Baradhuli mtanashati

Baradhuli mtanashati

Kuna mambo mawili duniani hutokea kwa namna mbili:
1. Kwa kutumia nguvukani yenye msukumo wa ziada kufanikisha jambo husika
2. Jambo lenyewe kufanyika kwa ufanisi mkubwa bila nguvukani kubwa na bila msukumo wa ziada.

Tukiishi kwenye dunia yenye mkanganyiko mkubwa. Kimetokea kizazi cha manabii na mitume wanaotumia nguvu kubwa na ushawishi wa ziada kujitangaza na kutangaza huduma zao. Wanatumia kila aina ya nyenzo kuiaminisha jamii kuwa wao ndio wao na wao ni bora na wa kuaminiwa kuliko wengine.

Akaondokea mtumishi wa Mungu aliyeishi kwa neno, akawa mwaminifu akashika neno, akatenda neno maisha yake yote ya utumishi na huduma kiimani na kiroho. Hakuipa shekeli kipaumbele, wala tamaa za kidunia wala karamu za walafi na vitu vya kujionesha na kujikweza.

Ni baada ya kumaliza utumishi wake ulioacha alama za kutukuka. Mungu akaamua kumkirimu baraka. Huyu mtu bila kutumia nguvukani yoyote tena akiwa porini mbali kabisa na dunia ya kileo yenye miundombinu ya kisasa na kila kitu. Alitangazwa akatangazika hadi nje ya mipaka ya nchi.

Pamoja na uduni wa huduma, ubovu wa miundombinu na kila aina ya shida. Watu maelfu kwa maelfu walipanga foleni kumfuata. Hapa ndipo utambue ya kwamba matendo ya Mungu si ya mwanadamu. Baradhuli hatambuliki mpaka uone matendo yake, na hata maneno yake.

Usisahau na maono yake pia. Anaweza kuwa msafi na mtanashati akiwa kavaa nguo za gharama na kupanda gari ya kifahari. Lakini atakaponena ama kutenda ndio utamtambua yeye ni nani.

Baradhuli ana ndimi mbili. Ya kwanza ya kunena. Ana maneno matamu kama yote na ushawishi wa ajabu mno. Atajipigapiga kifua na kuonesha uchungu wake lakini atakapokuja na ya pili. Midomo na mikono yake vinatisha na ni vichungu kama pakanga.

Hakuna binadamu asiyependa kusifiwa. Hakuna binadamu asiyependa kutambuliwa utu wake. Hakuna binadamu asiyependa kuonekana mwema mbele ya wote. Ni mahitaji ya kiasili mno ya kiumbe mwanadamu.

Lakini roho yako ikiwa imekunjamana utayapata haya kwa kulazimisha na kwa kutumia nguvu kubwa. Ila kama roho yako ni safi nyeupe isiyo na chembe ya ubaya. Utayapa haya yote bure na kwa ukubwa usiomilithilika.

Mioyoni mwa watu, mitandaoni, kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye magari kila mahali kila wakati gumzo litakuwa juu yako
Wabaya wako watajitahidi kukuandika vibaya, kukubeza na hata kukukejeli lakini matendo ya mwili hayawezi kuzidi ya rohoni. Jua halikingwi kwa viganja na ukimpiga chura teke unamwongezea hatua.

Ukiwa baradhuli pamoja na utanashati wako wote lakini macho ya rohoni yanakuona unavyoumia na kuteseka sana. Sumu inakudondoka moyoni ukitamani wewe ndio ungekuwa yeye. Usikauke midomoni mwa kila mtu. Mijadala yote iwe juu yako. Kitaifa na kimataifa. Uwe wewe. Wewe. Wewe.

Wahenga walisema HIARI YASHINDA UTUMWA. USILAZIMISHE KUPENDWA.

Jr[emoji769]
.
IMG-20190224-WA0133.jpeg


Jr[emoji769]
 
HABARI MPYA: Mahakama Kuu imekubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa ni Mwanyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF)-MCL

Jr[emoji769]
 
Duu kweli huyo ni baladhuli mtanashati...

Alafu mbona ni kama unamsimanga fulani...


Cc: mahondaw
 
. DEMOKRASIA MSALABANI TANZANIA

Na Bollen Ngetti

HATIMAYE Rais Magufuli ameusaini Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019 na kuanzia sasa ni Sheria rasmi nchini Tanzania. Nimetokwa na machozi baada ya kuona giza nene tuendako ambako hakuko mbali sana!

Wito wangu kwa kila asomaye posti hii na atakayebahatika kusimuliwa kuhusu jambo hili afanye kila analoweza hata kama ni mara ya kwanza kujishughulisha na mambo haya kupata nakala ya Sheria hii na kuisoma kifungu kwa kifungu na kuielewa barabara ili kutoa elimu kwa wasiojua kusoma. Nimeumia mno! Ninaumia mno kuona tunavyoipeleka nchi yetu kwenye bonde la mauti lililojaa mizoga na mifupa mikavu kwa mikono yetu wenyewe!

Sheria hii italeta machafuko makubwa katika nchi hii na kuchafua kabisa taswira ya nchi yetu ya amani na utulivu tulioachiwa na waasisi wetu. Nahisi uchungu na heri siku hizo zisiwepo katika kalenda.

Ni ukweli usiopingika kwamba ni rasmi Tanzania imerudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja bila kuulizwa kwa kupitisha kura ya maoni. Hii ni hatua moja kubwa kwa nchi inayotaka kujaribu mfumo wa Imla katika nchi. Polepole anaposema CCM imejiandaa kutawala hadi 2100 sasa mueleweni!

Natoa mfano mmoja tu Kati ya mifano Tele: Sheria hii inampa mammals Msajili wa Vyama (Mteule wa M/Kiti wa CCM) kuingilia mchakato wa chama chochote na kumchagulia nani awe mgombea wa nafasi Fulani ndani ya chama au ya Kiserikali.

Kwa mfano: Chadema imchague Tundu Lissu kugombea Urais. Jaji Mutungi ataingia Chadema na kukiamuru kumsimamisha Joseph Haule "Prof. Jay" ndiye agombee Urais. Swali, wafuasi wa Chadema na Lissu watakubali? Varangati!

ACT-Wazalendo wanaweza kumteua Maalim Seif kugombea Urais Zanzibar lakini Jaji Mutungi akasema hapa, Ado Shaibu ndiye agombee. Je, wafuasi wa Seif wanaohama na ofisi watakubali? Mitulinga!

Sheria hii inaende kuangamiza demokrasia Tanzania kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea nchi hii! Huu ni ufedhuli usiovumilika kwa viwango vyote maana tulikwisha kupiga hatua kubwa.

Bila kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, rangi, kabila kila mtu apige kelele kwa kiwango cha umbali wa sauti yake. Iwe ni mashambani au mijini. Hii ni kwa faida yetu sote hata na aliyeisaini. Jumuiya za Kimataifa zisituache Tanzania kama yatima, zitusaidie tunakwenda kuzimu! Rais bado anayo nafasi ya kurejea uamuzi wake.

Asasi za kiraia zijitokeze kupiga mayowe. Viongozi wa dini waoneshe uongozi katika hili. Ukimya wetu ni maafa yetu katika suala Zima la demokrasia. Wabunge wa CCM mmetafuta laana katika hili kwa kutumia wingi wenu kuiangamiza demokrasia. Mzee Jakaya Kikwete jitokeze ulisemee hili! Tunakwenda wapi?

Wanasheria mnisaidie naweza kufungua kesi binafsi mahakama kuu ili sheria hii ifutwe kwa maslahi ya umma? Nisaidieni!
#AchaWoga2020
Bngetti@2019

Share kwa wingi hata mara 100000

Jr[emoji769]
 
[emoji125][emoji125][emoji125]
tapatalk_1553404059936.jpeg


Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom