Wakenya wapo mbali kielimu pia hata kimtazamo, japo ni mabepari wao maslahi ya taifa mbele kwanza
hapo sioni kama kuna maslahi ya taifa mbele. kila mtu yuko bize kujilimbikizia kwa kadri awezavyo na pia kusambaza faida hiyo kwa jamii yake na siyo kwa taifa.
kila kukicha ni ugomvi wa makabila na maeneo, kila kabila/jamii/eneo wanataka mtu wao akae sehemu yenye maslahi ili arudishe maendeleo kwa jamii/kabila/eneo lake. hapo ndiyo kuna maslahi ya taifa kweli?
wangeshughulikia matatizo ya inequality kati ya maeneo/makabila na maswala ya ardhi na katiba inayotoa fursa sawa kwa wakenya wote bila kuipendelea serikali iliyo madarakani ningeweza kusema kwamba kweli hawa jamaa wameweka maslahi ya taifa mbele!