A
Anonymous
Guest
Mimi naitwa Matson Mathias Ngonyani ni Baba wa Watoto wanne na nina ulemavu wa masikio, kitaaluma ni Afisa Muuguzi niliajiriwa na Wizara ya Afya Mwaka 2019 kisha nikahamishiwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) kwa mpango wa kuazimwa Mwaka 2021.
Nilipohamia Dodoma katika Ofisi ya TNMC nilifanya kazi vizuri tu lakini baadaye nilianza kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubaguzi.
Ilipofika Mwaka 2022 niliomba kuhama kwenda OSHA akini sikufanikiwa kuhama.
Mwaka 2023 nilipewa tuhuma za ajabu ambazo ni dhahiri kwamba zilitengenezwa ili kuniondoa kazini.
Sehemu niliyokuwa nafanyia kazi walikuwa na jukumu la kuandaa mitihani ya leseni na usajili kwa wauguzi. Jambo lilitokea ni kwamba Mkuu wa Idara alifanya uzembe kwa kutozingatia utaratibu unaotakiwa.
Kawaida zoezi la uaandaji hufanywa na Watu Maalumu kwa kutumia Computer maalumu za ofisi lakini kilichofanyika katika maandalizi ya mtihani huo ni tofauti.
Hakukuwa na Maafisa usalama na ulinzi, mtihani uliovuja ulikuwa ukiandaliwa na mtumishi ambaye alikuwa anatumia laptop yake binafsi. Jambo ambalo ni kinyume na utaratibu. Kilichotokea ni kwamba laptop ya Mtumishi yule ili-collapse katika jitihada za kujaribu kurekebisha laptop kwa mafundi, maswali yakavuja.
Lakini kilichofanyika ni ukiukwaji wa haki kwa kuendesha shauri bila kuzingatia taratibu sahihi;
Mfano
Walinituhumu kwa makosa ya jinai yasiyo na ushahidi wa moja kwa moja, na kuamua kutumia Polisi kunikamata kuniweka mahabusu na kunipa mateso ili nikiri kosa kwa siku nne.
Yaani waliniandikisha maelezo kisha kunilazimisha kusaini na nilipoomba kesi iende Mahakamani walipuuza, hivyo walitumia maelezo yale batili kunihukumu Ofisini badala ya Mahakamani.
Mtihani uliandaliwa na watumishi watatu ambao walifanya uzembe kwa kutumia laptop binafsi lakini hawajaguswa.
Katika mahojiano na kamati ya uchunguzi pamoja na kwamba mwajiri alijua fika changamoto yangu ya usikivu nilipoomba niwe na Mwanasheria kwa ajili ya kunitetea walipuuza.
Katika mahojiano hayo mwajiri aliandaa mashahidi watatu ambao ni Wanafunzi wenye historia ya kufeli mtihani huo zaidi ya mara 3 hadi 4.
Hawakuwa na ushahidi wowote na wala hakuna aliyeonyesha ushahidi wowote lakini katika mwenendo wameandika tofauti.
Jambo la kutia shaka ni kwamba mashahidi wale wote baada ya kushuhudia na kusema uongo tarehe 15 Februari 2024 na siku ya pili yaani 16 Februari 2024 walifanya tena mtihani na wote watatu walifaulu😭.
Baada ya mahojiano yale mwajiri alishindwa kuonyesha ushahidi thabiti na aliomba mbele ya kamati kwamba anaomba MAMBO YALE YASIENDE JUU.
Ilipofika Mwezi Machi 2024 nilirudishwa kazini lakini katika barua hiyo ilieleza kwamba nimepatikana na hatia 2 kati ya 5, hivyo mwajiri ameamua kunipa adhabu ya kukatwa mshahara Asilimia 15 kwa miaka 3, nilistaajabu sana.
Niliomba nakala ya Hukumu / mwenendo wa shauri kwa barua lakini cha kusikitisha nikakataliwa.
Baada ya kunyimwa mwenendo wa shauri nilikata RUFAA kwenda Tume ya Utumishi wa Umma lakini sikueleza kiundani sakata hilo nikitarajia pengine Tume ingeniita na kunisikiliza lakini haikuwa hivyo.
Nilikata RUFAA Aprili 2024 lakini nilijibiwa October 2024, sikuitwa kusikilizwa wala kuonyeshwa ushahidi badala yake nikapewa barua ya kuachishwa kazi.
Tarehe 12/12/2024 nilikata RUFAA kwenda kwa Ofisi ya Rais kupitia KATIBU MKUU KIONGOZI.
Nilikaa nakusubiri majibu kwa muda mrefu huku nikiandika/ barua ya kukumbushia majibu zaidi ya mara 8. Sikupata majibu. Mwezi Agosti 2025 nilifika Chamwino Ikulu kwa ajili ya kukumbushia hapo nilijulishwa kwamba Ofisi ilitoa majibu ya awali tangu tarehe 28 Januari 2025 kunijulisha kwamba Rufaa imepokelewa na nakala zilienda kwa Mamlaka ya Nidhamu na Tume ya Utumishi wa Umma zikiwapa maelekezo wawasilishe vielelezo vilivyotumika.
Jambo la kushangaza ni kwamba barua hiyo ilipofika nilipokuwa nafanyia kazi ILIFICHWA na nikaipata baada ya miezi nane😭
Hii hapa barua ya majibu awali Januari 28 lakini nilipata Agosti 2025.
Mamlaka hizo hazijawasilisha vielelezo vilivyotumika hadi leo miezi 12.
Nilifanya ufuatiliaji Tume ya Utumishi wa Umma walikiri kwamba waliwasilisha vielelezo ingawa walinilaumu kwamba sikujieleza kwa kina kwenye barua ya Rufaa kwenda kwao katika Rufaa ya Awali ndio maana walifanya maamuzi wakidhani taratibu zilifuatwa.
Hivyo, niliambiwa kwa kuwa wao tayari kwao ilipita basi nifuatilie tu Ofisi ya KATIBU MKUU KIONGOZI.
Hadi sasa ninavyoandika ujumbe huu jambo langu lina miaka 2.5 na Rufaa yangu kwa KMK ina siku 380 sijapata majibu.
Napata shida sina chanzo cha mapato familia inanitegemea sina mtetezi.