishana na watu kama ninyi mlioko kazini saa hizi kwasasabu manzozijua ninyi.Nimeirusha hii thread ili watu wahabarike na sio jukwaa la malumbano yasiyokuwa na mashiko..kama mnataka malumbano basi anzisheni thread zenu sio kudandia kwa wenzenu ebo!shit...mkiendeka for sure natuma PM kwa wahusika waifunge thread hii..

GS
You are very right nakugongea....... thanks
 
Bull,Butola Kubwajinga na Waberoya
Naona wengine hapa hamjazungumza siku nyingi na mmepata pa kusemea..Binafsi sina muda wa kubaishana na watu kama ninyi mlioko kazini saa hizi kwasasabu manzozijua ninyi.Nimeirusha hii thread ili watu wahabarike na sio jukwaa la malumbano yasiyokuwa na mashiko..kama mnataka malumbano basi anzisheni thread zenu sio kudandia kwa wenzenu ebo!shit...mkiendeka for sure natuma PM kwa wahusika waifunge thread hii..

Hey!!
Jf nisehemu ya kudadisi mambo kwakina, kama lengola thread yako nikutoa habari tu basi peleka huko kwenye board ya Chadema, hapa jf tunadadisi kiutaalam habari zote.

Kama utaki udadisi, usilete tena thread zako humu jf, peleka hukohuko chadema wanaoshindwa kuandaa na ku-control hata vichaguzi vya vijana wao.
Kama chadema wanashindwa kuzuia fraud ndani ya chama chao, watwezaje kuendesha nchi kama hiii? wacha sensitivity zako za ki-gender zisizo na maana
 
Bull

CHADEMA wanahitaji kupongezwa kwa kutovumilia tuhuma za rushwa wala za kuongezeka kwa wajumbe na kuamua kufuta uchaguzi ule wa mwanzo. Ni dalili njema kuwa wakiingia madarakani hawa watachukua hatua mapema bila kuangaliana sura. CCM mkutano wao wa UVCCM na UWT ilikuwa na rushwa na wizi mtupu lakini pamoja na kuwa walikuwa na usalama wa taifa, TAKUKURU na dola kudhihirisha wazi mambo yote hayo hawakuweza kuchukua hatua. Sasa kati ya CHADEMA na CCM naye ameshindwa kusimamia uchaguzi hapo? CHADEMA imesimamia uchaguzi na kuamua kufikia hatua hata ya kufuta baada ya kubaini kasoro

serayamajimbo
 
Bull,Butola Kubwajinga na Waberoya
Naona wengine hapa hamjazungumza siku nyingi na mmepata pa kusemea..Binafsi sina muda wa kubaishana na watu kama ninyi mlioko kazini saa hizi kwasasabu manzozijua ninyi.Nimeirusha hii thread ili watu wahabarike na sio jukwaa la malumbano yasiyokuwa na mashiko..kama mnataka malumbano basi anzisheni thread zenu sio kudandia kwa wenzenu ebo!shit...mkiendeka for sure natuma PM kwa wahusika waifunge thread hii..

Kumbe wana Chadema mna mkwara hivi? ndio maana hamkosi kutoana nundu.
Lile doa, lileeee kwa wengine halitafutika. Haingii akilini kuwa chama cha demokrasia ili hali hamfanyi uchaguzi wa mwenyekiti. Ile ni aibu ambayo wewe G.S huwezi kuibeba na ndio unaishia hasira tu

Muombe Invisible aweke password nyingine kila zinapowekwa thread za chadema humu ndani. Kwangu mimi mko group moja tu na CCM. Kuanzia vitabia, mienendo yenu, ubwenyenye, uvivu wa kufikiri, kudanganya raia kuwa nyie ni wapinzani na kujipa moyo kwa matumaoni yasiyokuwepo.

You rel need to preach what you can practise. Hamna sababu ya kutofanya uchaguzi wa Mwenyekiti, nardia tena ili kama unatoka povu basi liwe jeupe zaidi. Ukikasirika sana piga ngumi PC yako!

Halafu hizo post hazikutumwa kwako zilitumwa kwa yeyote yule, msalaba wa chadema utauweza mkuu?? wengine huwa wanaanzisha thread kwa lengo la kuto habari hauwaoni tena!

wakereketwa wa vyama mnapata presha humu mpaka nawaonea huruma!!

kipendacho roho

Unakikumbusha mwana CCM mmoja unamwambia nyie mafisadi, anakasirika mpaka anagoma kula! you know what made him angry?? kuwa eti tangu alipoanza kusikia madai ya ufisadi yeye hajawahi kupata mgawo!!!!!!!LMAO!

Naona wewe ndio unaiga tabia typical za Mbowe na wazee wa chama, andika hiyo PM kwa mods .Mbona Mnyika,Kitila hata uwapige swali nasty namna gani huwa hawana hasira nyie wengine siasa mnaijuaje? ukiona watu wauliza hivi ujue wapendwa yakhe! anzisha thread ya NCC R uone kama kuna mtu atachangia! grow up man! politics is all about anything!!
 
Sikutegemea maneno haya yatolewe na Waberoya haya hutolewa na wanawake wanaosutana mabarazani.... kama kimekuuma chukua kamba ujitundike...nk inavyoonekana wewe ndiye roho inayokuuma otherwise unge ignore na kuzungumzia issue.
 
Kwani demokrasia ni kuchaguliwa Zitto tu hata angeshiriki unajuaje angeshinda demokrasia si kuchagua viongozi tu hata kujiunga na chadema ni demokras pia haulazimishwi

WAMEBAKA NA KUDUMAZA KADEMOKRASIA KETU
August@2009

Wakati watanzania walio wengi wanaamka na kuonyesha utayari wa kuchukua jukumu la kuleta mabadiliko ya kweli ambayo yataliwezesha taifa letu kusonga mbele katika harakati za kujenga mfumo wa kidemokrasia nchini, ndugu zetu wa CHADEMA wameamua kubaka na kudumaza mfanikio madogo yaliyoweza kupatikana hadi hivi sasa.

Kwa kifupi tukio la kumshinikiza ama kumshawishi kama ambavyo wanapenda watu wajue, kiongozi wao mahiri Zitto Kabwe kuacha kushindana kidemokrasia na Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe katika kugombea nafasi ya mwenyekiti kinatafsirika kwa maneno machache sana. CHADEMA wamebaka na kudumaza harakati za demokrasia nchini.

Kama kuna chama ambacho watanzania hasa vijana walikuwa na matumaini makubwa ya kuwaondoa katika madhila ya ukiritimba wa miaka mingi ulioshiwa na tija wa CCM, basi chama hicho kilikuwa ni CHADEMA.

Natumia neno kilikuwa na matumaini kwa kuwa naamini kuwa kwa hali ilivyo sasa ni vigumu na kama sio kitu kisichowezekana kwa watanzania kuendelea na imani waliyoanza kuijenga kwa chama hicho kuwa kingeliweza kuwakomboa kutoka kwa maovu ya CCM ambayo yanaonekana kukosa dawa.

CHADEMA wamefanya yale ambayo hata mahasimu wao CCM hawakutegemea kuyaona. Wameweza kutupa baharini nafasi ya kipekee ya kuhakikisha ushindi wa kutosha kwa chama hicho katika chaguzi zinazokuja na kuamua kujichimbia kaburi la kisiasa. Yaani wameamua kujiunga na historia ya vyama ambavyo vilikuwa tishio kwa CCM, kuanzia enzi za NCCR Mageuzi hadi CUF ambavyo kwa sasa vimebaki historia tu kama vyama mbadala vya CCM.

Hapa nisingependa kuzungumzia ni nini CHADEMA ingeweza kufaidika ama kuathirika endapo wangelimchagua Zitto Kabwe kama mwenyekiti wao mpya. Ninachojaribu kuchambua ni faida gani CHADEMA kama chama na wapenda demokraisia nchini wangeliweza kupata na hasara gani ambazo uamuzi wa kumshawishi ama kumshinikiza Zitto kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Ukweli ni kuwa kitendo cha mwanachama mwenye ushawishi mkubwa kama alivyo Zitto Kabwe kuthubutu kusimama kushindana na Mwenyekiti aliyeko madarakani kilifungua nafasi kubwa sana kwa CHADEMA. Kitendo hicho kimeweza kuonyesha kwa vitendo kuwa chama chao ni kweli chama cha demokrasia na maendeleo na maneno hayo sio kauli mbiu tu.
Wapo watu wengi, vijana kwa wazee ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na CHADEMA.

Na kama ilivyo utamaduni wa watanzania, wengi wao bado walikuwa wanasubiri uhakikisho kuwa CHADEMA ni mbadala makini wa CCM ili wajiunge katika harakati za kuleta mabadiliko makubwa kisiasa. Wengi wao kuingia kwa Zitto katika kinyang'anyiro hicho ilikuwa ni ishara kuwa CHADEMA inaweza kuaminiwa kwa yale wanayoyasema kwani wanaonyesha kuyatenda.

Ukiangalia kwa undani utaghamua kuwa kule kuingia tu katika kinyang'anyiro hicho kwa Zitto Kabwe kulikuwa ni mtaji mkubwa kwa CHADEMA na zaidi kwa maendeleo ya demokrasia nchini.

Kitendo cha Zitto Kabwe ambaye amekuwa kama kioo cha mafanikio ya wanasiasa vijana wenye uthubutu wa kusimama kupambana na mfumo kandamizi uliokuwa ukiwatisha kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani kuthubutu kuingia katika kinyang'anyiro hicho kulikuwa ni mwaliko wa wazi kwa maelfu ya vijana kujiunga na CHADEMA.

Kama CHADEMA wangeweza kuendelea na kufanya uchaguzi wao na mwishoni mshindwa akamkumbatia mshindi basi ni wazi hilo lingejenga imani kubwa kwa chama hicho miongoni mwa wapenda mabadiliko makini ambao hadi sasa wanashindwa kuamini vyama vyetu vya kisiasa na wanasiasa kwa ujumla.

Kwa watanzania ambao tungependa kuona kunakuwa na mfumo ambao unawezesha nchi yetu kuwa na demokrasia ya kweli yenye kujenga umakini wa kisiasa katika kuchagua viongozi wetu na kufanya maamuzi makubwa na madogo ya kikatiba, kisheria, kisera, kifalsafa na kiutawala. Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na chama ambacho kitaweza kwanza kuondoa ukiritimba wa CCM katika vyombo vya maamuzi na baadae kutupa chaguo mbadala pale itakapowezekana kubadilisha chama tawala.

CHADEMA ilishaanza kujenga muono huo miongoni mwa watanzania walio wengi. Zitto Kabwe ni mmoja wa watu ndani ya CHADEMA ambao wameweza kujenga hisia miongoni mwa jamii kuwa kama wangendelea vizuri ni muonekano wa kidemokrasia na maendeleo, basi wangeweza kujenga imani miongoni watanzania hao. Yaani CHADEMA walikuwa ndio wanaelekea katika kufanikiwa kujenga imani kuwa lipo chaguo mbadala la CCM katika nchi yetu.

Ukweli ni kwamba baada ya kuyafanya waliyoyafanya, ni wazi kama ilivyo vigumu kwa viongozi wa CCM kuzungumzia vita dhidi ya ufasadi mbele ya watanzania, kwa CHADEMA itakuwa ni vigumu kwa viongozi wao kusimama kuongelea umuhimu wa demokrasia na kupiga vita ukandamizaji nchini na kuaminika ama hata kueleweka.

Ni wazi CHADEMA wamejifunga uhalali hata wa kuongelea UFISADI ambayo imekuwa ajenda yao muhimu katika miaka ya kariuni. Kwani hapa wameonyesha ufisadi wa hali ya juu dhidi ya misingi ya kidemkrasia ambayo ina nafasi kubwa katika kufikia maamuzi ya kisiasa miongoni wa wapenda mabadiliko katika nchi yetu.

Kitendo walichokifanya, tena kwa kumkandamiza Zitto Kabwe ambaye ni alama ya uthubutu na umakini miongoni mwa vijana ambao ndio mtaji mkuu katika chaguzi zinazokuja, CHADEMA wamewaondolea hata nafasi waliyokuwa nao baadhi ya vijana wao katika kushinda kwenye chaguzi zijazo.

Ni wazi kutokana na hali iliyotokea kuanzia sasa itakuwa vigumu sana kwa vijana wa CHADEMA ambao walikuwa nyota zinazotegemewa kubadili sura ya siasa katika uchaguzi ujao kuweza kuwashinda vijana wenzao wa CCM. Hii inatokana na ukweli kuwa hata wao o wamejijengea taswira ya ama kuunga mkono, kubariki ama kunyamazia nguvu za wazee ndani ya chama chao zikifisadisha misingi ya kidemorasia ambayo wao walipaswa vijana hao walipaswa kusimama kidete kuitetea na kuipigania. Ni wazi kuwa kuanzia sasa itakuwa vigumu kwa vijana wa CCM kusimama mbele ya vijana wenzao katika chaguzi zijazo na kuwashawishi kuwa wao ndio chaguo la mabadiliko ya kweli.

Zaidi, sababu ya kumshikiza Zitto kuacha kushindana na Mwenyekiti wao aliyekuwepo madarakani ili kuepusha mpasuko ndani ya chama ni sababu inayoleta maswali zaidi ya majibu.

Kwa chama ambacho kinasema kinapigania demokrasia na maendeleo nchi kuamini kuwa kuwaacha viongozi wawili kushinda katika uchaguzi ni tishio la umoja wa chama ni sawa na kukubaliana na fikiria mgando zilizomo miongoni mwa wahafidhina ndani ya CCM kuwa kuruhusu ushindani wa haki na huru kati ya vyama vya siasa nchini ni kuhatarisha amani na maelewano ya nchi yetu.

Pia, kusema kuwa Mbowe akipata mshindani mkali kutaleta mtafaruku ndani ya chama kunatoa sura ya ama wazee kumuogopa Mbowe ama kukiri kuwa CHADEMA hawawezi kufanya siasa za kiungwana na zisizo na chuki ambazo zingeleta mgawanyiko. Ni wazi fikira kama hizo sio tu zitazuia wengi wengine kujiunga na chama hicho lakini pia si ajabu tukasikia kuendelea kwa mlolongo wa wanachama na viongozi wa chama hicho kuondoka na kwenda kujiunga na jinamizi walilolizoea yaani CCM.

Ndio maana baada ya kuona hili nimekuwa nikijiuliza sana ukweli wa sababu za viongozi na wanachama kadhaa wa CHADEMA ama kuhama, kusimamishwa ama kufukuzwa uanachama katika miaka ya karibuni. Nimekuwa nikijiuliza kama ni kweli hawa walikuwa vidudu mtu vinavyohatarisha ustawi wa chama ama kuna tatizo la kiuongozi ndani ya chama hiki. Kutokana na maamuzi yaliyofanyika hivi karibuni nachelea kuamini kuwa wapo walio ondoka CHADEMA baada ya kushindwa kuvumilia kuvunjika moyo katika nia yao ya kujenga mabadiliko ya ndani ili kuweza kushawishi mabadiliko ya nje.

Na katika hili, ni wazi muathirika si Zitto, si Mbowe na wala sio CHADEMA tu bali ni mustakali mzima wa mapambano ya kujenga demokrasia nchini.

Kitendo cha kuonyesha taswira ya kuwa kuna uwezekano wa kiongozi wa CHADEMA kuwa tayari kutumia mbinu zozote zile, halali na haramu, makini na hovyohovyo, salama na hatari ili kulinda nafasi yake kileleni, kinaonyesha kuwa ile ndoto ya vyama vya upinzani kuungana ili kukishinda chama dola cha CCM zinaendelea kubaki hivyo, yaani ni ndoto tu.

Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa kitendo hiki kinahalalisha propaganda ya CCM na dola kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wamegubikwa na ubinafsi na hawana nia ya kuwakomboa watanzania kama wasemavyo.

Na hapa napenda kuwashauri wana CHADEMA kuacha kutumia ujanja wa CCM kama sababu ya yaliyotokea na yanayoendelea kuwakumba. Kufanya hivyo ni sawa na kuwaunga mkono watwala wetu wa sasa ambao daima hawachoki kuwalaumu wazungu ama wakoloni kwa umasikini na madhila waliyowezesha katika nchi yetu kutokana na makosa yao wenyewe. Ilichofanya CHADEMA ni kujianika mbele ya mashamulizi ya CCM na maadui wengi. Na itakuwa ajabu sana kama madui hao wataacha nafasi hii kuwashambulia na hata kuwamaliza kabisa wakati huu nyeti wa kuelekea katika chaguzi za kitaifa.

Zaidi, kitendo walichokifanya CHADEMA kinawapa nafasi na nguvu zaidi maadui wa demokrasia kuendelea kudhihaki harakati za demokrasia nchini. Wapo ambao wamekuwa wakipita mitaani kusema kuwa wanaopiga kelele kutaka demokrasia hawana nia ya kweli ya kuleta demokrasia ya kweli bali ni mbinu tu ya kuweza kujipatia madaraka na baadae kufanya yaleyale ambayo wanayalalamikia wakati wasipokuwa madarakani.

Hatua ya kumshikinikiza Zitto Kabwe kutotumia haki yake ya kidemokrasia ya kuomba ridhaa ya kuongoza chama chake kwa wanachama wenzake kinahalalisha mitazamo ya maadui wa demokrsia kama hao.

Ni wazi, uamuzi wa wazee wa CHADEMA kumshinikiza Zitto Kabwe kujitoa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chake kwa kuhofia uwepo wa siasa chafu zitakazoweza kugawanya chama chao ulichofanikiwa ni kuhalalisha matumizi ya siasa chafu na hovyohovyo na hivyo kudumaza kabisa ndoto na juhudi za watanzania wanaopenda kuona mfumo wa demokrasia makini unatawala nchini mwetu.

Baada ya kufuatilia kwa karibu mwenendo wa siasa zetu wakati wa uchaguzi uliopita (2005) na baadae kupata taarifa za ufisadi mkubwa uliokuwa na na bado unaendelea katika nchi yetu mara baada utawala Mwalimu Nyerere, nilikuja katika hitimisho kuwa CCM na wadau wake wamelibaka taifa letu, na sasa nachelea kuhitimisha kuwa CHADEMA wamebaka kademkorasia ketu ambako katika miaka ya hivi karibuni tulianza kujenga imani na matarajio nako.
 
Bull,Waberoya,Omar!nawasikitikia sana..inaonyesha ni jinsi gani roho zinavyowauma maskini weee poleni sana ndio ukubwa huo!Siasa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.. Hata mkisema humu haisaidii kwani uchuguzi ulishafutwa na sasa umetangazwa upya anyetaka aende akajaze fomu..UKWELI UTBAKI KUWA UKWELI MILELE hata mkijitahdi kupotosha..Haki wakati mwingine inagombewa hata kwa ngumi ni jambo la kawaida..Ngumi ngumi tu mpaka kieleweke!
 
Sikutegemea maneno haya yatolewe na Waberoya haya hutolewa na wanawake wanaosutana mabarazani.... kama kimekuuma chukua kamba ujitundike...nk inavyoonekana wewe ndiye roho inayokuuma otherwise unge ignore na kuzungumzia issue.

ujajibu hoja, kwanza nani kakuambia mimi mwanaume? ni ignore kesho mkishika nchi yatokee kama ya kenya?

Bull,Waberoya,Omar!nawasikitikia sana..inaonyesha ni jinsi gani roho zinavyowauma maskini weee poleni sana ndio ukubwa huo!Siasa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.. Hata mkisema humu haisaidii kwani uchuguzi ulishafutwa na sasa umetangazwa upya anyetaka aende akajaze fomu..UKWELI UTBAKI KUWA UKWELI MILELE hata mkijitahdi kupotosha..Haki wakati mwingine inagombewa hata kwa ngumi ni jambo la kawaida..Ngumi ngumi tu mpaka kieleweke!

ona tofauti yako wewe na SERA YA MAJIMBO hapo juu, hapa ni kujibu hoja au kukaa kimya. ulichoandika hapa hakiondoi ukweli kuwa uchanguzi wa mwenyekiti hamkufanya na hili linawadisqualify kuwa nyie ni chama cha demokarsia. ndio tumeuliza kwa nini msimteue tu huyo mwenyekiti wa vijana tuwaze uchaguzi mkuu?

you know what, mimi kuandika hapa hakuipunguzii chadema chochote , wala member 10000 wa JF wote wakipiga kura ni negligible comparing na milioni 40 huko.This challenge meant to make you improve and see reality.

yaliyotokea humo ndio mtaji wa CCM kupigiwa kura! sasa wewe gombana na watu humu ukose usingizi,
 
Kila la Kheri CHADEMA katika uchaguzi wa Baraza la Vijana BAVICHA
 
Back
Top Bottom