Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania(CPCT) lakemea watumishi wa Mungu wanaotapeli waumini kwa kuwauzia vifaa vya upako

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Tamko la Baraza la Maaskofu wa CPCT kuhusu mafundisho na matendo ya kuuza na kuvitumia vitu kwa madai vina upako katika kuwahudumia watu kwa maombezi

Baraza la Maaskofu wa CPTC, limekemea vikali matumizi ya vitu ambavyo wanaojiita watumishi wa Mungu, mitume na manabii huviuza kwa Jina la (vifaa vya upako)
kama vile;

- Mafuta
- Chumvi
- Maji
- Udongo
- Vijiti vya kuchokonolea meno
- Soda
- Keki
- Pipi
- Vitambaa

Nimependa Kipengele:
4(d). Ni Utendaji wa uganga wa kienyeji, na hivyo kuwapotoa kutoka kwenye Nguvu za kweli za Mungu na njia ya kweli (2 Wakolintho 2:17).

1575365057841.png

1575365098077.png
 
Nadhani kuna wivu ndani yake.

Biblia ni pana sana na haifai kukaririshwa Yale tu walitufundisha wakoloni wamisionari.

kama watu wanapona, tatizo liko wapi
Kiongozi

mambo yamekwiva

mLizoea kukwiba va watu kwa mazingaombwe

mkatafute kaz halali sasa kabla hamjaanza kuaibika

mirija yoooote inakatwa sasa mmoja baada ya mwngine
 
Kiukweli haya mambo yalikua yanachafua sana image ya kanisa na Ukristo at large. Wapentekoste tunaamini Mungu mwenyewe anafanya kazi na hahitaji conlmliments za mbadala. Kibaya ni pale hivi 'vitendea kazi' vinapowatoa washirika kwenye lengo la kumtumaini Kristo na kuwa dependant kwa hivyo.

And by the way, Kristo amesema mmepewa bure, toeni bure. Kinachoniuma zaidi ni kama vile African Pentecostalism is turning into a business thing sababu ya up rise of stupid false prophets and apostles wanaokimbilia mijini wakiuza hayo mafuta nk.

Rafiki tangu mmoja akanambia kwenda kuonana na mtumishi fulani mpaka uwe na appointment na lazima ulipe kiasi fulani. Hiyo ni kumuona tu, bado 'maombi'

It's so disgusting
 
Kwa kweli hali inasikitisha sana, Yani unakuta mwamini yeye fedha ya kujikimu hana lakini anatoa pesa na kumpa Mtumishi !

Yani kuna mambo huko?!

Wazazi wengine wanalilia shida watoto wao, wakishawapa hela wanazipeleka kwa watumishi

Yani inatia huruma sana jinsi watu wengi walivyokuwa brain stormed!
 
Back
Top Bottom