Chipsi yaipembeni
Senior Member
- Jan 8, 2015
- 128
- 93
Wakuu,
Asubuhi majira ya saa mbili nilienda hadi Posta Mpya kufanya shughuli zangu za kila siku, lakini nilipokuwa njiani kuelekea huko nilikutana na magari ya kawaida ya Polisi yakiwa yamejaza Askari, kuna wanaotoka Mjini kuelekea Morocco na kuna mengine yanaelekea Posta.
Nimepata dharura nimepitia barabara hii hii ya Bagamoyo kuelekea Tegeta, ila kwa muda huu ninaona Land Rover za Polisi zimeongezeka mno yakiwa yamejaza Askari, pia kuna gari moja linalofanyasafari kati ya Posta na Tegeta naona limejaza Askari ambao wengine wamekosa hata sehemu za kukaa wamesimama.
Hii inamaanisha kwamba majeshi yetu yamekwisha jiandaa na uchaguzi, ila hawa Polisi wengi ninaowaona huku itakuwa ndio wametoka CCP Moshi...kwa vyovyote vile watakuwa hawajamaliza mafunzo, chonde chonde ninyi maaskari ambao hamjamaliza mafunzo mtakapoanza kusimamia uchaguzi huu...msiwaige wale wengine ambao wakipewa amri wanatekeleza kwa kupiga binadamu wenzao bila kujali kuwa hata wao wakirudi uraiani (baada ya kustaafu) watakutana na mabomu.
Kueni watii kwa mujibu wa sheria na sivinginevyo, nawatakia majukumu mema kuelekea uchaguzi Mkuu.