Baraza jipya la mawaziri kimeo

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
waungwana husema nyota njema uonekana asubuhi,
kura zinazoendelea ktk gazeti la mwananchi juu ya mitazamo ya watu ya hili baraza jipya la mawaziri hadi sasa wanaoongoza ni wale wanaosema "sijalifurahia kabisa"
nadhani hayo yote ni matokeo ya kuwarudisha mawaziri wengi wa baraza lililopita ambalo lilikuwa kimeo,sasa hao watawatumikia wakina nani iwapo hata kazi hawajaanza na watu hawana imani nao?
 
Hawa mawaziri CV zao zingekuwa zinawekwa wazi zikionyesha shule zao na mafanikio yako kwenye utendaji wa kazi, wananchi wangepata picha nzuri. Ila mkuu alishasema eti uwaziri hausomewi:hungry:
 
cha ajabu wengi wana kesi za kujibu mahakamani tokana na ubunge wao kupataikana ktk mtindo wa kuchakachua matokeo
mifano michache ni makongoro mahanga,mary nagu
 
Je umelipenda Baraza jipya la Mawaziri?
Select Poll

Je umelipenda Baraza jipya la Mawaziri?
Sijalipenda kabisa!
286 33.2%
Nimelipenda kwa kiasi
191 22.2%
Bado niko njia panda
148 17.2%
Nimelipenda sana!
124 14.4%
Sijalipenda kwa kiasi
113 13.1%

Number of Voters : 862
First Vote : Thursday, 25 November 2010 10:01
Last Vote : Sunday, 28 November 2010 13:44
 
:target: Hakuna kitu kabisa wala jipya ni sawa na kutoa Dirisha bovu kwenye nyumba na unalipeleka upande mwingine kwenye nyumba hiyohiyo.Waache siku zao zinahesabika nani alitegemea kuwa Obamma ataluwa Rais wa Marekani?au Kamuzu banda wa malawi alijiita (the life presedent|)? Mabotu yuko wapi au rais Rais wa Zambia ?kila kitu kina mwanzo na mwisho.
 
Pata picha hao ni watanzania wachache waliopata nafasi ya kutoa hayo maoni,je wakipata taarifa watanzania wengine kama kuna kura za maoni zinaendelea ni wangapi watasema hawalipendi kabisa?na hapa ni kura za siku 3 tu,je ikifika wiki nzima s itakuwa aibu?
 
Tatizo linalomsumbua JK ni USWAHIBA! Yeye badala ya kuunda kwanza Wizara halafu ndo atafute mawaziri, hua anaanza kuandaa orodha ya Maswahiba wake kwanza, halafu ndo anaunda baraza! Issue hapo inakuwa ni "Technical know who" and not "Technical know how" Matokeo yake Baraza linakua kimeo zaidi ya mno! Hivi mtu kama Maghembe unakwenda kumpa uwaziri wa Kilimo... Kama si uchawi ni nini??..
 
JK anamaliza muda wake wala hana pressure maana hata ahadi zake za kuweka ma highway Dar nk alisema wazaramo wakapiga makofi akapata kura akalala mbele hakuna lolote litatokea kazi iko kwa huyo ajaye 2015 kutuelezea ahadi za JK maana zitakuwa kwenye kitabu chao na kama siyo basi Uchakachuaji CCM utakuwa wa hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom