Baraza kuu CHADEMA kukutana Dodoma

Vugu-Vugu

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
1,344
1,531
Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kinatarajiwa kufanya kikao chake cha Baraza kuu Taifa mwishoni mwa mwezi huu mjini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza kuu ni wenyeviti na makatibu wote wa chama katiaka wilaya zote za Tanzania Bara na Visiwani,Wajumbe wote wa kamati kuu Taifa, Wajumbe maalumu wa kualikwa na Mwenyekiti pamoja na viongozi wa kanda zote 10 za kichama, Kikao hiki kitafanyiki chini ya Mwenyekiti wake Mh Freeman Alkael Mbowe (Mb) akisaidiwa kwa karibu na Katibu wa Chadema Taifa Mh Vicent Biyegela Mashinji.

Agenda kuu ni namna ya kumalizia kazi hii rahisi iliyobaki ya kwenda Ikulu 2020 bila kumwaga damu wala kuchana shati! Wakuu mimi nimeteteswa hivyo na mjumbe hauwawi.

CCM Mwafwaaaaaaaaa!
 
Naomba ajenda kuu iwe ni kuhusu uchaguzi wa wabunge wa EALA... Chadema ifuate taratibu ambazo vyama vingine vimepitia. Ipeleke majina ya kutosha ili yakapigiwe kura na wabunge... Waache mambo ya kufosi fosi... CHADEMA kuna watu wametaabika na kujitoa kutumikia chama miaka kibao, sasa vinafasi vimepatikana ili nao wale kwenye kijani kibichi mnaenda kuwapa kina Masha ambao hawajasulubika kwa ajili ya chama na wakati kuna watu ambao wamekaa hadi mahabusu kwa ajili ya chadema, hasa wale vijana wa BAVICHA!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kinatarajiwa kufanya kikao chake cha Baraza kuu Taifa mwishoni mwa mwezi huu mjin
Agenda kuu ni namna ya kumalizia kazi hii rahisi iliyobaki ya kwenda Ikulu 2020 bila kumwaga damu wala kuchana shati! Wakuu mimi nimeteteswa hivyo na mjumbe hauwawi.

CCM Mwafwaaaaaaaaa!
Kikao chema makamanda ila mujiandae kwa hujuma toka kwa CCM na jeshi letu pendwa la policcm
 
watakutana nyumbani kwa mwenye chama Lowasa au? maana hawana ukumbi Dodoma...CHADEMA wanatia aibu sana chama kina ruzuku Zaidi ya milioni 400 kwa mwezi hawana hata Ukumbi wa mikutano? ruzuku yote inaliwa na Mbowe
 
Lini CDM watakuwa na agenda ya maendeleo, hata ya kujenga ofisi zao tu kama wanashindwa kuhamasisha maendeleo ya majimbo yao. Lissu jimbo lake kuna umaskini wa hatari ila kila kukicha yeye anahangaika na kesi za kipuuzi.
 
Naomba ajenda kuu iwe ni kuhusu uchaguzi wa wabunge wa EALA... Chadema ifuate taratibu ambazo vyama vingine vimepitia. Ipeleke majina ya kutosha ili yakapigiwe kura na wabunge... Waache mambo ya kufosi fosi... CHADEMA kuna watu wametaabika na kujitoa kutumikia chama miaka kibao, sasa vinafasi vimepatikana ili nao wale kwenye kijani kibichi mnaenda kuwapa kina Masha ambao hawajasulubika kwa ajili ya chama na wakati kuna watu ambao wamekaa hadi mahabusu kwa ajili ya chadema, hasa wale vijana wa BAVICHA!
Hei, badilisha mtazamo vinginevyo uache siasa. Ujumbe wa EALA siyo tuzo wala chanzo cha mapato kwa wanachama walikifia na kukitaabikia chama, la hasha, ni uwezo (significant capacity of a Chadema member) kuwakilisha ipasavyo Jamhiri ya Muungano katika bunge husika. Umeelewa?
 
watakutana nyumbani kwa mwenye chama Lowasa au? maana hawana ukumbi Dodoma...CHADEMA wanatia aibu sana chama kina ruzuku Zaidi ya milioni 400 kwa mwezi hawana hata Ukumbi wa mikutano? ruzuku yote inaliwa na Mbowe
Hiyo isikusumbue kichwa wanayo pesa ya kumwaga watakodi ukumbi.
 
Back
Top Bottom