barabara ya Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

barabara ya Nyerere

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 20, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JANA majira ya jioni saa 1 katika barabara ya Nyerere kulikuwa na foleni ndefu ya magari isiyo na mfano isiyotembea hali iliyofanya raia wawili wa kizungu kung’aka kwa hasira na hatimaye kushuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa miguu kuwahi Uwan ja
  Ilikuwa ni mtihili ya mchezo wa kuigiza ama watu wanarekodi filamu ya kibongo katika barabara hiyo ambapo watu wa kada na rika mbalimbali wakionekana kuchoshwa na hali ya foleni na hatima yake watu kuchukua uamuzi wa kushuka kwenye mabasi na kuanza kutembea kwa miguu

  Hali hiyo ilifanya wazungu hao nao kuhaha kwa kuona muda unayoyoma na dakika zinasonga mbele na gari walilokuwa wakilitumia liko palepale zaidi ya saa moja hali hiyo nayo iliwafanya wahamaki na kufungua milango ya gari hioyo kuchukua mizigo na kukimbia kwa miguuu kuelekea uwanja wa ndege

  Walipopata kama dakika moja wazungu hao kuonekana wakitembea kwa miguu wakiwa na mizigo yao mgongoni na kumuacha dereva wao barabarani, wafanyabiashara wa usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’ walifika na kuanza kugombania wateja hao hali iliyofanya kutembea ngumi wenyewe kwa wenyewe kugombania wateja hao

  NIFAHAMISHE ilishuhudia madereva hao wawili wakigombania mizigo ya raia mmoja ambapo dereva mwingine aliwahi kupakia mizigo ya mmoja na kumkimbiza na kubaki madereva wawili wakimgombania aliyebaki hali iliyopelekea mzungu huyo kung’aka kwa kile ambacho alichokuwa anafanyiwa na wafanyabiashara hao

  Hata hivyo dereva mmoja alionekana kuzidiwa nguvu na mwenzake na kunyakua mteja huyo na kumkimbizqa uwanja wa ndege na mwingine akibaki kuugulia maumivu ya ngumi alizozipata kwa mwenzake

  Foleni hiyo iliyoshuhudiwa na nifahamishe ilidumu kwa takribani masaa mawili magari hayatembei ilisababishwa na magari ya mizigo yaliyokuwa yakitokea bandarini kufunga barabara hiyo na sababu nyingine iliyozidisha foleni ilitokana na kufungwa kwa barabara moja ya Mandela eneo la Buguruni kutokana na ujenzi ambao unaendelea.
   
Loading...