Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania(CPCT) lakemea watumishi wa Mungu wanaotapeli waumini kwa kuwauzia vifaa vya upako

1a94c6b8-a0c5-4384-a0a9-13421b4f2cef.jpg
 
Paulo alimpinga Petro waziwazi kwa sababu ya unafiki wake,kwa hiyo kupingana kwa vitu vidogo vidogo sio jambo geni, lakini cha msingi wote wanamhubiri kristo,wanaamini kuwa ni Bwana,wanaamini kuzaliwa na kifo na ufufuo wake.
Acha uongo leta maandiko
 
Waumini wanadanganywa wanauziwa maji ya kutoka mto Yordan! Maji ya 100 wanauziwa 10,000!? Dah kweli wajinga ndio waliwao
 
Hii mbona hatuoni wakipingana mafundisho

Kwann unatumia maandiko kuhalalisha utapel
Hata wao wanapingana vitu vidogo vidogo,lakini wote wanamkiri Yesu ni Bwana,wanaamini alikuja katika mwili,wanaamini alikufa na kufufuka na kuwa ni mwana wa Mungu,kwa kuamini hayo ndio misingi ya ukristo mengine ziada.
 
Tapeli huyu
Kwenye Biblia
Habili alifanya vizuri akapata kibali mbele za Mungu akabarikiwa.Kaini nduguye akanuna alipoona Mibaraka ya Habili aliyokuwa akipata.Mungu akamuuliza kwa Nini unamnununia nduguyo anavyobarikiwa? Na wewe ukiganya vyema si utapata kibali na kubarikiwa?

Mitume na manabii makanisa yao yamekuwa yakikua kwa kasi ya ajabu na kujaza watu kibao

Viongozi wengine Wenye Roho ya Kaini wananuna na kuwashambulia mitume na manabii

Fanyeni vizuri Mungu atawapa na nyie kibali
 
Tunashukuru MUNGU tangazo muhimu limetolewa ifikie kipindi hawa waganga wa kienyeji (manabii na mitume) wafungiwe huduma wanazofanya..
Hili wimbi la manabii feki likiachwa liendelee kutakuwa na shida huko mbeleni hasa Sisi wakristo
Wanakueleza, ujinga ni fursa.

Isemwe mara ngapi juu ya unabii wa uongo wa hao wanamazingaombwe?

Hata ukikemea utapeli huo kwa kuwachapa viboko hao wajinga ili wasiende huko, sanasana utashitakiwa wewe kwa kujichukulia sheria mkononi, lakini hizo 'kondoo' haziwezi kukoma kwenda kupigwa.
 
Majibu yako mepesi sana

Nani kakwambia kila mmoja ana kanisa ili asambaze kaz kirahisi?

Hujawahi kuona eneo kama ubungo kibangu tu lina manabii hata watano na kila mmoja kanisa lake lina jina tofauti na mafundisho mengi wanatofautiana, au unaongea tu usichokifahamu?

Unazungumzia Kakobe kwenda kwa Gwajima , unajua alienda kufanya nn? Alienda kumsafisha kuhusu kuvuja clip ya ngono

Ila mafundisho ya Kanisa la kakobe mengi yanatofautiana na Gwajima

Naongea kitu ninachokijua kwa 100%

Ndio maana huwez kukuta waumin WA gwajima waliokaribu na Kanisa la mwingira au kakobe wakaenda kusali kwa kakobe ,

Unajua kwann ni u tofauti wa mafundisho


Nipe Aya inayosema wauzie watu mafuta ,chumvi na keki

Tofautisha Sadaka na bei za kuuziwa Mafuta ,chumvi n.k

Sadaka ni hiari yako

Ulishaona kwa Mwamposa anagawa mafuta bure ? Kwann yana bei maalumu?
Siku za ibada mafuta mbona bure?
 
Aaron Arsenal, Aaron Arsenal, Ndugu nakushauri uweke akiba ya maneno.
Usihukumu, usije ukahukumiwa.

Rum 14:4 imeandikwa, Wewe U nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine??? Kwa BWANA wake mwenyewe yeye husimama au huanguka.

***Galatia 6:7 imeandikwa, Msidanganyike, MUNGU hadhihakiwi,
Kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Rum 14: Ile imani uliyonayo uwe nayo nafsini mwako mbele za MUNGU.
Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika lile "NENO" analolikubali.
Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani.
***Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Aaron Arsenal, kila mwanadamu ana haki ya kuabudu kile anachokiamini katika maisha yake. Yumkini hauharibu au kuzuia uhuru wa mwanadamu mwingine tena kwa lazima, ila kila mmoja anafanya kwa utashi wake na hiari yake na imani yake, hapo siyo kosa.

Hakuna kitu kibaya duniani hapa chini ya jua kama kumhukumu mtu , tena bila ushahidi na sababu ya msingi, huko ni kujitafutia laana tena kubwa.
Ushauri wangu kwako, " wewe Aaron Arsenal waombee hao ili kama watumwa na MUNGU basi huduma zao ziwafikie wengi, na kama hawajatumwa na MUNGU, basi waombee rehema juu ya wanayoyafanya kama ni machukizo kwa MUNGU aliye Hai.

Uzingatie hayo juu.
 
Aaron Arsenal,
Hivi Roho Mtakatifu aliyemponya na kumnyanyua kilema akatembea pale kwenye geti kwa kutumia mamlaka aliyoiweka ndani ya Petro wakiwa na Yohana, siku hizi amepungukiwa nini hadi asaidwe na vitambaa, maji , mafuta n.k. Mimi nashukuru sana Mungu kwamba wachungaji wangu wote wa TAG Tanzania nzima, wanalichukia sana hili jambo, zaidi ya wanavyouchukia ukoma! Nawasifu sana wachungaji wa TAG
 
DECI watu waliaminishwa kuvuna mara mbili wakati ni uongo wakati mitume na manabii wanawaaminisha vitu ambavyo huja kuwa kweli,maana wanapona,wanafunguliwa vifungo vyao n.k.ndio maana akinunua kikiisha anarudi tena kununua.
Sawa mkuu, ngoja tuwaachie wenye imani zao masuala ya imani. Ila naona tunapoelekea hakutakuwa na tofauti na wazee wa tunguli
 
Halafu siyo hao manabii wakubwa tu wenye majina tu lakini mitaani kuna ambao ni wa kawaida nao wanawapiga watu vilevile

Walokole buana
 
Yani kama uko na m(wa)zazi mlokole halafu kila ukimrushia hela baada ya muda mfupi anakupa Hadith ya kukuomba hela kama ameokoka mfuatilie utakuta fedha yako akipokea toka kwako anaipeleka kwa Nabii/Mtumishi

Wao wanaila hela yako kilainiiiii
 
Yesu alimshinda adui kwa Neno tu

Alimwambia imeandikwa!

Ukifanyika kuwa mwanafunzi mzuri wa Kristo, ukaishi kwa Imani yaani kwa kulifuata Neno huku ukiwa na dhamiri safi na njema na kufurika pendo la Kristo wala hautahitaji maji , chumvi wala mafuta ya upako

Utapata wepesi na majibu mazuri ktk mambo yako!

Utabarikiwa kuliko wote waliozaliwa kabla yako Yani katika ukoo na mababu zako kwa baba na mama hakuna aliyeinuliwa wewe ni kwanza na labda watakaofuata baada yako, hiyo inawezekana kabisa ukimwamini Mungu na kujishusha na kusoma/ kufanya kazi kwa bidii, maarifa, weledi n.k
 
Back
Top Bottom