Baradhuli mtanashati

Baradhuli mtanashati

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,092
Kuna mambo mawili duniani hutokea kwa namna mbili:
1. Kwa kutumia nguvukani yenye msukumo wa ziada kufanikisha jambo husika
2. Jambo lenyewe kufanyika kwa ufanisi mkubwa bila nguvukani kubwa na bila msukumo wa ziada.

Tukiishi kwenye dunia yenye mkanganyiko mkubwa. Kimetokea kizazi cha manabii na mitume wanaotumia nguvu kubwa na ushawishi wa ziada kujitangaza na kutangaza huduma zao. Wanatumia kila aina ya nyenzo kuiaminisha jamii kuwa wao ndio wao na wao ni bora na wa kuaminiwa kuliko wengine.

Akaondokea mtumishi wa Mungu aliyeishi kwa neno, akawa mwaminifu akashika neno, akatenda neno maisha yake yote ya utumishi na huduma kiimani na kiroho. Hakuipa shekeli kipaumbele, wala tamaa za kidunia wala karamu za walafi na vitu vya kujionesha na kujikweza.

Ni baada ya kumaliza utumishi wake ulioacha alama za kutukuka. Mungu akaamua kumkirimu baraka. Huyu mtu bila kutumia nguvukani yoyote tena akiwa porini mbali kabisa na dunia ya kileo yenye miundombinu ya kisasa na kila kitu. Alitangazwa akatangazika hadi nje ya mipaka ya nchi.

Pamoja na uduni wa huduma, ubovu wa miundombinu na kila aina ya shida. Watu maelfu kwa maelfu walipanga foleni kumfuata. Hapa ndipo utambue ya kwamba matendo ya Mungu si ya mwanadamu. Baradhuli hatambuliki mpaka uone matendo yake, na hata maneno yake.

Usisahau na maono yake pia. Anaweza kuwa msafi na mtanashati akiwa kavaa nguo za gharama na kupanda gari ya kifahari. Lakini atakaponena ama kutenda ndio utamtambua yeye ni nani.

Baradhuli ana ndimi mbili. Ya kwanza ya kunena. Ana maneno matamu kama yote na ushawishi wa ajabu mno. Atajipigapiga kifua na kuonesha uchungu wake lakini atakapokuja na ya pili. Midomo na mikono yake vinatisha na ni vichungu kama pakanga.

Hakuna binadamu asiyependa kusifiwa. Hakuna binadamu asiyependa kutambuliwa utu wake. Hakuna binadamu asiyependa kuonekana mwema mbele ya wote. Ni mahitaji ya kiasili mno ya kiumbe mwanadamu.

Lakini roho yako ikiwa imekunjamana utayapata haya kwa kulazimisha na kwa kutumia nguvu kubwa. Ila kama roho yako ni safi nyeupe isiyo na chembe ya ubaya. Utayapa haya yote bure na kwa ukubwa usiomilithilika.

Mioyoni mwa watu, mitandaoni, kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye magari kila mahali kila wakati gumzo litakuwa juu yako
Wabaya wako watajitahidi kukuandika vibaya, kukubeza na hata kukukejeli lakini matendo ya mwili hayawezi kuzidi ya rohoni. Jua halikingwi kwa viganja na ukimpiga chura teke unamwongezea hatua.

Ukiwa baradhuli pamoja na utanashati wako wote lakini macho ya rohoni yanakuona unavyoumia na kuteseka sana. Sumu inakudondoka moyoni ukitamani wewe ndio ungekuwa yeye. Usikauke midomoni mwa kila mtu. Mijadala yote iwe juu yako. Kitaifa na kimataifa. Uwe wewe. Wewe. Wewe.

Wahenga walisema HIARI YASHINDA UTUMWA. USILAZIMISHE KUPENDWA.

Jr[emoji769]
 
Kuna mambo mawili duniani hutokea kwa namna mbili
1. Kwa kutumia nguvukani yenye msukumo wa ziada kufanikisha jambo husika
2. Jambo lenyewe kufanyika kwa ufanisi mkubwa bila nguvukani kubwa na bila msukumo wa ziada....
Tukiishi kwenye dunia yenye mkanganyiko mkubwa... Kimetokea kizazi cha manabii na mitume wanaotumia nguvu kubwa na ushawishi wa ziada kujitangaza na kutangaza huduma zao... Wanatumia kila aina ya nyenzo kuiaminisha jamii kuwa wao ndio wao na wao ni bora na wa kuaminiwa kuliko wengine....
Akaondokea mtumishi wa Mungu aliyeishi kwa neno, akawa mwaminifu akashika neno, akatenda neno maisha yake yote ya utumishi na huduma kiimani na kiroho... Hakuipa shekeli kipaumbele, wala tamaa za kidunia wala karamu za walafi na vitu vya kujionesha na kujikweza...
Ni baada ya kumaliza utumishi wake ulioacha alama za kutukuka.. Mungu akaamua kumkirimu baraka... Huyu mtu bila kutumia nguvukani yoyote tena akiwa porini mbali kabisa na dunia ya kileo yenye miundombinu ya kisasa na kila kitu.. Alitangazwa akatangazika hadi nje ya mipaka ya nchi... Pamoja na uduni wa huduma, ubovu wa miundombinu na kila aina ya shida... Watu maelfu kwa maelfu walipanga foleni kumfuata... Hapa ndipo utambue ya kwamba matendo ya Mungu si ya mwanadamu....
Baradhuli hatambuliki mpaka uone matendo yake, na hata maneno yake... Usisahau na maono yake pia... Anaweza kuwa msafi na mtanashati akiwa kavaa nguo za gharama na kupanda gari ya kifahari.... Lakini atakaponena ama kutenda ndio utamtambua yeye ni nani.... Baradhuli ana ndimi mbili.... Ya kwanza ya kunena... Ana maneno matamu kama yote na ushawishi wa ajabu mno... Atajipigapiga kifua na kuonesha uchungu wake lakini atakapokuja na ya pili... Midomo na mikono yake vinatisha na ni vichungu kama pakanga.....
Hakuna binadamu asiyependa kusifiwa
Hakuna binadamu asiyependa kutambuliwa utu wake
Hakuna binadamu asiyependa kuonekana mwema mbele ya wote
Ni mahitaji ya kiasili mno ya kiumbe mwanadamu.... Lakini roho yako ikiwa imekunjamana utayapata haya kwa kulazimisha na kwa kutumia nguvu kubwa.... Ila kama roho yako ni safi nyeupe isiyo na chembe ya ubaya... Utayapa haya yote bure na kwa ukubwa usiomilithilika....
Mioyoni mwa watu, mitandaoni, kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye magari kila mahali kila wakati gumzo litakuwa juu yako
Wabaya wako watajitahidi kukuandika vibaya, kukubeza na hata kukukejeli lakini matendo ya mwili hayawezi kuzidi ya rohoni... Jua halikingwi kwa viganja na ukimpiga chura teke unamwongezea hatua....
Ukiwa baradhuli pamoja na utanashati wako wote lakini macho ya rohoni yanakuona unavyoumia na kuteseka sana.. Sumu inakudondoka moyoni ukitamani wewe ndio ungekuwa yeye.... Usikauke midomoni mwa kila mtu... Mijadala yote iwe juu yako... Kitaifa na kimataifa... Uwe wewe... Wewe... Wewe......
Wahenga walisema HIARI YASHINDA UTUMWA.....
USILAZIMISHE KUPENDWA.....!!!!!

Jr[emoji769]
Ntarudi Teena hata sjaelewa vzr,.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anasifiwa kwa matendo yake pia,wenyewe wanajua kama yanastahili sifa au kinyume chake. Inaweza kuwa ni sababu ya wao kutomjua vema.

Usisahau pia kuwa Baradhuli ana roho ya 'Heri Tukose Wote'. Lakini pale Mungu anapokuwa amepanga lake kwa mtumishi wake mwaminifu,mwanadamu hawezi kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... duh! hii ni falsafa ya hali ya juu sana! Ila umenishtua na matumizi ya maneno "Mungu" na "neno" ambalo umelirudia mara kadhaa ukimaanisha Neno la Mungu. Siku zote naamini wewe ni Mchawi bingwa na hata kipindi fulani uliwahi kuwa na cheo katika group lenu la kichawi kiasi naogopa hata kutia comments kwenye nyuzi zako! Anyway, hayo hayaondoi uhalali wa ulichoandika Mkuu.
 
Anasifiwa kwa matendo yake pia,wenyewe wanajua kama yanastahili sifa au kinyume chake.

Usisahau pia kuwa Baradhuli ana roho ya 'Heri Tukose Wote'. Lakini pale Mungu anapokuwa amepanga lake kwa mtumishi wake mwaminifu,mwanadamu hawezi kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja tuuachie wakati utasema.... Wakati ni hakimu wa haki.... Goliath alianguka kwa kombeo tuu... Tafsiri za kiroho si za kimwili

Jr[emoji769]
 
Mpaka sasa hivi kaishaiba zaidi ya 2.4 bln kwa kutumia vote 20, anataka kuombewa ili azile bila miiba na asifiwe na kila mtu akiwemo Lissu, Lissu yeye badala ya kumsifia anaonyesha sura kamili ya jiwe, sasa tumemjua analazimisha kupendwa wakati ni baradhuri mkubwa tena muuaji mkubwa anayenuka damu za watu
 
... duh! hii ni falsafa ya hali ya juu sana! Ila umenishtua na matumizi ya maneno "Mungu" na "neno" ambalo umelirudia mara kadhaa ukimaanisha Neno la Mungu. Siku zote naamini wewe ni Mchawi bingwa na hata kipindi fulani uliwahi kuwa na cheo katika group lenu la kichawi kiasi naogopa hata kutia comments kwenye nyuzi zako! Anyway, hayo hayaondoi uhalali wa ulichoandika Mkuu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]matendo ya Mungu si ya mwanadamu na giza kamwe halijawahi kuishinda nuru... Ndio maana kila kukichwa lazima kupambazuke.....!!!

Jr[emoji769]
 
Mpaka sasa hivi kaishaiba zaidi ya 2.4 bln kwa kutumia vote 20, anataka kuombewa ili azile bila miiba na asifiwe na kila mtu akiwemo Lissu, Lissu yeye badala ya kumsifia anaonyesha sura kamili ya jiwe, sasa tumemjua analazimisha kupendwa wakati ni baradhuri mkubwa tena muuaji mkubwa anayenuka damu za watu
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji848][emoji22][emoji22][emoji22]

Jr[emoji769]
 
Ngoja tuuachie wakati utasema.... Wakati ni hakimu wa haki.... Goliath alianguka kwa kombeo tuu... Tafsiri za kiroho si za kimwili

Jr[emoji769]
Tatizo ni hofu ambayo kwake ni asili. Ingawa si rahisi kulibaini hilo,labda kwa maombi na ufunuo.

Nakumbuka wakati fulani kijana mmoja baada ya kuoneshwa mtihani(feki) wa hesabu na akaufanya akijua ndio wenyewe. Alipofika kwenye chumba cha mtihani akakuta mambo ni tofauti aligonga dawati na kumwambia msimamizi mtihani ulionipa sio wenyewe.
Kwa busara msimamizi akamjibu chukua huo wako ufanye.
Baradhuli hajui ni mtihani gani ambao ni muhimu kwake kwa sasa.

Nimeipenda hekima ya msimamizi.... Je tunao wasimamizi wangapi wenye hekima kama hii?

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom