Acha tutukanwe Tanzania tumezidi upumbavu inakuwaje hawa waisrael watujengee UDSM, Bugando Hospital na taasisi mbalimbali pia kutoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshi letu makanda wetu kama Luteni Jenerali Imran Kombe, Luteni Jenerali Silas Mayunga, Meja Jenerali Muhdini Kimario na wengine walipata mafunzo ya kijeshi Israel lakini tuliamua kuachana na Israel ili tujiunge na upande wa wapalestina wanaonyanyaswa na Israel tukidhania wapestina ni ndugu zetu na tunawalilia wajikomboe lakini matokeo yake wapestina hawatuthamini na wala hawatupi heshima inayostahili kwa kuwaunga mkono sisi na kujikuta tunapoteza manufaa mbalimbali kwa kuwa na urafiki na Israel.
Angalia Rais wa kwanza wa Tanzania aliyewapigania wapalestina alipofariki wapalestina hawakutuma ujumbe wowote wa juu ukiachilia Yasser Arafat mwenyewe kutohudhuria tulitegemea watu kama Mahmoud Dahlan, Ahmed Qurei, Sakri Habashi, Salim al-Zaanoun, Mahamoud Abbas au Saeeb Erakat mmoja wapo ahudhurie lakina hakuna isipokuwa balozi wa Palestina nchini Tanzania ndiye aliyehudhuria lakini wakati alipofariki Mfalme Hussein wa Jordan na Rais Hafidh Assad wa Syria ujumbe wa Palestina ulijazana kwenye mazishi kama njugu ndio nikagundua hawa jamaa hujali zaidi undugu wa kiarabu na sio undugu katika mapambano toka siku hiyo siwaoni wa maana tena, na kuwa upande wao Tanzania tunapoteza zaidi kuliko kupata manufaa nchi kibao na mataifa ya kiaarabu na kiislamu kama Mauritania, Niger, Misri, Jordan, Saud Arabia, Uturuki, Indonesia, Malaysia yana uhusiano wa karibu na Israel na yanafaidi kwanini sisi tujitenge na Israel kwa ajili ya watu wasio tunathamini matokeo yake tunaishia kuwa losers?
Kama haitoshi alipofariki Waziri Mkuu wa Israel Yizhaki Rabin bado wapalestina walituma ujumbe wa juu wa watu watatu sasa kama mtesaji wenu anafariki mnatuma ujumbe wa juu? kwanini anayewatetea anapofariki msitume ujumbe wa juu? lipi bora? jjbu hamthaminiki kivile kwa mnaowatetea.