Barabara za mzunguko Dodoma kujengwa kwa miezi 36

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1572424478151.png


Ujenzi wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma zenye urefu wa kilomita 112.3 utafanyika kwa miezi 36 huku Sh17 bilioni zikitengwa kuwalipa wananchi fidia. Kiasi cha Sh494 bilioni za ujenzi wa barabara hizo kitatolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Tanzania.

Akizindua ujenzi huo leo Jumanne Oktoba 29, 2019 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema Tanzania itatoa Sh82 bilioni. “Fidia itafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi. Tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huu," amesema Kamwelwe. Patrobas Katambi, mkuu wa Wilaya ya Dodoma akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema Mkoa utasimamia ulipaji fidia kuhakikisha kila kinachohitajika katika ujenzi huo kinapatikana.

Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amesema uombaji zabuni kwa ajili ya makandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo utafunguliwa Desemba 12, 2019, kwamba ujenzi huo utafanyika kwa miezi 36.
 
Wanajitahidi kuifanya dodoma kuwa mji mzuri ,but safari bado ndefu na gharama kubwa zitatumika bila return. Wangejipa muda mji ungekuwa wenyewe kupitia shughuli za kibiashara
Unataka return ipi, kwani Serikali imeenda pale kufanya biashara?
 
Hii picha mnayoonyesha ndio design yenyewe?patapendeza sana,ila watu waboreshe makazi yao,ukiwa unashuka kwa ndege mji unaonekana mchafu sana

Hahahahaaa makazi unaweza kuyaboresha tu kwa kuongeza vipato vya watu ili waweze kujenga na kuishi kwenye makazi bora.
 
Wanajitahidi kuifanya dodoma kuwa mji mzuri ,but safari bado ndefu na gharama kubwa zitatumika bila return. Wangejipa muda mji ungekuwa wenyewe kupitia shughuli za kibiashara
Return ni kuwa na barabara na miundo mbinu mizuri itakayowenzesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii vizuri, serikali haipo kwa ajili ya biashara....pia fedha hizi ni mkopo tunakopa tunaingiza fedha kwenye mzunguko tunanufaila wananchi pamoja na serikali kupitia kodi ambazo zitafanya mambo mengine...
 
Wanajitahidi kuifanya Dodoma kuwa mji mzuri but safari bado ndefu na gharama kubwa zitatumika bila return. Wangejipa muda mji ungekuwa wenyewe kupitia shughuli za kibiashara.
Shughuli zipi wakat serikal kazi yake n kujenga miundombinu bora ili kurahisisha raia kufanya biashara..?
 
diana chumbikino,

Hii picha mnayoonyesha ndio design yenyewe? patapendeza sana, ila watu waboreshe makazi yao. Ukiwa unashuka kwa ndege mji unaonekana mchafu sana.
Watu hawawezi hyo shughuri ya kujenga, apartments za kisasa zijengwe na govt na real estate companies bila hvyo jiji litakuwa la hovyo tu kama unabisha angalia opposite ya mji wa govt uone nyumba za hovyo tu
 
Kwanini mnatumia picha ya mchoro wa nchi nyingine? Au design bado?
 
Return ni kuwa na barabara na miundo mbinu mizuri itakayowenzesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii vizuri, serikali haipo kwa ajili ya biashara....pia fedha hizi ni mkopo tunakopa tunaingiza fedha kwenye mzunguko tunanufaila wananchi pamoja na serikali kupitia kodi ambazo zitafanya mambo mengine...
Mwambie huyo, maana wengi hawaelewi faida za uwekezaji wa serikali. Mfano mmoja mzuri ni ile taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete. Upasuaji unaofanyika pale sasa umeweza saidia kuokoa maisha na fedha nyingi serikali ilizokuwa ikizitumia kupeleka watu India.
 
Zisingenunulia hayo madege

Kwanhizo hela za ndege mngeweza ifanya dom Dubai fasta Sana

Ila we endelea tu
 
Kwanini mnatumia picha ya mchoro wa nchi nyingine? Au design bado?

Mi mwenyewe nimeshangaa eti wanazindua ujenzi halafu hata zabuni hazijakamilika ndo kwanza watazifungua Desemba. Sasa hapo wanazindua ujenzi wa nini sijui?
 
Back
Top Bottom