Baraza jipya la Mawaziri la Serikali ya Ufaransa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza jipya la Mawaziri la Serikali ya Ufaransa

Discussion in 'International Forum' started by MAMMAMIA, May 17, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu mteule wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ametangaza baraza la mawaziri 34 (wakiwa ni pamoja na manaibu mawaziri).

  Baadhi ya sifa za baraza hili:
  - Idadi sawa ya wanawake na wanaume (17 wanawake na 17 wanaume).
  - Mawaziri 7 kati yao wana umri chini ya miaka 40
  - Mawaziri 7 wana asili ya kigeni, wakiwemo wenye asili ya Afrika ya Kaskazini, Carrebian na Korea.
  - Mishahara yao imepungua kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mawaziri wa serikali iliyopita, ambapo Sarkozy alijiongezea mshahara kwa asilimia 170 (Euros 19,000 kwa mwezi).

  Nadhani yapo tunayoweza kujifunza kutoka baraza la mawaziri kama hili, hasa katika masuala ya uwiano wa kijinsia na kubana matumizi.
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Tujiulize, nchi tajiri kuliko sisi -ikiwa na uwanja mpana zaidi wa shughuli za serikali- inawezaje kuwa na mawaziri wachache?

  ...Baraza la mawaziri la kisasa kabisa, likiwakilisha hali halisi ya nchi.

  ...Nadhani, somo la kwanza ni "ukubwa wa pua, si wingi wa makamasi".

  ...Bila kusahau asili ya kigeni.
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona siku nyingi walishajifunza sema vichwa vigumu na kupeana ulaji kwa hawa viongozi wetu ndo kila siku hatusogei kimaendeleo
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Haya mliyoyataja ndiyo Watanzania wengi wenye akili zetu hatuachi kujiuliza, "kwa nini nchi tajiri zinakuwa na matumizi madogo ya kiuendeshaji wakati sisi masikini tunaokwenda tukiomba kwao tunafuja pesa kwa kugawana ngawira?"
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  cha umuhimu hapo ni ujuzi wa watu na sio idadi au jinsia...kama wanawake wengi wana ujuzi zaidi nitaweka wanawake zaidi au kama ni wanaume hivo hivo...ukifuatilia usawa kwanza badala ya ujuzi serikali inaweza isifanye kazi vizuri na wanachi wakalalamika
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ufaransa ni nchi tajiri kuwa waziri ni kwa ajili ya umaarufu na siyo kwa ajili ya kipato hapa kwetu uwaziri ni kazi kama vile Mkurugenzi mkuu, Katibu Mkuu, Meneja mkuu nk. hivyo kuwa na mawaziri wengi ni sehemu ya sera ya serikali ya kutoa ajira kwa wananchi wake (FULL EMPLOYMENT POLICY)
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliasana na wazo la kujali zaidi uwajibikaji kuliko kukimbilia uwiano, lakini kweli inawezekana kuwa katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 40 kusipatikane na wanawake na wanaume wachache wenye uwezo wa hali ya juu? Hasa ikitiliwa maana kuwa uwaziri ni suala la kisiasa zaidi kuliko utaalamu.

  Ikiwa umekusudia kuchekesha, nimecheka sana na hii sera ya ajira. Nakumbuka hata mheshimiwa mmoja alijisifia kuwa ukosefu wa maji nchini umepelekea kuwa na "vijana wengi wajasirimali" kujiajiri kwa kubeba maji. Ooooooh Masikini Tanzania!
   
Loading...