SERIKALI IMEWATENDEA MADAKTARI NDIVYO SIVYO: AIBU
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiyaya madaktari nchini Dk Steven Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa katikamsitu wa pande.Watanzania mnaelewa usaniiulioendelea kufanywa na watawala. Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa mudausiojulikana huku filamu ya danganya toto za Mkenya kutajwa kuhusika nakumteka, kumtesa na kumtupa Dk Ulimboka katika msitu wa pande, ikichezwa nakamanda Kova. Lakini pia mahakama imetumika kama kichaka cha kujificha nakuwafunga watu midomo wasizungumze. Tunajua si hili tu ila yapo matukio mengiya ukatili na yanayokiuka haki za binaadamu ambayo yamepelekwa mahakamanilakini kila mtu anelewa kuwa hakuna nia ya dhati ya kuwashughulikia wahusikaila hisia inayojitokeza na huenda ikawa ndiyo nia halisi ni kuwafunga watu midomo. Funika chungu mwanaharamu apite. Kwa maneno mengine ni upepo tuutapita.Mgomo wa madaktari ulilengakuishinikiza serikali kuboresha huduma za afya ikiwemo madawa, vifaatiba na uboreshwajiwa mazingira ya kazi. Hii ikiwa ni pamoja na kuboresha majengo ya hospitali,zahanati na vituo vya afya vikienda sambamba na uboreshaji au ununuzi wa vifaamuhimu kama CT scan, mashine za X-ray na uongezwaji wa vitanda kwa wagonjwakuepukana na tatizo la wagonjwa kulala chini hata katika hospitali ya TaifaMuhimbili achilia mbali hospitali zilizopo mikoani maana hali inafahamika.Lakini pia madaktari waliitakaserikali kuongeza mishahara na posho mbalimbali ili ziendane na hali ya maishaya sasa. Yaliyotokea sote tunajua. Vitisho na ubabe vilitawala huku baadhi yaviongozi waandamizi wa serikali wakitoa matamko ya kuvunja moyo "asiyetaka kazi aache, serikali haina uwezo" Ninakumbuka vema madaktarihawakuishia kuainisha madai yao ya msingi ila walitoa mapendekezo ya kiwangocha mshahara na posho mbalimbali. Hili ni jambo la kawaida mahali popoteduniani. Hata makampuni ya uchimbaji madini hutoa mapendekezo ya kiwangoyanachoweza kuilipa serikali halafu serikali nayo huangalia na kuamua kuikubaliau kuzungumza zaidi na hatimaye kuelewana. Inakumbukwa vizuri serikali ilitumiamahakama, vitisho na matamko ambayo hayakulenga kutatua mgogoro wake namadaktari.
Vitisho na unyama uliofanyika ni wazi kuwa hakukuwa na nia ya dhatiya kutatua tatizo. Madaktari waliokuwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa(interns) ambao kwa kiasi kikubwa ndio hufanya kazi nyingi katika hospitali takribanizote za rufaa hapa nchini walifukzwa maeneo ya kazi.Baada ya tukio hilo ni wazi kuwa madaktaripia waligawanyika na kupoteza mwelekeo. Siwalaumu ila nadhani kutokea kwa hilolilikuwa haliepukiki maana kama wasingepoteza muelekeo na kugawanyika huendayangetokea yale yaliyotokea nchi za Tunisia na Misri. Kwa namna moja aunyingine japo haki na madai ya madaktari yamekandamizwa na kuzimwa kwa sasa lakini nadhani wameepushamauaji na vita kati ya serikali na wananchi. Ni kweli vita hii si njema lakinipale watawala wanapoiomba kutoka kwa wananchi kwa kuwanyamazisha nakuwakandamiza basi ni afadhali vita ya aina hiyo kuliko mateso kwa wananchi,tena mateso yanayofanyiwa na watu waliowachagua kama viongozi wengi wanavyodai.Japo ni wazi kuwa si wote wanaochaguliwa na wananchi.Madaktari zaidi ya 394walisimamishwa kwa zaidi ya miezi sita na ushee, tangu tarehe 29 mwezi Juni2013 hadi sasa.
Kabla ya yote najiuliza kama mgomo ulikua unahatarisha maishaya watanzania Je kipindi chote hiki ambacho madaktari hawa walikuwawamesimamishwa maisha ya wagonjwa yalikuwa salama? Na ni kitu gani hasa kilichopelekeaserikali kuwasimamisha na kisha kukaa kimya kwa zaidi ya nusu mwaka, haditarehe 6 Novemba mwaka huu ndipo waanze kuwahoji?Tukio la kutekwa, kuteswa nakutupwa katika msitu wa pande Dk Steven Ulimboka limefikia wapi? Je waliotajwana gazeti la Mwanahalisi wamechukuliwa hatua yoyote, hata kuhojiwa tu? Hivikamanda Kova na IGP Mwema wanaweza kumtia hatiani mfanyakazi wa Ikulu ambaye raisamekana watu wake kuhusika? JWatanzania tunajiuliza hivi kweli haki itatendekana ionekane ikitendeka? Na kama haki haitatendeka nini kitafuata? Hata mimisijui ila nina uhakika hakitakuwa chema. Baada ya kimya cha zaidi ya nusumwaka ndipo baraza la madaktari ambalo kwa sasa sidhani kama ni chombo hurulilianza kuwahoji interns. Tena kwa kuwaita Dar es salaam. Ifahamike kuwa hawani vijana wadogo tu ambao ndio wametoka vyuoni kwa hiyo unaweza ukatambua uwezowao kifadha hasa ukizingatia kuwa hawakuwa na kazi kwa muda wa zaidi ya nusumwaka. Kabla ya kuzungumzia kilichotokea kwa hao walioweza kufika na kuhojiwakisha kuadhibiwa ni wazi kuwa wapo wengi ambao hawakuweza kuhudhuria kwa sababumbalimbali ya kifedha ikiwa mojawapo lakini pia kutopata taarifa za uhakika.Baraza la madaktari ni chombokinachofanya kazi kwa mfumo wa kimahakama na ofisi ya mwanasheria mkuu waserikali inahusika moja kwa moja. Kwa kifupi ni chombo kikubwa kilichopaswakuwa huru. Kwa mtazamo wangu kwa sasa chombo hiki si huru kwa sababu kuu moja,kuwa chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ni serikali.
Sidhanikama mtu mwenye akili timamu anaweza kutegemea serikali ijihukumu yenyewe nakujiadhibu. Nikiangalia na kufuatilia kwamakini utendaji kazi wa Baraza la Madaktari MCT, na kwa kuzingatia hatua namaamuzi iliyoyafanya kuhusu hawa madaktari waliokuwa wamesimamishwa najisikiaaibu. Mimi simo ndani ya MCT lakini ilichokifanya ni aibu ambayo haikutegemewa.Chombo hiki kimewaacha wachambuzi wa mambo ya siasa na wanaharakati midomo wazikutokana na maamuzi yake yasiyo na kichwa wala miguu.Makosa ambayo madaktari hawawalishtakiwa nayo katika chombo hiki ni kushiriki katika mgomo uliokuwa batilina kuvunja kanuni na maadili ya kazi ya udaktari. Lakini kosa jingine lilikuwani kuhatarisha maisha ya wagonjwa. Hakuna daktari hata mmoja aliyekuwa na kosatofauti na haya. Hukumu iliyotolewa na baraza la madaktari, MCT inashangazakama ifuatavyo. Kwanza onyo, adhabu ya pili ni onyokali, nyingine ni kusimamishwa kwa muda. Na katika waliosimamishwa, wapowaliosimamishwa mwezi mmoja, wapo waliosimamishwa miezi miwili, wengine miezimine na wapo waliosimamishwa miezi sita. Na kwa hawa waliosimamishwa miezi sitakuwafanya kukaa bila kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kumbuka hawa ni wanataalumawanaohitajika kwa kiasi kikubwa hapa nchini na zaidi sana wanaweza kwendakufanya kazi mahala popote duniani. Lakini pia, pamoja na kwamba wotewalishtakiwa kwa makosa yanayofanana lakini adhabu ni tofauti kwa kiasi kikubwacha kushangaza.Kwa macho ya kawaida kabisayasiyohitaji elimu ya kisheria, ni kwamba inawezekanaje kukawa na tofauti kubwaya hukumu kwa watu waliotiwa hatiani kwa makosa yanayofanana? MCT inawezakutuambia ni vifungu gani vilitumika kumhukumu kila mmoja? Na imetokea vipikosa moja au makosa yanayofanana kuwa na aina nyingi za hukumu kiasi hicho?Nilipochunguza kwa makini na kufuatilianani kapewa adhabu gani nimegundua kuwa waliosimamishwa wengi wao ni ambao amawalisikika au kuandikwa na vyombo vya habari wakizungumza au kueleza madai yamadaktari. Kwa mwenye akili timamu atajiuliza kwani hawa walikuwa na mashtakaya ziada? Kama hapana sasa iweje watendewe hivi?Swali jingine la kujiuliza nikwamba wakati haya yakitokea na interns hawa kupewa adhabu na baadhi yaokutakiwa kurudi kazini kuanzia Januari 14 mwakani hali katika hospitali zetuikoje? Mazingira yameboreshwa? Madawa na vifaatiba vipo vya kutosha?Achilia mbali adhabu zilizotolewana baraza hilo lakini pia taarifa kutoka ndani ya baraza hilo zinasemamadaktari 49 wamefutiwa mashtaka. Hii ni baada ya kukutikana hawana hatia.
Ifahamike hawa ni wale ambao ama walikuwa wagonjwa, au katika ruhusa kwa sababumbalaimbali ikiwa ni pamoja na misiba, ugonjwa au harusi. Lakini ifahamike kuwahawa nao hawakuwa kazini kwa kipindi kisichopungua nusu mwaka kabla ya kufutiwamashtaka. Hii inatupa taswira gani hasa ya utendaji wa baraza na serikali kwaujumla? Ilkuwaje hawa nao wakasimamishwa kwa muda wote huo? Ni nani aliyeamuahivyo na kuhatarisha maisha ya wagonjwa ambao wanateseka kwa ukosefu wamadaktari nchini? Ni nani anayeweza kusimama kifua mbele na kusema serikali ipomakini? Ni nani anayeweza kutuambia kuwa baraza la madaktari ni chombo makini?Kama baraza liliweza kuwasimamisha kazi madaktari ambao hawakuwapo katika mgomo,Je linaweza kutenda haki pasi na shaka?Baraza hili limeonesha udhaifumkubwa pale lilipokaa kimya pasipokueleza hatima ya madaktari interns ambaohawakuweza kufika Dar es Salaam ili wahojiwe kwa sababu mbalimbali, tatizo lakifedha likiwa mojawapo. Lakini si hivyo tu ifahamike kuwa baraza hilihalikutumia njia inayofaa kuwataarifu madaktari juu ya kufika Wizarani Dar esSalaam ili wahojiwe. Baraza lilibandika tangazo wizarani na kuwatumia meseji yaujumla ikisema interns ambao majina yao yamebandikwa wizarani wafike hapokuhojiwa kulingana na tarehe waliyopangiwa. Baraza halikutoa taarifa kwa mhusikammoja mmoja kuwa unahitajika kufika wizarani lini na kwa ajili gani.
Nasemabaraza hili limetia aibu maana nina uhakika wa taarifa kutoka ndani ya baadhiya wajumbe wa baraza hilo kuwa hata sasa hawana uhakika kama hao madaktariambao hakuweza kuhudhuria walipata taarifa au la. Ni ukweli usiopingika kuwa baadhi ya wajumbewa baraza la madaktari wameoneka kutoridhishwa na utaratibu na maamuziyaliyofanyika. Hili limethibitika kwa maneno yao wenyewe. Wengine wamesikikawakisema haki ilikuwa ikitendeka kipindi cha Nyerere na si sasa. Swali ambalo watanzania tunapaswakujiuliza ni, Je mazingira ya kazi kwa madaktari hawa ambao waligoma kwa sababuya mazingira magumu yameboreshwa? Je madawa yanapatikana? Siku hizi sionimatangazo ya Mseto (ALU) dawa yenye nembo ya jani. Najiuliza imekwenda wapi?Maana najua inauzwa elfu moja. Kwa sasa haipo yenye nembo ya jani na zilizoponi shilingi elfu saba kwa dozi moja. Swali ni kwamba waziri wa Afya ana lipi lakutueleza? Mbona amekaa kimya?Katika hospitali ya mkoa wa Dodomaambayo imepandishwa hadhi na kuwa hospitali ya rufaa ya mkoa hali ya vitendeakazi ni mbaya. Kati ya tarehe 2 haditarehe 18 nimethibitisha hospitali kukosa dawa ya uchungu (Oxytocin) kwa wazaziwanaotaka kujifungua. Lakini kipindi hicho hicho pia hakukuwa na vitambaa(Gauze) na hivyo wagonjwa kutakiwa kununua halafu ndio wafanyiwe upasuaji baadaya vitambaa hivyo kuwa sterilized. Tarehe 23 mwezi desemba hospitali ya rufaa yamkoa wa Dodoma haikuwa na na chlorine kwa ajili ya kusafishia vifaavilivyotumika kwenye upasuaji n.k. Hivi karibuni hospitali ya Bundahaikuwa na umeme wala maji. Hospitali ya Temeke Dar es Salaam mgonjwa anatakiwakununua sindano, maji ya dripu na karibu kila dawa.
Hivi kweli kati yamadaktari na serikali nani anahatarisha maisha ya wagonjwa katika mahospitali?Hivi hawa madakatari waliotendewa dhuluma kama hii kweli wanaweza kufanya kazikwa moyo mmoja? Mungu tusaidiewatanzania. Binafsi nimeshuhudia baraza hili lamadaktari, MCT likitoa hukumu kwa jazba na hasira hasa daktari anayehojiwaanapoeleza ukweli wa hali mbaya ya huduma katika hospitali zetu na paleanapoeleza uonevu uliofanywa na unaoendelea kufanywa na serikali ikiwemoyenyewe MCT. Sidhani kama huu ndio utakuwa mwisho wa madaktari kudai haki yaostahiki na sidhani kama wataacha kupigania huduma bora kwa watanzania.Inawezekana wasigome leo au kesho ila nina uhakika wa kutokea mgomo mbaya zaidiikiwa hali ya huduma za afya na mazingira ya kazi yasiposhughulikiwa ipasavyo.Maana si madaktari watakaoanzisha mgomo bali wagonjwa na ndugu zao nawatanzania kwa ujumla. Nguvu ya umma haitazuiliwa na chochote. Si vitisho, simahakama wala risasi itakayoweza kuwazuia wananchi wakichukua hatua ya kudaihaki yao kwa pamoja. Zipo namna nyingi ambazo watanzaniawanaweza kutumia kuiadibisha serikali. Nimekuwa nikisikiliza sana hotuba zarais wa Marekani Barack Obama. Mara nyingi amekuwa akisema ushindi wake niushindi wa wamarekani na maendeleo yaliyofikiwa na Marekani yanatokana nawamarekani.
Ila hapa kwetu nadhani mnaelewa kiongozi haoini aibu kusemamaendeleo yanaletwa na chama chake. Baraza la madaktari Tanganyika(MCT), Wizara ya Afya ni vema mkatoa ufafanuzi wa ukiukwaji, ukandamizaji nauonevu huu mkubwa waliofanyiwa madaktari (Interns na registras). Nadhani niwakati wa wanaharakati, chama cha madaktari na yeyote aliye na nia njema kwanafasi yake kuandaa muswada wa kuirekebisha MCT ili iwe chombo huru nakurudisha heshima iliyopotea ya chombo hiki. Ili kiweze kuwa huru kutenda hakina kuepusha hisia za chombo hiki kusukumwa na watawala kifanye watakavyo wao.Mungu ibariki Tanzania Munguibariki Afrika
George Adriano