Baraza la Mawaziri SADC, Laridhia Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu, Kudhibiti Maambukizi ya Corona

Baraza la Mawaziri SADC, Laridhia Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu, Kudhibiti Maambukizi ya Corona

Joined
Apr 4, 2020
Posts
16
Reaction score
7
1586275668753.png


Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), limeridhia usafirishaji wa bidhaa muhimu katika ukanda huo wakati wa janga la homa ya mapafu (Covid-19) ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa nchi wanachama.

Akizungumza katika Mkutano wa dharura wa Maafisa Waandamizi wa SADC, kuhusu Covid-19, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC na Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Tanzania, Prof.Palamagamba kabudi alisema kuwa Baraza limepitisha mapendekezo ya Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Afya uliofanyika Machi 9, 2020, Dar es Salaam, Tanzania.

“Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Afya wa tarehe 9, Machi 2020, ulitoa mapendekezo ambayo yamefanyiwa kazi na Mkutano wa Baraza la Mawaziri yakiwa ni ufuatiliaji na utekelezaji masuala ya afya kuhusu mlipuko wa Covid-19, kujadili namna ya kujiandaa na kukabiliana na virusi vya Covid -19,kubaini wagonjwa na kufuatilia waliokutana nao na huduma za tiba katika ukanda wetu” Alisema Prof. Kabudi.

Alisema masuala mengine ni uchunguzi na upimaji wa kimaabara, uzuiaji na udhibiti wa maambukizi, uelimishaji wa madhara na ushirikishaji wa jamii, uratibu wa kikanda wa kukabiliana na Covid-19, uwezeshaji na usafirishaji wa bidhaa muhimu katika ukanda huo wa SADC wakati huu wa Covid-19.

Mengine yaliyopitishwa ni Covid-19 na uwezeshaji wa biashara, Covid-19 na masuala ya udhibiti biashara na usimamizi wa majanga hatarishi katika ukanda huo wa Nchi za Kusini mwa Afrika, mapendekezo hayo yanatokana na ukweli kwamba Covid-19 imeendelea kusambaa duniani kwa hiyo Jumuiya ikaona iweke mikakati madhubuti kukabiliana na ugonjwa huo.

“Mkutano huu wa Baraza la Mawaziri SADC uliitishwa kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi na vifo katika baadhi ya nchi Duniani, kwa mujibu wa taarifa namba 76 ya Shirika la Afya Duniani(WHO), ya April 5, 2020 inaeleza kuwa takribani watu 1,133,759 wameambukizwa ugonjwa huo na kati ya hao matukio mapya ni 82,061 na vifo 62,784 huku Afrika kwa nchi 51 kuna wagonjwa 9,198 na vifo viko chini ya watu 500, lakini kwa ukanda wetu wa SADC kuna matukio 2,127 katika nchi 14 huku vifo vikiwa 38” Alisema Prof.Kabudi.

Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri uliofanyika sambamba na Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa SADC ulilenga katika kupokea taarifa ya wataalamu pamoja na muongozo wa urazinishaji na uwezeshaji usafirishaji wa bidhaa muhimu na huduma katika nchi za SADC wakati huu wa mlipuko wa Covid-19.

Bidhaa zilizopitishwa kwenye muongozo ni pamoja na usafirishaji wa vyakula, vifaa tiba, Dawa na vifaa vya kujinga na Corona, mafuta na mkaa wa mawe, pembejeo za kilimo na madawa, vifungashio, bidhaa zote zinazotumika katika utengenezaji, uchakataji na uhifadhi wa vyakula na vifaa ambavyo vinahusu usalama na dharura kwenye majanga mbalimbali.

Prof. Kabudi aliongeza kuwa SADC wamefanya hivyo ili kuzuia kuenea kwa Covid-19 na kuwezesha utekelezaji mikakati ya kitaifa ya kupambana na ugonjwa huo na kuwezesha upatikana wa bidhaa muhimu ili kuzuia usafirishaji usio wa lazima kwa abirika katika ukanda huo wa Afrika .
 
Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
 
What is SADC, takataka tupu! Sana sana wanakwenda kufanya shopping za wake zao na mahala. I can imagine EU foreign Ministers meeting to deliberate on Corona??????
 
https://dailynews.co.tz/news/2020-04-075e8cab35a8f8c.aspx
Burundi iliamua kupiga marufuku Gari zote zinazopitia Rwanda kuingia Burundi kwa hofu ya kuingiza Virusi vya Corona nchini Burundi.

Katika kujibu mapiga, Rwanda ilizijulisha Kenya na Uganda kwamba, nchi hiyo haitoruhusu mzigo wowote unaokwenda Burundi kupitia katika ardhi yake.

Huku nchi za EAC kila moja ikipiga vita kwa mpango wake, ikiwemo kujitengenezea vifaa tiba vya kupambana na Corona kwa matumizi yake binafsi, nchi za SADC zimekubaliana kupambana kwa kushirikian, kujua nani anatengeneza nini, na nchi gani inahitaji nini ili kusaidiana.

Pia wamekubaliana kuruhusu bidhaa na biashara kuendelea kufanyika bila vikwazo vyovyote ili kupunguza athari za kiuchumi zinazosababishwa na Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
https://dailynews.co.tz/news/2020-04-075e8cab35a8f8c.aspx
Burundi iliamua kupiga marufuku Gari zote zinazopitia Rwanda kuingia Burundi kwa hofu ya kuingiza Virusi vya Corona nchini Burundi.

Katika kujibu mapiga, Rwanda ilizijulisha Kenya na Uganda kwamba, nchi hiyo haitoruhusu mzigo wowote unaokwenda Burundi kupitia katika ardhi yake.

Huku nchi za EAC kila moja ikipiga vita kwa mpango wake, ikiwemo kujitengenezea vifaa tiba vya kupambana na Corona kwa matumizi yake binafsi, nchi za SADC zimekubaliana kupambana kwa kushirikian, kujua nani anatengeneza nini, na nchi gani inahitaji nini ili kusaidiana.

Pia wamekubaliana kuruhusu bidhaa na biashara kuendelea kufanyika bila vikwazo vyovyote ili kupunguza athari za kiuchumi zinazosababishwa na Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua wakati mwingine busara inaweza kutatua yanayoendelea sasa EAC! Sasa imagine Uganda na Rwanda wanafungiana mipaka halafu Burundi na Rwanda pia! Ila zote ni nchi landlocked na zinategemea nchi zenye bahari kama Tanzania na Kenya! Kiufupi magari yanayoenda Burundi kwa kupitia Rwanda ni yale yatokayo bandari Mombasa na pia yale yanayoenda Rwanda kupitia Uganda! Yaani yanatumia Northern corridor! An alternative central corridor is open for them!
 
Tanzania na Kenya zikifunga mipaka kuna nchi zitaangua kilio
 
Back
Top Bottom