Ni muhimu sana kubadili mfumo wa kupata viongozi wa mikoa, wilaya n.k. Tuachane na mfumo wa kupeana uongozi mezani. wapigiwe kura na wananchi.
Chaos iliyopo Dar ni kwa sababu mkuu wa mkoa, mayor na wenziwe wamekuwa ni watu wa kufungulia milango wanasiasa.
Hivi kama mayor wa dar hajifunzi kutoka nchi nyingine? Jiji la biashara kama dar hata alama za barabarani zimewashinda?
Nipo barabarani kutokea kimara kuelekea mjini. Njiani ni balaa tupu kwa sababu kuna michepuko ya barabara isiyo na alama yoyote. Nimeingia barabara moja nikaenda kama kilometa 3 nikakuta kizuizi. Ikabidi nirudi tena nilikotoka. Kilometa 3! Nikatafuta sehemu nyingine ya kuingilia na baada ya muda nikagundua nimepotea tena. Tupo wengi
tunaopotea; kwani hakuna alama yoyote kuonyesha mwelekeo ni upi.
Nimechukua masaa mawili kufika maeneo ya ubungo. Hapo nimekuta chaos! chaos! chaos! Haijulikani magari yanaelekea mwelekeo upi! Magari na malori yamekutana uso kwa uso kila mahali na kuzifunga barabara. Huwezi kuamini kuwa hii ni nchi ya kistaarabu hata kidogo. Hakuna mataa na hakuna askari wa kuyaongoza magari yanayopita ovyo na mwishowe kuyabana magari mengine. Sote tumesimama.
Najiuliza: hivi hawa wakubwa wana habari jinsi nchi inavyosulubiwa? Wana habari kuwa tumegeuzwa vichekesho? Je wana habari kuwa huko Ujerumani inakotoka kampuni haiwezekani kufanyika kitu kama hiki na wakapona? Wana habari kuwa viongozi wote waliohusika kuleta upuuzi huu wanaweza kufutwa kazi immediately? Na Uchina viongozi na watendaji waliofanya hii kandarasi ya kiwendawazimu wangenyongwa?
Lakini kwetu ni business as usual. Kila kitu kiko sawa tu. Hakuna anayejali. Badala yake vinaonyeshwa vipindi vya tv kusifia huu upuuzi!
Na kinachoudhi zaidi ni kwamba huu mradi ni wa ulaji tu. Hakuna kitakachosaidia kupunguza foleni kwa kujenga barabara maalum ya mabasi yaendayo kasi. Wakubwa wetu hawajui kuwa wanaopanda magari yao binafsi hawatasubstitute magari yao kwa kupanda mabasi yanayonuka. No. Wataendelea kuendesha magari yao na foleni itaongezeka pia. Wakati wenzetu wanajenga miundombinu ya karne ya 22 sisi tunajenga barabara maalumu ya mabasi! Mungu tusaidie! Kwani hawa wenzetu wakienda kutembea huko nje kila siku hawaoni kinachoendelea huko au alimradi wapate chao mfukoni kwa kuleta miradi aghali na ya kipuuzi isiyo na tija kwetu? Hata wao wanajua huu mradi ni danganya toto tu na ndio maana hata Prof. Tibaijuka alisema huu mradi hauwezi kuondoa foleni! Sasa kama hata yeye anajua hivo huu mradi ni kwa faida ya nani? Kwa nini tutaabike hivi kwa mradi ambao we know for sure it is useless? Nawaonea huruma watu wangu!
Mkuu sijakuelewa hii maana yake nini? barabara ya morogoro road.
Ni kielelezo cha ujinga wa Magufulu... sio ujinga wetu.
Huu mradi haiko Wizara ya Ujenzi, ni mradi maalumu uko Ofisi ya Waziri Mkuu. Je, ni another Richmond?
Really? !!!
Makubwa
Naona wewe ni kama Thomaso, mpaka uone!!! Soma kwanza maelezo haya:
DART is an acronym for Dar Rapid Transit Agency.The Dar Rapid Transit (DART) Agency, came fully into force on 16th June 2008, established by GN.120 of 25th May, 2007, under the Executive Agencies Act, No.30 of 1997. It was established to achieve the following objectives:
Establish and operate Bus Rapid transit in Dar Es Salaam
Ensure smooth mobility on urban streets and roads, and
Ensure effective Management of DART Agency
Baada ya hapo, ebu tembelea hii website hii hapa
Background
Strabag ni janga