Barabara ya polisi ufundi mpaka mbagala

Barabara ya polisi ufundi mpaka mbagala

HM Hafif

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2009
Posts
1,359
Reaction score
20
Hii ni barabara mpya inayojengwa kutokea mivinjeni mpaka mbagara rangi tatu iliwa ni main road kuelekea Kilwa kupitia kwetu Rufiji. Barabara hii ilifunguliwa na mbwembwe na Rais JK ikijengwa na wajapan.

Barabara hii ina kasoro nyingi sana hata kwa sisi tusiokuwa waandisi. Kwanza barabara wametumia mtindo wa vipita shoto (Keep left) na hivyo kuuwa njia za kukatiza. mfano ukiwa umetoka uwanja wa sabasaba ukitaka kwenda town inakubidi uende ufate njia mpaka kwa aziz alli na pale utazunguka ndio uanze kurudi kurejea mjini.Na kuna sehemu nyingine nyingi zenye matatizo kama hayo.

Hii ni kuzidisha foleni zisizo na lazima.

vile vile viwango vyake ni duni sana. imejengwa hata miezi sita bado
imesha anza kuharibika.

Kwa kweli hilo ni kero. nauliza waandisi wetu wa TANROAD mpo wapi?
 
mfano ukiwa umetoka uwanja wa sabasaba ukitaka kwenda town inakubidi uende ufate njia mpaka kwa aziz alli na pale utazunguka ndio uanze kurudi kurejea mjini.

Utoke saba saba mpaka kwa aziz ali? mbona mbali hivyo!!
 
kwani wamejenga kwa pesa zao si msaada na we hujui kuwa misaada ian masharti yake.! siku zote itajengwa duni isiyo na plan kwa wakati huo na bado tutailipia kwani sie wananchi walipakodi ndio tunaoumizwa hali wasaini hiyo mikataba matumbo juu.
 
Utoke saba saba mpaka kwa aziz ali? mbona mbali hivyo!!

Mbona manakuwa wa kuja hivyo?? Hamjatembea nchi nyingine?? Nenda ulaya au marekani uone, dereva ukijichnganya ukakosea njia yako ili upate mahala pa kurudia unaweza kuwa umekwenda km hata 20.

Hiyo wala siyo tatizo sana labda useme hilo la ubora wa barabara.
 
Magezi,

Acha kukurupuka soma mada, tafakari na kisha lete jibu muafaka.

Kwanza lazima ujue hiyo barabara ni moja kati ya barabara kubwa kwenda Lindi. na hivyo lazima itakuwa na magari mengi sana kuelekea huko mbagala. Sasa chukulia wakati ule wa maonyesho ya sabasaba magari mengi yanatoka ndani sabasaba na kutaka kwenda mjini. Kuingia barabara kubwa lazima yaende mpaka Kwa Aziz Ali kisha yazunguke na kurudi.

hata ukiwa na ufinyu wa akili utaona hapo unasababisha foleni zisizo na msingi. Na lengo la kujenga barabara hii ikiwa pamoja na kuweka njia vizuri vile vile kuondoa misongamano isiyo na msingi.

nafikiri jitahidi kidogo kufikiria hilo na hiyo ni sehemu moja bila shaka kuna nyingine nyingi.

treni watu wanadandia kwa nyuma sio kwa mbele. Pole sana
 
Mbona manakuwa wa kuja hivyo?? Hamjatembea nchi nyingine?? Nenda ulaya au marekani uone, dereva ukijichnganya ukakosea njia yako ili upate mahala pa kurudia unaweza kuwa umekwenda km hata 20.

Hiyo wala siyo tatizo sana labda useme hilo la ubora wa barabara
,

Hivi wewe unaijua mbagala kweli au unalipuka tu?

hebu pita hiyo njia uone hadha zake.
 
Back
Top Bottom