Baraza la Vijana CHADEMA latangaza Uchaguzi wake wa Marudio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Vijana CHADEMA latangaza Uchaguzi wake wa Marudio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Feb 7, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Feb 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Habari nilizozipata ni kuwa Baraza La Vijana CHADEMA(BAVICHA) limetangaza uchaguzi wa ngazi ya taifa ambao ulifanyika mwezi agosti lakini ukafutwa..Habari zilizonifikia ni kuwa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu linaanza tarehe 8 mpaka 22 mwezi huu.Vijana wote wa CHADEMA wenye nia ya kugombea wameombwa wajitokeze kufanya hivyo.Fomu zitapatikana katika ofisi zote za CHADEMA za mikoa na Makao Makuu ya chama hicho..
   
 2. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakuja kuchukua fomu...
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Wa mwenyekiti wa chama lini vile?
   
 4. b

  bambumbile Senior Member

  #4
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wataurudia mpaka wampate anayekubaliwa na wenye CHAMA. Hiki eti ndio chama mbadala cha kumkomboa Mtanzania, what a joke!
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Feb 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  huo ni ulongo na ufitini kama si majungu...............huu ni uchaguzi baada ya ule wa kwanza kuvurugwa, wewe ulitegemea nini katika uchaguzi ambao kura zilizidi wapiga kura....?
   
 6. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 901
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  ...hatugawi fomu hapa lakini nakushauri ukachukue huko.
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 901
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  That's a good move, keep it up CHADEMA.
   
 8. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna haja gani ya kufanya uchaguzi kama akishinda asiyekubalika kwa vingunge wa chama uchaguzi utarudiwa tena? Si wampe tu wanayemtaka na kuacha kutuzuga na kutupotezea muda wetu?
   
 9. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 463
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi nafikiri uchaguzi wowote ule lazima uwe fair na uwe wazi, the last tatizo lililojitokeza ni kwamba final results ilionyesha kuwa kura zilizidi watu waliopiga au waliokuwepo so kwa vigezo hivo ungempa ushindi aliyeshinda ina maana the whole election isingekuwa na legitimacy yoyote ile. Mimi nafikiri ni jambo la busara na lilikuwa jambo la busara kufuta matokeo na kwenda kwenye episode nyingine ambayo ni ya marudio.

  Hii inaonyesh kupevuka na pia inaonyesha the integrity democrasy ndani ya chama, ni mfano wa kuigwa.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  For sure wewe ni kubwa jinga hata hujui kinachoendela unakurupuka tu.
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa wajumbe wenye sifa ya kupiga kura walikuwa wanajulikana kwanini wasingerudia tena kupiga kura ndani ya muda wa uchaguzi ule?? haihitaji kuwa na akili kubwa kujua kuwa kama wajumbe walikuwa wanajulikana na walikuwa hawazidi 2000 unaweza kabisa kurudia kupiga kura na hasi-cheat ata mpiga kura mmoja.

  Tatizo halikuwa hilo, tatizo ambalo hawawezi kulisema ni kuwa aliyeshinda na ambaye waliamini angeweza kushinda endapo uchaguzi ungefanyika kipindi kile siye mtu ambaye viongozi wakuu wa chama walimtaka, na kwa kuwa hawakuwa tayari kufanya nae kazi wakaona pamoja na gharama za kurudisha wajumbe Dar kwa uchaguzi mara ya pili ni bora uchaguzi uhairishwe kwanza mpaka mazingira yatakaporuhusu kumpata wanayemtaka wao.

  Viongozi wa Chadema kama wanataka chama kikue na kutimiza lengo la kuchukua dola wanapaswa kujifunza kufanya kazi pia na watu wenye fikra na mitazamo tofauti, hauwezi kujenga chama kwa kuwa tu na watu ambao mnakubaliana nao muda wote bali kwa kuwa na watu wanaokukosoa na kukupa changamoto, kwani wanakupa nafasi ya kujitathmini na kujisahihisha.
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Acha kupotosha ndugu yangu..ukweli sio huo unaoudai wewe..Ukweli ni kwamba idadi ya kura ilizidi waliohudhuria.Isingewezekana kurudia kwa muda ule kwasababu mbalimbali moja ikiwa ni gharama za uchaguzi lakini pia muda hakuwepo kwani CHADEMA ilikuwa na chaguzi nyingine..Lakini pili ilikuwa ni vyema kujipanga vizuri ili kuzuia kurudia makosa yale yale...ndugu yangu kubali tu ukweli ulishindwa na umeshindwa na umefulia fanya mabo mengine haya hayatakusaidia hata kidogo.
   
 13. B

  Bull JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Kijichama fisadi! Chadema wanafanya ufisadi ktk uchaguzi mdogo wa vijana na wanashindwa ku control kura mpaka zinaibiwa, uchaguzi unarudiwarudiwa kweli hiki ni chama kinaweza kuendesha nchi? chadema ni kichekesho !!

  Say no to CHADEMA, wanashindwa kusimamia uchaguzi wa vijana wao! wataweza nini?
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kama kura zilizidi, kwanini wasingerudia kupiga kura kwa uhakiki yakinifu wa kila anayepiga kura? Hivi haujui kuwa kwa kuhairisha uchaguzi gharama zinakuwa ni kubwa zaidi kuliko kurudia kupiga kura?

  Kujipanga upya Yes, ilikuwa ni muhimu ku-buy time mpaka mazingira yatakabadilika ili kuruhusu kuchagulika mtu anayetakiwa na viongozi, , hii ndiyo sababu pekee inayoingia akilini ukizingatia kuwa hili lilikuwa shakani kama uchaguzi ungefanyika wakati ule, lakini matokeo ya mtazamo kama huu ni kupoteza credibility ya chama kwa wananchi na kukosa fursa ya kupata watu makini wenye mawazo huru na matokeo yake kubakia na kina ndiyo mzee.

  Usijifanye unanijua kaka/dada...
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu hatuko hapa katika kutukanana ama kubishana..tuko hapa katika kupashana habari na si vingenevyo..wewe kama unayako ishia zako..UMEFULIA.Teh teh teh.Vipi umemaliza kufanya mikatano yako ya hadhara?
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unafahamu ni muda gani uchaguzi wa BAVICHA ulimalizika ni usiku wa manane kwa siku hiyo isingewezekana kurudiwa unasema kuahirisha ni gharama kuliko kurudia kama unasema kurudia kabla ya wajumbe kusambaa inawezekana lakini hiyo itakuwa gharama zaidi

  kwa sababu itabidi wajumbe wagharimiwe posho ya kawaida na overtime juu na booking zote za malazi usafiri ziwe cancelled na hela hairudishwi na vile vile inategemea na wajumbe ambao ni wafanyakazi maana likizo yao inabidi pia wa extend kwa siku kadhaa kwa hiyo kazi si rahisi kama unavofikiri
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Nauliza hivi! hiivi,kuwa uchaguzi wa mwenyekiti unaanyika lini? kipi bora mwenyekiti au kiognozi wa vijana? kwa nini wazee wasimweke tu huyo wanaemtaka??

  nitauliza mpaka nijue uchaguzi wa mnweyekiti ni lini!
   
 18. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hivi unajua kuwa kwenye chaguzi za CHADEMA mshindi ni lazima apate 50%?hivi inaingia kweli akilini kuwa chama makini ambacho kinajua kina kanuni kama hiyo kinaweza kupanga ratiba ya uchaguzi mkuu wa kitaifa uliojumuisha wajumbe toka mikoa 26 ya nchi kwa gharama kubwa sana bila kuweka "Factor of Safety" in case upigaji kura unarudiwa? hilo haliwezi kutokea katika hali ya kawaida unless kuna suala nyeti sana kwa maslahi ya wenye chama ambalo haliwezi kutolewa hadharani.
   
 19. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Gender S, Kwani kinachoendelea ni kipi tusichokijua maana tunavyofahamu ni kuwa uchaguzi unarudiwa kwa sababu aliyechaguliwa hapo awali hakukubalika na wenye chama. Hivi unafikiri kuna kijana yeyote atakayegombea uongozi kama sio chaguo la wenye kampuni? Kwani wao hawaogopi kufukuzwa chamani kama mwenzao aliyefikiri CHADEMA kuna demokrasia badala yake akapigwa nyundo?
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Luteni, Na wewe una sababu za kitoto kwelikweli. Huo uchaguzi ulifanyikia wapi ambapo usiku unakimbiwa? Si ukubali tu kuwa wenye chama walimzima mshikaji wake Zitto?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...