Baraza Kuu la UVCCM lamkataa Mizengo Kayanza Peter Pinda

Ole Shider

Member
Oct 17, 2014
16
15
Kutoka Dodoma;

Pamoja na kutumia zaidi ya Milioni 50 Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM linaloendelea Dodoma Limemkaata kwa kauli moja Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Pinda.

Pinda kakataliwa kuwa Naibu Kamanda wa Vijana Bara huku kwa upande wa Zanzibar Balozi Seif Iddy Makamu wa pili wa Raus akichukua nafasi hiyo na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiendelea kutetea nafasi yake ya Kamanda Mkuu wa Vijana Taifa.

Jambo hili kimsingi limeonekana kuwa fedheha kubwa na aibu ya kufunga mwaka kwa Waziri Mkuu wa Taifa hili hasa ukizingatia kiasi cha pesa alichomwaka kwa Vijana Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Vijana kutoka Mkoa wa KATAVI Ndgu. Kelvin Mbogo ambaye ndiye anayetumika na Pinda kurubuni Vijana alisikika akilalamika kwa jazba na hasira hasa akielekeza lawama zake kwa Viongozi wakuu ambao ni Sadifa, Sixtus na bwana mmoja aliyemtaja kwa jina la Omary Sleiman; malalamiko ya Mbogo ni kwamba hao mabwana wamepewa fedha nyingi tena zingine kawakabidhi yeye mwenyewe ila wameshindwa kumtetea Pinda katika swala la Unaibu Kamanda hivyo wamemsaliti Mzee wao Asali.

"Hawa kina Sadifa na Sixtus na Sleiman ni washenzi na wapuuzi kweli kweli haiwezekani wachukue fedha zote hizo halafu washindwe kumtetea mzee. Ni wasaliti na wanafiki wakubwa na watarudisha fedha zote washenzi hawa" Alisikika akilalama bwana Mbogo.

Wajumbe wa Baraza hilo wengi wakionekana wenye Mapenzi mema na Lowassa walisikika wakisema katika hili lazma hili Baraza livunjwe hakuna mtu wa kulambishwa asali kisa Unaibu Kamanda...... Pinda abaki kuutaka Uraisi na Jumuiya hii aieche kabisa. Kuna waliotujengea Vitega Uchumi vya maana lakini wameshindwa kuwaona hao wanatuletea majina ya watangaza nia wa Uingereza na wa maembe.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wamewapongeza sana Vijana kwa kulikataa jina la Pinda lakini vile vile wamesema hili ni aibu kubwa sana kwa mtu wa Kada ya Pinda ni bora wangemwacha mzee na nafasi zake za heshma kuliko kadhia na fedheha waliyomsababishia Pinda.

Kwa upande mwingine kuna baadhi ya Vijana walisikika wakisema Sadifa atakuwa amefanya hivyo kwa makusudi ili kumuumiza Pinda. "Jamani ni nani asiyejua mrengo wa Sadifa?? Halafu ngoja niwaambie watu huwa wanamwona Sadifa kama chizi lakini huyo jamaa na shidaaa ana akili zake mwenyewe. Sisi tunajua Sadifa ni wa Lowassa asilimi 1, 000 eti leo ampe Pinda Unaibu!! Sadifa kacheza Umafia na nakwambia Sadifa akitaka jambo lake lazma liwe sasa hili kalishindwa je?? Nyie acheni bana strategy za Lowassa Nchi hii hakuna mwenye uwezo nao....... Ona sasa walivyomtia aibu Mzee wa watu pamoja na Uwaziri wake Mkuu" Walisikika baadhi ya Vijana hapa Dodoma.......

Pinda alialikwa majuzi kufungua Semina ambapo pamoja na mengi Vijana wameshambatiza jina la mzee wa Maembe kutokana na kushawishi Vijana kumuunga mkono ktk upandwaji wa Maembe..........

Hili ni Aibu kubwa kwa Pinda ni Fedheha kubwa kwake, Ni kadhiha kubwa kwake na nafasi yake pia ukijumlisha na swala la IPTL mwelekeo wake kwisha........

UPDATE:
Salaam, kumekua na maneno mengi ya upotoshwaji kipindi hiki dhidi ya Mh. Pinda,yote yanatokana na hofu ya Lowassa na watu wake, Baraza kuu la umoja wa vijana halijajadili wala kuongelea swala la unaibu kamanda na wala halijafikishwa kwenye baraza kuu la vijana ni upotoshaji na uoga wa watu wa lowassa kutoka kukubalika kwa Pinda na kuonekana vijana wanamkubali na wanaweza kumpendekeza kuwa Naibu kamanda.

1) kama ukamanda UVCCM Taifa unauwezo wa kumpa mtu Urais basi mzee Kingunge angekuwa rais
2) Wajumbe wa baraza Kuu Taifa( Jumuiya zote ) hawaingii kwenye kikao cha kuweza kumtetea,kumzungumzia mgombea yeyote yule aliyetoswa na Chama Bali huingia kwenye kikao kimoja kinachowataka kuchagua mmoja kati ya watatu watakaofikishwa kwenye mkutano mkuu.

Hivyo kama kuna wajumbe wenye nguvu za kumjenga, kumuokoa ama kumtetea mgombea yeyote yule ni Kamati Kuu" CC" na "Nec"

Hivyo ni busara kutorubuni wasiojua wakati sote tunajua ukweli.

Ugawaji wa milioni 50!!
Haiingii akilini bali inadhihirisha ni kwa namna gani aliejitahidi kusambaza uvumi huo dhahifu amefirisika kifikra na ni mgeni hata wa kumiliki milioni moja.

Mbio za Urais ndio kwanza zimeanza, wenye vikao na wenye kura za maamuzi watathibitisha wanaemtaka.
 
Akataliwe tu hana maana tumemchoka, tupa kuleeee P Pinda.
 
Sasa huyo Kingunge atawashauri nini zaidi ya ushirikina? Nyie vijana wa CCM mbona hamjui kusoma alama za nyakati...

Mtagawana hadi mbao mwaka huu na tamaa zenu za madaraka lakini kipigo toka UKAWA kiko palepale
 
Hata hvy nafasi zote alizopita na hata hii aliyopo ni za kipewa hana maamuzi kiongozi huyu!
 
Kama kuna ushahidi wa chaguzi za CCM haziambatani na rushwa hapa nchini basi naomba modi anipe bani,,Hawa intarahamwe hata uchaguzi wa Nani aafanye ktk familia moja ya baba,mama,kaka dada nk watahongana tu
 
Hii ni vita haramu,silaha inayotumika ni rushwa kwahiyo anaeshinda na anaeshindwa wote hovyo tu.

Maneno mengi utazani kuna la maana kumbe ni kutembeza mlungula tu.

Hiki chama kimeoza mpaka kwenye shina!
 
Kweli maCCM ni ukoo wa panya, kama hawa ndio vijana wao je wazee wao wako vipi? Kuna haja ya taifa kutumia anointing water ya tb joshua ili kukififisha hiki kizazi cha maCCM na mapepo yaobya rushwa na ufisadi.
 
Mmmh!!! Kweli vijana. Kwa hiyo ktk baraza la wazee wa ccm uyo kingunge aendi...kweli uzee mwisho UKAWA, ccm kila mtu.......
 
Ninachokiona hapa, ni kwamba rushwa ya lowasa imekuwa kubwa kuliko ya pinda. Labda aongeze dau watam support kwenye uraisi.

Ccm Rest In Pieces!
 
Hiki Chama cha kishenzi ndicho kilichoharibu nchi yetu, kila sehemu wakienda wao ni kutoa rushwa, wabunge wote wa chama cha mahuni ni mitoaji rushwa na michukuaji rushwa. Kuanzia Kikwete mpaka majinga ya vijana wao. Wameweka matumbo yao mbele na kuliacha taifa nyuma.
 
Hao UVCCM wa sasa, they are nothing kabisa, UVCCM sasa doesn't matter much kama zamani, hata wasipompitisha Pinda kuwa naibu kamanda wa vijana, it makes no diference!, kama ni Pinda, ni Pinda tuu!, vijana watake wasitake, they are just nothing!. UVCCM ilikuwa ni ile ya kina John John na Emanueli!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom